1
Hili ni neno la Yahwe lililomjia Yeremia nabii kuhusu mataifa.
2
Juu ya Misri; "Hili ni juu ya jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri aliyekuwako Karkemishi kando ya mto Frati. Hili ni jeshi alilolishinda Nebukadneza mfalme wa Babeli likishindwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:
3
Wekeni tayari ngao ndogo na kubwa, na msonge mbele vitani.
4
Watieni farasi lijamu na hatamu, na mpande juu yao, ninyi wapanda farasi. Jiwekeni mahali penu, mkiwa mmevaa helmeti vichwani mwenu. Inoweni mishale yenu na kuvaa silaha zenu.
5
Ninaona nini hapa? Wana woga na wanakimbia, maana askari wao wameshindwa kabisa. Wanakimbia kwa usalama na hawaangalii nyuma. Kitisho kipo mahali pote--ili ni tamko la Yahwe--
6
wepesi hawawezi kukimbia, na askari hawezi kukwepa. Wana jikwaa kaskazini na kuanguka kando ya mto Frati.
7
Ni nani huyu ainukaye kama Nile, ambaoye maji yake yanaruka juu na chini kama mito?
8
Misri huinuka kama mto Nile, na maji yake yanaumuka juu na chini kama mito. Misri inasema, 'nitapanda juu na nitaifunika nchi. Nitaiharibu miji na watu wakaao ndani yake.
9
Nyanyukeni, farasi. Iweni na hasira, enyi magari ya vita. Askari na waende, Kushi na Putu, watu walio na ujuzi wa ngao, na Ludimu, watu wenye ujuzi wa kupiga pinde zao.
10
Siku hiyo itakuwa siku ya kisasi kwa Bwana Yahwe wa majeshi, naye atajilipizia kisasa juu ya adui zake. Upanga utararua na kujiridhisha. Utakula na kujishibisha kwa damu yao. Kwa maana kutakuwa na sadaka ya kafara kwa Bwana Yahwe wa majeshi katika nchi ya kaskazini kando ya mto Frati.
11
Panda Gileadi ujipatie dawa, binti wa Misri uliyebikra. Haifai kwamba unaweka dawa nyingi juu yako. Hakuna uponyaji kwako.
12
Mataifa wamesikia kuaibika kwako. Nchi imejawa na fedheha yako, maana askari hujikwaa juu ya askari; na wote wawili uanguka pamoja."
13
Hili ndilo neno Yahwe alilomwambia nabii Yeremia wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli alipokuja na kushambulia nchi ya Misri:
14
Toa taarifa kwa Misri na isikike katika Migdoli na Memfisi. Wamesema katika Tapenesi. Chukua kituo chako na jiweke imara, kwa maana upanga utakula wote kati yenu.
15
Kwa nini Apis mungu wenu amekimbia? Kwa nini ng'ombe dume mungu wenu hakuweza kusimama? Yahwe amemwangusha chini.
16
Ameongeza idadi ya waliojikwaa. Kila askari anamwangukia yule anayefuata nyuma yake. Wanasema, "Inuka. Haya twende nyumbani. Haya na turudi kwa watu wetu, katika nchi yetu ya asili. Na tuwe mbali na upanga wa mwangamizi."
17
Walitangaza pale, "Farao mfalme wa Misri ni kelele tu, aliyeiacha fursa yake ipotelee mbali."
18
Kama niishivyo--hili ni tamko la mfalme, ajulikanaye kwa Jina la Yahwe wa majeshi--kuna mtu atakuja aliye kama Mlima Tabori na Mlima Karmeli kando ya bahari.
19
Wekeni masanduku yenu kuyachukua uhamishoni, binti mwishio Misri. Kwani Memfisi itakuwa, magofu. itakuwa ukiwa kwa moto, na hakuna atakayeishi huko.
20
Misri ni mtamba mzuri sana, lakini mdudu aumaye anakuja kutoka kaskazini. Anakuja.
21
Askari wake wakukodiwa ni kama dume la ng'ombe lililonona kati yake, lakini wao pia watageuka na kukimbia. Hawatasimama pamoja, kwani siku yao ya madhara inakuja kunyume chao, wakati wa kuadhibiwa kwao.
22
Misri anatoa sauti kama ya nyoka na kuondoka kwa kutambaa, maana adui yake anakuja kinyume chake. Wanamkabili kama mkata miti aliye na shoka.
23
Wataangusha misitu--japokuwa ni mingi sana--hili ni tamko la Yahwe. Kwa maana adui watakuwa wengi kuliko nzige, wasioweza kuhesabika.
24
Binti wa Misri ataaibishwa. Atawekwa mkononi mwa watu kutoka kaskazini."
25
Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema, "Tazama, niko karibu kumwadhibu Amoni wa Thebesi, Farao, Misri na miungu yake, Mafarao wafalme wake, na wote wanaomtumaini.
26
Ninawaweka katika mkono wake atafutaye maisha yao, na katika mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli na watumishi wake. Kisha baada ya haya Misri itakaliwa kama mwanzo-- asema Yahwe."
27
Lakini wewe, Yakobo mtumishi wangu, usihofu. Usifadhaike, Israeli, maana tazama, nitayari kukurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya mateka. Kisha Yakobo atarudi, nakuwa katika amani; na kuhifadhiwa salama, na hapatakuwa na wa kumwogofya.
28
Wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope--asema Yahwe--kwa maana nipo nawe, hivyo nitaleta maangamizi makamilifu dhidi ya mataifa yote nilikokupeleka. Lakini sitakuharibu kabisa. Hata hivyo nitakuadhibu kwa haki na hakika sitakuacha bila adhabu."