Sura 15

1 Baadhi ya watu fulani walishuka kutoka Uyahudi na kuwafundisha ndugu, wakisema, "msipotahiriwa kulingana na desturi ya Musa, hamwezi kuokolewa." 2 Hili lilileta Paulo na Barnaba kwa mzozo na mjadala mkali pamoja nao. Hivyo Paulo na Barnaba, pamoja na baadhi ya wengine miongoni mwao, waliteuliwa kwenda Yerusalemu kukutana na mitume na wazee kuhusu swali hili. 3 Kwa hiyo, kwa kutumwa kwao na kanisa, walipitia Foinike na Samaria wakitangaza kugeuzwa nia kwa watu wa Mataifa. Walileta furaha kuu kwa ndugu wote, 4 Walipokuja Yerusalem, walikaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, na waliwasilisha taarifa ya mambo yote ambayo Mungu amefanya pamoja nao. 5 Lakini watu fulani walioamini, waliokuwa katika kundi la Mafarisayo, walisimama nakusema, "ni muhimu kuwatahiri na kuwaamuru waishike sheria ya Musa." 6 Hivyo mitume na wazee walikusanyika pamoja kuzingatia jambo hili. 7 Baada ya majadiliano mengi, Petro alisimama na kusema kwao, "Ndugu mnajua kwamba zamani Mungualichangua kati yenu, hiyo kwa mdomo wangu Mataifa wasikie neno la injili, na kuamini. 8 Mungu, anayefahamu mioyo, ameshuhudia kwao, kwa kuwapa Roho mtakatifu, kama alivyofanya kwetu; 9 na hakufanya ubaguzi kati yetu na wao, akiifanya mioyo yao safi kwa imani. 10 Kwa hiyo, kwa nini mnamjaribu Mungu kwamba muweke nira juu ya shingo za wanafunzi ambayo hata baba zetu wala sisi hatukuweza kustahimili? 11 Lakini twaamini kwamba tutaokolewa kwa neema ya Bwana Yesu, kama wao." 12 Kusanyiko lote lilinyamaza walipokua wakimsikiliza Barnaba na Paulo walipokuwa wakitoa taarifa ya ishara na maajabu ambayo Mungu alifanya pamoja nao kati ya watu wa Mataifa. 13 Walipoacha kuongea, Yakobo alijibu akisema, "Ndugu nisikilizeni. 14 Simoni ameelezea jinsi kwanza Mungu kwa neema aliwasaidia Mataifa ili kwamba ajipatie kutoka kwao watu kwa ajili ya jina lake. 15 Maneno ya manabii yanakubaliana na hili kama lilivyoandikwa. 16 'Baada ya mambo haya nitarudi na kuijenga tena hema ya Daudi, iliyoanguka chini; nitainua na kuhuisha uhararibifu wake, 17 ili kwamba watu waliobaki wamtafute Bwana, pamoja na watu wa Mataifa walioitwa kwa jina langu.' 18 Hivi ndivyo asemavyo Bwana aliyefanya mambo haya yajulikanayo tangu enzi za zamani. 19 Hivyo basi, nimeamua, kwamba tusiwapatie shida watu wa Mataifa wamgeukiao Mungu; 20 lakini tutawaandikia kwamba wajiepushe mbali na uharibifu wa sanamu, tamaa za uasherati, na vilivyonyongwa, na damu. 21 Kutoka vizazi vya wazee kuna watu katika kila mji wahubirio na kumsoma Musa katika masinagogi kila Sabato." 22 Kwa hiyo ikaonekana kuwa imewapendeza mitume na wazee, pamoja na kanisa lote, kumchagua Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa viongozi wa kanisa, na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. 23 Waliandika hivi kwa mikono yao, "Kutoka kwa mitume, wazee na ndugu, kwa ndugu wa Mataifa walioko Antiokia, Shamu na Kilikia, salamu! 24 Kwa sababu tumesikia kwamba watu fulani ambao hatukuwapatia amri hiyo, walitoka kwetu na wamewataabisha kwa mafundisho yaletayo shida nafsini mwenu. 25 Kwa hiyo imeonekana vyema kwetu, ambao wametujia kwa nia moja, kuchagua watu na kuwatuma kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo, 26 watu walio hatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana Yesu Kristo. 27 Kwa hiyo tumemtuma Yuda na Sila ambao watawaambia mambo yayo hayo kwa maneno yao. 28 Kwa kuwa ilionekana vyema kwa Roho Mtakatifu na kwetu, kutoweka juu yenu mzigo mkubwa kuliko mambo haya yaliyo ya lazima: 29 kwamba mjizuie kutoka kwenye vitu vitolewavyo sadaka kwa sanamu, damu, vitu vya kunyongwa, na uasherati. Kama mtajiepusha na vitu hivi, mtafanya vyema kwenu. Kwa herini." 30 Hivyo basi, walivyotawanyishwa, waliteremkia Antiokia; baada ya kukusanya kusanyiko pamoja, waliwasilisha barua. 31 Walipokua wameisoma, walifurahi kwa sababu ya kutiwa moyo. 32 Yuda na Sila, na manabii, waliwatia moyo ndugu kwa maneno mengi na kuwatia nguvu. 33 Baada ya kukaa muda fulani huko, walisindikizwa mbali na kuagwa kwa amani kutoka kwa ndugu kwa wale waliowatuma. 34 [ Lakini ilionekana vyema Sila kubaki huko ] 35 Lakini Paulo na wengine walikaa Antiokia pamoja na wengine wengi, ambapo walifundisha na kuhubiri neno la Bwana. 36 Baada ya siku kadhaa Paulo alisema kwa Barnaba, "Na turudi sasa na kuwatembelea ndugu katika kila mji tulipohubiri neno la Bwana, na kuwaona walivyo. 37 Barnaba alihitaji pia kumchukua pamoja na Yohana aliyeitwa Marko. 38 Lakini Paulo alifikiri haikuwa vizuri kumchukua Marko, aliyewaacha huko Pamfilia na hakuendelea nao katika kazi. 39 Kisha hapo kukatokea mabishano makubwa kwa hiyo walitengana, na Barnaba alimchukua Marko na kusafiri kwa meli mpaka Kipro, 40 Lakini Paulo alimchagua Sila na kuondoka, baada ya kukabidhiwa na ndugu katika neema ya Bwana. 41 Na alienda kupitia Shamu na Kilikia, akiimarisha makanisa.