1
Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, toka familia ya kifalme, na maafisa baadhi wa mfalme, walikuja --wanaume kumi walikuwa pamoja naye -- kwa Gedalia mwana wa Ahikam, huko Mizpa. Walikula chakula pamoja huko Mizpa.
2
Lakini Ishmaeli mwana wa Nethania, na wanaume kumi ambao walikuwa pamoja naye waliinuka na kumvamia Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, kwa upanga. Ishmaeli alimuua Gedalia, ambaye mfalme wa Babeli alimweka kuwa msimamizi wa nchi.
3
Kisha Ishmaeli akawauwa Wayahudi wote ambao walikuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na Wakaldayo wanaume wa kupigana kukutwa hapo.
4
Kisha ilikuwa siku ya pili baada ya kumuua Gedila, lakini hakuna mmoja aliyefahamu.
5
Wanaume baadhi walikuja toka Shekemu, toka Shilo, na toka Samaria--wanaume themanini ambao walikuwa wamenyoa ndevu zao, walirarua nguo zao, na kujikata wenyewe-- pamoja na chakula cha sadaka na ubani katika mikono yao kwenda kwa nyumba ya Yahwe.
6
Basi Ishmaeli mwana wa Nethania alienda toka Mizpa kukutana nao kama walivyoenda, wakitembea na kulia. Kisha ilitokea kwamba kama alivyokutana nao, alisema nao, "Njoo kwa Gedalia mwana wa Ahikamu!"
7
Ilikuja kuwa kwamba wakati walipokuja katika mji, Ishmaeli mwana wa Nethania aliwauwa na kuwatupa kwenye shimo, yeye na wanaume ambao walikuwa pamoja naye.
8
Lakini palikuwa na wanaume kumi miongoni mwao ambao walisema kwa Ishmael, " Usituue, kwa kuwa kuna riziki zetu kwenye shamba: ngano na shayiri, mafuta na asali" Kwa hiyo hakuwauwa pamoja na rafiki zao wengine.
9
Kisima ambacho Ishmaeli alitupia miili yote ya waliokufa ambao yeye na Gedalia waliwapiga, kilikuwa ni kilekile ambacho mfalme Asa alichimba wakati alipokuwa akivamiwa na mfalme Baasha wa Israel. Ishmaeli mwana wa Nethania alilijaza wale ambao walikuwa wameuawa.
10
Kisha Ishmaeli aliwashika watu wengine wote ambao walikuwa huko Mizpa, mabinti wa mfalme na watu wote ambao walikuwa wameachwa huko Mizpa ambayo Nebuzaradani mlinzi mkuu alikuwa amewakabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu. Basi Ishmaeli mwana wa Nethania aliwashika na kuvuka kwa watu wa Amoni.
11
Lakini Yohanani mwana wa Karea na maamiri wote wa jeshi pamoja naye walisikia madhara yote ambayo Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amefanya.
12
Basi waliwachukua wanaume wao na kwenda kupigana dhidi ya Ishmaeli mwana wa Nethania. Walipigana naye huko kwenye bwawa kuu la Gibeoni.
13
Kisha ilitokea kwamba wakati watu wote ambao walikuwa na Ishmaeli kumuona Yohanani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi ambao walikuwa pamoja naye, walikuwa na furaha.
14
Basi watu wote ambao Ishmael alikuwa amewashika huko Mizpa waligeuka na kwenda kwa Yohanani mwana wa Karea.
15
Lakini Ishmaeli mwana wa Nethania alitoroka na wanaume nane toka kwa Yonathani. Alienda kwa watu wa Ammoni.
16
Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa jeshi pamoja naye walichukua toka Mizpa watu wote ambao walikuwa wameokolewa kutoka kwa Ishmaeli mwana wa Nethania. Hii ilikuwa baada ya Ishmaeli kuwa amemuuwa Gedalia mwana wa Ahikamu. Yohanani na rafiki zake walichukua wanaume shujaa, wanaume wapiganaji, wanawake na watoto, na matoashi ambao alikuwa wameokolewa huko Gibeoni.
17
Kisha walienda na kubaki kwa muda huko Geruthi Kimhamu, ambayo iko karibu na a Bethlehemu. Walikuwa wakienda Misri
18
kwa sababu ya Wakalidayo. Walikuwa wakiwaogopa kwani Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amemuua Gedalia mwana wa Ahikamu, ambaye mfamle wa Babeli amewekwa kwenye usimamizi wa nchi.