Sura 2

1 1Nitasimama kwenye nguzo ya ulinzi na kujiweka juu ya mnara,na nitazame nione atakaloniambia na nione vile nitakavyotoka kwa lalamiko langu. 2 Yahwe alinijibu na alisema, "Rekodi maono haya, na uandike dhahiri juu ya kibao ili kwamba anayesoma anaweza kukimbia. 3 Sababu maono haya bado ni kwa wakati ulioamriwa na yatashuhudia na hayatakosea.Ingawa yanakawia, yasubiri. Sababu kwa hakika itatimia na haitachelewa. 5 4 Tazama!yule ambaye hamu zake si haki ndani yake ni mwenye majivuno.lakini mwenye haki ataishi kwa imani. 5Kwa kweli,kama vile mvinyo ni mdanganyifu,hata hivyo mtu mwenye kiburi hakai nyumbani.Amefanya koo lake lipanuke kama kuzimu;na kama kifo,hatosheki.Ameyakusanya pamoja mataifa, na kujiwekea watu wote kwake. 6 Hawatachukua hawa wote methali na dhihaka, mafumbo kumhusu, wakisema ,'Ole wake yule aongezaye visivyo vya kwake! Ni kwa muda gani utaongeza uzito wa dhamana uliyochukua?' 7 Je hao wanaokuuma hawatainuka ghafla, na hao wanaokutisha kuamka? Utakuwa mwathirika kwa ajili yao. 8 Kwa sababu umeteka nyara watu wengi, mabaki yote ya watu yatakuteka nyara. Sababu umemwaga damu ya binadamu na umeitendea nchi udhalimu, miji, na wote wanaokaa ndani yake. 9 Ole kwa yule anayepata mapato maovu kwa ajili ya nyumba yake, hivyo apate kukiweka kiota chake juu ili apate kujiepusha na mkono wa uovu.' 10 Umebuni aibu kwa nyumba yako kwa kukatilia mbali watu wengi, na umefanya dhambi dhidi ya maisha yako. 11 Sababu mawe yatapasa sauti kutoka ukutani, na pao la mbao litawajibu, 12 'Ole wake yule ajengaye mji kwa damu, na anayeimarisha mji kwa uovu. 13 Haikutoka kwa Bwana wa majeshi kwamba watu wafanye kazi kwa ajili ya moto ,na mataifa yanajichosha yenyewe bure? 14 Bado nchi itajazwa na maarifa ya utukufu wa Bwana kama maji yaifunikavyo bahari. 15 'Ole wake yule anayelazimisha majirani wake kulewa _unaonyesha hasira yako na kuwafanya walewe ili uweze kutazama uchi wao.' 16 Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako!Kunywa, na utafichua govi lako ambalo halijatahiriwa! Kikombe cha mkono wa kuume wa Bwana kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako. 17 Udhalimu uliotendewa Lebanoni utakufunikiza na uharibifu wa wanyama utakuogopesha. Sababu umemwaga damu ya mtu na umei tendea nchi udhalimu, miji, na wote wanaokaa humo. 18 Ni faida gani iliyoko kwa sanamu ya kuchongwa? Sababu yule aliyeichonga hiyo!Au kinyago cha kuyeyuka, mwalimu wa uongo?Sababu aliyetengeneza hutumaini kile ametengeneza anapozifanya sanamu zisizo na faida. 19 'Ole kwa yule auambiaye ubao, Amka! Au kwa jiwe lisilo na uhai, Inuka!' Vitu hivi vinafundisha? Angalia, hiki juu kimefunikwa kwa dhahabu na fedha, lakini ndani yake hakina pumzi kabisa. 20 Lakini Bwana yumo katika hekalu lake takatifu! Nchi yote iwe kimya mbele zake.