1
Kisha maamiri wote wa jeshi na Yohanani mwana wa Karea, Jezania mwana wa Hoshaia, na watu wote kutoka mdogo hadi mkubwa walimkaribia Yeremia nabii.
2
Walisema naye, "Acha maombi yetu yaje mbele yako. Omba kwa ajili yetu kwa Yahwe Mungu wako kwa ajili ya watu hawa ambao wanabaki kwani tuko wachache katika idadi, kama unavyoona.
3
Muulize Yahwe Mungu wako atuambie sisi njia itupasayo kwenda na yapi yatupasayo kutenda."
4
Basi Yeremia nabii alisema nao, "Nimewasikia, Tazama, Nitaomba kwa Yahwe Mungu wenu kama mlivyoomba. Vyovyote Yahwe atavyonijibu, Nitawambia. Sitawaficha chochote ninyi."
5
Walisema na Yeremia, "Na Yahwe awe shahidi mkweli na mwaminifu dhidi yenu, kama hatutafanya kila kitu ambacho Yahwe Mungu wenu atwambia kufanya.
6
Hata kama ni vizuri au vibaya, tutatii sauti ya Yahwe Mungu wetu, ambaye tunawatuma ninyi, ili kwamba iwe vizuri pamoja nasi wakati tunatii sauti ya Yahwe Mungu wetu."
7
Basi ilitokea kwamba baada ya siku kumi, neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia.
8
Kwa hiyo Yeremia alimwita Yohanani mwana wa Karea na maamiri wote wa jeshi pamoja naye, na watu wote kutoka mdogo hata mkubwa.
9
Ndipo alisema nao, "Hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli-- ambaye mmenituma kwake ili niweze kuweka maombi yenu mbele zake--asema,
10
kama mtarudi na kuishi katika nchi hii, basi nitawajenga na sitawararua chini; Nitapanda na sitawang'oa, kwa kuwa nitageuza maafa ambayo nimeleta juu yenu.
11
Msimugope mfalme wa Babeli, ambaye mnamuogopa. Msimuogope--hili ni tamko la Yahwe--kwani niko pamoja nanyi kuwahifadhi na kuwaokoa toka mkononi mwake.
12
Kwa kuwa nitawapa rehema. Nitakuwa na huruma juu yenu, na nitawarudisha kwenye nchi yenu.
13
Lakini tudhani kwamba umesema, "Hatutakaa katika nchi hii"-- kama hamtasikiliza sauti yangu, sauti ya Yahwe Mungu wenu.
14
Tudhani kwamba mnasema, "Hapana! Tutaenda katika nchi ya Misri, ambayo hatutaona vita yoyote, ambayo hatutasikia sauti ya tarumbeta, na hatutaona njaa ya chakula. Tutaishi huko."
15
Sasa sikiliza neno hili la Yahwe, wewe mabaki ya Yuda. Yahwe Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, 'Kama kweli mtatoka kwenda Misri, kwenda na kuishi huko,
16
basi upanga ambao mnauogopa utawapitia huko kwenye nchi ya Misri. Njaa ambayo mnawasiwasi nayo itawafatilia huko Misri. Na mtakufa huko.
17
Basi itatokea kwamba wanaume wote waliondoka kwenda Misri kuishi huko watakufa kwa upanga, njaa, au pigo. Hapatakuwa na mwathirika wao, hakuna atakayetoroka maafa ambayo nitaleta juu yao.
18
Kwa kuwa Yahwe Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Kama gadhabu yangu na hasira yangu imemwagwa juu ya wakazi wa Yerusalemu, kwa njia hiyo hasira yangu itamwagwa juu yenu kama mtaenda Misri. Mtakuwa sababu ya hasira na hofu, sababu la kuzungumza laana, na kitu kisichokuwa na heshima. Na hamtaona eneo hili tena."
19
Basi Yeremia alisema, "Yahwe amezungumza kuhusu ninyi--mabaki ya Yuda. Msiende Misri! Unajua kwa hakika kwamba nimekuwa shahidi dhidi yenu leo.
20
Kwa kuwa mmejidanganya vibaya wenyewe wakati mliponituma mimi kwenda kwa Yahwe Mungu wenu na kusema, 'Omba kwa Yahwe Mungu wetu kwa ajili yetu. Kila kitu ambacho Yahwe Mungu wetu asema, tuambie, na tutaibeba.'
21
Kwa kuwa nimekwisha toa taarifa kwako leo, lakini hujasikiliza sauti ya Yahwe Mungu wenu au kwa chochote kuhusu ambacho alinituma mimi kwako.
22
Basi sasa, utajua kwa hakika kwamba utakufa kwa upanga, njaa, na pigo katika eneo ambalo ulitamani kwenda kuishi."