1
Hili ni neno la Yahwe lililokuja kwa Yeremia nabii juu ya Wafilisiti. Neno hili lilimjia kabla Farao hajaishambulia Gaza.
2
"Yahwe asema hivi: Tazama, mafuriko ya maji yanainuka huko kaskazini. Yatakuwa kama mto uliofurika! Kisha yataigharikisha nchi na kila kitu ndani yake, miji yake na watu wakaao ndani yake! Kila mmoja atapiga kelele ya kuomba msaada, na wakaaji wote wa nchi wataomboleza.
3
Kwa sauti ya vishindo vya kwato za farasi wao wenye nguvu, kwa ngurumo za magari yao ya kivita na kelele za magurudumu yake, wababa hawatawasaidia watoto wao kwa sababu ya udhaifu wa mikono yao.
4
Kwa maana siku inakuja itakayowaacha ukiwa Wafilisiti wote, kumwondoa kila mtu aliyesalia huko Tire na Sidoni anayetaka kuwasaidia. Kwa maana Yahwe anawaangamiza Wafilisiti, hao waliosalia katika kisiwa cha Kaftori.
5
Upaa utakuja juu ya Gaza. Hata kwa Ashikeloni amenyamazishwa. Nyie mliosalia bondeni hata lini mtaendelea kuomboleza kwa kujikatakata?
6
Ole, upanga wa Yahwe! itachukua muda gani hata unyamaze? Rudini alani mwenu! Acha na unyamaze.
7
Itawezaje kutulia wakati Yahwe ameiamuru, na ameiaagiza kumpiga Ashikeloni na mwambao wa pwani ya bahari?