Sura 1

1 Katika mwaka wa pili wa mfalme Dario, katika mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la JJehova lilikuja kwa mkono wa nabii Haghai kwenda kwa gavana wa Yuda, Zerubabeli mwana wa Sheatieli, na kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki, kusema, 2 "Bwana wa Majeshi asema: 'Hawa watu husema, "Si wakati wetu kuja au kujenga nyumba ya Jehova.""" 3 Tena neno la Bwana lilikuja kwa mkono wa nabii Haghai kusema, 4 "Je ni wakati kwenu wenyewe kuishi katika nyumba zilizokamilika, na wakati nyumba hii inaharibika? 5 Kwa hivyo sasa Bwana wa Majeshi asema hivi: 'zitafakarini njia zenu! 6 Mmepanda mbengu nyingi, lakini mkaleta mavuno kidogo; mnakula lakini hamshibi, mnakunywa lakini hamukulewa na vinywaji. Mnavaa nguo lakini hampati joto wenyewe, na mtu wa mshahara hupata pesa na kuziweka kwenye mfuko ulio na mashimo tu!' 7 Bwana wa Majeshi asema haya: 'Zitafakarini njia zenu! 8 Pandeni milimani, mkalete mbao, na mjenge nyumba yangu; ndipo nitaifurahia na nitatukuzwa!' Asema Bwana. 9 'Mmetazamia kupata vingi, lakini tazama! mmeleta nyumbani vichache, kwa kuwa nilivipulizia mbali! Kwa nini?'- Hivi ndivyo asemavyo Bwana wa Majeshi! Kwa sababu nyumba yangu inakaa kwenye uharibifu, lakini kila mtu yuko radhi kwenye nyumba yake. 10 Kwa sababu ya hii mbingu zimeshikiliwa zisitoe umande kwako, na ardhi imeshikilia mazao yake. 11 Nimeagiza ukame juu ya ardhi na juu ya milima, juu ya nafaka na juu ya divayi mpya, juu ya mafuta na juu ya mavuno ya ardhi, juu ya watu na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono yenu. 12 Kisha Zerubabeli mwana wa Shelitieli, na kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehozadaki, pamoja na mabaki ya watu, wakatii sauti ya Bwana Mungu wao, na maneno ya nabii Hagai, kwa sababu Bwana Mungu wao alikuwa amemtuma na watu wakaogopa uso wa Bwana. 13 Ndipo Hagai, mjumbe wa Bwana, akaongea ujumbe wa Bwana kwa watu na kusema,"'Niko pamoja na nanyi!'- Hivi ndivyo asema Bwana! 14 Bwana alitibua roho ya mkuu wa mkoa wa Yudah, Zerubabeli mwana wa Sheltieli, na roho ya kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki, na roho ya masalia ya watu, kwa kiasi kwamba wakaenda kufanya kazi katika nyumba ya Bwana Mungu wa majeshi, Mungu wao. 15 katika siku ya ishirini na Mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario.