Sura 3

1 Sasa Peter na Yohana walikuwa wanaelekea katika hekalu wakati wa maombi, saa tisa. 2 Sasa mtu fulani kiwete tangu kuzaliwa, alikuwa akibebwa kila siku na alikuwa akilazwa katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aweze kuomba sadaka kutoka kwa watu waliokuwa wakielekea hekaluni. 3 Alipowaona Petro na Yohana wanakaribia kuingia hekaluni, aliomba sadaka. 4 Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, alisema,"tutazame sisi." 5 Mtu yule kiwete akawatazama, akitazamia kupokea kitu fulani kutoka kwao. 6 Lakini Petro akasema, "fedha na dhahabu mimi sina, lakini kile nilichonacho nitakupa. Katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth, tembea." 7 Akimchukua kwa mkono wake wa kulia, Petro akamwinua juu na, mara moja miguu yake na vifundo vya mifupa yake vikapata nguvu. 8 Akiruka juu, mtu kiwete alisimama na akaanza kutembea; na akaingia pamoja na Petro na Yohana hekaluni, akitembea, akirukaruka, na kumsifu Mungu. 9 Watu wote walimwona akitembea na akimsifu Mungu. 10 Wakatambua kwamba alikuwa ni yule mtu ambaye alikuwa akiomba sadaka kwenye mlango mzuri wa hekalu; walijawa na mshangao na kustaajabu kwa sababu ya kile kilichotokea kwake. 11 AKiwa amewashikilia Petro na Yohana, watu wote kwa pamoja wakakimbilia kwenye ukumbi uitwao wa Sulemani, wakishangaa sana. 12 Petro alipoliona hili, yeye akawajibu watu, "Enyi watu wa Israel, kwa nini mnashangaa? Kwa nini mnayaelekeza macho yenu kwetu, kana kwamba tumemfanya huyu atembee kwa nguvu zetu wenyewe au uchaji wetu?." 13 Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Yakobo, Mungu wa Baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu. Huyu ndiye ambaye ninyi mlimkabidhi na kumkataa mbele ya uso wa Pilato, japo yeye alikuwa ameamua kumwachia huru. 14 Mlimkataa Mtakatifu na Mwenye Haki, na badala yake mkataka muuaji aachwe huru. 15 Ninyi mlimuua Mwanzilishi wa uzima, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu-- sisi ni mashahidi wa hili. 16 Kwa msingi imani katika jina lake, jina lake limemfanya mtu huyu, ambaye mnamwona na kumjua, alifanywa kuwa na nguvu. Imani ambayo nikupitia kwa Yesu imempa yeye afya hii kamilifu, mbele ya uwepowenu ninyi nyote. 17 Sasa, Ndugu, najua kwamba mlitenda katika ujinga, ndivyo pia walivyofanya watawala wenu. 18 Lakini mambo ambayo Mungu aliwaambia mapema kupitia vinywa vya manabii wote, kwamba huyu Kristo atateseka, sasa ameyatimiza. 19 Kwa hiyo, tubuni na kugeuka, ili kwamba dhambi zenu ziweze kuondolewa kabisa, kusudi zije nyakati za kuburudika kutokana na uwepo wa Bwana; 20 kusudi aweze kumtuma Kristo ambaye ameshateuliwa kwa ajili yenu, Yesu. 21 Yeye ndiye ambaye lazima mbingu zimpokee mpaka wakati wa kurejeshwa kwa vitu vyote, ambavyo Mungu alizungumzia kutoka zamani za kale kupitia kwa vinywa vya manabii watakatifu. 22 Hakika Musa alisema, 'Bwana Mungu atainua nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Lazima kusikiliza kila kitu ambacho atawaambia ninyi. 23 Itatokea kwamba kila mtu ambaye hasikilizi kwa nabii huyo ataangamizwa kabisa atoke kati ya watu.' 24 Ndiyo, na manabii wote tokea Samweli na wale waliofuata baada yake, walizungumza na kutangaza siku hizi. 25 Ninyi ni wana wa manabii na wa agano ambalo Mungu alilifanya pamoja na mababu, kama alivyosema kwa Abrahamu, 'Katika mbegu yako familia zote za dunia zitabarikiwa.' 26 Baada ya Mungu kumwinua mtumishi wake, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki ninyi kwa kugeuka kutoka katika uovu wenu."