Genesis 32

Genesis 32:1

Mahanaimu

"Jina la Mahanaimu lina maana ya "kambi mbili"

Genesis 32:3

Seiri

Hili ni eneo lenye milima katika eneo la Edomu.

Hivi ndivyo mtakavyosema kwa bwana wangu Esau: Hivi ndivyo mtumishi wako Yakobo asemavyo: 'Nimekuwa ... mbele zako

Hii ina nukuu ndani ya nukuu. Nukuu ya moja kwa moja inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Hivi ndivyo nataka ukamwambie bwana wangu Esau. Mwambie nimekuwa ... machoni pake."

bwana wangu Esau

Yakobo anatumia lugha ya upole na anamtaja kaka yake kama "bwana wangu".

mtumishi wakoYakobo

Yakobo anatumia lugha ya upole na anajiita mwenyewe kama "mtumishi wako".

ili kwamba nipate kibali mbele zako.

Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo ya mtu. "ili kwamba unithibitishe"

Genesis 32:6

watu mia nne

"wanamume 400"

alipoogopa

HIi ina maana ya hisia zisizo nzuri ambazo mtu anazo pale anapopata tishio la kudhuriwa kwake au wengine.

kutaabika

"tia wasiwasi" au "kutaabishwa"

kambi moja, ndipo kambi nyingine itakaposalimika

Hapa "kambi" ina maana ya watu. "kuwashambulia watu katika kambi moja, kisha watu wa kambi nyingine watatoroka"

Genesis 32:9

Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Yahwe

Hii haimanishi mungu wawili, lakini kwa Mungu mmoja wanaomuabudu wote. "Yahwe, ambaye ni Mungu wa babu yangu Abrahamu na baba yangu Isaka"

Yahwe, aliyeniambia, 'Rudi katika nchi yako na kwa jamaa yako, nami nitakustawisha

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isyo moja kwa moja. "Yahwe, wewe uliyesema ya kwamba nirudi katika nchi na kwa jamaa yangu, na kwamab utanifanikisha"

na kwa jamaa yako

"na kwa familia yako"

nitakustawisha

"Nitafanya mema kwako" au "Nitakutendea mema"

Mimi sistahili matendo yako yote ya agano la uaminifu na ustahilifu wote uliomfanyia mtumishi wako

Nomino zinazojitegemea "uaminifu" na "mkweli" inaweza kuwekwa kama "mwaminifu". "Sistahili wewe uwe mwaminifu kwa agano lako au kwako kuwa mwaminifu kwangu, mtumishi wako"

mtumishi wako

Hii ni njia ya upole ya kusema "mimi"

sasa nimekuwa matuo mawili

Hapa "nimekuwa" inamaana ya kile ambacho anacho sasa. "na sasa nina watu wa kutosha, mifugo, na mali kutengeneza kambi mbili"

Genesis 32:11

niokoe

"niokoe"

kutoka katika mikono ya ndugu yangu, mikono ya Esau

Hapa neno "mikono" ina maana ya nguvu. Misemo miwili ina maana moja. Msemo wa pili unaelezea ya kwamba kaka ambaye Yakobo alikusudia ni Esau. "kutoka kwa nguvu ya kaka yangu, Esau" au "kutoka kwa kaka yangu, Esau"

namwogopa, kwamba

"Ninaogopa ya kwamba"

Lakini ulisema, 'hakika nitakufanya ufanikiwe. Nitaufanya uzao wako ... hesabu.'

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Lakini ulisema ya kwamba utanitafanikisha, na kwamba utafanya uzao wangu .. hesabu"

nitakufanya ufanikiwe

"kufanya mema kwako" au "kukutendea mema"

Nitaufanya uzao wako kuwa kama mchanga wa bahari

Hii inazungumzia hesabu kubwa ya uzao wa yakobo kana kwamba hesabu yake itakuwa kama chembe za mchanga za pwani za baharini.

ambao hauwezi kuhesabika kwa hesabu yake

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambayo hakuna mtu awezaye kuhesabu kwa sababu ya hesabu yake"

Genesis 32:13

mia mbili

"200"

ishirini ... thelathini ... arobaini ... kumi

"20 ... 30 ... 40 ... 10"

na wana wao

"na watoto wao"

Akawaweka katika mikono ya watumishi wake, kila kundi peke yake.

Hapa "katika mikono" ina maana ya kutoa mamlaka juu yao. "Aliwagawa katika makundi madogo, na kuwapa kila mmoja wa watumishi wake mamlaka juu ya makundi"

mwache nafasi kati ya makundi ya wanyama

"na kila kundi lisafiri kwa umbali kutoka kwa kundi lingine"

Genesis 32:17

Akamwagiza

"Akamuamuru"

kukuuliza .... ambao wako mbele yenu?

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "kukuuliza bwana wako ni nani, unakwenda wapi, na nani anamiliki wanyama walio mbele yako"

ni wa nani?

"Bwana wako ni nani?"

wanyama hawa mbele yenu ni wa nani?

"Nani anamiliki wanyama hawa ambao wako mbele yako?"

Ndipo umwambie, 'Ni wa mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi wanaopelekwa kwa bwana wangu Esau. Na tazama, yeye pia anakuja nyuma yetu."

Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "Kisha ntataka kumwambia ya kwamba vitu vyote hivi ni vya Yakobo, mtumishi wake, na anampatia bwana wake, Esau. Na mwambie ya kwamba Yakobo yupo njiani kukutana naye"

mtumishi wako Yakobo

Yakobo anajifafanua kwa njia ya upole kama mtumishi wa Esau.

kwa bwana wangu Esau

Yakobo anajifafanua kwa Esau kwa njia ya upole kama bwana wake.

anakuja nyuma yetu

Hapa "yetu" ina maana ya mtumishi akizungumza na watumishi wengine kuleta mifugo kwa Esau.

Genesis 32:19

akatoa maelekezo kwa kundi la pili

"akaamuru kundi la pili"

Mnapaswa pia kusema, 'mtumwa wako Yakobo

Maana zaweza kuwa 1) "Utasema pia, 'Mtumishi wako Yakobo"' au 2) 'Utasema, "Pia, Mtumishi wako Yakobo"'.

nitamtuliza

"Nitamtuliza" au "Nitafanya hasira yake itoweke"

atanipokea

"atanikaribisha kwa upole"

Hivyo zawadi zikatangulia mbele yake

Hapa "zawadi" ina maana ya watumishi kupeleka zawadi zile.

Yeye mwenyewe akakaa

Hapa "mwenyewe" inasisitiza ya kwamba yakobo hakuwenda pamoja na watumishi wake.

Genesis 32:22

wajakazi wake wawili

"watumishi wake wawili wake zake". Hii ina maana ya Zilpa na Bilha.

kijito

sehemu ya kina kifupi ya mto ambayo ni rahisi kuvuka.

Yaboki

Hili ni jina la mto.

mali yake yote

"kila kitu alichokuwa nacho"

Genesis 32:24

mpaka alfajiri

"mpaka alfajiri"

nyonga

"kiungo cha paja". Hii ni sehemu ambapo mfupa wa juu wa mguu unaungana na nyonga.

Nyonga ya Yakobo ikatenguka alipokuwa akishindana naye

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mwanamume alijeruhi nyonga ya Yakobo aliposhindana naye"

kwani kunakucha

"jua litachomoza hivi karibuni"

umenibariki

Hapa "umenibariki" ina maana ya kutamka baraka maalumu juu ya mtu na kusababisha mambo mazuri kutokea kwa huyo mtu.

sitakuacha uende mpaka uwe umenibariki

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya chanya. "Haiwezekani! Lazima unibariki kwanza, ndipo nitakuacha uondoke"

Genesis 32:27

Israeli

"Jina la Israeli lina maana ya 'Anayeshindana na Mungu'"

na wanadamu

Hapa "wanadamu" ina maana ya "watu" kwa ujumla.

Genesis 32:29

Akasema, "Kwa nini kuniuliza jina langu?"

Akasema, "Kwa nini kuniuliza jina langu?" Swali hili la balagha lilitakiwa kushtua, kukaripia na kumfanya Yakobo awaze juu ya kilichotokea kati yake na mtu mwingine aliyeshindana naye. "Usiniulize jina langu!"

Penieli

"Jina la Penieli lina maana ya "uso wa Mungu".

uso kwa uso

Kuwa "uso kwa uso" ina maana ya watu wawili kutazamana ana kwa ana, kwa umbali mfupi.

na maisha yangu yamesalimika

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "na bado akasalimisha maisha yangu"

Genesis 32:31

Ndiyo maana wana hadi siku ya leo

Hii inafanya mabadiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu vizazi vya Israeli.

hadi siku ya leo

Hii ina maana siku ambayo mwandishi alikuwa akiandika hivi.

kano za nyonga

Hii ina maana ya msuri unaonganisha mfupa wa paja na kiungo cha paja.

kiungo cha nyonga

"kiungo cha paja"

alipotegua

"alipokuwa akipiga"