Sura 3

1 Maombi ya Habakuki nabii: 2 Yahwe, nimesikia habari zako, na mimi naogopa.Yahwe ,fufua kazi yako katikati ya nyakati hizi; katikati ya miaka hii fanya ijulikane; kumbuka kuwa na rehema katika ghadhabu yako. 3 Mungu alikuja kutoka Temani, na yule Mtakatifu kutoka Parani. Sela Utukufu wake umezifunika mbingu, na dunia ilikuwa imejaa sifa zake. 4 Na mng'ao kama mwanga,mionzi miwili ilimulika kutoka mkononi mwake; ambapo uweza wake ulifichwa. 5 Ugonjwa wa kufisha ulitangulia mbele yake, na tauni ilitoka miguuni pake. 6 Yeye alisimama na akaipima nchi; aliangalia na akayatikisa mataifa. Hata milima ya milele ikatawanyika, na vilima vya kale vikainama. Njia yake ni ya kale. 7 Niliona hema za Wakushi katika mateso, na vitambaa vya hema za nchi ya Midiani vinatetemeka. 8 Yahwe alikasirika pale mitoni? Ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya mito, au hasira yako dhidi ya bahari, unapopanda juu ya farasi na magari yako ya ushindi? 9 Umeleta upinde wako bila mfuniko; unaweka mishale kwenye upinde wako! Sela Uliigawa nchi na mito. 10 Milima ilikuona wewe na kugeuka kwa uchungu.Gharika ya maji ikapita juu yao; vilindi vikapaza sauti. vikainua juu mikono yake. 11 Jua na mwezi vilisimama imara juu mahali pake katika mwanga wa mishale yako ilipopaa, kwa mwanga wa mkuki wako umeremetao. 12 Umetembea juu ya nchi kwa hasira. Katika ghadhabu umewapura mataifa. 13 Ulikwenda nje kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa mteule wako. Wewe huponda kichwa cha nyumba ya mwovu kuweka wazi kutoka kwa msingi mpaka kwa shingo. Sela 14 Umekichoma kichwa cha mashujaa wake kwa mishale yake mwenyewe sababu walikuja kama mawimbi kututawanya; wivu wao ulikuwa kama mtu anayemwangamiza maskini mafichoni. 15 Umekanyaga juu ya bahari kwa farasi wako, na kuyarundika maji makuu. 16 Nilisikia, viungo vyangu vya ndani vilitetemeka! midomo yangu ilitetemeka kwa sauti ile.Uozo unakuja katika mifupa yangu, na chini yangu natetemeka nikisubiri kwa kimya siku ya dhiki iwajilie watu waliotushambulia. 17 Ingawa mtini hautachanua na hakuna mazao kutoka kwa mizabibu; ingawaje mazao ya mti wa mzaituni inakatisha tamaa na mashamba hayatoi chakula; iwapo kundi la mifugo limekatwa kutoka kwa kibanda na hakuna ng'ombe katika zizi, hiki ndicho nitakacho kifanya. 18 Bado, nitafurahia katika Bwana. Nitashangilia kwa sababu ya Mungu wa wokovu wangu. 19 Bwana Yahwe ni nguvu yangu na huifanya miguu yangu kama ya kulungu. Ananifanya niende mbele mahali pangu pa juu. - Kwa mwelekezi wa muziki, kwa vyombo vyangu vya nyuzi.