2 Mambo Ya Nyakati Sura 5

1 Wakati ilipomalizika kazi aliyofanya Sulemani kwa ajili ya Yahwe, Sulemani akapeleka vitu ndani, ambavyo Daudi, baba yake, aliviweka wakfu kwa kusudi hilo, pamoja na zile fedha, dhahabu, na vyombo vyote akavileta ndani ya hazina ya nyumba ya Mungu. 2 Kisha Sulemani akawakusanya wazee wa Israeli, wakuu wa makabila yote, na viongozi wa familia za watu wa Israeli, katika Yerusalemu, ili walilete sanduku la agano la Yahwe kutoka mji wa Daudi, ambao ni Sayuni. 3 Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika mbele za mfalme katika sikukuu, ambayo ilikuwa katika mwezi wa saba. 4 Wazee wote wa Israeli wakaja, na Walawi wakalichukua sanduku. 5 Wakalileta sanduku, hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote ambavyo vilikuwa ndani ya hema. Makuhani waliokuwa wa kabila la Lawi wakavileta vitu hivyo. 6 Mfalme Sulemani na kusanyiko lote la Israeli wakaja pamoja, mbele ya sanduku, wakitoa sadaka za kondoo na ng'ombe ambao hawakuweza kuhesabika. 7 Makuhani wakalileta sanduku la angano la Yahwe ndani mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, kwenye patakatifu pa patakatifu, chini ya mabawa ya makerubi. 8 Kwa kuwa makerubi walitandaza mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, na walilifunika sanduku na miti yake ya kulibebea. 9 Miti ilikuwa mirefu sana kwamba ncha zake zilionekana kutoka ile sehemu takatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuweza kuonekana kutoka nje. Zipo hapo hadi leo. 10 Hapakuwa na kitu katika sanaduku isipokuwa zile meza mbili ambazo Musa aliziweka humo huko Horebu, wakati Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka nje ya Misri. 11 Ilikuwa makuhani walipotoka nje ya sehemu takatifu. Makuhani wote waliokuwepo wakajiweka wakfu wenyewe kwa Yahwe, bila kujiamuru wenyewe kulingana na sehemu zao. 12 Pia makuhani waliokuwa waimbaji, wote kwa ujumla wao, pamoja na Asafu, Hemani, Yeduthuni, na wana wao na ndugu zao, wakiwa wamevalia kitani safi na wakipiga matoazi, vinanda, na vinubi, wakasimama upande wa mashariki wa mwisho wa madhabahu. Pamoja nao palikuwa na makuhani 120 wakipuliza tarumbeta. 13 14 Ikawa kwamba wapuruza tarumbeta na waimbaji wakafanya mziki pamoja, wakifanya sauti moja isikike kwa ajili ya kumsifu na kumshukuru Yahwe. Walipaza sauti zao kwa tarumbeta, toazi na vyombo vingine, na wakamsifu Yahwe. Wakaimba, "Kwa maana Yeye ni mwema, kwa kuwa uaminifu wa agano lake wadumu milele." Kisha nyumba, ile nyumba ya Yahwe, ikajawa na wingu. Makuhani hawakuweza kusimama ili wahudumu kwa sababu ya lile wingu, kwa maana utukufu wa Yahwe uliijaza nyumba yake.