Sura 9

1 Lakini Sauli, akiwa bado akiendelea kuongea vitisho hata vya mauaji ya wanafunzi wa Bwana, vilipelekwa kwa kuhani mkuu 2 na kumwomba barua kwa ajili ya masinagogi huko Dameski, ili kwamba akimpata mtu aliye katika Njia ile, awe mwanaume au mwanamke, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. 3 Alipokuwa akisafiri, ilitokea kwamba alipokaribia Dameski, ghafla ikamwangaza kotekote nuru kutoka mbinguni,' 4 naye akaanguka chini ardhini na akasikia sauti ikimwambia,"Sauli, Sauli, mbona wanitesa mimi?" 5 Sauli akajibu, "U nani wewe Bwana? Bwana akasema, " Mimi ndiye Yesu ambaye unamtesa; 6 Lakini inuka, ingia mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda 7 Wale watu waliosafiri pamoja na Sauli wakasimama kimya, wakisikiliza sauti, wasione mtu. 8 Sauli akainuka kutoka ardhini, na alipofungua macho yake, hakuweza kuona kitu, hivyo wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9 Kwa siku tatu alikuwa haoni, naye hakula, wala kunywa. 10 Basi palikuwapo mwanafunzi Dameski jina lake Anania. Bwana alisema naye katika maono, "Anania!" Akasema, "Ona, nipo hapa, Bwana. 11 "Bwana akamwambia, "Inuka uenda zako katika mtaa uitwao Nyofu, na katika nyumba ya Yuda na ukaulize mtu kutoka Tarso aitwaye Sauli; maana angali anaomba; 12 Ameona katika maono mtu jina lake Anania akiingia na kumwekea mikono juu yake ili apate kuona tena." 13 Lakini Anania akajibu, "Bwana, nimesikia kutoka kwa wengi kuhusu mtu huyu, kwa kiasi gani amewafanyia mabaya watu wako watakatifu walioko Yerusalemu; 14 Anayo mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kuweka katika vifungo kila mtu hapa anayeliitia jina lako." 15 Lakini Bwana akamwambia, "Nenda, kwa maana yeye ni chombo kiteule kwangu, kulibeba jina langu mbele ya watu wa Mataifa na wafalme na wana wa Israeli. 16 Kwa maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu". 17 Hivyo Anania akaondoka, akaingia mle nyumbani; Akaweka mikono yake juu yake, akasema, "Ndugu Sauli, Bwana Yesu, aliyekutokea katika njia ulipokuwa unakuja, amenituma ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu." 18 Mara moja kitu kama magamba kilianguka kutoka kwenye macho ya Sauli, naye akapata kuona, akasimama, na kubatizwa; 19 akala chakula na kupata nguvu. Akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa siku nyingi. 20 Wakati huo huo akamtangaza Yesu katika masinagogi, akisema kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. 21 Na wote waliosikia walishangaa na kusema, "Siyo mtu huyu aliyewaharibu wote walioita Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa amekuja kwa kusudi la kuwafunga na kuwapeleka kwa makuhani." 22 Lakini Sauli akawa na nguvu zaidi na zaidi, naye alikuwa akisababisha dhiki miongoni mwa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo. 23 Baada ya siku nyingi, Wayahudi walipanga shauri pamoja kumuua. 24 Lakini mpango wao ukajulikana kwa Sauli. Wakamvizia mlangoni mchana na usiku wapate kumuua. 25 Lakini wanafunzi wake wakamchukua usiku na kumteremsha kupitia ukuta, wakimshusha kwenye kikapu. 26 Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi lakini walikuwa wakimuogopa, wasisadiki kuwa yeye ni mwanafunzi. 27 Lakini Barnaba akamchukua na kumpeleka kwa mitume, na akawaeleza jinsi Sauli alivyomuona Bwana njiani na Bwana alivyozungumza naye, na jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski. 28 Alikuwa pamoja nao akiingia na kutoka Yerusalemu. Akinena kwa ujasiri kwa jina la Bwana Yesu, 29 na akajadiliana na Wayahudi wa Kiyunani lakini wakijaribu mara kwa mara kumuua. 30 Wakati ndugu walipojua jambo hili, wakamleta Kaisaria, na kumpeleke Tarso. 31 Basi kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria, lilikuwa na amani, na likajengwa, na likatembea katika hofu ya Bwana na faraja ya Roho Mtakatifu, kanisa likakua kwa kuongezeka idadi. 32 Sasa ilitokea kwamba, kama Petro alivyoenda akizungukazunguka pande zote za mkoa, alishuka pia kwa watu watakatifu wa Mungu ambao waishio katika mji wa Lida. 33 Akamuona huko mtu fulani jina lake Ainea, aliyekuwa kitandani kwa miaka minane; maana alikuwa amepooza. 34 Petro akamwambia, "Ainea, Yesu Kristo akuponya; Inuka na utandike kitanda chako," na mara akainuka. 35 Hivyo watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona mtu huyo, wakamgeukia Bwana. 36 Sasa palikuwa na mwanafunzi Yafa aitwaye Tabitha,( ambalo lilitafsiriwa kama "Dorcas") Huyu mwanamke alijaa kazi njema na matendo ya huruma aliyowatendea maskini. 37 Ilitokea katika siku hizo aliugua na akafa; walipomsafisha, walimpandisha chumba cha juu na kumlaza. 38 Kwa vile Lida ilikuwa karibu na Yafa, na wanafunzi walisikia kwamba Petro alikuwa huko, waliwatuma watu wawili kwake, wakimsihi, "Njoo kwetu bila kuchelewa". 39 Petro akaamka na akaondoka pamoja nao. Alipofika, walimleta katika chumba cha juu. Na wajane wote walisimama karibu naye wakilia, wakimwonyesha kanzu na nguo ambazo Dorcas aliwashonea wakati yeye alikuwa pamoja nao. 40 Petro akawatoa wote nje ya chumba, akapiga magoti akaomba, kisha akaugekia mwili, akasema, "Tabitha, amka". Basi akafungua macho yake na alipomwona Petro akaketi. 41 Kisha Petro akampa mkono wake akamwinua, na alipowaita watu watakatifu wa mungu na wajane, alimwasilisha kwao akiwa hai. 42 Jambo hili likajulikana kote Yafa yote, na watu wengi wakamwamini Bwana. 43 Ilitokea hivyo Petro akakaa siku nyingi huko Yafa na mtu mmja jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi.