Sura 14

1 Ikatokea ndani ya Ikonio kwamba Paulo na Barnaba waliingia pamoja ndani ya sinagogi la Wayahudi nakuongea namna ambayo kundi kubwa la watu Wayahudi na Wayunani waliamini. 2 Lakini wayahudi wasiotii waliwachochea fikira za watu wa mataifa na kuwatia uchungu dhidi ya ndugu zao. 3 Kwa hiyo walikaa huko kwa muda mrefu, wakiongea kwa ujasiri kwa nguvu ya Bwana, huku akitoa ushahidi kuhusu ujumbe wa neema yake. Alifanya haya kwa kuwapa ishara na majaabu vifanywe kwa mikono ya Paulo na Barnaba. 4 Lakini watu wa mji waligawanyika: wengine upande wa Wayahudi, wengine pamoja na mitume. 5 Kwa pamoja watu wa mataifa na Wayahudi (pamoja na viongozi wao) walifanya jaribio la kuwatenda vibaya na kuwaponda kwa mawe Paulo na Barnaba, 6 Lakini mara tu baada ya kulitambua hilo, walikimbilia katika miji ya Likaonia, Listra na Derbe, na maeneo yanayozunguka pale, 7 na huko waliendelea kuihubiri injili. 8 Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja aliyekaa, hakuwa na nguvu miguuni mwake, kilema kutoka tumboni mwa mama yake, ambaye hajawahi kutembea. 9 Mtu huyu alimsikia Paulo akiongea. Paulo alimkazia macho na akaona kwamba alikuwa na imani ya kuponywa. 10 Hivyo alimwambia kwa sauti kubwa, "Simama kwa miguu yako." Na yule mtu aliruka juu na kuanza kutembea. 11 Umati ulipoona alichokifanya Paulo, waliinua sauti zao, wakisema katika lahaja ya Kilikaonio, "miungu imekuwa kama wanadamu na imeshuka kwetu." 12 Walimwita Barnaba "Zeu," na Paulo "Herme" kwa sababu alikuwa msemaji mkuu. 13 Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje ya mji, alileta fahari la ng'ombe na mtungo wa maua mpaka kwenye lango la mji, yeye na umati walitaka kutoa sadaka. 14 Lakini mitume, Barnaba na Paulo, walipolisikia hili, walirarua mavazi yao na kwa haraka walikwenda nje kwenye umati, wakilia 15 na kusema, "Enyi watu, kwanini mnafanya mambo haya? Na sisi pia ni binadamu wenye asili sawa na yenu. Tunawaletea habari njema, kwamba inawapasa kugeuka kutoka kwenye vitu hivi visivyofaa na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu, dunia na bahari na kila kitu kilichomo. 16 Katika nyakati zilizopita, aliwaruhusu mataifa kutembea katika njia zao wenyewe. 17 Lakini bado, hakuondoka pasipo shahidi, katika hilo alifanya vizuri na akawapatia mvua kutoka mbinguni na nyakati za mazao, akiwajaza mioyo yenu kwa vyakula na furaha" 18 Hata kwa maneno haya, Paulo na Barnaba kwa shida waliuzuia umati kuwatolea sadaka. 19 Lakini baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio walikuja kuushawishi umati. Wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mji, wakidhani alikuwa amekufa. 20 Hata hivyo wanafunzi walikuwa wamesimama karibu naye, aliamka, na akaingia mjini. Siku inayofuata, alienda Derbe na Barnaba. 21 Baada ya kufundisha injili katika mji ule na kuwafanya wanafunzi wengi, walirudi Listra, hadi Ikonio, na hadi Antiokia. 22 Waliendelea kuziimarisha roho za wanafunzi na kuwatia moyo kudumu katika imani, wakasema, "Lazima tuingie katika ufalme wa Mungu kwa kupitia dhiki nyingi." 23 Walipo wateua kwa ajili yao wazee wa kila kanisa, na wakiwa wameomba na kufunga, waliwakabidhi kwa Bwana, ambaye wao walimwamini. 24 Kisha walipita katika Pisidia, walifika Pamfilia. 25 Wakati walipoongea maneno katika Perga, waliteremka kwenda Atalia. 26 Kutoka huko walipanda meli hadi Antiokia ambako walikuwa wamejitoa kwa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameikamilisha. 27 Walipofika huko Antiokia, na kulikusanya kanisa pamoja, wakatoa taarifa ya mambo ambayo Mungu amefanya kwao, na jinsi alivyowafungulia mlango wa imani kwa watu wa Mataifa. 28 Walikaa kwa muda mrefu na wanafunzi.