Sura 2

1 Katika Mwezi wa saba siku ya ishirini na moja ya mwezi, neno la Bwana lilikuja kwa mkono wa nabii Hagai, na kusema, 2 "Ongea na mkuu wa mkoa wa Yudah, Zerubabeli mwana wa Sheltieli, na kwa kuhani mkuu Yehozadaki; na kwa masalia ya watu. Sema, 3 Ni nani aliyebaki kati yenu aliyeuona utukufu wa nyumba hii iliyokuwa ya kwanza? Na mnaionaje kwa sasa? Je si kama si chochote machoni penu? 4 Sasa, muwe hodari, Zerubabeli' -hivi ndivyo asema Bwana - na uwe hodari, kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki; muwe hodari, enyi watu wa nchi! - hivi ndivyo asema Bwana - na mfanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi! Hivi ndivyo asema Bwana wa majeshi. 5 Na hii ndiyo agano niliyoiweka na nyinyi mlipokua mukitoka Misri, na Roho yangu anasimama katikati yenu. Msiwe na hofu! 6 Kwa kuwa Bwana wa majeshi anasema haya: 'kitambo kidogo kwa mara nyingine nitatikisa mbingu na dunia, bahari na nchi kavu! 7 Na nitalitikisa kila taifa, na kila taifa litaleta vitu vyao vya thamani kwangu, na nitaijaza nyumba hii na utukufu, asema Bwana wa Majeshi 8 Dhahabu na fedha ni yangu! - hivi ndivyo asema Bwana wa majeshi. 9 Utukufu wa nyumba hii utakuwa mkubwa siku zijazo kuliko utukufu wa nyumba ya kwanza, asema Bwana wa majeshi, na nitawapa amani mahali hapa! - hivi ndivyo asema Bwana wa majeshi." 10 Katika siku ya ishirini na nne mwezi wa tisa, mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Bwana lilimjia nabii Hagai na kusema, 11 "Bwana wa majeshi asema hivi: Muulizeni kuhani kuhusu sheria, na useme: 12 Kama mtu atabeba nyama iliyotolewa kwa Bwana katika pindo la vazi lake, kama upindo utagusa mkate au mchuzi, mvinyo au mafuta, au chakula kingine, je chakula hicho kinafanyika kitakatifu?" Kuhani alijibu akasema, "Hapana" 13 Halafu Hagai akasema. "Kama mtu najisi kwa ajili ya kumgusa maiti na kugusa vitu hivi, vyote vinaweza kuwa najisi?" Kuhani akajibu na kusema, "Ndiyo, vitakuwa najisi." 14 Kwa hiyo Haghai akajibu nakusema, "Ni pamoja na hawa watu na pamoja na taifa liliko mbele yangu! - haya anayasema Bwana- na pia kila kitu kimekwisha kwa mkono wake: walichotoa hakikuwa kisafi kilikuwa kichafu. 15 Kwa hiyo sasa, fikiria katika mawazo yenu kuhusu yaliyipita kabla siku hii ya leo. Kabla hata jiwe halijawekwa kwenye jiwe lingine katika hekalu la Bwana, 16 Ilikuwaje basi? Kila mtu alipokuja kwenye vipimo ishirini vya nafaka, kumbe kulikuwa na vipimo kumi tu: na aliyekuja na aliyekuja kuchota divai ya vipimo hamsini, kumbe kuliwa na vipimo ishirini tu. 17 Niliwataabisha ninyi na kazi za mikono yenu kwa doa na koga, na likini hamkunirudia'- asema Bwana. 18 tafakari siku hii ya leo na kuendelea, kutoka siku ya ishirini na nne katika mwezi wa tisa, toka siku ile msingi wa hekalu la Bwana uliwekwa. Tafakarini hilo! 19 Je, bado kuna mbegu katika ghala? Mzabibu, mti wa mtini, komamanga, na mti wa mzeituni havikuzaa matunda! lakini kutoka siku hii ya leo nitawabariki!"' 20 Tena neno la Bwana likaja kwa mara ya pili kwa Haghai siku ya ishiri na nne katika mwezi kusema, 21 "Sema na mkuu wa mkoa wa Yuda, Zerubabeli umwambie, 'Nitatikisa mbingu na dunia. 22 kwa hiyo nitaanhusha kiti cha falme na kuharibu nguvu ya falme za mataifa! nitaangusha magahari na wapandao; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa sababu ya upanga wa ndugu zake. 23 Siku hiyo '-hivi ndivyo asema Bwana wa Majeshi- 'Nitakuchukua wewe Zerubabeli mwana wa Sheltieli, kama mtumishi wangu!- hivi ndivyo Bwana anavyosema. "Nitakutumia kama pete ya muhuri wangu, kwa sababu mimi nimekuchagua!- asema Bwana wa majeshi!"