Genesis 21

Genesis 21:1

Yahwe akamsikiliza Sara

Hapa msemo "kumsikiliza" una maana ya Yahwe kumsaidia Sara kupata mtoto. "Yahwe alimsaidia Sara"

akamzalia Abrahamu mtoto wa kiume

"akamzaa mtoto wa kiume wa Abrahamu"

katika uzee wake

"Abrahamu alipokuwa mzee sana"

katika muda ule ule ambao Mungu alikuwa amemwambia

"katika muda haswa ambao Mungu alimwambia ingekuja kutokea"

Abrahamu alimuita mwanawe wa kiume, yule ambaye alizaliwa kwake, ambaye Sara alimzaa, Isaka

"Abrahamu alimuita mtoto wake wa kiume, yule ambaye Sara alimzaa, Isaka" au "Abrahamu alimuita mtoto wao wa kiume Isaka"

Abrahamu akamtahiri mwanawe Isaka alipofikisha siku nane

"Mwanae Isaka alipofikisha umri wa siku nane, Abrahamu alimtahiri"

siku nane

"siku 8"

amemwagiza

"alimuamuru Abrahamu kufanya"

Genesis 21:5

mia moja

"100"

Mungu amenifanya nicheke

Sara alikuwa akicheka kwa sababu alishangazwa na alikuwa na furaha. Hii inaweza kuwekwa wazi. "Mungu alinisababisha nicheke kwa furaha"

kila mtu atakaye sikia

Kile ambacho watu wangesikia kinaweza kuwekwa wazi. "kila mtu asikiaye kuhusu kile Mungu amefanya kwangu"

Nani angesema kwa Abraham kwamba Sara atalea mtoto

Hili swali la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakuna ambaye angeweza kusema kwa Abrahamu ya kwamba Sara atalea watoto"

atalea mtoto

Hii ni lugha ya upole ikimaanisha kunyonyesha watoto. "mnyonyeshe mtoto maziwa yake mwenyewe"

Genesis 21:8

Mtoto akakua ... Isaka aliachishwa

"aliachishwa" ni lugha ya upole ya kusema mtoto alimaliza kunyonyeshwa. "Isaka akakua, na pale alipokuwa hahitaji tena kunyonya, Abrahamu aliandaa karamu kubwa"

mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alikuwa amezaliwa kwa Abrahamu

Jina la mwana wa Hajiri linaweza kuwekwa wazi. "Ishmaeli, mwana wa Hajiri Mmisri na Abrahamu"

akidhihaki

Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba alimzomea au alimcheka Isaka. "alimcheka Isaka"

Genesis 21:10

akamwambia Abrahamu

"Sara akamwambia Abrahamu"

Mfukuze

"mfukuze aende zake" au "mtoweshe"

mwanamke huyu mtumwa pamoja na mtoto wake

Hii ina maana ya Hajiri na Ishmaeli. Sara hakuwatambua kwa majina kwa sababu alikuwa amekasirishwa nao.

pamoja na mwanangu Isaka

"pamoja na mwanangu Isaka"

Jambo hili likamuhuzunisha sana Abrahamu

"Abrahamu alikuwa na huzuni kuhusu kile alichosema Sara"

kwa sababu ya mwanawe

"kwa sababu ilikuwa inahusu mwanawe" Inamaanisha mwanawe, Ishameli"

Genesis 21:12

Usihuzunike kwa sababu ya kijana huyu, na kwa sababu ya mwanamke huyu mtumwa wako

"Usifadhaike kuhusu mvulana na mjakazi wako"

Sikiliza maneno asemayo Sara juu ya jambo hili

Hapa "maneno" yana maana ya kile kinachosemwa. "Fanya kila kitu ambacho Sara anakuambia kuhusu wao"

itakuwa kupitia Isaka kwamba uzao wako utaitwa

Msemo "utaitwa" una maana ya wale watakaozaliwa kupitia Isaka ndio wale Mungu anawatambua kuwa uzao ambao alimuahidi Abrahamu. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Isaka ndiye atakayekuwa baba wa uzao niliokuahidi kwako"

Nitamfanya pia mtoto wa mjakazi kuwa taifa

Neno "taifa" lina maana ya Mungu atampatia uzao mwingi ili kwamba wawe taifa kubwa la watu. "Nitamfanya mwana wa mwanamke mjakazi pia awe baba wa taifa kubwa"

Genesis 21:14

akachukua mkate

Maana zaweza kuwa 1) hii inaweza kumaanisha chakula kwa ujumla au 2) hii ina maana ya mkate mahususi.

kiriba cha maji

"mfuko wa maji". Chombo cha maji kilitengenezwa kwa ngozi ya mnyama.

Maji yalipokwisha kwenye kiriba

"Mfuko wa maji ulipokuwa tupu" au "Walipokunywa maji yote"

umbali kama wa kutupa mshale

Hii ina maana ya umbali ambao mtu anaweza kutupa mshale kwa upinde. Hiini kama mita 100.

nisitazame kifo cha mtoto

Kitenzi hiki cha kujitegemea "kifo" kinaweza kuwekwa kama "kufa". "Sitaki kutazama mwanangu akifa"

akapaza sauti yake akalia

Hapa "sauti" ina maana ya sauti ya kilio chake. "kupaza sauti yake" ina maana ya kulia kwa sauti kubwa. "alipaza kwa sauti kubwa na kulia" au "alilia kwa sauti"

Genesis 21:17

kilio cha kijana

"kilio cha kijana". Hapa "kilio" ina maana ya sauti ambayo kijana alilia au alizungumza. "sauti ya Ishmaeli"

malaika wa Mungu

"mjumbe kutoka kwa Mungu" au "Mjumbe wa Mungu"

kutoka mbinguni

Hapa "mbinguni" ina maana ya sehemu ambapo Mungu huishi.

Nini kinakusumbua

"Tatizo ni nini" au "kwa nini unalia"

kilio cha kijana mahali alipo

Hapa "kilio" ina maana ya sauti ambayo kijana alilia au alizungumza. "sauti ya kijana alipokuwa amelala pale chini"

msimamishe mtoto

"msaidie kijana asimame"

nitamfanya kuwa taifa kubwa

Kumfanya Ishamaeli kuwa taifa kubwa ina maana Mungu atampa uzao mwingi ambao utakua taifa kubwa. "Nitafanya uzao wake kuwa taifa kubwa" au "Nitamfanya awe baba wa taifa kubwa"

Genesis 21:19

Mungu akayafunua macho ya Hajiri

Mungu kumfanya Hajiri aweze kuona kisima inazungumzwa kana kwamba alimfungua macho kihalisia. "Mungu alisababisha Hajiri kuona" au "Mungu alimuonyesha Hajiri"

kiriba

"chombo kilichoundwa na ngozi" au "mfuko"

kijana

"mvulana" au "Ishameli"

Mungu akawa pamoja na kijana

Hapa msemo wa "akawa pamoja" ni lahaja ambayo ina maana ya Mungu alimsaidia au alimbariki mvulana. "Mungu alimuongoza mvulana" au "Mungu alimbariki mvulana"

akawa mwindaji

"akawa na uwezo sana wa kutumia upinde na mishale"

akampatia mke

"akapata mke"

Genesis 21:22

Ikawa kwamba katika wakati ule

Msemo huu unaweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

Fikoli

Hili ni jina la mwanamume.

kamanda wa jeshi lake

"kamanda wa jeshi lake"

jeshi lake

neno "lake" lina maana ya Abimeleki.

Mungu yuko pamoja na wewe katika yote uyatendayo

Hapa msemo "yuko pamoja nawe" ni lahaja yenye maana ya Mungu husaidia au humbariki Abrahamu. "Mungu hubariki kila kitu ufanyacho"

Sasa basi

Neno "Sasa" halimaanishi "katika muda huu", lakini linatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata. "Sasa basi"

niapie hapa kwa Mungu

Hii ni lahaja yenye maana ya kutoa kiapo cha dhati kinachoshuhudiwa na mamlaka ya juu, kwa hali hii ni Mungu. "niahidi mimi na Mungu kama shahidi"

kwamba hutanifanyia baya

"ya kwamba hutanidanganya"

kwamba hutanifanyia baya ... pamoja na uzao wangu

Hii inaweza kuelezwa kwa njia ya chanya. "utanifanyia haki mimi na uzao wangu"

Onesha kwangu ... gano lile lile la uaminifu ambalo nimekuonesha wewe

Wanamume wawili walifanya agano kati yao. Kitenzi kinachojitegemea "umaninifu" kinaweza kuelezwa kama "mwaminifu" au "mtiifu". "Uwe mwaminifu kwangu na kwa nchi kama nilivyokuwa kwako"

kwa nchi

Hapa "nchi" ina maana ya watu. "kwa watu wa nchi"

nina apa

Hii inaweza kuelezwa kwa taarifa iliyoeleweka. "Ninaapa kuwa mwaminifu kwako na kwa watu wako kama ulivyokuwa kwangu"

Genesis 21:25

Abraham pia akamlalamikia Abimeleki

Maana zaweza kuwa 1) Abrahamu alikuwa akilalamika kuhusu kile kilichotokea au 2) "Abrahamu pia alimkaripia Abimeleki"

kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamekinyang'anya

"kwa sababu watumishi wa Abimeleki walichukua kisima kimoja cha visima vya Abrahamu"

wamekinyang'anya kwake

"kuchukua kutoka kwa Abrahamu" au "wamekitawala"

sijalisikia hadi leo hii

"Hii ni mara ya kwanza nimesikia kuhusu jambo hili"

Abrahamu akachukua kondoo na ng'ombe maksai akampatia Abimeleki

Hii ni ishara ya urafiki na ya kwamba Abrahamu amekubali kuweka agano na Abimeleki.

Genesis 21:28

Abraham akatenga wanakondoo wa kike saba peke yao

"Abrahamu aligawanya kondoo saba wa kike kutoka kundini"

saba

"7"

Nini maana ya hawa wanakondoo wa kike saba ambao umewatenga peke yao?

"Kwa nini umegawanya hawa kondoo saba kutoka kundini?"

utawapokea

"utachukua"

kutoka mkononi mwangu

Hapa "mkononi" una maana ya Abrahamu. "kutoka kwangu"

iwe ushahidi

Neno "iwe" ina maana ya zawadi ya kondoo saba.

ili kwamba iwe ushahidi kwangu

Kitenzi kinachojitegemea "shahidi" kinaweza kuelezwa kama "kuthibitisha". "Kuthibitisha kwa kila mtu"

Genesis 21:31

akaita mahali pale

"Abrahamu akapaita mahali pale"

Beerisheba

"Beerisheba inaweza kuwa na maana ya "kisima cha kiapo" au "kisima cha saba".

wote

"Abrahamu na Abimeleki"

Fikoli

Hili ni jina la mwanamume.

wakarudi katika nchi ya Wafilisti

"wakarudi katika nchi ya Wafilisti"

Genesis 21:33

mti wa mkwaju

Huu ni mti wa kijani ambao unaota jangwani. Inaweza kusemwa kwa ujumla zaidi. "mti"

Mungu wa milele

"Mungu aishiye milele"

siku nyingi

Hii ina maana ya muda mrefu zaidi