Genesis 22

Genesis 22:1

Ikawa kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

baada ya mambo hayo

Msemo huu una maana ya matukio katika sura ya 21.

Mungu akampima Abrahamu

Inasemekana Mungu alimpima Abrahamu kujifunza kama Abrahamu atakuwa mwaminifu kwake. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. Mungu alipima uaminifu wa Abrahamu.

Mimi hapa

"Ndio, nasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

mwanao wa pekee

Inasemekana ya kwamba Mungu anajua ya kuwa Abrahamu ana mtoto mwingine, Ishmaeli. Hii inasisitiza ya kwamba Isaka ni mwana ambaye Mungu alimuahidi kumpa Abrahamu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "mwana wako wa pekee ambaye nilikuahidi"

umpendaye

Hii inasisitiza upendo wa Abrahamu kwa mwanawe, Isaka.

nchi ya Moria

"nchi inayoitwa Moria"

akatandika punda wake

"akambebesha punda wake" au "akaweka juu ya punda kile kilichohitajika kwa ajili ya safari"

vijana wake

"watumishi"

kisha akapanga safari

"alianza safari yake" au "alianza kusafiri"

Genesis 22:4

Katika siku ya tatu

Neno "tatu" ni nambari ya mpango kwa ajili ya tatu. "Baada ya kusafiri kwa siku tatu"

akaona mahali pakiwa mbali

"akaona kwa mbali sehemu ambayo Mungu alizungumzia"

vijana wake

"watumishi"

Tutaabudu

Neno "tutaabudu" ina maana ya Abrahamu pekee na Isaka.

tutarudi hapa penu

"nitarudi kwako"

akaziweka juu ya Isaka mwanawe

"akamfanya Isaka, mwanawe, kuibeba"

Mkononi mwake

Hapa "mkononi mwake mwenyewe" inasisitiza ya kwamba Abrahamu mwenyewe alibeba vitu hivi. "Abrahamu mwenyewe alibeba"

moto

Hapa "moto" ina maana ya sufuria yenye mkaa unaowaka au tochi au taa. "kitu cha kuanzishia moto"

wote wawili wakaondoka pamoja

"waliondoka pamoja" au "wote wawili waliondoka pamoja"

Genesis 22:7

Baba yangu

Hii ni njia ya upendo ya mwana kuongea kwa baba yake.

Nipo hapa

"Ndio, nasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

Mwanangu

Hii ni njia ya upendo ya baba kuongea kwa mwanawe.

moto

Hapa "moto" ina maana ya sufuria yenye mkaa unaowaka au tochi au taa. "kitu cha kuanzishia moto"

mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa

"mwanakondoo ambaye utamtoa kama sadaka wa kuteketezwa"

Mungu mwenyewe

Hapa "mwenyewe" inasisitiza ya kwamba Mungu atatoa mwanakondoo.

atatupatia

"atatupatia sisi"

Genesis 22:9

Walipofika mahali

"Abrahamu na Isaka walipofika katika sehemu ile"

akamfunga

"akamfunga kamba"

juu ya madhabahu, juu ya zile kuni

"juu ya kuni zilizokuwa juu ya madhabahu"

akanyoosha mkono wake akachukua kisu

"akaokota kile kisu"

Genesis 22:11

malaika wa Yahwe

Maana zinaweza kuwa 1) Yahwe alijifanya kuonekana kama malaika au 2) huyu alikuwa mmoja wa malaika wa Yahwe au 3) huyu alikuwa mjumbe maalumu kutoka kwa Mungu (baadhi ya wasomi wanadhani alikuwa Yesu). Kwa sababu msemo hauleweki vizuri, ni bora kutafsiri kama "malaika wa Yahwe" kwa kutumia neno la kawaida linalotumika kwa "malaika".

kutoka mbinguni

Hii ina maana ya sehemu ambapo Yahwe anaishi.

Mimi hapa

"Ndio,ninasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

usinyooshe mkono wako juu ya kijana, wala usifanye jambo lolote kumdhuru

Msemo "usinyooshe mkono wako juu ya" ni namna ya kusema "usimdhuru". Mungu alisema kitu kile kile mara mbili kusisitiza ya kwamba Abrahamu hakupaswa kumdhuru Isaka. "usimdhuru kijana kwa njia yoyote ile"

sasa najua ... kwa ajili yangu

Maneno "najua" na "yangu" yana maana ya Yahwe. Unapotafsiri kilichomo ndani ya nukuu, sema kwa namna ambayo Yahwe alitumia maneno ya "najua" na "yangu" alipomaanisha Yahwe.

unamcha Mungu

Hii ina maana ya kumheshimu Mungu kwa undani na kuonyesha heshima hiyo kwa kumtii yeye.

kuona

"kwa sababu ninaona"

hukumzuilia mwanao ... kwa ajili yangu

"haujamshikilia nyuma mwanao ... kwangu" Hii inaweza kusemwa kwa njia ya chanya. "ulikuwa tayari kumtoa mwanao ... kwangu"

mwanao, mwanao wa pekee

Inasemekana ya kwamba Mungu anajua ya kuwa Abrahamu ana mtoto mwingine, Ishmaeli. Hii inasisitiza ya kwamba Isaka ni mwana ambaye Mungu alimuahidi kumpa Abrahamu. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "mwana wako wa pekee ambaye nilikuahidi"

Genesis 22:13

tazama

Neno "tazama" hapa linatuamsha kuvuta nadhari kwa taarifa ya kushangaza inayofuata.

kulikuwa na kondoo mume amenaswa pembe zake kichakani

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kulikuwa na kondoo dume aliyekwama pembe zake kichakani" au "kulikuwa na kondoo dume aliyekwama kichakani"

akaenda akamchukua kondoo

"Abrahamu alienda kwa kondoo dume na kumchukua"

atatoa ... itatolewa

"atatupatia sisi"

hata leo

"hata sasa". Hii ina maana ya hata katika kipindi ambacho mwandishi alikuwa akiandika kitabu hiki.

itatolewa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Yeye atatoa"

Genesis 22:15

Malaika wa Yahwe

Maana zinaweza kuwa 1) Yahwe alijifanya kuonekana kama malaika au 2) huyu alikuwa mmoja wa malaika wa Yahwe au 3) huyu alikuwa mjumbe maalumu kutoka kwa Mungu (baadhi ya wasomi wanadhani alikuwa Yesu). Kwa sababu msemo hauleweki vizuri, ni bora kutafsiri kama "malaika wa Yahwe" kwa kutumia neno la kawaida linalotumika kwa "malaika".

mara ya pili

Neno "pili" ni namba ya mpango kwa ajili ya mbili

kutoka mbinguni

Hapa neno "mbinguni" lina maana ya sehemu anapoishi Mungu.

na kusema - Hiki ni kiapo cha Yahwe

"na kuzungumza ujumbe huu kutoka kwa Yahwe" au "na kutamka maneno haya ya Yahwe". Hii ni njia ya fasaha ya kusema ya kwamba maneno yanayofuata yanatoka moja kwa moja kwa Yahwe.

Kwa ajili ya nafsi yangu nimeapa

"Nimeahidi na mimi ni shahidi wangu mwenyewe". Msemo "kuapa kwa" una maana kutumia jina la kitu au mtu kama msingi au nguvu ambayo kiapo kinafanyika. Hakuna kitu chenye nguvu zaidi ya Yahwe kuapa kwa jina lake mwenyewe.

umefanya jambo hili

"umenitii"

hukunizuilia mwanao

"hukumzuia nyuma mtoto wako wa kiume". Hii inaweza kuwekwa katika hali ya chanya. "ulikuwa tayari kumtoa mwanao kwangu"

mwanao, mwanao wa pekee

Inaonyesha ya kwamba Mungu anajua ya kuwa Abrahamu ana mtoto mwingine, Ishmaeli. Hii inasisitiza ya kwamba Isaka ni mwana ambaye Mungu alimuahidi kumpatia Abrahamu.

hakika nitakubariki

"hakika nitabariki"

nitakuzidishia uzao wako

Nitasababisha uzao wako kuongezeka tena na tena" au "Nitasababisha uzao wako kuwa mwingi"

kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari

Mungu alifananisha uzao wa Abrahamu na nyota na mchanga. Kama vile watu wasivyoweza kuhesabu idadi kubwa ya nyota au chembe za mchanga, kwa hiyo kutakuwa na uzao mwingi wa Abrahamu ambao watu wasingeweza kuwahesabu. "zaidi ya kile uwezavyo kuhesabu"

kama nyota za angani

Hapa neno "mbinguni" ina maana ya kila kitu tunachoona juu ya dunia, kujumlisha jua, mwezi na nyota.

watamiliki lango la adui zao

Hapa "lango" linawakilisha mji wote. "Kumiliki lango la adui zake" ina maana ya kuangamiza adui zake. "atawashinda adui zake kabisa"

Genesis 22:18

Taarifa ya Jumla

Malaika wa Yahwe anaendelea kuzungumza na Abrahamu.

mataifa yote ya dunia watabarikiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mimi, Bwana, nitabariki watu wote wanaoishi mahali pote"

mataifa ya dunia

Hapa "mataifa" ina maana ya watu wa matiafa.

umetii sauti yangu

Hapa "sauti" ina maana ya kile ambacho Mungu alisema. "umetii kile nilichosema" au "umenitii"

Abraham akarejea

Ni Abrahamu pekee aliyetajwa kwa sababu alikuwa baba, lakini imeonekana ya kwamba mwanawe alikwenda naye. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Abrahamu na mwanawe walirejea"

vijana

"watumishi"

wakaondoka

"waliondoka sehemu ile"

akakaa Beerisheba

Ni Abrahamu pekee aliyetajwa kwa sababu alikuwa kongozi wa familia yake na watumishi wake, lakini imeonekana walikuwa pamoja naye. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Abrahamu na watu wake alikaa Beerisheba"

Genesis 22:20

Ikawa kwamba baada ya mambo haya

"Baada ya matukio haya". Msemo "mambo haya" una maana ya matukio ya Mwanzo 22:1-19

Abraham aliambiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mtu alimwambia Abrahamu"

Milka amemzalia pia watoto

"Milka pia alizaa watoto"

Milka

Hili ni jina la mwanamke

walikuwa ni Usi mzaliwa wa kwanza, Busi ndugu yake

"Jina la mwanawe wa kwanza lilikuwa Usi, na majina ya watoto waliosalia walikuwa Busi ndugu yake"

Usi ... Busi ... Kemueli ... Aramu ...Kesedi, Hazo, Pildasi, Yildashi, na bethueli

Haya yote ni majina ya wanamume. Hawa wote kasoro Aramu walikuwa watoto watoto wa nahori na Milka.

Genesis 22:23

Bethueli akawa baba wa Rebeka

"Baadae Bethueli akawa baba wa Rebeka"

Hawa walikuwa ni wale watoto wanane ambao Milka alizaa kwa Nahori, ndugu yake na Abraham

"hawa walikuwa watoto wanane wa Milka na Nahori, ndugu yake Abrahamu" Hii ina maana ya watoto waliorodheshwa katika 22:20.

nane

"8"

Suria wake

"Suria wa Nahori"

Reuma

Hili ni jina la mwanamke.

pia akamzaa

"pia akajifungua"

eba, Gahamu, Tahashi, na Maaka

Haya yote ni majina ya wanamume