2 Mambo Ya Nyakati Sura 15 24

1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala; akatawala kwa mika arobaini katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Sibia wa Beer-sheba. 2 Yoashi alifanya yaliyo mema katika macho ya Yahwe siku zote za Yehoyada, yule kuhani. 3 Yehoyada akajichukulia wake wawili kwa ajili yake, na akawa baba wa wana na mabinti. 4 Ikawa baada ya haya, kwamba Yoashi aliamua kuitengeneza nyumba ya Yahwe. 5 Akawakusanya pamoja makuhani na Walawi, na kusema kwao, " Nendeni nje kila mwaka kwenye miji ya Yuda na kukusanya fedha kutoka Israeli yote kwa ajili ya kuikarabati nyumba ya Mungu wenu. Hakikisheni kwamba mnaanza haraka." Walawi hawakufanya kitu kwanza. 6 Kwa hiyo mfalme akamuita Yehoyada, yule kuhani, na kumwambia, "Kwa nini hukuwaagiza Walawi kuleta kutoka Yud na Yerusalemu kodo iliyoagizwa na Musa mtumishi wa Yahwe na kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya amri za hema ya agano?" 7 Kwa maana wana wa Athalia, yule mwanamke muovu, walikuwa wameivunja nyumba ya Mungu na kuwapa Mabaali vitu vyote vitakatifu vya nyumba ya Yahwe. 8 Kwa hiyo mfalme aliamuru, na wakatengeneza kasha na kulileta nje kwenye lango kwenye nyumba ya Yahwe. 9 Kisha wakafanya tangazo katika Yuda na Yerusalemu, kwa ajili ya watu kuleta kwa Yahwe kodi aliyoiagiza Musa mtumishi wa Mungu juu ya Israeli jangwani. 10 Viongozi wote na watu wote wakafurahia na wakaleta fedha na kuiweka kwenye kasha hadi walipomaliza kulijaza. 11 Ikatokea kwamba kila lilipoletwa kasha kwa mikono ya Walawi kwa wakuu wa mfalme, na kila walipoona kwamba kulikuwa na fedha nyingi sana ndani yake, waandishi wa mfalme na mkuu wa kuhani mkuu walikuja, kulihamishia fedha kasha, na kulirudisha sehemu yake. Walifanya hivyo siku baada siku, wakikusanya kiasi kikubwa cha fedha. 12 Mfalme na Yehoyada akawapa zile fedha wale waliofanya kazi ya kuhudumu katika nyumba ya Yahwe, Watu hawa waliwaajiri waashi na maseremala ili waijenge nyumba ya Yahwe, na pia wale waliofanya kazi katika chuma na shaba. 13 Kwa hiyo wafanya kazi wakafanya kazi, na kazi ya kukarabati ikasonga mbele mikononi mwao; waakaisimamisha nyumba ya Mungu katika hali yake halisi na kuiimarisha. 14 Walipomaliza, wakaleta fedha zilizobaki kwa mfalme na Yehoyada. Fedha hizo zilitumika kutengenezea samani kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vyombo vya huduma na kutolea dhabihu—vijiko na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa bila kukomaa katika nyumba ya Yahwe kwa siku zote za Yehoyada. 15 Yehoyada akazeeka na alaaikuwa amejaa siku, na kisha akafa; alikuwa na umri wa mika 130 alipokufa. 16 Wakamzika katika aamji wa Daudi miongoni mwa wafalme, kwa sababu alikuwa amefanya mema katika Israeli, kwa Mungu, na kwa ajili ya nyumba ya Mungu, 17 Sasa baada ya kifo cha Yehoyada, kiongozi wa Yuda akaja na kutoa heshima kwa mfalme. Kisha mfalme akawasikiliza. 18 Wakaiacha nyumba ya Yahwe, Mungu wa babu zao, na kuwaabudu miungu na maashera na sanamu. Ghadhabu ya Mungu ikaja juu ya Yuda na Yerusalemu kwa sababau ya hili kosa lao. 19 Bado akatuma manabii kwao ili kuwaleta tena kwake, Yahwe, manabii wakatangaza juu ya watu, lakini walipuuza kusikiliza. 20 Roho wa Mungu akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada, yule kuhani; Zekaria akasimama juu ya watu na kusema kwao, "Mungu anasema hivi: Kwa nini mnazivunja amri za Yahwe, ili kwamba msifanikiwe? Kwa kuwa mmemsahau Yahwe, pia amewasahau ninyi." 21 Lakini wakapanga njama dhidi yake; kwa amri ya mfalme, wakampiga kwa mawe katika uwanja wa nyumba ya Yahwe. 22 Katika namna hii hii, Yoashi, yule mfalme, akapuuza ukarimu ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alikuwa amemfanyia. 23 Ikawa karibu mwisho wa mwaka, kwamba jeshi la Aramu wakaja juu yake Yoashi. Wakaja Yuda na Yerusalemu; wakawaua viongozi wote wa watu na kupeleka nyara zote kutoka kwao kwa mfalme wa Dameski. 24 Jeshsi la Waaramu walikuwa wamekuja na jeshi dogo, lakini Yahwe akawapa ushindi juu ya jeshi kubwa, kwa sababu Yuda alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao. Katika namna hii Waaramu wakaleta hukumu juu ya Yoashi. 25 Katika muda ambao Waaramu walikuwa wameondoka, Yoashi alikuwa amejeruhiwa vikali. Watumishi wake wakapanga njama dhidi yake kwa sababu ya mauaji ya wana wa Yehoyada, yule kuhani. Wakamuua katika kitanda chake, na akafa; wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya wafalme. 26 Hawa walikuwa watu waliopanaga njama dhidi yake: Zabadi mwana wa Shimeathi, Mwamoni; na Yehozabadi mwana wa Shimrithi, Mwanamke Mmoabu. 27 Sasa matukio kuhusu wanaye, unabii muhimu uliokuwa umesemwa kumhusu yeye, na kujengwa tena kwa nyumba ya Mungu, ona, yameandikwa katika Kamusi ya kitabu cha wafalme. Amazia mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.