Sura 12

1 Wakati huo mfalme Herode aliwatia mikononi baadhi ya watu wa kanisa ili apate kuwatesa. 2 Akamwuua Yakobo nduguye Yohana kwa upanga. 3 Baada yake kuona kwamba hili liliwapendeza Wayahudi, alienda kumkamata Petro pia. Hiyo ilikuwa katika siku za mikate isiyotiwa chachu. 4 Alipomkamata, akamweka gerezani na akamweka chini ya vikosi vinne vya askari ili kumlinda; alikuwa akitarajia kumpeleka kwa watu baada ya Pasaka. 5 Petro akawekwa gerezani, lakini maombi yalifanywa kwa bidii na kanisa kwa ajili yake kwa Mungu. 6 Usiku kabla Herode hajaenda kumtoa kwa ajili ya kesi, Petro alikuwa amelala katikati ya maaskari wawili, akiwa amefungwa na minyororo miwili, huku walinzi wakiwa mbele ya mlango walikuwa wakilinda gereza. 7 Tazama, malaika wa Bwana ghafla akamtokea na nuru ikang'aa ndani ya gereza. Akampiga Petro ubavuni na kumwamsha akisema, "Amka haraka,"na minyororo yake ikaanguka kutoka mikononi mwake. 8 Malaika akamwambia, "Vaa nguo zako na vaa viatu vyako." Petro akafanya hivyo. Malaika akamwambia, "Vaa vazi lako la nje na unifuate." 9 Hivyo Petro akamfuata Malaika na akatoka nje. Hakujua kama kwamba kilichofanywa na malaika kilikuwa halisi. Alidhani anaona maono. 10 Baada ya kuwa wamepita lindo la kwanza na la pili, wakafika kwenye lango la chuma la kuingilia kwenda mjini; likafunguka lenyewe kwa ajili yao. Wakatoka nje na wakashuka kwenye mtaa, mara Malaika akamwacha. 11 Petro alipojitambua, akasema, "Sasa nimeamini kwa kweli Bwana alimtuma Malaika wake ili kunitoa katika mkono wa Herode, na kwa matarajio ya watu wote wa uyahudi." 12 Baada ya kujua haya, akaja kwenye nyumba ya Mariamu mama yake Yohana ambaye pia huitwa Marko; ambapo Wakristo wengi walikuwa wamekusanyika wakiomba. 13 Alipobisha kwenye mlango wa lango, mtumishi mmoja msichana anayeitwa Roda akaja kufungua. 14 Alipotambua ni sauti ya Petro, kwa furaha akashindwa kuufungua mlango; badala yake, akakimbia ndani ya chumba; na kuwajulisha kuwa Petro amesimama mbele ya mlango. 15 Hivyo, Wakamwambia, "Wewe ni mwendawazimu" lakini alisisitiza kuwa ni kweli ni yeye. Wakasema "Huyo ni malaika wake." 17 16 Lakini Petro aliendelea kubisha, na walipofungua mlango, wakamwona na wakashangaa sana. Petro akawaashiria kwa mkono wake ili wanyamaze na akawaambia jinsi Bwana alivyomtoa kutoka Gerezani. Akasema, v "Wajulishe haya mambo Yakobo na ndugu." Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine. 18 Sasa ilipokuwa mchana, hakukuwa na usumbufu mdogo kati ya askari, kuhusiana na kilichotokea kwa Petro. 19 Baada ya Herode kumtafuta bila kuweza kumpata akawauliza walinzi na akaamuru wauawe. 20 Sasa Herode alikasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Walimwendea kwa nia moja, na wakawa na urafiki na Blasto msaidizi wa mfalme, ili awasaidie, wakaomba amani, kwa sababu nchi yao ilipokea chakula kutoka katika nchi ya mfalme. 21 Siku iliyokusudiwa Herode alivaa mavazi la kifalme na kukaa kwenye kiti chake cha kifalme; na akawahutubia. 22 Watu wakapiga kelele, "Hii ni sauti ya muungu wala si sauti ya mwanadamu!" 23 Mara malaika akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango na akafa 24 Lakini neno la Mungu likaongezeka na kusambaa. 25 Basi Barnaba na Sauli walipokamilisha huduma yao wakarudi kutoka Yerusalemu, wakamchukua pamoja nao Yohana aitwaye Marko.