Genesis 39

Genesis 39:1

Yusufu akaletwa chini Misri

Kusafiri kwenda Misri inasemekana mara kwa mara kama "chini" tofauti na kwenda "juu" katika nchi ya ahadi. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Muishmaeli alimchukua Yusufu mpaka Misri"

Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu

Hii ina maana ya kwamba Yahwe alimsaidia Yusufu na alikuwa pamoja naye mara zote. "Yahwe alimuongoza Yusufu na kumsaidia"

Aliishi katika nyumba

Hapa mwandishi anazungumzia kufanya kazi ndani ya nyumba ya bwana wake kana kwamba alikuwa akiishi ndani ya nyumba ya bwana wake. Watumishi wanaoaminiwa pekee waliruhusiwa kufanya kazi ndani ya nyumba ya bwana wao. "alifanya kazi ndani ya nyumba".

Mmisri bwana wake

Yusufu sasa alikuwa mtumwa wa Potifa.

Genesis 39:3

Bwana wake akaona kwamba Yahwe alikuwa pamoja naye

Hii ina maana ya kwamba bwana wake aliona jinsi Yahwe alivyokuwa akimsaidia Yusufu. "Bwana wake aliona ya kwamba Yahwe alikuwa akimsaidia Yusufu"

kwamba Yahwe alifanikisha kila kitu alichokifanya

"Yahwe alisababisha kila kitu alichofanya Yusufu kufanikiwa"

Yusufu akapata kibali machoni pake

"Kupata kibali" ina maana ya kukubalika na mtu. Nomino ya "machoni pake" ina maana ya maoni ya mtu. Maana zaweza kuwa 1) "Potifa alifurahishwa na Yusufu" au 2) "Yahwe alifurahishwa na Yusufu"

Akamtumikia Potifa

Hii ina maana ya kwamba alikuwa mtumishi wa binafsi wa Potifa.

Potifa akamfanya msimamizi juu ya nyumba yake, na kila alichokimiliki

"Potifa alimweka Yusufu kusimamia nyumba yake na kila kitu kilichokuwa cha Potifa"

akakiweka chini ya uangalizi wake

Pale ambapo kitu "kinakuwa chini ya uangalizi wa mtu" ina maana ya kwamba mtu anawajibika na utunzanji na uhifadhi wake. "alimfanya Yusufu kutunza"

Genesis 39:5

Ikawa alipomfanya

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

alipomfanya msimamizi juu ya nyumba yake na juu ya kila kitu alichomiliki

"Potifa alimweka Yusufu kuwa msimamizi juu ya nyumba yake na juu ya kila kitu alichomiliki"

Baraka

Hapa "baraka" ina maana ya kusababisha mema na yenye manufaa kutokea kwa mtu au kitu kinachobarikiwa.

Baraka za Yahwe zilikuwa juu ya

Hapa mwandishi anazungumzia baraka ambayo Yahwe alitoa kana kwamba ilikuwa mfuniko wa kihalisia uliofunika kitu. "Yahwe alibariki"

kila kitu alichokuwa nacho Potifa nyumbani na shambani

Hii ina maana ya nyumba na nafaka na mifugo yake. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Nyumba ya Potifa na nafaka na mifugo yake yote"

Potifa akaweka kila alichokuwa nacho chini ya uangalizi wa Yusufu

Kitu kinachokuwa "chini ya uangalizi wa mtu" ina maana ya kwamba mtu huyo anawajibika kutunza na kulinda. "Kwa hiyo Potifa alimweka Yusufu kuwa mwangalizi wa kila kitu ambacho alikuwa nacho"

Hakuwa na haja ya kufikiri juu ya lolote isipokuwa chakula alichokula tu.

Hakuhitaji kuwaza juu ya jambo lolote katika nyumba yake; alipaswa kufanya maamuzi juu ya kile alichotaka kula. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya chanya. "Potifa alitakiwa kuwaza kuhusu kile alichotaka kula tu. Hakuhitaji kuwaza juu ya kitu kingine ndani ya nyumba yake"

Basi

Neno "basi" linaweka alama ya pumziko katika simulizi ambapo mwandishi anatoa taarifa ya nyuma kuhusu Yusufu.

mzuri na wa kuvutia

Maneno haya mawili yana maana moja. Yanalenga uzuri wa muenekano wa Yusufu. Yawezekana alikuwa mwenye sura nzuri na mwenye nguvu. "mwenye sura nzuri na nguvu"

Genesis 39:7

Ikawa baada ya hayo

"Na kwa hiyo". Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya tukio jipya katika simulizi.

Tazama

"Sikia". Yusufu anatumia neno hili kuvuta nadhari ya mke wa Potifa.

bwana wangu haangalii chochote nikifanyacho nyumbani

"bwana wangu hajishughulishi juu ya nyumba yake napokuwa msimamizi." Hii inaweza kuandikwa katika hali ya chanya. "bwana wangu ananiamini na nyumba yake"

ameweka kila kitu anachokimiliki chini ya uangalizi wangu

Kitu kinachokuwa "chini ya uangalizi wa mtu" ina maana ya kwamba mtu huyo anawajibika kutunza na kulinda. "Kwa hiyo Potifa alimweka Yusufu kuwa mwangalizi wa kila kitu ambacho alikuwa nacho"

Hakuna mtu aliye mkuu katika nyumba hii kuliko mimi

Hapa mwandishi anazungumzia juu ya mamlaka kana kwamba yalikuwa ukubwa. "Nina mamlaka katika nyumba hii kuliko mtu yeyote yule"

Hajanizuia chochote isipokuwa wewe

Hii inaweza kusemwa katika hali ya chanya. "Amenipatia kila kitu isipokuwa wewe"

Ni kwa namna gani basi naweza kufanya uovu mkuu namna hii na kumtenda dhambi Mungu?

Yusufu anatumia swali kuonyesha msisitizo. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Hakika siwezi kufanya jambo hili ovu na kutedna dhambi dhidi ya Mungu"

Genesis 39:10

Alizungumza na Yusufu siku baada ya siku

Hii ina maana ya kwamba aliendelea kumuuliza kulala naye. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Aliendelea kumuuliza Yusufu alale naye"

kuwa naye

"kuwa karibu naye"

Ikawa

"Na kwa hiyo". Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya sehemu mpya ya tukio katika simulizi.

Hakuna mtu yeyote wa nyumbani

"hakuna mwanamume yeyote aliyefanya katika nyumba"

akakimbia, na kutoka nje

"na akakimbia nje haraka" au "na kwa haraka akakimbia nje ya nyumba"

Genesis 39:13

Ikawa ... akawaita

"Kisha ... akawaita." Msemo "ikawa kwamba" unatumika hapa kuweka alama kwa tukio lifuatalo katika simulizi.

na kwamba amekimbia nje

"na kwa haraka alikimbia nje ya nyumba"

watu wa nyumbani mwake

"wanamume waliofanya kazi katika nyumba yake"

Tazama

"Sikiliza". Mke wa Potifa anatumia neno hili kuvuta nadhari ya watumishi wake.

Aliingia kulala nami

Hapa mke wa Potifa anamtuhumu Yusufu kwa kujaribu kumkamata na kulala naye.

Ikawa aliponisikia nikipiga kelele, akaniacha

"Ikawa aliponisikia nikipiga kelele, akaniacha". Msemo "ikawa kwamba" unatumika hapa kuweka alama kwa tukio lifuatalo la simulizi.

Genesis 39:16

bwana wake

"Bwana wa Yusufu." Hii ina maana ya Potifa.

Akamwambia maelelezo haya

"Alielezea namna hii"

uliyemleta kwetu

Neno hili "kwetu" ina maana ya Potifa, mke wake, na inamaanisha nyumba yake yote.

aliingia kunidhihaki

"alikuja ndani kunifanya mpumbavu". Hapa neno "dhihaki" ni tafisida ya "kumkamata na kulala naye". "alikuja nilipokuwepo na akajaribu kunilazimisha nilale naye"

Ikawa

"Kisha". Mke wa Potifa anatumiamsemo huu kuweka alama ya tukio linalofuata katika habari anayomwambia kuhusu Yusufu kujaribu kulala naye.

akakimbia nje

"alikimbia haraka nje ya nyumba"

Genesis 39:19

Ikawa

"Na kwa hiyo". Msemo huu unatumika kuweka alama ya tukio jipya katika simulizi.

bwana wake

"Bwana wake Yusufu". Hii ina maana ya Potifa. Taarifa hii inaweza kuwekwa wazi. "Bwana wake Yusufu, Potifa"

aliposikia maelezo aliyoambiwa na mkewe

"alimsikiliza mke wake akimuelezea kwake". Neno "wake" na "kwake" hapa yana maana ya Potifa.

alikasirika sana

"Potifa akawa na hasira sana"

mahali walipowekwa wafungwa wa mfalme

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mahali ambapo mfalme huweka wafungwa wake"

Akawa pale

"Yusufu alikaa pale"

Genesis 39:21

Lakini Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu

Hii ina maana ya namna Yahwe alivyomtunza Yusufu na kuwa mema kwake. "Lakini Yahwe alikuwa mwema kwa Yusufu" au "Lakini Yahwe alimtunza Yusufu"

Akampa kibali mbele ya mlinzi wa gereza

Hii ina maana Yahwe alisababisha mlinzi wa gereza kumkubali Yusufu na kumtendea wema. "Yahwe alisababisha mlinzi wa gereza kufurahishwa na Yusufu"

mlinzi wa gereza

"msimamizi wa gereza" au "mtu mwenye usamamizi na gereza"

akawaweka mikononi mwa Yusufu

Hapa "mkononi" unawakilisha nguvu ya Yusufu au uaminifu. "kumweka Yusufu juu ya"

Chochote walichokifanya, kilikuwa chini ya uangalizi wa Yusufu

"Yusufu alikuwa mwanaglizi wa kila kitu walichofanya pale"

kwa sababu Yahwe alikuwa pamoja naye

Hii ina maana ya jinsi Yahwe alivyomsaidia Yusufu na kumuongoza. "kwa sababu Yahwe alimuongoza Yusufu"

Yahwe akafanikisha kila alichokifanya.

"Yahwe alisababisha kila kitu ambacho Yusufu alifanya kufanikiwa"