Genesis 27

Genesis 27:1

macho yake kuwa mazito

Hii inazungumzia kuhusu kuwa karibu na kupofuka kana kwamba macho yalikuwa taa na mwanga ulikuwa ukitoweka. "alikaribia kupofuka" au "kidogo apofuke"

akamwambia

"Na Esau akajibu"

Mimi hapa

"Nipo hapa" au "Ninasikiliza'

Akamwambia

"Kisha Isaka akasema"

Tazama hapa

Msemo wa "tazama hapa" unaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata. "Sikiliza kwa makini"

Sijui siku ya kufa kwangu

Inasemekana Isaka anajua atakufa hivi karibuni. "Naweza kufa siku yoyote toka sasa"

kufa

Hii ina maana ya kifo cha mwili.

Genesis 27:3

Taarifa ya Jumla

Isaka anaendelea kutoa maelekezo kwa mwanae mkubwa Esau.

silaha zako

"vifaa vyako vya kuwindia"

podo lako

Podo ni kasha la kushikilia mishale. "podo lako la mishale"

ukaniwindie mnyama

"winda mnyama pori kwa ajili yangu"

Uniandalie chakula kitamu, aina ile niipendayo

Neno "kitamu" lina maana ya kitu chenye ladha nzuri sana. "Nipikie nyama tamu ninayoipenda"

kukubariki

Kipindi cha Biblie, baba mara nyingi hutamka baraka juu ya watoto wake.

Genesis 27:5

Basi

Neno "basi" linaonyesha badiliko la msisitizo kwa Rebeka na Yakobo.

Rebeka akasikia Isaka alipoongea na Esau mwanawe

"Rebeka alimsikia Isaka akizungumza na mwanawe Esau"

Esau akaenda ... kuja nayo

Neno "kwa hiyo" inaweza kuongezwa kuonyesha ya kwamba Rebeka anazungumza na Yakobo kwa sababu ya kile alichosikia, na anaongea naye wakati Esau ameondoka. "Kwa hiyo Esau alipokuwa ameondoka ...kuja nayo"

na Esau mwanawe ... na Yakobo mwanawe

Esau na Yakobo walikuwa wote wawili watoto wa Isaka na Rebeka. Wanaitwa "mtoto wake" na "mwanawe" kusisitiza ya kwamba mzazi mmoja alimpendelea mtoto mmoja juu ya mtoto mwingine.

Tazama

Msemo "tazama hapa" unaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata. "Sikiliza kwa makini"

Akasema, 'Niletee mnyama na unitengenezee chakula kitamu, ili nikile na kukubariki mbele za Yahwe kabla ya kufa kwangu

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kusemwa katika hali isiyo moja kwa moja. Alimwambia Esau "kuwinda mnyama pori, na kumtengenezea nyama tamu anayoipenda". Kisha kabla hajafa, Isaka atambariki Esau mbele ya Yahwe.

'Niletee mnyama

"Niletee mnyama pori utakayemwinda na kumuua"

unitengenezee chakula kitamu

"nipikie nyama tamu ninayoipenda"

kukubariki mbele za Yahwe

"kukubariki mbele ya Yahwe"

kabla ya kufa kwangu

"kabla sijafa"

Genesis 27:8

Taarifaya Jumla

Rebeka anaendelea kuzungumza kwa mtoto wake mdogo Yakobo.

sasa

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

usikilize sauti yangu kama ninavyokuagiza

Rebeka alisema "sauti yangu" kumaanisha kile alichokuwa akisema. "unitii na ufanye kile nachokuambia"

nitaandaa chakula kitamu kutokana nao kwa ajili ya baba yako, kwa namna aipendayo

Neno "kitamu" ina maana ya kitu chenye ladha nzuri sana.

Utakipeleka kwa baba yako

"Kisha peleka kwa baba yako"

ili kwamba akile, na kukubariki

"na atakapokila, atakubariki"

kukubariki

Neno "kubariki" lina maana ya baraka maalumu ambayo baba hutamka kwa watoto wake.

kabla hajafa

"kabla hajafa"

Genesis 27:11

mimi ni mtu lain

"Mimi ni mwanamume mwenye ngozi laini" au "Mimi sina manyoya"

nami nitaonekana kama mdanganyifu kwake

"na atafikiri ya kwamba mimi ni muongo" au "atajua ya kwamba ninamdanganya"

nitajiletea laana badala ya baraka

Kulaaniwa au kubarikiwa inazungumziwa kana kwamba laana na baraka ni vitu vinavyowekwa juu ya mtu. "Kisha kwa sababu ya hili, atanilaani na hatanibariki"

Genesis 27:13

Mwanangu, acha laana yoyote iwe juu yangu

"acha laana yako na iwe juu yangu, mwanangu". Kulaaniwa inazungumziwa kana kwamba laana ni kitu kinachowekwa juu ya mtu. "acha baba yako anilaani badala yako, mwanangu"

sikiliza sauti yangu

Rebeka akasema "sauti yangu" kumaanisha kile alichokuwa akizungumza. "utii kile ninachokuambia" au "unitii"

uniletee

"niletee mwanambuzi mchanga"

akaandaa chakula kitamu, kama alichokipenda baba yake

Neno la "kitamu" lina maana ya kitu chenye ladha nzuri sana.

Genesis 27:15

Akamvalisha ngozi ya mwanambuzi katika mikono yake

Ngozi ya mbuzi ilikuwa bado ina manyoya juu yao.

Akaweka katika mikono ya Yakobo kile chakula kitamu na mkate aliokuwa ameuandaa.

"Alimpatia mtoto wake Yakobo chakula kitamy na mkate aliokuwa ameandaa"

Genesis 27:18

akasema

"Na baba yake akajibu" au "Isaka akajibu"

Mimi hapa

"ndio, nasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

nimefanya kama ulivyoniagiza

"Nimefanya kile ulichonimbia kufanya"

sehemu ya mawindo yangu

Neno "windo" lina maana ya wanyama pori ambayo mtu huwinda na kuua.

Genesis 27:20

akamwambia

"Yakobo alijibu"

ameniletea

Hii ni lahaja yenye maana ya kwamba Mungu alisababisha itokee. "alinisaidia kufanikiwa nilipokuwa nawinda"

kama kweli wewe ni mwanangu Esau au hapana

"kama kweli wewe ni mwanangu Esau"

Genesis 27:22

Yakobo akamkaribia Isaka baba yake

"Yakobo alimkaribia Isaka baba yake"

Sauti ni sauti ya Yakobo

Isaka anafananisha sauti ya Yakobo na Yakobo mwenyewe. "Unasikika kama Yakobo"

lakini mikono ni mkikono ya Esau

Isaka analinganisha mikono ya Esau kwa Esau mwenyewe. "lakini mikono yako inaonekana kama mikono ya Esau"

Genesis 27:24

Akasema

Isaka anauliza swali hili kabla hajambariki mwanawe. "Lakini kwanza Isaka alimuuliza Isaka"

nile mawindo yako

Neno "windo" lina maana ya mnyama pori ambaye watu huwinda na kuua.

akanywa

"na Isaka akainywa"

Genesis 27:26

akanusa harufu ya nguo zake na kumbariki

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba nguo zilinuka kama nguo za Esau. "alinusa nguo zake na zilinuka kama nguo za Esau, kwa hiyo Isaka akambariki"

naye akanusa

"na Isaka akanusa"

harufu

"marashi"

na kumbariki

"na kisha akambariki". Hii ina maana ya baraka maalumu ambayo baba hutamka kwa watoto wake.

Tazama, harufu ya mwanangu

Neno "tazama" linatumika kama msemo wa mkazo kumaanisha "ni kweli". Hakika, harufu ya mwanangu"

alilolibariki Yahwe

Hapa neno "alilolibariki" lina maana ya Yahwe alisababisha mambo mazuri kutokea kwenye shamba na ikawa na matunda. "ambayo Yahwe amesababisha kuzaa sana"

Genesis 27:28

Taarifa ya Jumla

Hii ni baraka ya Isaka. Alifikiri alikuwa akizungumza na Esau, lakini alikuwa akizungumza na Yakobo.

akupe

Hapa "akupe" ni katika hali ya umoja na ina maana ya Yakobo. Lakini baraka ingeweza kuhusika kwa vizazi vya Yakobo.

umande wa mbinguni

"umande" ni matone ya maji yanayounda juu ya mimea wakati wa usiku. Hii inaweza kuwekwa wazi. "umande wa usiku kutoka mbinguni kumwagilia mimea yako"

unono wa nchi

Kuwa na nchi yenye mbolea inazungumziwa kana kwamba nchi ilikuwa nene au tajiri. "udongo mzuri kwa ajili ya kuzaa mimea"

wingi wa nafaka na mvinyo mpya

Kama "nafaka" na "mvinyo" havijulikani, vinaweza kuwekwa kwa ujumla zaidi. "chakula na kinywaji kingi"

Genesis 27:29

wakutumikie ... zako

Hapa hivi viwakilishi vipo katika umoja na vina maana ya Yakobo. Lakini baraka pia inalenga vizazi vya Yakobo.

mataifa yainame

Hapa "mataifa" ina maana ya watu. "watu kutoka mataifa yote yainame"

yainame

Hii ina maana ya kuinama na kutoa heshima na taadhima ya unyenyekevu kwa mtu.

Uwe bwana juu ya ndugu zako

"Kuwa bwana juu ya ndugu zako"

ndugu zako ... wana wa mama yako

Isaka anazungumzia baraka hii moja kwa moja kwa Yakobo. Lakini, inahusika kwa vizazvi vya Yakobo ambao watatawala vizazi vya Esau na vizazi vya ndugu yeyote wa Yakobo ambaye anaweza kuwa naye.

na wana wa mama yako wainame chini yako

"na wana wa mama yako watakusujudu"

Kila anayekulaani na alaaniwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Na Mungu alaani kila mtu anayekulaani"

kila anayekubariki abarikiwe

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Na Mungu abariki kila mtu anayekubariki"

Genesis 27:30

ametoka mbele ya Isaka baba yake

"ameondoka tu katika hema la Isaka baba yake"

chakula kitamu

"nyama tamu nayoipenda"

baadhi ya mawindo ya mwanao

Hapa "ya mwanao" ilikuwa njia ya upole ya Esau kumaanisha chakula chake mwenyewe alichokiandaa.

mawindo ya mwanao

Neno "windo" lina maana ya wanyama pori ambao watu huwinda kwa ajili ya kula.

kunibariki

Hii ina maana ya baraka maalumu ambayo baba hutamka kwa watoto wake.

Genesis 27:32

akamwambia

"akamwambia Esau"

Isaka akatetemeka

"Isaka akaanza kutetemeka"

aliyewinda mawindo

Windo ina maana ya mnyama pori ambao watu huwinda na kuua.

Genesis 27:34

akalia kwa kilio kikubwa na cha uchungu sana

Uchungu wa Esau ulikuwa sawa na ladha ya kitu kichungu. "alilia kwa sauti kubwa"

amechukua baraka yako

Huu ni msemo wenye maana ya Yakobo alichukua kilichokuwa cha Esau. "Nimembariki badala yako"

Genesis 27:36

Je hakuitwa Yakobo kwa haki?

Esau anatumia swali kuweka msisitizo juu ya hasira yake kwa Yakobo. "Yakobo ni jina sahihi kwa kaka yangu!"

Yakobo

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi mafupi yanayosema: "Jina la Yakobo lina maana ya "yeye akamataye kisigino". Katika lugha ya asili jina la "Yakobo" linatamkika kama neno la "mdanganyifu"

Alichukua ... baraka

Hii inazungumzia kuhusu haki ya mzaliwa wa kwanza kana kwamba ilikuwa kitu ambacho mtu anaweza kukichukua. "Alinidanganya kumpatia mara mbili ya urithia ambayo ningepaswa kupokea kama mzawa wa kwanza!"

sasa amechukua baraka yangu

Hii inazungumzia juu ya baraka kana kwamba ilikuwa kitu ambacho mtu anaweza kuchua. "na sasa amekudanganya kumbariki yeye badala yake"

Je haukuniachia baraka

Esau anajua ya kwamba baba hawezi kumbariki na vitu vile vile alivyombariki Yakobo. Esau anauliza kama kuna kitu kinachosalia kusemwa kwake ambacho Isaka hakusema alipokuwa akimbariki Yakobo.

Je nikufanyie nini mwanangu?

Isaka anatumia swali kuweka msisitizo ya kwamba hakuna kilichobaki atakachofanya. "Hakuna kitu kingine nachoweza kufanya kwako!"

Genesis 27:38

Je hauna hata baraka moja kwa ajili yangu, babangu

Hii inaweza kuelezwa kwa njia ya chanya. "Baba yangu, je hauna baraka moja zaidi kwa ajili yangu"

Genesis 27:39

kumwambia

"akasema kwa Esau"

Tazama

Hii inaongeza msisitizo kwa kile Isaka anachosema baadae. "Sikiliza" au "Vuta nadhari kwa kile nachokwenda kukuambia"

mbali na utajiri wa nchi

Huu ni msemo unaomaanisha nchi yenye rutuba. "mbali na udongo wenye rutuba"

yako ... nawe

Katika 27:39-40 hivi viwakilishi vipo katika umoja na vina maana ya Esau, lakini kile Isaka anachosema pia kinaashiria kwa vizazi vya Esau.

umande juu angani

"umande" ni matone ya maji yanayounda juu ya mimea wakati wa usiku. Hii inaweza kuwekwa wazi. "umande wa usiku kutoka mbinguni kumwagilia mimea yako"

Kwa upanga wako utaishi

Hapa "upanga" ina maana ya vurugu. "Utaiba na kuua watu ili kupata kile unachohitaji kuishi"

utaiondoa nira yake shingoni mwako

Hii inazungumzia juu ya mtu kuwa na bwana kana kwamba utawala wa bwana juu ya mtu ulikuwa ni nira ambayo mtu anaweza kubeba. "utajifanya huru kutoka kwa utawala wake"

Genesis 27:41

Esau akajisemea moyoni

Hapa "moyoni" ina maana ya Esau mwenyewe. "Esau alijisemea mwenyewe"

Siku za maombolezo kwa ajili ya baba yangu zinakaribia

Hii ina maana ya idadi ya siku mtu huomboleza pale ambapo mmoja wa familia anapokufa.

Rebeka akaambiwa maneno ya Esau mwanawe mkubwa

Hapa "maneno" yana maana ya kile Esau alichosema. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtu alimwambia Rebeka kuhusu mpango wa Esau"

Tazama

"Sikiliza" au "Vuta nadhari"

anajifariji

"anajifanya ajisikie vizuri"

Genesis 27:43

sasa

Hii haimaanishi "katika muda huu", lakini inatumika kuvuta nadhari kwa jambo muhimu linalofuata.

kukimbilia kwa Labani

"ondoka hapa haraka na uende kwa Labani"

kwa muda

"kwa kipindi cha muda"

mpaka hasira ya ndugu yako itakapopungua

"hadi kaka yako atakapopoa"

hata hasira ya ndugu yako itakapokuondokea

Kutokuwa na hasira inazungumziwa kana kwamba hasira hugeukia upande tofauti kutoka kwa mtu. "hadi pale atakapokuwa hana hasira na wewe"

Kwa nini niwapoteze ninyi nyote katika siku moja?

Rebeka anatumia swali kuweka msisitizo juu ya mawazo yake kwa suala hili. "Sitaki kuwapoteza wote wawili katika siku moja!"

niwapoteze ninyi nyote katika siku moja

Inasemekana ya kwamba iwapo Esau atamuua Yakobo, basi watamuua Esau kama muuaji.

niwapoteze

Hii ni njia ya upole inayomaanisha wanawe kufa.

Genesis 27:46

Nimechoka na maisha

Rebeka anatia chumvi kuweka msisitizo jinsi alivyofadhaishwa kuhusu mwanamke Mhiti ambaye Esau alimuoa. "Nimefadhaishwa sana"

binti za Hethi

"hawa wanawake wahiti" au "vizazi vya Wahiti"

kama wanawake hawa, baadhi ya binti za nchi

Msemo "binti wa nchi" ina maana ya wanawake wenyeji. "kama wanawake hawa wanaoishi katika nchi hii"

maisha yatakuwa na maana gani kwangu?

Rebeka anatumia swali kuweka msisitizo jinsi atakavyofadhaishwa iwapo Yakobo atamuoa mwanamke Mhiti". "Maisha yangu yatakuwa mabaya!"