Sura 45

1 Hili ni neno ambalo Yeremia nabii alimwambia Baruku mwana wa Neria. Hii ilitokea wakati alipoandika kwenye kitabu maneno haya kwa imla ya Yeremia--hii ilikuwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, na alisema, 2 "Yahwe, Mungu wa Israel, asema hivi kwako, Baruku: 3 Umesema, Ole mimi, kwa kuwa Yahwe ameongeza uchungu wa maumivu. Kuugua kwangu kumenichosha; sipati pumziko.' 4 Hivi ndivyo unapaswa kusema kwake: "Yahwe asema hivi: Ona, nilichokijenga, sasa ninakirarua chini. Nilichopanda, sasa ninaking'oa. Nitafanya hivi kote duniani. 5 Lakini je, unategema mambo makubwa kwa ajili yako? Usitegemee hayo. Uone, maafa yanakuja juu ya binadamu wote--hii ni tamko la Yahwe--lakini ninakupa maisha yako kama nyara popote utakakoenda."