Genesis 44

Genesis 44:1

Maelezo ya Jumla:

Hii inaanza sehemu mpya ya tukio katika simulizi. Inawezekana hii ni asubuhi iliyofuata baada ya sherehe.

msimamizi wa nyumba yake

"msimamizi" alikuwa na wajibu wa kusimamia matukio ya nyumba ya Yusufu.

pesa ya kila mtu

Pesa yao ilikuwa sarafu za fedha yawezekana ndani ya mfuko mdogo.

katika mdomo wa gunia lake

"katika gunia lake"

Uweke kikombe changu, cha fedha

"Weka kikombe changu cha fedha"

katika mdomo wa gunia la mdogo

Neno "ndugu" linaeleweka. "ndani ya gunia la ndugu mdogo"

Genesis 44:3

Kukapambazuka asubuh

"Mwanga wa asubuhi ulionekana"

wale watu wakaruhusiwa kuondoka, wao na punda zao

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "waliwatuma watu waondoke, pamoja na punda zao"

Kwa nini mmelipa uovu badala ya mema?

Swali hili linatumiwa kukaripia wale ndugu. "Mmetutendea vibaya, baada ya sisi kuwa wema kwenu!"

Je hiki siyo kikombe ambacho bwana wangu hukinywea, na kikombe akitumiacho kwa uaguzi?

Swali hili linatumika kukaripia wale ndugu. "Tayari mnafahamu ya kwamba hiki ni kikombe ambacho bwana wangu hutumia kunywea na kwa uaguzi!"

Mmefanya vibaya, kwa jambo hili mlilolifanya.

Hii inarudia "mmefanya" kuonyesha msisitizo. "Kile mlichofanya ni kibaya sana"

Genesis 44:6

kuwambia maneno haya

Hapa "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. "alizungumza kile Yusufu alichomuambia kusema"

Kwa nini bwana wetu anasema maneno kama haya?

Hapa "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. Ndugu wanataja msimamizi kama "bwana wangu". Hii njia maalumu ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi. Inaweza kuwekwa katika lugha ya upili. "Kwa nini unasema hivi, bwana wangu?"

Na iwe mbali na watumishi wako kwamba wanaweza kufanya jambo hili

Ndugu wanajitambua wenyewe kama "watumishi wako" na "wao". Hii ni njia maalumu ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi. "Hatuwezi kufanya jambo kama hilo!"

Na iwe mbali na watumishi

Jambo ambalo mtu hawezi kufanya inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kitu ambacho mtu anataka kukiweka mbali nacho.

Genesis 44:8

Tazama

Hii inaongeza msisitizo kwa kile ndugu wanasema baadae.

pesa tulizozikuta katika midomo ya magunia yetu

"unajua pesa ambayo tumeipata ndani ya magunia yetu"

tulizileta kwako kutoka katika nchi ya Kanaani

"tumerudisha kwako kutoka Kaanani"

Ni kwa jinsi gani basi tunaweza kuiba katika nyumba ya bwana wako fedha au dhahabu?

Ndugu wanatumia swali kuweka msisitizo ya kwamba hawawezi kuiba kutoka katika bwana wa Misri. "Kwa hiyo hatuwezi kuchukua kitu chochote kutoka kwenye nyumba ya bwana wako!"

fedha au dhahabu

Maneno haya yanatumiwa pamoja kumaanisha ya kwamba hawawezi kuiba kitu chochote chenye thamani yoyote.

Yeyote kitakayeonekana kwake miongoni mwa watumishi wako

Ndugu wanajitambua wao kama "watumishi wako". Hii njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. Inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu mmoja. Pia, "kitakayeonekana" linaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Ukikuta ya kwamba mmoja wetu ameiba kikombe"

nasi sote tutakuwa watumwa wa bwana wangu

Msemo "bwana wangu" una maana ya mtunzaji. Hii inaweza kuwekwa katika lugha ya upili. "Unaweza kutuchukua kama watumwa wako"

Basi na iwe kwa kadiri ya maneno yenu

Hapa "basi" haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata. Pia "maneno" ina maana ya kile kilichosemwa. "Vizuri sana. Nitafanya kile ulichosema"

Yeye ambaye kikombe kitaonekana kwake atakuwa mtumwa wangu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kama nikikuta kikombe ndani ya moja ya magunia yenu, mtu huyo atakuwa mtumwa wangu"

Genesis 44:11

kulishusha gunia lake chini

"akateremsha gunia lake"

mkubwa ... kwa mdogo wa wote

Neno "ndugu" linaeleweka. "ndugu mkubwa ... ndugu mdogo wa wote"

mdogo wa wote, na kikombe kikaonekana katika gunia la Benyamini

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya na katika hali ya kutenda. "mdogo wa wote. Mtunzaji alikuta kikombe ndani ya gunia la Benyamini"

Wakararua mavazi yao

Neno "wakararua" ina maana ya wale ndugu. Kurarua nguo ilikuwa ishara ya dhiki na majonzi makubwa.

nao wakarudi

"na wakarudi"

Genesis 44:14

Bado alikuwepo pale

"Yusufu alikuwa bado yupo pale"

wakainama mbele zake

"wakaanguka mbele yake". Hii ni ishara ya ndugu kutaka bwana awe na huruma kwao.

Je hamjui kwamba mtu kama mimi anafanya uaguzi

Yusufu anatumia swali kukaripia ndugu zake. "Hakika mnajua ya kwamba mtu kama mimi naweza kujifunza mambo kwa uaguzi!"

Genesis 44:16

Je tunaweza kumwambia nini bwana wangu? Tuseme nini? au ni jinsi gani twaweza kujithibitisha wenyewe?

Maswali yote 3 yana maana moja. Wanatumia maswali haya kuweka msisitizo ya kwamba hakuna kitu wanaweza kusema kuelezea kilichotokea. "Hatuna kitu cha kusema, bwana wangu. Hatuwezi kuzungumza jambo lolote la maana. Hatuwezi kujithibitisha"

Je tunaweza kumwambia nini bwana wangu ... watumwa wa bwana wangu

Hapa "bwana wangu" ina maana ya Yusufu. Hii njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. Inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa pili. "Tunaweza kusema nini kwako ... watumwa wako"

Mungu ameona uovu wa watumishi wako

Hapa "ameona" haimaanishi Mungu ameona tu kile ndugu walichofanya. Ina maana Mungu sasa anawaadhibu kwa kile walichofanya. "Mungu anatuadhibu kwa dhambi zetu za zamani"

uovu wa watumishi wako

Ndugu wanajitambulisha wenyewe kama "watumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. Inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa kwanza. "dhambi zetu"

na yule ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake

Hapa "mkononi" ina maana ya mtu mzima. Pia, "kimeonekana" inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "na yule ambaye alikuwa na kikombe"

Na iwe mbali nami kwamba naweza kufanya hivyo

Kitu ambacho mtu hawezi kufanya inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kitu mtu anataka kuweka mbali na yeye. "sio kawaida yangu kufanya jambo kama hili"

Mtu ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake

Hapa "mkononi" ina maana ya mtu mzima. Pia, "kimeonekana" inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "mtu aliyekuwa na kikombe changu"

Genesis 44:18

alipomkaribia

"akakaribia"

mwache mtumishi wako

Yuda anajitambulisha kama "mtumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza kwa mtu mwenye mamlaka zaidi. Hii inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa kwanza. "niruhusu mimi, mtumishi wako"

aseme neno katika masikio ya bwana wangu

Hapa "neno" ni lugha nyingine yenye maana ya kile kilichosemwa. Na "masikio" ni lugha nyingine yenye maana ya mtu mzima. "kuzungumza na wewe, bwana wangu"

masikio ya bwana wangu

Hapa "bwana wangu" ina maana ya Yusufu. Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka zaidi. Hii inaweza kuwekwa katika lugha ya mtu wa pili. "kwako"

na usiziache hasira zako kuwaka dhidi ya mtumishi wako

Kuwa na hasira inazungumzwa kana kwamba ilikuwa moto unawaka. "tafadhali usiwe na hasira na mimi, mtumishi wako"

kwani wewe ni kama Farao

Yuda anamlinganisha bwana yule na Farao kusisitiza nguvu kubwa ambayo bwana yule alikuwa naye. Pia anadokeza ya kwamba hakutaka bwana kuwa na hasira na kumuadhibu. "kwa maana wewe kama Farao mwenye mamlaka na unaweza kuwaamuru askari wako kuniua"

Bwana wangu aliwauliza watumishi wake, kusema, Je mnaye baba au ndugu?'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Bwana wangu alituuliza kama tuna baba na ndugu"

Bwana wangu aliwauliza watumishi wake

Yuda anamtambua Yusufu kwa maneno haya "bwana wangu" na "wake". Pia anajitambulisha mwenyewe na ndugu zake kama "watumishi wake". "Wewe, bwana wangu, alituuliza, watumishi wako" au "Ulituuliza"

Genesis 44:20

Maelezo ya Jumla:

Yuda anaendelea kuzungumza mbele ya Yusufu.

Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Tunaye baba ... baba yake anampenda.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Nasi tukamwambia bwana wetu ya kwamba tuna baba ... baba yake anampenda"

tukamwambia bwana wangu

Yuda anamtambua Yusufu kama "bwan wangu". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. "tulisema kwako, bwana wangu"

baba yake anampenda

Hii ina maana ya upendo kwa rafiki au mmoja wa familia.

Nawe ukawambia watumishi wako, 'Mleteni ili nimwone.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Nawe ukasema kwa mtumishi wako ya kwamba tunapaswa kumleta ndugu yetu mdogo kwako ili uweze kumuona"

Nawe ukawambia watumishi wako

Yuda anajitambulisha mwenyewe na ndugu zake kama "watumishi wako". "Kisha ulisema kwetu, watumishi wako"

Mleteni ili nimwone

Ilikuwa kawaida kutumia neno "chini" pale ilipozungumziwa safari ya kutoka Kanaani kwenda Misri. "Mleteni kwangu"

Baada ya hapo, tukamwambia bwana wangu, 'Kijana hawezi ... baba yake angekufa.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Kwa kujibu, tulisema kwa bwana wangu ya kwamba kijana hawezi ... baba yake angekufa"

baba yake angekufa

Inadokezwa ya kwamba baba yao angekufa kwa huzuni.

Genesis 44:23

Maelezoya jumla:

Yuda anaendelea simulizi yake kuhusu Yusufu.

Na ukawambia watumishi wako, 'Mdogo wenu asipokuja pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Kisha ulisema kwa watumishi wako ya kwamba hadi pale ndugu yetu mdogo aje pamoja nasi, hatutaweza kukuona tena"

Na ukawaambia watumishi wako

Yuda anajitambulisha mwenyewe na ndugu zake kama "watumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka zaidi. "Kisha ukasema kwetu, watumishi wako"

asipokuja ... kushuka

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kushuka" kuzungumzia safari ya Kaanani kwenda Misri.

hamtauona uso wangu tena

Hapa "uso" ina maana ya mtu mzima. "Hamtaniona tena"

Ikawa

Msemo huu unatumika kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

tulipokwenda kwa mtumishi wako baba yangu

Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kwenda" kuzungumzia safari kutoka Misri kwenda Kaanani.

tulimwambia maneno ya bwana wangu

Yuda anamtambua Yusufu kama "bwana wangu". Pia "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. "tulimwambia ulichosema, bwana wangu"

Na baba yetu akasema, Nendeni tena, mkatununulie chakula

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Baba yetu alituambia kurudi tena Misri kununua chakula kwa ajili yetu na familia zetu"

Nasi tukasema, "Hatuwezi kushuka. Ikiwa mdogo wetu ... pamoja nasi,

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Kisha tukamwambia ya kwamba hatuwezi kushuka Misri. Tulimwambia ya kwamba iwapo ndugu yetu mdogo atakuwa pamoja nasi ... pamoja nasi"

kuuona uso wa mtu

Hapa "uso" ina maana ya mtu mzima. "kumuona yule mtu"

Genesis 44:27

Maelezo ya Jumla:

Yuda anaendeleza simulizi yake kwa Yusufu

akatuambia, 'Mnajua kwamba mke wangu alinizalia wana wawili. Na mmoja akatoka kwangu nami nikasema, "Bila shaka ameraruliwa vipande, na tangu hapo sijamwona." Nanyi mkimchukua huyu naye kutoka kwangu mabaya yanaweza kumpata, mtashusha mvi zangu kwa kaburini kwa huzuni.

Hii ina madaraja mawili na daraja la tatu la nukuu. Yanaweza kuwekwa kama nukuu zisikzokuwa moja kwa moja. "akatuambia ya kwamba tunafahamu ya kuwa mke wake, Raheli, alimzalia watoto wawili tu, na kwamba mmoja wao alitoweka na mnyama alimrarua vipande vipande, na hajamuona tangu siku hiyo, kisha tutamfanya afe kwa huzuni"

akatuambia

Hapa "akatuambia" haimjumlishi Yusufu.

Mnajua

Hapa "mnajua" ni wingi na ina maana ya wale ndugu.

ameraruliwa vipande

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mnyama pori alimrarua vipande vipande"

mabaya yanaweza kumpata

Jambo baya linalotokea kwa mtu inazungumziwa kana kwamba "baya" lilikuwa kitu ambacho husafiri na kuja kwa mtu.

mtashusha mvi zangu kwa kaburini kwa huzuni

"kushusha ... Kuzimu" ni njia ya kusema watasababisha afariki na kushuka Kuzimu. Anatumia neno "shuka" kwa sababu iliaminika Kuzimu ilikuwa sehemu ya chini. "kisha mtanisababisha, mtu mzee, kufa kwa huzuni"

mvi zangu

Hii ina maana ya Yakobo na inasisitiza umri wake mkubwa. "mimi, mtu mzee"

Genesis 44:30

Kwa hiyo

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika hapa kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

basi, nitapokuja ... huzuni ya kuzimu

Yuda anaelezea kwa Yusufu suala la ukweli lakini la kubuni ambalo linatarajiwa kutokea kwa Yakobo atakaporudi bila Benyamini.

nitapokuja kwa mtumishi wako

Hapa "nitakapokuja" inaweza kutafsiriwa kama "kwenda" au "kurudi".

kijana hayupo nasi

"kijana hayupo pamoja nasi"

kwa kuwa uhai wake umefungamanishwa katika uhai wa kijana

Baba anasema ya kwamba atakufa iwapo mwanawe atangekufa inazungumziwa kana kwamba maisha yao mawili yaliunganishwa pamoja kimwili. "kwa maana alisema angekufa iwapo kijana hangerudi"

itakuwa

Yuda anazungumzia kuhusu suala la kubuni katika wakati wa mbele kana kwamba ingetokea kweli.

watumishi wako watazishusha mvi za mtumishi wako baba yetu kaburini kwa masikitiko

"watazishusha ... Kuzimu" ni njia ya kusema watasababisha afariki na kushuka Kuzimu. Anatumia neno "shuka" kwa sababu iliaminika Kuzimu ilikuwa sehemu ya chini. "kisha mtanisababisha, mtu mzee, kufa kwa huzuni"

watumishi wako

Yuda anajitambulisha mwenyewe na ndugu zake kama "watumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka zaidi. "Nasi, watumishi wako" au " Na sisi"

mvi za mtumishi wako baba yetu

Hapa "mvi" ina maana ya Yakobo na inasisitiza umri wake mkubwa. "baba yetu mzee"

Kwani mtumishi wako alikuwa mdhamini wa kijana kwa baba yangu

Nomino hii inayojitegemea "mdhamini" inaweza kuwekwa kama kitenzi "aliahidi". "Maana nimuahidi baba yangu kuhusu kijana huyu"

Kwani mtumishi wako

Yuda anajitambulisha kama "mtumishi wako". "Kwa maana mimi, mtumishi wako" au "Kwa maana mimi"

ndipo nitakapokuwa mwenye hatia kwa baba yangu

Kuchukuliwa mwenye hatia inazungumziwa kana kwamba "hatia" ilikuwa kitu ambacho mtu hubeba. "kisha baba yangu anaweza kunilaumu"

Genesis 44:33

sasa

Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

mwache mtumishi wako

Yuda anajitambulisha mwenyewe kama "mtumishi wako". Hii ni njia rasmi ya kuzungumza na mtu mwenye mamlaka makubwa. "niruhusu mimi, mtumishi wako" au "niruhusu mimi"

kwa bwana wangu

Yuda anamtambua Yusufu kama "bwana wangu". "kwako, bwana wangu" au "kwako"

umwache kijana aende juu

Alikuwa akienda kutumia msemo wa "aende juu" pale alipozungumzia safari ya kutoka Misri kwenda Kaanani.

Kwa maana nitakwenda jinsi gani kwa baba yangu ikiwa kijana hayupo nami?

Yuda anatumia swali kuweka msisitizo wa majonzi ambayo angeyapata iwapo Benyamini asingerudi nyumbani. "Siwezi kurudi kwa baba yangu iwapo kijana hatakuwa pamoja nami"

Ninaogopa kuona mabaya yatakayompata baba yangu

Mtu anayeteseka vibaya inazungumziwa kana kwamba "uovu" ilikuwa kitu kinachokuja juu ya mtu. "Ninaogopa kumuona jinsi baba yangu atakavyoteseka"