Genesis 34

Genesis 34:1

Basi

Hapa neno hili linatumika kuweka alama kwa sehemu mpya ya simulizi.

Dina

Hili ni jina la binti wa Lea.

Mhivi

Hili li jina la kundi la watu.

mwana wa mfalme wa nchi

Hii ina maana ya Hamori na sio Shekemu. Pia "mwana wa mfalme" hapa haimaanishi mtoto wa mfalme. Ina maana ya Hamori alikuwa kiongozi wa watu katika eneo hilo.

akamkamata kwa nguvu na kulala naye

Shekemu alimbaka Dina.

Akavutiwa na Dina

"Alivutiwa sana na yeye". Hii inazungumzia juu ya Shekemu kumpenda Dina na kutaka kuwa naye kana kwamba kuna jambo lililokuwa likimlazimisha kwenda kwa Dina. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Alitaka sana kuwa na Dina"

kuongea naye kwa upole

Hii ina maana aliongea naye kwa upole kumuaminisha ya kwamba alimpenda na kwamba alimtaka pia ampende yeye.

Genesis 34:4

Basi Yakobo

"basi" inatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Yakobo.

Yakobo akasikia kwamba alikuwa

Neno "alikuwa" lina maana ya Shekemu

alikuwa amemchafua

Hii ina maana ya kwamba Shekemu alivunja sana heshima na kumuabisha Dina kwa kumlazimisha alale naye.

akawangoja

Hii ni namna ya kusema ya kwamba Yakobo hakusema au kufanya jambo kuhusu suala hili.

Genesis 34:6

Hamori ... akaenda kuongea na Yakobo

"Hamori ... akaenda kuongea na Yakobo"

Watu hawa walichukizwa

"Wanamume walikasirika"

Walikasirika sana ... halikupasa kutendeka

Hii inaweza kuwekwa kama nukuu ya moja kwa moja iliyozungumzwa na wana wa Yakobo.

amemwaibisha Israeli

Hapa neno la "Israeli" lina maana ya kila mtu katika familia ya Yakobo. Israeli kama kundi la watu liliabishwa."ameabisha familia ya Israeli" au "ameleta aibu juu ya watu wa Israeli"

kumlazimisha binti wa Yakobo

"kumvamia binti wa Yakobo"

kwa maana jambo kama hilo halikupasa kutendeka

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwa maana hakupaswa kufanya jambo baya kama hilo"

Genesis 34:8

Hamori akaongea nao

"Hamori alizungumza na Yakobo na wanawe"

anampenda binti yenu

Hapa neno "anampenda" lina maana ya upendo wa kimahaba kati ya mwanamume na mwanamke. "anampenda na anataka kumuoa"

mpeni kuwa mke wake

Katika baadhi ya tamaduni, wazazi huamua watoto wao wataolewa na nani"

Mwoane nasi

Kuoana ni kuoa mtu wa jamii, kabila, au dini tofauti. "Ruhusu ndoa kati ya watu wako na wetu"

nchi itakuwa wazi kwa ajili yenu

"nchi itakuwa wazi kwako"

Genesis 34:11

Shekemu akamwambia baba yake

"Shekemu alimwambia baba yake Dina Yakobo"

Na nione kibari machoni penu, na chochote mtakachoniambia nitatoa

Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo ya mtu. "Kama utanipa kibali, basi nitakupa chochote utakachokiomba"

mahari

Katika baadhi ya tamaduni, ni kawaida kwa mwanamume kutoa fedha, mali, ng'ombe, na zawadi zingine kwa familia ya mwanamke katika kipindi cha ndoa.

Wana wa Yakobo wakamjibu Shekemu na Hamori baba yake kwa hila

Nomino inayojitegemea ya "hila" inaweza kuwekwa kama kitenzi cha "kudanganya". "Lakini wana wa Yakobo walimdanganya Shekemu na Hamori walipowajibu"

Shekemu alikuwa amemnajisi Dina

Hii ina maana ya kwamba Shekemu aliwavunjia heshima sana na kumuabisha Dina kwa kumlazimisha kulala naye.

Genesis 34:14

Wakawambia

"wana wa Yakobo waliwaambia Shekemu na Hamori"

Hatuwezi kufanya jambo hili, kumpa dada yetu

"Hatuwezi kukubali kumtoa Dina katika ndoa"

kwani hiyo ni aibu kwetu

"kwa maana hiyo itasababisha aibu kwetu". Hapa "kwetu" ina maana ya wana wa Yakobo na watu wote wa Israeli.

tutakapowapa binti zetu ... tutachukua binti zenu kwetu sisi wenyewe

Hii ina maana wataruhusu mtu kutoka familia ya Yakobo kuoa mtu anayeishi katika nchi ya Hamori.

Genesis 34:18

Maneno yao yakawafurahisha Hamori na Shekemu mwanaye

Hapa "maneno" ina maana ya kile kilichosemwa. "Hamori na mwanawe Shekemu walikubali na kile ambacho wana wa Yakobo walisema"

kufanya walichokisema

"kufanyiwa tohara"

binti wa Yakobo

"binti wa Yakobo Dina"

kwa sababu alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana katika nyumba ya babaye

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba Shekemu alijua wanamume wengine wangekubali kufanyiwa tohara kwa sababu walimheshimu sana. "Shekemu alijua wanamume wote katika nyumba ya baba yake watakubaliana naye kwa sababu alikuwa akiheshimiwa zaidi kati yao"

Genesis 34:20

lango la mji wao

Ilikuwa kawaida kwa viongozi kukutana katika lango la mji kufanya maamuzi rasmi.

Watu hawa

"Yakobo, wanawe, na watu wa Israeli"

wana amani nasi

Hapa "nasi" inajumlisha Hamori, mwanawe na watu wote waliozungumza nao langoni mwa mji.

waishi katika nchi na kufanya biashara humo

"waruhusu waishi na kufanya biashara katika nchi"

maana, kweli, nchi ni kubwa ya kuwatosha

Shekemu anatumia neno "kweli" kuongeza msisitizo kwa kauli yake. "kwa sababu, hakika, nchi ni kubwa ya kutosha kwa ajili yao" au "kwa sababu, haswa, kuna nchi ya kutosha kwa ajili yao"

tuwachukue binti zao ... tuwape binti zetu.

Hii ina maana ya ndoa kati ya wanawake wa kundi moja na wanamume wa kundi lingine.

Genesis 34:22

Taarifa ya Jumla:

Hamori na Shekemu mwanawe wanaendelea kuzungumza na viongozi wa mji.

Kwa sharti hili pekee watu hawa wanakubali kuishi nasi na kuwa wamoja: ikiwa kila mwanamme miongoni mwetu atatahiriwa, kama wao.

"Kwa sharti hili pekee iwapo kila mwanamume kati yetu atafanyiwa tohara, kama wanamume wa Israeli walivyotahiriwa, ndipo watakubali kusihi miongoni mwetu na kujiunga nasi kama kundi moja"

Je wanyama wao na vitu vyao - wanyama wao wote kuwa wetu?

Shekemu anatumia swali kusisitiza ya kwamba mifugo wa Yakobo na mali zitakuwa za watu wa Shekemu. Hii inaweza kutafsiriwa kama kauli. "Wanyama wao wote na mali zitakuwa zetu"

Genesis 34:24

Kila mwanamme alifanyiwa tohara

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kwa hiyo Hamori na Shekemu wakawa na mtu wa kufanya tohara kwa wanamume wote"

Katika siku ya tatu

"tatu" ni nambari za mpango kwa namba tatu. Inaweza kuwekwa bila nambari za mpango. "Baada ya siku mbili"

walipokuwa katika maumivu

"wakati wanamume wa mji walipokuwa bado na maumivu"

wakachukua kila mmoja upanga wake

"wakachukua panga zao"

kuushambulia mji

Hapa "mji" una maana ya watu. "waliwashambulia watu wa mji"

ulinzi wake, nao wakauwa wanamume wote

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "ulinzi. Simoni na Lawi waliwaua wanamume wote wa mji ule"

kwa makali ya upanga

Hapa "makali" yana maana ya ubapa wa upanga. "kwa ubapa wa panga zao" au "kwa upanga wao"

Genesis 34:27

maiti

"maiti ya Hamori, Shekemu na wanamume wao"

pora mji

"waliiba kila kitu chenye thamani katika mji ule"

kwa sababu watu wale walikuwa wamemnajisi dada yao

Shekemu pekee alimnajisi Dina, lakini wana wa Yakobo walichukulia familia yote ya Shekemu na kila mtu katika mji kuhusika na tendo hili.

walikuwa wamemnajisi

Hii ina maana ya kwamba Shekemu alimvunjia heshima na kumuabisha sana Dina kwa kumlazimisha kulala naye.

Wakachukua makundi yao

"wana wa Yakobo wakachukua mifugo ya watu wale"

utajiri wao wote

"mali zao zote na fedha"

Watoto na wake zao wote, wakawachukua

"Waliwakamata watoto wao na wake zao wote"

Genesis 34:30

Mmeleta shida juu yangu

Kusababisha mtu kupitia shida inazungumziwa kana kwamba shida ilikuwa kitu kinacholetwa na kuwekwa juu ya mtu. "mmesababisha shida kubwa kwangu"

kunifanya ninuke kwa wenyeji wa nchi

Kusababisha watu katika maeneo yanayozunguka kumchukia Yakobo inazungumziwa kana kwamba wana wa Yakobo walimfanya anuke vibaya kihalisia. Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Mmenifanya nionekane kwa kinyaa kwa watu wanaoishi katika nchi"

Mimi nina watu wachache ... dhidi yangu na kunishambulia, kisha nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu.

Hapa maneno "Mimi" na "yangu" yana maana ya nyumba yote ya Yakobo. Yakobo anasema "Mimi" au "yangu" kwa maana yeye ni kiongozi. "Nyumba yangu ni ndogo ... dhidi yetu na kutuvamia, kisha watatuangamiza sisi wote"

watajikusanya pamoja dhidi yangu na kunishambulia

"wataunda jeshi na kunishambulia" au "wataunda jeshi na kutushambulia"

kisha nitaangamizwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wataniangamiza" au "watatuangamiza"

Je Shekemu alipaswa kumtendea dada yetu kama kahaba?

Simoni na Lawi wanatumia swali kusisitiza ya kwamba Shekemu alifanya kosa na alistahili kufa. "Shekemu hakupaswa kumtenda dada yetu kama kahaba!"