2 Mambo Ya Nyakati Sura 15 25

1 Amaza alikuwa na umri wa amiaka ishirini na na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yehoadani, wa Yerusalemu. 2 Alifanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, lakini siyo kwa moyo uliojitoa kikamilifu. 3 Ikawa kwamba mapema utawala wake ulipokuwa umeimarika, aliwaua watumishi ambao walikuwa wamemuua baba yake, mfalme. 4 Lakini hakuwaua watoto wa wale wauaji, bali alitenda kama kama ilivyoaandikwa katika sheria, katika kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamru. "Baba hatajuta kwa ajili ya watoto, wala watoto hawatakufa kwa ajili ya baba zao. Badala yake, kila mtu lazima afe kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe". 5 Aidha, Amazia aliwakusanya Yuda pamoja, na akawaandikisha kwa kufuata nyumba za babu zao, chini ya maakida wa maelfu na maakida wa mamia --wote wa Yuda na wa Benyamini. Akawahesabu kuanzia wa mika ishirini na kuendelea, na akawaona wako 300, 000 wanaume waliochaguliwa, wawezaoa kwenda vitani, walioweza kushika mkuki na ngao. 6 Pia alikodi wanaume wa kupigana 100, 000 kutoka Israeli kwa fedha mia moja. 7 Lakini mtu wa Mungu alikuja kwake na kusema, " Mfalme, usiliache jeshi la Istaeli kwenda nawe, kwa maana Yahwe hayupo pamoja na Israeli -wala na mtu Yeyote wa Efraimu. 8 Lakini hata kama mtaenda na mkiwa wenye ushupavu na imara katika vita, Mungu atawatupa chini mbele ya adui, kwa maana Mungu ana nguvu za kusaidia, na nguvu za kurusha chini". 9 Amazia akasema kwa mtu wa Mungu, "Lakini tutafanyaje kuhusu talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, Yahwe anauwezo wa kukupa vingi zaidi kuliko hivyo." 10 Kwa hiyo Amazia akalitenganisha jeshi lilokuja kwake kutoka Efraimu; akawarudisha nyumbani tena. Hivyo hasira yao iliwaka sana zidi ya Yuda, na walirudi nyumbani kwa hasara kali. 11 Amazia akajipa ujasiri na kuwaongoza watu wake kwenda nje kwenye bonde la chumvi, huko akawashinda wanaueme elfu kumi wa Seiri. 12 Jeshi la Yuda likawachukua elfu kumi wengine wakiwa hai. Wakawapeleka juu ya mwamba na kuwarushwa chini kutoka huko, hivyo wote wakavunjika vunjika katika vipande. 13 Lakini watu wa jeshi ambalo Amazia alilirudisha, ili kwamba wasiende naye vitani, wakauvamia mji Yuda kuanzia Somaria hadi Beth- horoni. Wakawapiga watu elfu tatu na kuwateka wengi sana. 14 Sasa ikawa kwamba baada ya Amazia kurudi kutoka kuwachinja Waedomu, akaileta miungu ya watu wa Seiri, na kuisimamisha iwe miungu yake. Akainama chini mbele ya hiyo miungu na kuitolea sadaka za uvumba. 15 Hivyo hasira ya Yahwe ikawaka zidi ya Amazia. Akamtuma nabii kwake, ambaye alisema, "Kwa nini umeitafuta miungu ya watu ambayo haikuwaokoa hata watu wake yenyewe zidi ya mkono wako?" 16 Akiwa kwamaba yule nabii alipokuwa anaongea naye, mfalme akamwambia, "Je, wewe tumekufanya kuwa mshauri wa mfalme? Acha! Kwa nini ujitakie kuuawa?" Kisha nabii akaacha na kusema, ninajua kwamba Mungu ameamua kukuangaamiza kwa sababu umefanya tendo hili na hujasikilisa ushauri wangu." 17 Kisha Amazia akashauriana na washauri na kutuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israel. akisema, "Njoni, tukutane uso kwa uso katika vita". 18 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amaziahi mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi ulioko Lebanoni, ukisema, Mtoe binti yako kwa mwanangu awe mke wake; lakini akapita hayawani katika Lebanoni akatembea na kuukanyaga chini mbaruti. 19 Umesema, 'Ona, nimeipiga Edomu,' na moyo wako umekuinua juu. Jipe fahari katika ushindi wako, lakini ukae nyumbani, kwa maana ni kwa nini ujisababishie matatizo mwenyewe na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?' 20 Lakini Amazia hakusikiliza, kwa sababu tukio hili lilikuwa limetoka kwa Mungu, ili awatie Waisraeli katika mkono wa adui zao, kwa sababu walikuwa wametafuta ushauri kutoka kwa miungu ya Edomu. 21 Kwa hiyo, Yehoashsi, mfalme wa Israeli, akavamia; yeye na Amazia, mfalme wa Yuda, wakakutana uso kwa uso huko Beth -shemishi, ulioko Yuda. 22 Yuda akashindwa mbele za Israeli, na kila mtu akarudi nyumbani. 23 Yehoashi, mfalme wa Israeli, akamkamata Amazia mwana wa Yehoashi mana wa Ahazia, mfalme wa Yuda, huko Beth - shemeshi. Akamleta Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi kona ya Lango, umbali wa mikono mia nne. 24 Akachukua dhahabu na fedha zote, vitu vyote vilivyoonekana akatika nyumba aya Mungu kwa Obedi Edomu, na vitu vya thamanai katika nyumba ya mfalme, na mateka pia, na akarudi Samaria. 25 Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, aliishi miaka kumi na tano baada ya kifo cha Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli. 26 Kwa mambo mengingine kuhusu Amzia, mwanzo na mwisho, tazama, je, hayajaandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli? 27 Sasa kutoka wakati amabaoa Amazia aligeukia mbali asimfuate Yahwe, walianza kupanga njama zidi yake katika Yerusalemu. Akakimbilia Lachishi, lakini wakatuma watu nyuma yake wamfuate Lachishsi na walimuua huko. 28 Wakamleta juu ya farasis na wakamzika pamoja na babu zake kataika Mji wa Yuda.