Genesis 24

Genesis 24:1

Sasa

Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya kuonyesha mapumziko kwa simulizi kuu. Hapa mwandishi anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi.

Weka mkono wako chini ya paja langu

Abrahamu alikuwa akitaka kumuliza mtumishi wake kuapa kufanya jambo. Kuweka mkono chini ya paja la Abrahamu ingeonyesha ya kwamba hakika angefanya kile alichotaka kuapa kukifanya.

nitakufanya uape

Hii inaweza kuelezwa kama amri. "apa"

uape kwa Yahwe

Msemo "uape kwa" una maana ya kutumia jina la kitu au mtu kama msingi au nguvu ambayo kiapo kinafanywa. "niahidi mimi pamoja na Yahwe kama shahidi wako"

Mungu wa Mbingu na Mungu wa nchi

"Mungu wa mbingu na nchi". Maneno "mbingu" na "nchi" yanatumika pamoja kumaanisha kila kitu ambacho Mungu aliumba. "Mungu wakila kitu mbinguni na nchini"

mbingu

Hii ina maana ya sehemu ambayo Mungu anaishi.

kutoka kwa mabinti wa Wakanaani

"kutoka kwa wanawake wa Kanaani" au "kutoka kwa Wakaanani". Hii ina maana ya wanawake wa Kanaani.

miongoni mwao wale nikaao kati yao

"miongoni mwao wale namoishi" Hapa "nikaapo" ina maana ya Abrahamu na familia yake yote na watumishi. "miongoni mwao tunapoishi"

Lakini utakwenda

Hii inaweza kuelezwa kama amri. "Apa ya kwamba utakwenda" au "Lakini ondoka"

ndugu zangu

"familia yangu"

Genesis 24:5

Itakuwaje

"nitafanyaje iwapo"

hatakuwa tayari kufuatana nami

"hatanifuata" au "akikataa kurudi pamoja nami"

Je nitamrudisha mwanao katika nchi ambayo ulitoka

"Je nimchukue mwanao kuishi katika nchi ambayo umetoka"

Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu kule

Msemo "hakikisha" unasisitiza amri inayofuata. "Kuwa mwangalifu usimpeleke mwanangu kule" au "Hakika hautakiwi kumpeleka mwanangu kule"

ambaye alinitoa mimi kutoka katika nyumba ya baba yangu

Hapa "nyumba" ina maana ya watu katika familia. "aliyenichukua kutoka kwa baba na familia yangu yote"

aliniahidia kwa kiapo maalumu

"aliapa kiapo kwangu"

akisema, 'Nitawapa uzao wako nchi hii,'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "akisema kwamba angempataia nchi hii kwa uzao wake"

atatuma malaika wake

Maneno "atatuma" na ":wake" yana maana ya Yahwe.

Genesis 24:8

Taarifa ya Jumla:

Mstari wa 8 ni muendelezo wa maelekezo Abrahamu alimpatia mtumishi wake.

Lakini ikiwa mwanamke hatakuwa tayari kukufuata

"Lakini kama mwanamke anakataa kurudi pamoja nami." Abrahamu alikuwa akijibu swali la mtumishi wake kutoka 24:5.

utakuwa huru katika hiki kiapo changu

"utafunguliwa kutoka kwa kiapo ulichokifanya kwangu". Kutokamilisha kiapo inazungumziwa kana kwamba mtu anakuwa huru kutoka kwa kitu ambacho kimemkamata. "hautapaswa kufanya kile ulichoapa kwangu ambcho ulipaswa kufanya"

akaweka mkono wake jini ya paja la Abrahamu bwana wake

Hii ilikuwa ikionyesha ya kwamba hakika angefanya kile alichoapa kufanya.

akaapa kwake

"akafanya kiapo kwake"

kuhusiana na jambo hili

"kuhusu ombi la Abrahamu" au "ya kwamba angefanya kile alichoambiwa na Abrahamu"

Genesis 24:10

na akaondoka. Akachukua pia

Sentensi inayoanza na "Akachukua pia" inatupa taarifa ya nyongeza kuhusu nini mtumishi alichukua katika safari. Alivikusanya kabla ya kuondoka.

Akachukua pia aina zote za zawadi kutoka kwa bwana wake

Hii ina maana alichukua pia vitu vingi ambavyo bwana wake alitaka akawapatie familia ya mwanamke.

Akaondoka na kwenda

"akajiandaa na kuondoka" au "aliondoka na kwenda"

mji wa Nahori

Maana zaweza kuwa 1) "mji ambapo Nahori aliishi" au 2) "mji ulioitwa Nahori".

Akawapigisha magoti ngamia

Ngamia ni wanyama warefu wenye miguu mirefu. Aliwafanya wainamishe miguu yao na kushusha miili yao ardhini. "Aliwafanya ngamia kulala chini"

kisima cha maji

"kisima cha maji" au "kisima"

kuchota maji

"kufuata maji"

Genesis 24:12

Kisha akasema

"Kisha mtumishi akasema"

anijalie kufanikiwa leo na aoneshe agano la uaminifu kwa bwana wangu Abrahamu

Unaweza kuiweka hii kwa neno kiunganishi "kwa". Hii inaonyesha kwa uwazi jinsi mtumishi anataka Mungu amuonyeshe uaminifu wake. "Onyesha agano la uaminifu kwa bwana wangu Abrahamu kwa kunipatia mafanikio leo"

anijalie kufanikiwa

"nipatie mafanikio". Mtumishi alitaka kupata mke mwema kwa mwana wa Abrahamu. Nomino inayojitegemea ya "mafanikio" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "nisaidie nifanikiwe" au "nifanye niweze kufanya kile nilichokuja kukifanya"

aoneshe agano la uaminifu kwa bwana wangu Abrahamu

Huu ni uaminifu kwa sababu ya agano ambalo Mungu alifanya na Abrahamu. Nomino inayojitegemea ya "uaminifu" inaweza kuelezwa "uwe mwaminifu". "Uwe mwaminifu kwa bwana wangu Abrahamu kwa sababu ya agano lako"

Tazama

Hapa neno "tazama" linaongeza msisitizo kwa kile kifuatacho.

chemchemi ya maji

"chemichemi" au "kisima"

binti za watu wa mji

"wanawake vijana wa mji ule"

Na itokee kama hivi

"Na itokee kwa namna hii" au "Fanya hii ifanyike"

Nikimwambia msichana, 'tafadhari tua mtungi wako ili niweze kunywa maji,'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Hii inaweza kuelezwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Ninapomuuliza msichana aniruhusu kunywa maji kutoka kwenye mtungi wake"

tafadhari tua mtungi wako

Wanawake walibeba mitungi juu ya mabega yao. Alitakiwa kushusha na kumpatia mwanamume anywe.

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

kuwa umeonesha agano la uaminifu kwa bwana wangu

Nomino inayojitegemea "uaminifu" inawezakuelezwa kama "alikuwa mwaminifu". "ya kwamba ulikuwa mwaminifu kwa bwana wangu kwa sababu ya agano lako"

Genesis 24:15

Ikawa kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama

tazama

Neno "tazama" hapa linatuamsha kusikiliza taarifa ya kushangaza inayofuata.

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

Rebeka alizaliwa na Bethueli mwana wa Milka, mke wa Nahori, ndugu yake na Abrahamu

"Baba yake Rebeka alikuwa Bethueli. Wazazi wa Bethueli walikuwa Milka na Nahori. Nahori alikuwa kaka yake Abrahamu"

Bethueli

Bethueli alikuwa baba yake Rebeka.

Nahori

Hili ni jina la mwanamume.

Milka

Milka alikuwa mke wa Nahori na mama yake Bethueli.

kashuka kisimani ... na kupanda juu.

Kisima kilikuwa sehemu ya chini katika muinuko wa chini ambapo mtumishi alikuwa amesimama.

Genesis 24:17

kumlaki yule msichana

"kukutana na yule msichana"

maji kidogo

"maji kiasi"

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

bwana wangu,

"bwana". Hapa mwanamke anatumia msemo huu wa heshima kwa mwanamume, ingawa yeye sio mtumwa wake.

kwa haraka akatua mtungi wake juu ya mkono wake

"alishusha mtungi wake haraka". Alikuwa akibeba mtungi juu ya bega lake. Ilimbidi ahushe ili apate maji kwa ajili ya mtumishi.

Genesis 24:19

Nitachota maji

"Nitafuata maji"

Hivyo akaharakisha akamwaga maji yaliyokuwa mtungini

"Kwa hiyo aliyatoa maji ndani ya mtungi haraka"

chombo cha kunywshea mifugo,

"chombo cha kunywshea wanyama". Chombo cha kunyweshea wanayma ni chombo kilicho wazi kinachoshikilia maji kwa ajili ya wanyama kunywa.

Genesis 24:21

Yule mtu

"Mtumishi"

akamtazama msichana

"akamtazama Rebeka" au "alimtazama yule msichana"

kuona

Kujifunza jambo huwa kunazungumzwa kana kwamba kinaweza kuona. "kujua" au "kukusudia"

amefanikisha njia yake

"Kutimiza lengo la safari yake" au "alifanya safari yake iwe ya mafanikio". Unaweza kuiweka wazi nini mtumishi alijaribu kukusudia. "alimwonyesha mwanamke nani ambaye angekuwa mke wa Isaka"

au la

unaweza kuweka kwa uwazi taarifa inayoeleweka. "au kutofanikiwa katika safari yake"

pete ya pua ya dhahabu yenye uzito wa nusu shekeli

"pete ya pua ya dhahabu ambayo ilikuwa na uzito wa gramu sita". Uzito unaonyesha thamani ya pete hiyo. "pete ya pua ya dhahabu ya gharama"

bangili mbili za dhahabu kwa ajili ya mikono yake zenye uzito wa shekeli kumi

"bangili mbili za dhahabu kwa ajili ya mikono yake zenye uzito wa gramu 110". Uzito unaonyesha ukubwa na thamani yao. "bangili mbili za dhahabu kwa ajili ya mikono yake"

wewe ni binti wa nani

"Nani baba yako"

Je kuna nafasi nyumbani mwa baba yako

"Je kuna nafasi katika nyumba ya baba yako"

kwa ajili yetu

Ni wazi ya kwamba wanamume wengine walikuwa katika safari hii na mtumishi wa Abrahamu. Hapa "yetu" ina maana mtumishi na wale aliokuwa amesafiri pamoja naye.

kupumzika usiku

"kukaa usiku huu" au "kukaa usiku wa leo"

Genesis 24:24

Akamwambia

"rebeka alisema" au "msichan yule alisema"

kwake

"kwa mtumishi"

Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, ambaye alimzaa kwa Nahori

"Bethueli ni baba yangu, na wazazi wake ni Milka na Nahori"

Tunayo malisho tele na chakula

Inaeleweka ya kwamba malisho na chakula yalikuwa kwa ajili ya ngamia. "Tuna malisho na chakula cha kutosha kwa ajili ya ngamia"

kwa ajili yako kulala usiku

"kwa ajili yako kulala usiku" au "ambapo utalala kwa usiku huu"

kwa ajili yako

Hapa "yako" ina maana ya mtumishi na wale aliosafiri naye"

Genesis 24:26

yule mtu

"mtumishi"

akainama chini

Hii ni ishara ya unyenyekevu mbele za Mungu.

hakuacha agano lake la uaminifu na kweli yake mbele ya bwana wangu

"hakuacha kuonyesha agano lake la uaminifu na kweli kwa bwana wangu." Nomino zinazojitegemea "uaminifu" na "kweli" zinaweza kuelezwa kama "kuwa mwaniminfu na mkweli". "ameendelea kuwa mwaminifu na mkweli kwa sababu ya agano lake na bwana wangu"

hakuacha

Hii inaweza kuelezwa kwa namna ya chanya. "anaendelea kuonyesha"

ndugu zake

"familia" au "ukoo"

Genesis 24:28

akakimbia na kwenda kuwaeleza watu wa nyumba ya mama yake

Hapa "nyumba" ina maana ya watu waliokuwa wakiishi katika nyumba ya mama yake. "alikimbia katika nyumba na kumwambia mama yake na kila mtu pale"

mambo yote haya

"kila kitu ambacho kilitokea"

sasa

Neno hili linatumika hapa kuweka alama kuweka mapumziko katika simulizi kuu. hapa mwandishi anaelezea taarifa ya nyuma kuhusu Rebeka. Mwandishi anamtambulisha kaka yake, Labani, katika simulizi.

Akisha kuona hereni ya puani ... na kusikia maneno ya Rebeka dada yake

Mambo haya yalitokea kabla hajakimbia nje kwa mwanamume. Hii inatuambia kwa nini Labani alikimbia nje kwa mwanamume yule.

na kusikia maneno ya Rebeka dada yake, "Hivi ndivyo yule mtu alicho niambia,"

Hii inaweza kuelezwa kama nukuu isiyokuwa moja kwa moja. "alipokuwa amesikia ya kuwa dada yake Rebeka amemwambia nini mwanamume amekisema kwake"

tazama

"naam". Neno "tazama" hapa linaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata.

Genesis 24:31

Njoo

"Njoo ndani" au "Ingia"

uliye barikiwa na Yahwe

"wewe ambaye Yahwe amekubariki"

uliye

Hapa neno la "uliye" lina maana ya mtumishi wa Abrahamu.

Kwa nini umesimama nje?

Labani alitumia swali hili kumkaribisha mtumishi wa Abrahamu katika nyumba yake. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hauhitaji kubaki nje"

Kwa hiyo yule mtu akaingia ndani ya nyumba

Neno "akaingia" linaweza kutafsiriwa kama "akaenda"

kashusha mizigo kutoka kwa wale ngamia

Haipo wazi nani alifanya kazi hii. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtumishi wa Labani alishusha mizigo kutoka kwa ngamia" au "ngamia walishushwa mizigo"

Ngamia wakapatiwa malisho na chakula, na maji yakatolewa

Hii haisemi nani alifanya kazi hii. Iwapo utaweka hii katika hali ya kutenda basi sema "watumishi wa Labani" kama jambo. "Watumishi wa Labani waliwapa malisho na chakula ngamia, na wakatoa maji"

kuosha miguu yake ... naye

"kwa watumishi wa Abrahamu na wanamume waliokuwa naye kuosha miguu yao"

Genesis 24:33

Wakaandaa

Hapa neno "wakaandaa" lina maana ya watu wa familia ya Labani au watumishi wa nyumbani.

chakula mbele yake

"kumpatia mtumishi chakula"

niseme kile ninacho paswa kusema

"kuzungumza maneno yangu" au "nimekuambia kwa nini nipo hapa"

amekuwa mtu mkuu

Hapa neno "amekuwa" lina maana ya Abrahamu.

amekuwa mkuu

"amekuwa tajiri sana"

Amempatia

Neno "amempatia" lina maana ya Yahwe.

Genesis 24:36

Taarifa ya Jumla:

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

alimzalia mwana bwana wangu

"alimzaa mtoto wa kiume"

amempatia ... mwanawe

"bwana wangu amempatia ... kwa mtoto wake wa kiume"

Bwana wangu aliniapisha, akisema

"Bwana wangu amenifanya niape ya kwamba nitafanya kile alichonimabia kufanya. Alisema"

kutoka kwa mabinti wa Wakanaani

Hii ina maana ya wanawake wa Kaanani. "kutoka kwa wanawake wa Kaanani" au "kutoka kwa Wakaanani"

ambao kwao nimefanya makazi

"miongoni mwa wale ninamoishi". Hapa "ninamoishi" ina maana ya Abrahamu na familia yake yotena watumishi wake. "miongoni mwa wale tuishipo"

kwa ndugu zangu

"kwa ukoo wangu"

Genesis 24:39

Taarifa ya Jumla:

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

pengine mwanamke huyo asikubali kufuatana nami

Hili ni jambo ambalo linaweza kutokea. "Je kama mwanamke hatakuja pamoja nami" au "Nitafanyaje iwapo mwanamke huyu hatakuja pamoja nami?"

mbaye ninakwenda mbele yake

Kumtumikia Yahwe inazungumzwa kana kwamba Abrahamu alikuwa akitembea ndani ya uwepo wa Yahwe. "ambaye namtumikia"

atakufanikisha njia yako

"atafanya safari yako kufanikiwa"

ukoo wa baba yangu

"familia"

Lakini utakuwa huru katika kiapo changu ikiwa utafika kwa ndugu zangu na wasikuruhusu kuja naye. Ndipo utakuwa huru katika kiapo changu

Hii ni nadharia tete ambayo Abrahamu alifikiri isingeweza kutokea. Maana zaweza kuwa 1) "Kuna njia moja tu ya kuwa huru na kiapo changu: iwapo utakuja kwa ndugu zangu na hawatakupatia mwanamke kwako, basi utakuwa huru kutoka kwa kiapo changu" au 2) kujengea mstari wa 40, "iwapo utaenda kwa familia ya baba yangu na kumuuliza msichana, utakuwa umefanya kile nilichokuomba ufanye. Iwapo hawatakupatia msichana kwako, basi utakuwa huru kwa kipao ulichoapa kwangu"

Lakini utakuwa huru katika kiapo changu

"utafunguliwa kutoka kwa kiapo ulichofanya kwangu". Kushindwa kutimiza kiapo inazungumzwa kana kwamba mtu yupo huru na kitu kilichomfunga. "hautapaswa kufanya kile ulichoapa kwangu ambacho ungefanya"

ikiwa utafika kwa ndugu zangu

Lugha zinatumia maneno "njoo" na "kwenda" tofauti. "iwapo utafika kwa nyumba ya ndugu zangu" au "utakapokwenda kwa ndugu zangu"

Genesis 24:42

Taarifa ya Jumla:

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

kisima

"kisima"

niko hapa nimesimama karibu na kisima cha maji

Mtumishi alikatisha kile alichokuwa akimuuliza Mungu kwa kuvuta nadhari ya Mungu kwa pale alipokuwa amesimama.

na iwe kwamba binti ajaye ... nitakayemwambia ... mwanamke atakayeniambia

Mtumishi alirudia kueleza ombi lake, na alikuwa na mambo matatu kusema juu ya mwanamke ambayo alitumaini yangekuja.

kuchota maji

"kuchukua maji"

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

awe ndiye mwanamke

Mtumishi alikamilisha ombi lake.

Genesis 24:45

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

kuzungumza moyoni mwangu

Kuomba kimoyo moyo katika akili ya mtu inazungumzwa kana kwamba alikuwa akizungumza ndani ya moyo wake. Neno "moyo" lina maana ya mawazo yake na fikra zake. "kuomba" au"kuomba kimya kimya"

tazama

"naam" au "ghafla". Neno "tazama" hapa linatuamsha kusikiliza taarifa inayoshangaza inayofuata.

mtungi

chombo cha ukubwa wa kati kilichoundwa na udongo kinachotumika kubeba na kumwaga vimiminikio.

akashuka chini kisimani

Msemo "akashuka chini" unatumika kwa sababu kisima kilikuwa sehemu ya chini zaidi ya mahali watumishi walipokuwa wamesimama.

kisimani

"kisima"

akawanywesha ngamia

"wakawapa ngamia maji"

Genesis 24:47

Taarifa ya Jumla

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

Binti wa Bethueli, Mwana wa Nahori, ambaye Milka alizaa kwake

"Baba yangu Bethueli. Wazazi wake ni Nahori na Milka"

pete ... bangili

Katika simulizi hii, vitu vyote hivi vilikuwa vya dhahabu.

nikainama

Hii ni ishara ya unyenyekevu mbele za Mungu.

ameniongoza katika njia sahihi

"amenileta hapa"

ambaye ameniongoza

Neno la kiunganishi "kwa sababu" linaweza kutumika kuonyesha hii ni sababu mtumishi alimuabudu Mungu. "kwa sababu Yahwe aliniongoza"

ndugu za bwana wangu

Hii ina maana ya Bethueli, mwana wa Abrahamu kaka yake Nahori.

Genesis 24:49

Taarifa ya Jumla:

Mtumishi wa Abrahamu anaendelea kuzungumza kwa familia ya Rebeka.

Kwa hiyo

"Kwa hiyo". Hapa "kwa hiyo" haimaanishi "katika muda huu", lakini unatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimi linalofuata.

ikiwa mko tayari kumfanyia rehema na kweli, niambieni

Namna gani wangeonyesha uaminifu wao na ukweli inaweza kuelezwa kwa uwazi. "niambie kama utakuwa mwaminifu na mkweli kwa bwana wangu kwa kunipatia Rebeka awe mke wa mwana wake"

mko

Neno "mko" ina maana ya Labani na Bethueli.

uaminifu na kweli

Hizi nomino zinazojitegemea zinaweza kuelezwa kama "umanifu na ukweli"

uaminifu wa familia

Huu ni uaminifu wa watu wa familia

Lakini kama sivyo

Taarifa inayoeleweka inaweza kuelezwa kwa uwazi. "Lakini kama haujajiandaa kumtendea bwana wangu kwa uaminifu na ukweli wa familia"

ili kwamba niweze kwenda upande wa kulia, au kushoto

Maana zaweza kuwa 1) kuamua nini cha kufanya kunazungumzwa kana kwamba mtu atageuka upande mmoja au mwingine. "ili kwamba nijue nini cha kufanya" au 2) mtumishi anataka kujua kama anahitaji kusafiri sehemu nyingine. "ili kwamba niendelee na safari yangu"

Genesis 24:50

Bethueli

Huyu alikuwa baba wa Labani na Rebeka.

Jambo hili limetoka kwa Yahwe

"Yahwe alisababisha haya yote kutokea"

hatuwezi kusema kwako aidha neno baya au zuri

Wanasema hawana mamlaka ya kuamua kwamba aliyofanya Mungu ni mema au mabaya. "hatuthubutu kuhukumu kile ambacho Yahwe anatenda"

Tazama

Neno "tazama" hapa linaongeza msisitizo kwa kile kifuatacho.

Rebeka yu mbele yako

"Huyu hapa Rebeka"

Genesis 24:52

maneno yao

"Maneno ya Labani na Bethueli". Hapa "maneno" ina maana ya kile walichosema. "kile ambacho Labani na Bethueli walisema"

akainama mwenyewe chini

Kuinama chini mbele ya Mungu ni ishara ya kumuabudu yeye.

vipande vya fedha na vipande vya dhahabu

"vipande vya fedha na dhahabu" au "vitu vilivyotengenezwa kwa fedha na dhahabu"

zawadi zenye thamani

"zawadi za gharama" au "zawadi za thamani"

Genesis 24:54

yeye na watu aliokuwa nao

"Watumishi wa Abrahamu na wanamume wake"

wakakaa pale mpaka usiku

"walilala pale usiku ule"

walipoamka asubuhi

"waliamka asubuhi iliyofuata"

Niruhusuni niende

"Niruhusu niondoke na kurudi"

kwa siku chache zingine, angalau siku kumi

"angalau siku kumi zaidi"

kumi

"10"

baada ya hapo

"Kisha"

Genesis 24:56

akasema

"Mtumishi wa Abrahamu akasema"

kwao

"kwa kaka wa Rebeka na mama yake"

msinizuie

"Msinikawize" au "Msinifanye nisubiri"

Yahwe amefanikisha njia yangu

Hapa "njia" ina maana ya safari. "Yahwe amefanya nifanikiwe katika lengo la safari yangu"

Niruhusuni niende

"Niruhusu niondoke"

Genesis 24:59

Kwa hiyo wakampeleka dada yao Rebeka

"Kwa hiyo familia ilimpeleka Rebeka"

dada yao

Rebeka alikuwa dada wa Labani. "ndugu yao" au "dada wa Labani"

mtumishi wake wa kike

Hii ina maana ya mtumishi wa kike ambaye alimlisha Rebeka alipokuwa mtoto mchanga, akamtunza alipokuwa mtoto, na alimtumikia.

Dada yetu

Rebeka hakuwa adad kwa kila mtu katika familia yake. Lakini walimuita kwa jinsi hii kuonyesha walimpenda. "Dada yetu Rebeka"

na uwe mama wa maelfu na wa makumi elfu

Hapa "mama" ina maana ya mama. "na uwe mama wa mamilioni wa watu" au "na uwe na uzao mkubwa"

maelfu na wa makumi elfu

Hii ina maana ya idadi kubwa au idadi isiyohesabika.

uzao wako upate kumiliki lango la wale wanao wachukia

Majeshi huvunja katika malango ya miji ya adui zao na kuwashinda watu. "na uzao wako wawashinde kabisa wale wawachukiao"

Genesis 24:61

Kisha Rebeka akasimama, yeye na watumishi wake wakawapakia ngamia

"Kisha Rebeka akasimama, yeye na watumishi wake wakawapakia ngamia"

Hivyo watumishi wakamchukua Rebeka, na wakaenda zao

"Katika njia hii mtumishi wa Abrahamu alimchukua Rebeka pamoja naye na kurudi naye mahali alipotoka"

Nyakati hizo

Neno hili linaweka alama ya kubadili simulizi. Ilikuwa inaeleza juu ya mtumishi kutafuta mke, na sasa itaanza kueleza kuhusu Isaka.

Beerlahairoi

Hili ni jina la maji ya kisima kule Negebu.

Genesis 24:63

Isaka akaenda kutafakari shambani jioni

"jioni moja Isaka alitoka shambani kufikiri". Hii inaweza kuwa muda mrefu baada ya mtumishi na Rebeka kuondoka nyumbani kwake kwa maana walisafiri umbali mrefu.

Alipotazama akaona, natazama, kulikuwa na ngamia wakija!

Hili neno "tazama" hapa linatumasha kusikiliza kwa taarifa ya kushangaza inayofuata. "Alipotazama juu akashangaa kuona ngamia wakija"

Rebeka akatazama

"Rebeka akatazama juu"

akaruka kutoka kwenye ngamia

"alishuka juu ya ngamia haraka"

akachukua shela yake akajifunika

"Kwa hiyo alijifunika uso na shela yake". Hii ni ishara ya heshima na adabu kwa mwanamume atakayemuoa. Maana kamili inaweza kuelezwa wazi.

shela

Kipande cha kitambaa kilichotumika kufunika kichwa cha mtu, mabega na uso.

Genesis 24:66

akamchukua Rebeka, na akawa mke wake

Misemo hii miwili ina maana ya kwamba Isaka alimuoa Rebeka. "na akamuoa Rebeka" au "na akamchukua kama mke wake"

Kwa hiyo Isaka akafarijika

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kwa hiyo Rebeka alimfariji Isaka"