Genesis 31

Genesis 31:1

Basi

Neno hili linatumika hapa kuweka alama kuweka nafasi katika simulizi kuu. Hapa mwandishi anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi.

Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema

Hapa "maneno" yana maana ya kwa yale waliokuwa wakisema. "Yakobo alisikia ya kwamba wana wa Labani wakisema"

Yakobo amechukuwa yote yaliyokuwa ya baba yetu

Wana wa Labani walikuza kwa sababu walikuwa na hasira. "Kila kitu ambacho Yakobo anacho ametoa kwa baba yetu"

Yakobo akaona mwonekano katika uso wa Labani. Akaona kwamba nia yake imebadilika

Sentensi hizi mbili zina maana moja. Ya pili inaelezea muonekano ambao Yakobo aliona kwa uso wa Labani. "Yakobo aligundua ya kwamba Labani hakufurahishwa naye tena"

baba zako

"baba yako Isaka na babu yako Abrahamu"

Genesis 31:4

Yakobo akatuma kuwaita Raheli na Lea uwanjani katika kundi lake la mifugo

"Yakobo akatuma kuwaita Raheli na Lea uwanjani katika kundi lake la mifugo"

katika kundi lake la mifugo naye akawambia

Hii inaweza kuwekwa kama sentensi mbili fupi. "katika mifugo yake. Akawaambia"

Naona nia ya baba yenu kwangu imebadilika

"Nimegundua baba yenu hafurahishwi na mimi tena"

mnajua kwamba ni kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu

Neno "mnajua" hapa lina maana ya wote Raheli na Lea. Pia linaongeza msisitizo. "Nyie wenyewe mnajua ya kwamba nimetumikia baba yenu kwa nguvu zangu zote"

Genesis 31:7

amenidanganya

"amenidanganya" au "hajanitendea haki"

ujira wangu

"alichosema atanilipa"

kunidhuru

Maana zaweza kuwa 1) kudhuru kwa mwili au 2) kusababisha Yakobo ateseke kwa namna yoyote.

Wanyama wenye mabaka

"Wanyama wenye madoa"

kondoo wote walipozaa

"mifugo wakazaa"

wenye milia

"Wanyama wenye milia"

Kwa njia hii Mungu amemnyang'anya mifugo baba yenu na kunipa mimi

"Hivi ndivyo Mungu aliwapatia wanyama wa baba yenu kwangu"

Genesis 31:10

Taarifa ya Jumla

Yakobo anaendelea simulizi yake kwa wake zake Lea na Raheli.

Wakati fulani wa majira ya kupandana

"Wakati wa msimu wa kupandana"

yaliyowapanda kundi

Hapa "kundi" ina maana ya mbuzi wa kike. "kupandana na mbuzi wa kike wa kundi"

yalikuwa ya milia, mabaka na madoa

"walikuwa na milia, madoa kidogo,na mabaka makubwa"

Malaika wa Mungu

Maana zaweza kuwa 1) Mungu mwenyewe alijitokeza kama mtu au 2) mmoja wa wajumbe wa Mungu alijitokeza. Kwa maana msemo haueleweki vizuri, ni vyema kutafsiri kama "malaika wa Mungu" kwa kutumia neno la kawaida linalotumika kwa "malaika".

Nikasema

"Na nikajibu"

Mimi hapa

"Ndio, ninasikiliza" au "Ndio, kuna nini?"

Genesis 31:12

Taarifa ya Jumla:

Malaika wa Bwana anaendelea kuzungumza na Yakobo.

Inua macho yako

Hii ni namna ya kusema "Tazama juu"

wanaolipanda kundi

Hapa "kundi" lina maana ya mbuzi wa kike. "ambao wanawapanda na mbuzi wa kike wa kundi"

Wana milia, madoa na na mabaka

"wana milia na madoa"

mahali ulipoitia nguzo mafuta

Yakobo alimwaga mafuta juu ya nguzo kuiweka wakfu kwa Mungu.

nchi uliyozaliwa

"nchi ambayo ulizaliwa"

Genesis 31:14

Raheli na Lea wakajibu na kumwambia

Hii haimaanishi walizungumza katika wakati mmoja. Inasisitiza ya kwamba walikubaliana wao kwa wao.

Je kuna sehemu yoyote au urithi wetu katika nyumba ya baba yetu?

Raheli na Lea wanatumia swali kusisitiza ya kwamba hakuna kitu kilichosalia kutoka kwa baba yao kuwapatia. "Hakuna kitu chochote kabisa kilichobaki kwa ajili yetu kurithi kutoka kwa baba yetu!"

Je hatutendei kama wageni?

Wanatumia swali kuonyesha hasira yao kuhusu jinsi baba yao anavyowatendea. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Baba yetu anatutendea kama wanawake wageni badala ya binti zake!"

Kwa maana ametuuza na kwa ujumla ametapanya pesa zetu. 16Mali zote

Hii inaweza kuwekwa kwa uwazi zaidi. "Ametuuza kwa manufaa yake mwenyewe"

na kwa ujumla ametapanya pesa zetu

Labani kutumia fedha yote ambayo alipaswa kuwapatia binti zake inazungumziwa kana kwamba alikuwa mnyama pori aliyekula fedha yote kana kwamba ilikuwa chakula. "alitumia fedha yetu yote"

na sasa ni zetu na watoto wetu

"inakuwa ya kwetu na watoto wetu"

Sasa basi

Hapa "sasa" haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

lolote Mungu alilokuambia, fanya

"fanya yote ambayo Mungu alikuambia kufanya"

Genesis 31:17

wanawe

Yakobo aliwachukua watoto wake wote. Inataja watoto wa kiume pekee kwa sababu walikuwa muhimu kama warithi wake.

Akawaongoza mifugo wake wote

"Akawaongoza mifugo wake wote" Hapa "mifugo" ina maana ya wanyama wake wote wa kufuga.

wakiwemo wanyama aliowapata huko Padani Aramu

"wakiwemo mifugo wengine ambao aliwachukua umiliki alipokuwa Padani Aramu"

Kisha akaenda kuelekea kwa Isaka baba yake katika nchi ya Kanaani

"Alienda katika nchi ya Kaanani, ambapo Isaka baba yake alikuwa akiishi"

Genesis 31:19

Labani alipokuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo wake

"Wakati Labani alipoondoka kukata manyoya ya kondoo"

mto

Hii ina maana ya mto wa Frati.

akaenda kuelekea

"kusafiri kuelekea"

vilima ya Gileadi

"milima ya Gileadi" au "Mlima Gileadi"

Genesis 31:22

Labani akaambiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "mtu mmoja akamwambia Labani"

Siku ya tatu

Ilikuwa utamaduni wa Kiyahudi kuhesabu siku ya kuanza safari kama siku ya kwanza. "Siku mbili baada ya kuondoka"

kwamba Yakobo amekimbia

Yakobo pekee ndiye anayetajwa kwa sababu ndiye kiongozi wa familia. Inaweza kuwekwa wazi ya kwamba familia yake ilikwenda naye. "ya kwamba Yakobo alitoroka na wake zake na watoto wake"

Hivyo akawachukua

"Kwa hiyo labani akachukua"

na kumfuatia

"na kumfukuza Yakobo"

kwa safari ya siku saba

Labani alitumia siku saba akitembea kumfikia Yakobo.

Akampita

"Alimfikia"

Genesis 31:24

Basi Mungu akaja kwa Labani Mwarami katika ndoto usiku

Neno "basi" linatumika kuweka alama kwa badiliko kutoka kwenye simulizi ya taarifa ya nyuma kuhusu Labani. "usiku huo Mungu alikuja kwa Labani ndotoni"

Ujiadhari kumwambia Yakobo jambo lolote liwe jema au baya

Msemo huu "jema au baya" unatumika pamoja kumaanisha "chochote". "Usiseme chochote kujaribu kumsimamisha Yakobo kuondoka"

Labani akampata Yakobo. Basi Yakobo alikuwa amepiga hema yake katika nchi ya vilima. Labani pia akapiga kambi pamoja na ndugu zake katika nchi ya kilima ya Gileadi

Neno "basi" inatumika hapa kuweka alama ya badiliko ya simulizi kwa taarifa ya nyuma kuhusu Yakobo na Labani. "Labani alipomfikia Yakobo, Yakobo aliweka hema lake katika nchi ya vilima. Kisha Labani na ndugu zake pia waliweka mahema katika nchi ya Gileadi.

Genesis 31:26

umewachukua binti zangu kama mateka wa vita

Labani anamzungumzia Yakobo kuchukua familia yake pamoja naye mpaka katika nchi ya Kaanani kana kwamba Yakobo aliwachukua mateka baada ya vita na anawalazimisha wao kuondoka nao. Labani anatia chumvi kwa sababu ana hasira na anajaribu kumfanya Yakobo asikie hatia kwa kile alichokifanya.

umekimbia kwa siri

"kukimbia kwa siri"

kwa sherehe

"kwa furaha"

kwa matari na vinubi

Vyombo hivi ni vya muziki. "na kwa muziki"

matari

chombo cha muziki chenye kichwa kama ngoma ambacho kinapigwa na kina vipande vya chuma kimekizunguka pembeni vyenye sauti pale chombo kikitikiswa.

niwabusu wajukuu wangu

Hapa "wajukuu" wanajumlisha wajukuu wote wakiume na kike. "kubusu wajukuu wangu"

Basi umefanya upumbavu

"umefanya upumbavu"

Basi

Hapa haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.

Genesis 31:29

Iko katika uwezo wangu kukudhuru

Neno "kukudhuru" ni wingi na una maana ya kila mmoja aliyekuwa na Yakobo. "Nina watu wa kutosha pamoja nami kuwadhuru nyote"

Jiadhari usimwambie Yakobo neno la heri wala shari

Maneno "heri au shari" yanatumika pamoja kumaanisha "chochote". "Usiseme chochote kujaribu kumzuia Yakobo kuondoka"

umeondoka

Hapa "umeondoka" ni umoja na ina maana ya Yakobo.

nyumba ya baba yako

Hapa "nyumba" ina maana ya familia. "kuwa nyumbani na baba yako na familia yako yote"

miungu yangu

"sanamu zangu"

Genesis 31:31

kwa sababu niliogopa na kudhani kuwa ungeninyang'anya binti zako kwa nguvu ndiyo maana nikaondoka kwa siri

"Niliondoka kwa siri kwa sababu niliogopa ya kwamba ungewachukua binti zako kutoka kwangu kwa lazima"

Yeyote aliyeiiba miungu yako hataendelea kuishi

Hii inaweza kuwekwa katika hali ya chanya. "Tutamuua yeyote aliyechukua miungu yako"

Mbele ya ndugu zetu

Neno "zetu" lina maana ya ndugu wa Yakobo na inajumuisha ndugu za Labani. Ndugu wote watatazama kuhakikisha kila kitu ni cha haki na kweli.

onesha chochote kilichochako nilichonacho na uchukue

"tafuta chochote tulichonacho ambacho ni chako na uchukue"

Kwa maana Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameviiba

Hii inabadilisha kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Yakobo.

Genesis 31:33

wajakazi wawili

Hii ina maana ya Zilfa ba Bilha.

hakuviona

"hakupata sanamu zake"

Genesis 31:34

Basi Raheli ... juu yake

Neno "basi" linatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Raheli.

tandiko

kiti kinachowekwa mgongoni mwa mnyama ili mtu aweze kukaa juu yake.

bwana wangu

Kumuita mtu "bwana wangu" ni njia ya kumheshimu.

siwezi kusimama mbele yako

"kwa sababu siwezi kusimama mbele zako"

kwani nipo katika kipindi changu

Hii ina maana ya kipindi cha mwezi ambapo mwanamke hutokwa na damu kutoka kwenye uzazi wake.

Genesis 31:36

Akamwambia

"Yakobo alimwambia Labani"

Kosa langu ni nini? Dhambi yangu ni ipi, hata ukanifuatia kwa ukali?

Misemo ya "Kosa langu ni nini" na "Dhambi yangu ni ipi" zina maana moja. Yakobo anamuuliza Labani amwambie ni kipi alichokosea. "Kosa langu ni lipi mpaka unifuate namna hii?"

ukanifuatia kwa ukali

Hapa neno la "ukali" ina maana ya Labani kumfukuza kwa haraka kwa lengo la kumkamata.

Umeona nini kati ya kitu chochote cha nyumbani mwako

"Umepata nini ambacho ni cha kwako?"

Viweke hapa mbele ya ndugu zetu

Hapa neno "zetu" ina maana ya ndugu wa Yakobo na inajumuisha ndugu wa Labani. "Laza chochote ulichokuta mbele ya ndugu zetu"

waamue kati yetu wawili

Hapa "yetu wawili" ina maana ya Yakobo na Labani. Msemo "waamue kati" ina maana ya kuamua mtu yupi yupo sahihi katika ugomvi huu. "wanaweza kuhukumu kati yetu"

Genesis 31:38

Taarifa ya Jumla:

Yakobo anaendelea kuzungumza na Labani.

miaka ishirini

"miaka 20"

Kondoo

kondoo wa kike

hawakutoa mimba

Hii ina maana ya kwamba hawajawa na mimba iliyokatishwa mapema na bila matarajio na mwanakondoo au mbuzi kuzaliwa amekufa.

Kilichoraruliwa na mnyama sikukuletea

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mnyama pori alipowaua mmoja wa wanyama wako sikukuletea kwako"

Badala yake, nilichukua upotevu huo

Kwa Yakobo kuhesabu wanyama wa Labani waliokufa kama hasara kutoka kwa mifugo wake inazungumzwa kana kwamba ilikuwa mzigo ambao angeubeba begani mwake. "badala ya kuhesabu hasara kutoka kwa mifugo yako, nimehesabu kama hasara kutoka kwa mifugo yangu"

Nilikuwepo wakati wote; mchana joto lilinipata, na baridi wakati wa usiku

Kuteseka wakati wa jua kali na halijoto chini inazungumzwa kana kwamba halijoto ilikuwa wanyama waliokuwa wakimla Yakobo. "Nilikaa na mifugo wako hata wakati wa joto kali la siku na wakati wa baridi wa usiku"

Genesis 31:41

Taarifa ya Jumla

Yakobo anaendelea kuzungumza na Labani.

Miaka hii ishirini

"Miaka hii 20 iliyopita"

miaka kumi na nne

"miaka 14"

Umebadili ujira wangu mara kumi

"amebadili kile alichosema angenilipa mara kumi"

Isipokuwa Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu, yule Isaka anayemwofu, amekuwa nami

Yakobo ana maana ya Mungu yule yule na sio kwa miungu watatu tofauti. "Kama Mungu wa Abrahamu, na Isaka, baba yangu, asingekuwa na mimi"

Mungu wa baba yangu

Hapa neno "baba" lina maana ya mzazi wake, Isaka.

yule Isaka anayemwofu

Hapa neno "anayemwofu" lina maana ya "hofu ya Yahwe" ambayo ina maana ya kumheshimu kwa ndani na kuonyesha heshima hiyo kwa kumtii yeye.

mikono mitupu

mikono Hii ina maana kutokuwa na kitu. "bila kitu chochote"

Mungu ameliona teso langu na jinsi nilivyofanya kazi kwa bidii

Nomino inayojitegemea "teso" inaweza kuwekwa kama "kuteswa". "Mungu ameona jinsi nilivyofanya kazi kwa bidii na jinsi ulivyonitesa"

Genesis 31:43

akini nitafanya nini leo kwa hawa binti zangu, au kwa watoto wao waliowazaa?

Labani anatumia swali kusisitiza ya kwamba hakuna awezalo kufanya. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Lakini hakuna kitu nachoweza kufanya kuwarudisha binti zangu na wajukuu wangu kwangu"

liwe shahidi

Hapa neno "shahidi" haimaanishi mtu, lakini linatumika kwa mfano na lina maana ya agano ambalo Yakobo na Labani walifanya. Agano linazungumzwa kana kwamba lilikuwa mtu ambaye alikuwa pale wakati walipokubaliana kufanya amani kati yao.

Genesis 31:45

nguzo

Hii ina maana ya kwamba jiwe kubwa liliwekwa mwishoni pake kuweka alama ya sehemu ambapo tukio hili la muhimu lilitokea.

kufanya rundo

"kuzipangilia juu ya nyenzake"

Kisha wakala pale kati ya lile rundo

Kula chakula pamoja ilikuwa sehemu ya kufanya agano baina yao. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi.

Yega Saha Dutha

"Jina la Yega Saha Dutha lina maana ya "fungu la mashahidi" kwa lugha ya Labani.

Galedi

"Jina la Galedi lina maana ya "fungu la mashahidi" kwa lugha ya Yakobo.

Genesis 31:48

Rundo hili ni shahidi kati yangu nawe leo

Mawe hayawi mashahidi halisi kwa ajili ya mtu. "Rundo hili litakuwa ukumbusho kati yangu na wewe"

Galedi

"Jina la Galedi lina maana ya "fungu la mashahidi" kwa lugha ya Yakobo.

Mispa

"Jina la Mispa lina maana ya "mnara".

tunapokuwa hatuonani

Hapa "nje ya macho" ina maana ya kutokuwa machoni pa mwenzako. "tutakapokuwa hatupo machoni mwetu sisi wawili"

japokuwa hakuna mwingine yupo nasi

Hapa "nasi" ina maana ya Labani na Yakobo. "hata kama hakuna mtu wa kutuona"

tazama

"kumbuka". Hii inaongeza msisitizo kwa kile kinachosemwa baadae.

Genesis 31:51

Rundo hili ni shahidi

Marundo haya ya mawe yalikuwa tendo ya kumbukumbu na alama ya mpaka kwa Yakobo na Labani kuhusu makubaliano yao ya amani. Yanazungumzwa kana kwamba ni mashahidi kama watu.

Mungu wa Ibrahimu, na mungu wa Nahori, miungu ya baba zao, waamue kati yetu

Abrahamu ni babu yake Yakobo. Nahori ni babu yake Labani. Baba wa Abrahamu na Nahori ni Tera. Sio wote walimuabudu Yahwe.

Hofu ya Isaka baba yake

Hapa neno "Hofu" lina maana ya Yahwe, ambaye Isaka alimheshimu kwa ndani na kuonyesha heshima hiyo kwa kumtii yeye.

Genesis 31:54

akawaita ndugu zake kula chakula

Kula chakula pamoja ilikuwa sehemu ya kufanya agano baina na mtu. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi.

asubuhi na mapema ... kurudi kwake

Mstari wa 55 ni mstari wa kwanza wa sura ya 32 katika maandishi ya asili ya Kihebrania, lakini mstari wa mwisho wa suraya 31 katika Biblia za sasa. Tunashauri kufuata hesabu ya Biblia ya lugha yako.

kuwabariki

Hii ina maana ya kuweka nia kwa mambo chanya na yenye manufaa yanayotokea kwa mtu.