2 Mambo Ya Nyakati Sura 6

1 Kisha Sulemani akasema, "Yahwe alisema kwamba ataishi katika giza nene, 2 lakini nimekujengea makao makuu, sehemu kwa ajili yako ya kuishi milele." 3 Kisha mfalme akageuka nyuma na kuwabariki kusanyiko lote la Israeli, wakati kusanyiko lote la Israeli walikuwa wamesimama. 4 Akasema, "Yahwe, Mungu wa Israeli, usifiwe, uliyesema na Daudi baba yangu, na ametimiza kwa mikono yake mwenyewe, akisema. 5 'Tangu siku nilipowaleta watu wanagu nje ya nchi ya Misiri, sikuchagua mji wowote nje ya makabila yote ya Israeli ambamo nyumba ingejengwa, ili jina langu liwe humo. Wala sikuchagua mtu yeyote kuwa mfalme juu ya watu wangu Israeli. 6 Aidha, nimechagua Yeruselemu, ili kwamba jina langu liwe humo, na nimemchagua Daudi kuwa juu ya watu wanagu Israeli. ' 7 Sasa ilikuwa ndani ya moyo wa Daudi baba yangu, kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli. 8 Lakini Yahwe alisema kwa Daudi Baba yangu. 'Kwamba ilikuwa ndani ya moyo wako kujenga nyumba kwa ajili ya jina langu, ulifanya vizuri kwa hili kuliweka moyoni mwako. 9 Aidha, hutaijenga ile nyumba, badala yake, mwanao, mmoja atakayetoka kwenye viuno vyako, ataijenga nyumba kwa ajili ya jina langu.' 10 Yahwe ameyatimiza maneno aliyokuwa amesema, kwa maana nimeiinua sehemu ya Daudi baba yangu, na nitakaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, kama alivyoahidi Yahwe. Nimeijenga nyumba kwa ajii ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli. 11 Nimeliweka humo sanduku, ambamo kuna agano la Yahwe, alilofanya na watu wa Israeli." 12 Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya Yahwe mbele za kusanyiko lote la Israeli, na akanyosha mikono yake. 13 Kwa maana alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, lenye urefu wa mikono mitano, upana wa mikono mitano, urefu wake kwenda juu mikono mitatu. Alikuwa ameliweka katikati ya uwanja. Akasimama juu yake na kupiga magoti mbele ya kusanyiko la Israeli, kisha akanyosha mikono yake kuzielekea mbingu. 14 Akasema, "Yahwe, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe katika mbingu, au juu ya dunia, ambaye anatunza agano na upendo imara na watumishi wako ambao hutembea mbele zako kwa moyo wao wote; 15 wewe uliyemtimizia Daudi baba yangu, uliyokuwa umemwahidi. Ndiyo, ulisema kwa kinywa chako na umetimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo. 16 Sasa, Yahwe, Mungu wa Israeli, tunza ahadi uliyoahidi kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, uliposema, 'Hautashindwa kupata mtu mbele yangu wa kukaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, ikiwa tu uzao wako ni waangalifu kutembea katika sheria zangu, kama wewe ulivyotembea mbele zangu. 17 Sasa, Mungu wa Israeli, ninaomba kwamba ahadi uliyofanya kwa mtumishi wako Daudi itakuwa kweli. 18 Lakini kweli Mungu ataishi na wanadamu juu ya dunia? Angalia, dunia yote na mbingu yenyewe haviwezi kukubeba -sembuse na hekalu hili nililojenga! 19 Nakusihi yaheshimu maombi haya ya mtumishi wako na ombi lake. Yahwe Mungu wangu; sikia kilio na maombi ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako. 20 Fumbua macho yako kuelekea hekalu hili usiku na mchana, sehemu ambayo uliahidi kuliweka jina lako. Nakuomba usikie maombi atakayoomba mtumishi wako kuelekea sehemu hii. 21 Hivyo sikia maombi ya mtumishi na watu wako Israeli tunapoomba kuelekea sehemu hii. Ndiyo, sikia kutoka mahali unapoishi, kutoka mbinguni; na unaposikia, samehe. 22 Kama mtu atamtenda dhambi jirani yake na ikampasa kuapa kiapo, na ikiwa atakuja na kuapa kiapo mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii, 23 basi sikia kutoka mbinguni kutenda. Ukawahukumu watumishi wako, ukamlipizie mwovu, ili kuyaleta matendo yake juu ya kichwa chake. Ukamtangaze mwenye haki kuwa hana hatia, ili kumlipa thawabu kwa ajili ya uaminifu wake. 24 Watu wako watakaposhindwa na adui kwa sababu wamekutenda dhambi, kama watageuka nyuma kwako, wakilikili jina lako, wakisali na kuomba msamaha mbele zako hekaluni— 25 basi tafadhali sikia mbinguni na usamehe dhambi za watu wako Israeli; uwarudishe katika nchi uliyoitoa kwa ajili yao na baba zao. 26 Wakati mbingu zimefungwa na hakuna mvua kwa sababu watu wamekutenda dhambi—ikiwa wataomba kuelekea sehemu hii, wakilikili jina lako, na kuziacha dhambi zao utakapokuwa umewaadhibu— 27 basi sikia mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na watu wako Israeli, utakapowaelekeza kwenye njia njema iwapasayo kutembea. Tuma mvua juu ya nchi yako, ambayo umewapa watu wako kama urithi. 28 Kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna ugonjwa, tauni au ukungu, nzige au viwavijeshi, au kama adui wake wameyavamia malango ya mji katika nchi yao, au kwamba kuna pigo lolote au ugonjwa— 29 na ikiwa sala na maombi yamefanywa na mtu au watu wako wote Israel—kila mmoja akilijua pigo na huzuni katika moyo wake akinyosha mikono yake kuelekea hekalu hili. 30 Basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi; samehe, na umlipe kila mtu kwa njia zake zote; uhaujua moyo wake, kwa sababu wewe ni wewe pekee unaijua mioyo ya wanadamu. 31 Fanya hivyo ili kwamba wakuogope wewe, ili waweze kutembea katika njia zako siku zote ambazo wataishi katika nchi uliyowapa baba zetu. 32 Kwa mgeni ambaye siyo sehemu ya watu wako Israeli, lakini ambaye- kwa sababu ya ukuu wa jina lako, mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulionyoshwa- akija na kuomba kuelekea sehemu nyumba hii, 33 basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi, na fanya yote ambayo mgeni atakuomba, ili kwamba watu wote wa dunia walijue jina lako na kukuogopa wewe, kama wafanyavyo watu wako Israeli, na kwamba waweze kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako. 34 Ikiwa kwamba watu wako wakaenda nje kupigana dhidi ya adui zao, kwa njia yoyote ambayo unaweza kuwatuma, na ikiwa kwamba wakaomba kwako kuelekea mji huu ambao umeuchagua, na kuelekea nyumba ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako. 35 Basi sikiliza maombi yao mbinguni, ombi lao, na uwasaidie. 36 Kama wametenda dhambi dhidi yako—kwa kuwa hakuna asiye tenda dhambi—na ikiwa una hasira nao na kuwakabidhi kwa adui zao, ili kwamba adui wakawabeba na kuwachukua kama mateka katika nchi zao, iwe mbali au karibu. 37 Kisha wakatambua kuwa wako katika nchi ambako wamewekwa utumwani, na ikiwa watatubu na kutafuta msaada kwako katika utumwa wao. Ikiwa watasema, 'Tumetenda kinyume na kutenda dhambi. Tumetenda kwa uovu,' 38 ikiwa watarudi kwako kwa mioyo yao yote na kwa nia yao yote katika nchi ya utumwa wao, ambako walichukuliwa kama mateka, na ikiwa wataomba kukabili nchi yao, uliyowapa babu zao, na kukabili mji ambao uliuchagua na kukabili nyumba ambayo niliijenga kwa ajili ya jina lako. 39 Basi sika kutoka mbinguni, mahali unapoishi, sikia kuomba kwao na maombi na wayaombayo, na uwasaidie shida zao. Wasamehe watu wako, ambao wamekutenda dhambi. 41 42 40 Sasa, Mungu wangu, ninakusihi, uyafungue macho yako, na masikio yako yasikie maombi yatakayofanywa katika sehemu hii. 41 Sasa basi, amka, Yahwe Mungu, kwenye mahali pako pa kupumzikia, Wewe na sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Yahwe Mungu, wavikwe wokovu, na watakatifu wako wafurahi katika wema. 42 Yahwe Mungu, usiugeuze nyuma uso wa masihi wako. Yakumbuke matendo yako katika agano lako la ufalme kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako.