Sura 26

1 Makati Jesu achameria kudeda madedo ghose agho, wawaghorie wanafunzi wake, 2 "Mdaichi kwamba baada ya maruwa awi dimakwaka na sikukuu ya pasaka, na mvalwa wa Adamu dimawafunyigwa ili asulubiwe."

3 Baadae wabaha wa makuhani na waghosi wa wandu wakwana andu amweri katika makao gha kuhani mbaha, warikogho akiwangwa koyafa. 4 Kwa andu amweri wapangie njama ya kumwhada Jesu kwa kiviso na kumbwagha. 5 Kwa wuja wadedie, "isabonyeke makati gha sikukuu, kusudiisacxhezuka ghasia imbiri ya wandu."

6 Makati Jesu wakogho Bethania katika iwacha ja simoni mkoma, 7 Warikogho wakighaghoa mzenyi, mndumka umweri wachee kwake akika wadwa mkebe gwa Alabasta irikogho na mavuda yakona thamani mbaha, na waghamimina ighu ya chongo chake. 8 Ela wanafunzi wake wachawona ilagho ijo, wazamiwe na kudeda, "Ni indoi sababua ya hasara ihi? 9 Agha kumacha ghadimikana kudagwa kwa kiasi kibaha na kunekwa maskini."

10 Ela Jesu akika adaichi iji, wawaghorie, "kwa indoi mdamgaisha mndumka uyu? kwa wuja wabonya kilambo chiboie kwapwa. 11 Maskini mkonao maruwa ghose, ela ndamkagha andu amweri na nyi daima. 12 Kwa sababu andu wamimina mavuda agha ighu ya muiwi gwapwa, wabonyi huwo kwa ajili ya mariko ghapwa. 13 Loli nawaghorienyi, kokose injili ihi ikahubiriwa katika urumwengu mlanzi, kitendo wachibonya uyu mndumka, pia dima waka chikidedigwa kwa ajili ya kumkumbuka."

14 Niko umweri wa waja kumi na iwi, wawangiwe Yuda iskariote, waghendie kwa wabaha wa makuhani. 15 Na kudda, "dimamwanineka indoi nikamsaliti? Wakampimia Yuda viwande thelathini va fedha. 16 Tangu mudaugho walolie nafasi ya kumsaliti.

17 Hata maruwa gha kilindiri gha mikate isakumbagwa chachu, wanafunzi wamghendia Jesu na kudeda, "Hao ukundi dikuandalie uje vindo va pasaka?"

18 Akawaghoria, "Ghendenyi mzinyi kwa mundu fulani na mghorienyi, mwalimu adadeda, "mudagwapwa gwakaribia. Dimanaitimira pasaka andu amweri na wanafunzi wapwa katika iwacha jako." 19 Wanafunzi wabonyie sa wuja Jesu andu wawalagiza, na waandalie vindo va pasaka.

20 Ichafika kwenyi, wakee kuja vindo andu amweri na waja wanafunzi kumi na iwi. 21 Warikogho wadaja vindo, wadedie, "loli nawaghoria kwamba umweri wenyu dimawanisaliti."

22 Wawonie mbazi nanganyi, na kila umweri waanzie kumkotia, "Je, hakika sio nyi, Mzuri

23 Wawajibie, "Uja ambae achovyaa mkonu gwake andu amweri nanyi katika ibakuli nie ambae dimawanisaliti. 24 Mvalwa wa Adamu dimawainga kama andu waandikiwa. Ela ole wake mundu ambae dimawamsaliti mvalwa wa Adamu! kumachayakanicha kwa mundu uyo kama kumachandavalwe." 25 Yuda ambae kumachamsaliti wadedie, "Je! Ninyi Rabi?" Jesu akamghoria, "Wadeda ilagho ijo we mweni."

26 Warikogho wakija vindo, Jesu wawusie mkate, akaghubariki na kuubegha. Akawaneka wanafunzi wake akideda, "Wusenyi, mje uhu nimuwi gwapwa." 27 Akawusa kikombe na kushukuru, akawaneka na kudeda, "Nyweni wose katika ichi. 28 Kwa wuja ihi ni bagha ya iagano japwa, idiwa gwa kwaajili ya wengi kwa msamaha gwa zambi. 29 Ela nawaghorienyi, sinywagha sena matunda gha mzabibu ughu, hata maruwa ghaja ninywa gha mwishi amweri na inyo katika Ufalme gwa Aba wapwa."

30 Warikogho wameria kubora lumbo, wafumie kughenda lughongo lwa mizeituni.

31 Kisha JJesu wawaghoria, kio ichi inyo wose dima mwakikuwa kwasababu yapwa, kwa wuja yaandikigwa, dimanamkaba mlisha na ng'ondi wa ikundi dimawawaghanyika. 32 Ela baada ya kufufuka kwapwa, dimanawakiria kughenda Galilaya."

33 Ela Petro wamghoria, Ata kama wose dimawakulegha kwa sababu ya malagho ambagho dimaghakupata, nyi sikuleghagha."

34 Jesu wamjibie, "loli ndakughoria, kio ichi kabla jogholo ndaisire kema, dimawanikana mara idadu."

35 Petro akamghoria, "Ata kama kumacha yanipasa kufwa ni we, sikuksnaa." Na wanafunzi wamwi wose wakadeda woruwo uwo.

36 Baadae Jesu waghendie nawo andu kuwangwaa Gethsemane na wawaghoria wanafunzi wake, "kenyi aha wakati nikighenda uko na kutasa." 37 Akamwusa Peto na wawiu wa zebedayto na waanzie kuhuzunika na kusononeka. 38 Kisha wawaghoria, "Ngolo yapwa ikona huzuni mbaha sana, hata kiasi cha kufwa. Bakinyi aha na mlale meso andu amweri nanyi." 39 Akaghenda imbiri kidogo, akagwa kifudifudi, na kutasa. Akadeda, "Aba wapwa, ngelo idadimikana, kikombe icghi chiniepuke. Isake andu ndikundii nyi, bali sa andu ukundii we." 40 Akawaghendia wanafunzi na akawadoka watungura dilonyi, na akamghoria Petro, "Kwa indoi ndamdimie kulala meso nanyi kwa isaa jimweri? 41 Lalenyi meso na kutasa kusudi msangie majaribuni. Ngolo iradhi, ela muwi ni dhaifu."

42 Akaghenda chia rake mara ya kawi na kutasa, akadeda, "Aba wapwa ngelo ilagho iji ndajidimikana kuepukika na ni lazima nichinywee kikombe ichi, mapenzi ghako ghatimizwe."

43 Akawuya sena kuwadoka watungura dilonyi, kwa wuja meso ghawhe ghakogho ghakurie. 44 Kisha akawasigha sena akaghenda chia rake. Akatasa mara ya kadadu akideda madedo gha ja gheni. 45 Baadae Jesu wawaghendia wanafunzi wake na kuwaghoria, "bado mwamtungura tu na kukisoghosha? guwenyi, saa yakaribia, na mvalwa wa Adamu adasalitiwa mikonunyi mwa weni zambi. 46 Wukienyi, ndiinge. Guwa, uja anisalitiagha wakaribia."

47 Makati wakogho bado akiaria, Yuda umweri wa waja kumi na iwi, wafikie. Kundi ibaha jafikie andu amweri nae jikifumira kwa wabaha wa makuhani na waghosi wa wandu. Wachee na malwamba na marungu. 48 Sena mundu wakusudie kumsaliti Jesu wakogho wawaneka ishara, akideda, "Uja nimbusu, nio ye mwhadenyi." 49 Mara iyo wachee kwa Jesu na kudeda, "Salamu, Mwalimu!" na wambusu.

50 Jesu akamghoria, Amwedu jibonye jija ambajo jakureda. "Niko wakacha, na kumghaghoia mikonu Jesu, na kumwhada. 51 Guwa, mundu umweri warikogho andu amweri na Jesu, waghaghoa mkonu gwake, akafunya luwamba lwake, na akamkaba mtumishi wa kuhani mbaha, na kumdema kudu kwake. 52 Niko Jesu akamghoria, wuja luwamba lwako aja andu walufunya, kwa wuja wose watumiaa lwamba dimawaangamizwa kwa luwamba. 53 Mdadhani kuwa sidimagha kumwanga Aba wapwa, na ye akanidumia majeshi zaidi ya kumi na iwi gha malaika?" 54 Ela basi jinsi ki maandiko ghadima kutimiza gwa, uwu niko idapasa kufumira?"

55 Makati agho Jesu akaughoria umati, "Je! machana na malwamba na marungu kunuwhada sa mnyang'anyi? kila siku nakaiye hekalunyi nikifundisha, na ndamniwhadie! 56 Ela ghose agha ghabonyeka ili maandiko gha walodi ghatimie." Niko wanafunzi wake wakamsigha na kukimbia.

57 Waja wawhadie Jesu wamhadie Jesu wamghenjie kwa kuyafa, kuhani mbaha, andu ambako waandishi na waghosi wakogho waka andu amweri. 58 Ela Petro wamnughie nyuma kwa kala kula hata katika ukumbi gwa kuhani mbaha. Wangie ndenyi na kuka andu amweri na walinzi awonechifumiriagha.

59 Basi wabaha wa makuhani na ibaraza jose warikogho wakilola ushahidi gwa tee dhidi ya Jesu, kusudi wapate kumbwagha. 60 Ingawa wakakitokeza mashahidi wengi, ela ndawapatie sababu yoyose ela baaadae mashahidi wawi wakitokeza imbiri. 61 N kudeda, "Mundu uyu wadedie, "Nadimagha kujichukanya ihekalu ja Mlungu na kujiagha sena kwa maruwa adadu."

62 Kuhani mbaha wakee kimsi na kumkotia, "Ndudi magha kujibu? awa wadakushuhudia indoi dhidi yako?" 63 Ela Jesu wanyamie kima kuhani mbaha akamghoria, "sa Mlungu andu aishivyo, ndakuamuru udighorie, ngelo we ni Kristo, mvalwa wa Mlungu?"

64 Jesu wamjibie, "We mweni wadeda ilagho ijno. Ela ndakughoria, toka ijiaha na kuendelea dimawamwona mvalwa wa Adamu waka mkonu gwa kujo ukona ndighi, na akicha katika madulu gha mbingunyi."

65 Niko kuhani mbaha wararua mavazi ghake na kudeda, "Wakufuru! Je dahitaji sena ushahidi gwa, tayari mwasikira akikufuru. 66 Je! mtenganyai? wajibie na kudeda, "adastahili kifwa." 67 Kisha wamchiye mada wushunyi na kumkaba ngumi, na kumchapa makofi kwa mikonu yawhe, 68 Na kudeda, "Ditabirie, we Kristo. Ni ani wakuchapa?"

69 Wakati ugho Petro warikogho waka shighadi katika ukumbi, na myumishi wa kiwaka wamghendia na kudeda, "We pia wakogho andu amweri na Jesu wa Galilaya."

70 Ela wakanie imbiri yawhe wose, akideda, simanyagha kilambo udedaa."

71 Wachaghenda shighadi ya ilango, mtumishi umwi wa kiwaka wamwonie na kuwaghoria wakongo aho," mundu uyu pia wakogho andu amweri na Jesu wa Nazareti."

72 Wakanie sena kwa kirawo, "Nyi simu ichi mundu uyu.

73 Muda mfupi baadae, waja waja wakogho wakakimsi karibu, wamghendia na kudeda na Petro, "kwa hakika we pia ni umweri wawhe, kwa wuja hata lafudhi yako idaonesha."

74 Niko waanzie kulaani na kulawa, "Nyi simmanya mundu uyu," na mara iyo jogholo akakema.

75 Petro wamkumbukie madedo waghoriweghe ni Jesu, "kabla jogholo ndaisire kema dimawanikana mara idadu."