Sura 24

1 Baada ya siku tano, Anania kuhani mkuu, baadhi ya wazee na msemaji mmoja aitwaye Tertulo, wakaenda pale. Watu hawa wameleta mashtaka dhidi ya Paulo kwa gavana. 2 Paulo alipo simama mbele ya gavana, Tertulo akaanza kumshitaki na kusema kwa gavana, "kwa sababu yako tuna amani kuu; na kwa maono yako yanaleta mageuzi mazuri katika taifa letu; 3 basi kwa shukurani yote tunapokea kila kitu ukifanyacho,Mheshimiwa Felix. 4 Lakini nisikuchoshe zaidi, nakusihi kkwa fadhili zako utusikilize kwa ufupi. 5 Kwa maana tumempata mtu huyu mkorofi, na anasababisha Wayahudi wote kuasi duniani. Tena ni kiongozi wa madhehebu ya Wanazorayo. (Zingatia: Sehemu ya maneno ya mstari huu 24: 6 6 Na tena alijaribu kulitia hekalu unajisi hivyo tukamkamata., haumo kwenye nakala bora za kale). (Zingatia: Mstari huu 7 Lisiasi, afisa, alikuja na akamchukua kwa nguvu mikononi mwetu., haumo kwenye nakala bora za maandiko ya kale). 8 Ukimchunguza Paulo kuhusu mambo haya, hata utaweza kujifunza ni kitu gani tumemshtakia." 9 Wayahudi nao wakamshtaki Paulo, wakisema kwamba haya mambo yalikuwa kweli. 10 Liwali alipompungia mkono ili Paulo aongee, Paulo alijibu, "Ninajua ya kwamba kwa miaka mingi umekua mwamuzi wa taifa hili, na nina furaha kujieleza mwenyewe kwako. 11 Waweza kuhakikisha kuwa hazijapita siku zaidi ya kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda kuabudu Yerusalemu. 12 Na waliponikuta katika hekalu, sikubishana na mtu yeyote, na sikufanya fujo katika mkutano, wala katika masinagogi wala ndani ya mji; 13 na wala hawawezi kuthibitisha kwako mashitaka wanayoyashitaki dhidi yangu. 14 Ila nakiri hili kwako, ya kwamba kwa njia ile ambayo wanaiita dhehebu, kwa njia iyo hiyo ninamtumikia Mungu wa baba zetu, nikiamini mambo yote kulingana na maandiko ya manabii. 15 Nina matumaini yaleyale kwa Mungu ambayo hata hao pia wanayo, kwamba kutakuja ufufuo wa wote wenye haki na wasio na haki pia; 16 na kwa hili, ninajitahidi ili niwe na dhamira isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu. 17 Sasa Baada ya miaka mingi nilikuja kuleta msaada kwa taifa langu na zawadi ya fedha. 18 Nilipofanya hivi, Wayahudi fulani wa Asia wakanikuta ndani ya sherehe ya utakaso ndani ya hekalu, bila kundi la watu wala ghasia. 19 Watu hawa ambao imewapasa kuwapo mbele yako sasa hivi na waseme kile walichonacho juu yangu kama wana neno lo lote. 20 Au watu hawa wenyewe na waseme ni kosa gani jingine waliloliona kwangu niliposimama mbele ya baraza la kiyahudi, 21 isipokuwa ni kwa ajili ya kitu hiki kimoja nilichokisema kwa sauti niliposimama katikati yao, ' ni kuhusu ufufuo wa wafu ambao kwa huo niko hukumuni mbele yenu leo ."' 22 Ndipo Feliki ambaye alikuwa na uelewa mzuri kuhusu Njia, na akauahirisha mkutano. Akasema, "Lisia jemedari atakapokuja chini kutoka Yerusalemu nitatoa maamuzi dhidi ya mashitaka yenu." 23 Ndipo akamwamuru akida amlinde Paulo, ila awe na uhuru kiasi kwamba na hatakuwepo mtu wakuwakataza rafiki zake kumhudumia kwa mahitaji yake. 24 Baada ya siku kadhaa, Feliki akarudi na Drusila mkewe aliyekuwa Myahudi, akatuma kumwita Paulo na akasikiliza toka kwake habari za imani ndani ya Kristo Yesu. 25 Ila Paulo alipokuwa akijadiliana naye kuhusu haki, kuwa na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akapata hofu akajibu, "nenda mbali kwa sasa, ila nikipata muda tena, nitakuita." 26 Muda uo huo, alitumai Paulo atampa fedha kwa hiyo alimwita mara nyingi akaongea naye. 27 Ila miaka miwili ilipopita, Porkio Festo akawa Liwali baada ya Feliki, ila Feliki alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, hivyo akamwacha Paulo chini ya uangalizi.