Abiathari alikuwa kuhani mkuu wa taifa la Israeli wakati wa mfalme Daudi. Mfalme Sauli alipowaua manabii, alitoroka na kwenda kwa Daudi nyikani. Abiathari na kuhani mkuu mwingine aitwaye Zadoki walimhudumia Daudi kwa uaminifu katika kipindi chote cha utawala wake. Baada ya kifo cha Daudi, Abiathari alijaribu kumsaidia Adoniya kuwa mfalme badala ya Sulemani. Kwa sababu hii mfalme Sulemani alimuondoa Abiathari kutoka kwenye ukuhani.
Abimeleki alikuwa mfalme wa Wafilisti huko Gera katika kipindi ambacho Abrahamu na Isaka wanaishi katika nchi ya Kaanani. Abrahamu alimdanganya Abimeleki kwa kumwambia kuwa Sara alikuwa dada yake badala ya mke wake. Abrahamu na Abimeleki walikubaliana kuhusu umiliki wa visima vilivyopo Belisheba. Miaka mingi baadaye Isaka naye akamdanganya Abimeleki na watu wengine wa Gera kwa kumwambia kuwa Rebeka alikuwa dada yake na sio mke wake. Mfalme Abimeleki alimkemea Abrahamu na Isaka kwa kumdanganya. Mtu mwingine aliyeitwa Abimeleki alikuwa mtoto wa Gidioni na kaka wa Yoramu.
Abinieri alikuwa binamu wa mfalme Sauli katika agano la Kale. Abinieri alikuwa mkuu wa majeshi ya Sauli na alimtambulisha kijana Daudi kwa Sauli baada ya Daudi kumuua Goliati. Baada ya kifo cha Sauli Abinieri alichaguliwa na mtoto wa Sauli Ishibosheti kuwa mfalme wa Israeli wakati Daudi akiteuliwa kuwa mfalme katika Yuda. Baadaye Abinieri aliuawa kikatili na mkuu wa majeshi ya Daudi, Yoabu.
Abiya lilikuwa jina la Mfalme wa Yuda aliyetawala tangu 915-913 BC. Alikuwa mtoto wa mfalme Rehoboamu. Walikuwepo watu wengine walioitwa Abiya katika agano la kale. Watoto wa Samweli Abiya na Yoeli walikuwa viongozi wa wana wa Israeli huko Belisheba. Kwa kuwa Abiya na kaka yake hawakuwa waaminifu watu walimuomba Samweli ateue mfalme mwingine wa kuwaongoza. Abiya mwingine ni yule aliyekuwa kwenye hekalu la kinabii wakati wa mfalme Daudi. Abiya lilikuwa jina la mtoto wa mfalme Yeroboamu. Abiya pia lilikuwa jina la kuhani mkuu aliyerudi na Zerubabeli Yerusalemu toka utumwani Babiloni.
Abiya ni jina la watu mbalimbali katika agano la kale. Wafuatao ni watu hao:
Abramu alikuwa Mkalidayo toka mji wa Urialiyechaguliwa na Mungu kuwa baba wa Waisraeli. Mungu alibadilisha jina lake na kuwa "Abrahamu."
Abusalomu alikuwa mtoto wa tatu wa mfalme Daudi. Alijulikana kwa utanashati wake pamoja na hasira kali.
Adamu alikuwa binadamu wa kwanza aliyeumbwa na Mungu. Yeye na mke wake Hawa walitengenezwa kwa mfano wa Mungu.
Adoniya alikuwa mtoto wa nne wa mfalme Daudi.
Ahabu alikuwa mfalme muovu sana katika ufalme wa Kaskazini mwa Israeli toka 875-854 BC.
Ahabu na mkewe walifanya mambo mengi maovu ikiwemu kutumia nguvu zao kuwaua watu wasio na hatia.
Ahazi alikuwa mfalme muovu aliyetawala ufalme wa Yuda toka 732-716 BC. Hii ilikuwa yapata miaka 140 kabla ya wakati ambao wana wa Israeli na Yuda walichukuliwa mateka Babiloni.
Lilikuwa jina la wafalme wawili: mmoja alitawala Israeli mwingine alitawala ufalme wa Yuda.
Ahusuero alikuwa mfalme aliyetawala ufalme wa Perusia kwa miaka ishirini.
Katika agano la kale, Ai lilikuwa jina la mji wa Kaanani uliopo kusini mwa Betheli na takribani kilometa 8 kaskazini mashariki mwa Yeriko.
Alikuwa Mkristo wa kiyahudi aliyeishi Ponto.
Waamaleki ni wafugaji walioishi Kusini mwa Kaanani, toka jangwa na Negevu mpaka nchi za uarabuni. Watu hawa walikuwa uzao wa Ameleki, mjukuu wa Esau.
Amazia alikuwa mfalme ya Yuda baada ya baba yake mfalme Yuashi kuuawa.
Amnoni alikuwa mtoto mdogo wa mfalme Daudi na mke wake Ahinoamu.
"Waamoni" lilikuwa kundi la watu walioishi Kaanani. Walikuwa uzao wa Benyamini, aliyekuwa mtoto wa Lutu.
Amosi alikuwa Nabii wa Kiisraeli aliyeishi kipindi cha mfalme Uzia wa Yuda.
Amozi alikuwa baba wa nabii Isaya.
Anasi alikuwa kuhani mkuu wa Kiyahudi kwa miaka 20 toka AD 6-AD 15. Kisha akaondolewa kwenye ukuhani mkuu na serikali ya Kirumi japokuwa aliendelea kuwa kiongozi mwenye ushawishi kati ya Wayahudi.
Andrea alikuwa mmoja kati ya wanafunzi kumi na wawili aliowachangua Yesu kuwa karibu naye ambao baadaye waliitwa Mitume.
Antiokia ni jina la miji miwili katika agano jipya. Mji wa kwanza ulikuwa Siria karibu na bahari ya Mediterania na mji mwingine ulikuwa Rumi katika jimbo la Pisidia.
Apolo alikuwa Myahudi toka katika nchi ya Misri aliyekuwa na uwezo wa kipekee wa kufundisha kuhusu Yesu.
Katika agano la kale "Araba" imetumika kuelezea jangwa kubwa au maeneo tambarare yanayojumuisha bonde jirani na mto Yordani hadi kusini kwenye ncha ya kaskazini mwa bahari ya shamu.
Araba pia yaweza kuwa sehemu yoyote yenye jangwa.
"Arami" ni jina la watu wawili katika agano la kale. Pia lilikuwa jina la mji uliopo kaskazini mashariki mwa Kaanani, ambayo kwa sasa ni Siria.
Kwenye Biblia "Ararati" ni jina la mahali, ufalme na milima mbalimbali.
Artashasta alikuwa mfalme aliyetawala ngome ya Peru toka 464-424 BC.
Asa alikuwa mfalme aliyetawana ufalme wa Yuda kwa miaka arobaini. toka 913-873 BC.
Asafu alikuwa kuhani wa Kilawi na mtaalamu wa muziki aliyetunga mziki wa Zaburi ya mfalme Daudi. Pia aliandika zaburi yake mwenyewe.
Ashdodi ulikuwa ni moja kati ya miji mitano muhimu kwa Wafilisti. Mji huu ulikuwa kusinimagharibi mwa Kanani karibu na bahari ya Mediterranean, kkati ya miji ya Gaza na Jopa.
Ashera lilikuwa jina la mungu wa kike aliyeabuniwa na Wakaanani kipindi cha agano la kale. Ashtorethi ni jina lingine la Ashera.
Asheri alikuwa mtoto wa nane wa Yakobo. Uzao wake unaunda moja ya makabila kumi na mbili ya Israeli ambalo pia linaitwa Asheri.
Katika Biblia, Ashikelo ni mji wa wafilisti ulioko pwani Bahari ya Mediterania. Bado ipo mpaka leo Israeli.
Ashuru lilikuwa taifa lenye nguvu kipindi ambacho wana wa Israeli walikuwa wakiishi Kaanani. Ngome ya waashuru ilikuwa ni kundi la mataifa waliotawaliwa na mfalme wa Ashuru.
Katika Biblia Asia ni jina la jimbo la utawala wa Kirumi. Ilikuwa magharibi mwa nchi inayoitwa Uturuki kwa sasa.
Athalia alikuwa mke mbaya wa Yehoramu mfalme wa Yuda. Alikuwa mjukuu wa mfalme muovu wa Israeli, mfalme Omri.
Ayubu alikuwa mtu anayeelezwa katika Biblia kama mtu asiye na hatia na mwenye haki mbele ya Mungu. Anajulikana zaidi kwa kutunza imani yake katika Mungu katika nyakati za mateso makali.
Ayubu aliishi katika nchi ya Usi iliyokuwa sehemu ndani ya nchi ya Kanaani, inawezekana katika maeneo ya Edomu. Inafikiriwa kuwa aliishi wakati wa Esau na Yakobo kwa sababu mmoja wa marafiki wa Ayubu alikuwa "Mtemani," ambalo lilikuwa jina la kundi lililoitwa baada ya mjukuu wa Esau. Kitabu cha Agano la Kale cha Ayubu kinaelezea jinsi Ayubu na wengine walivyoitikia mateso yake. Pia inatoa mtazamo wa Mungu kama muumbaji mwenye enzi na mtawala wa ulimwengu. Baada ya maafa hayo yote, hatimaye Mungu alimponya Ayubu na kumpa watoto wengine na utajiri. Kitabu cha Ayubu kinasema kuwa alikuwa mzee sana alipokufa.
Azaria ni jina la watu kadhaa kwenye agano jipya.
"Baali" maana yake "bwana" lilikuwa jina la mungu wa kwanza wa uongo aliyekuwa akiabudiwa na Wakanaani.
Baasha alikuwa miongoni mwa wafalme waovu wa Israeli,waliowashawishi Waisraeli kuabudu vinyago.
Babeli ulikuwa mji mkuu katika eneo lililoitwa Shinari kusini mwa Mesopotamia. Shinari ulikuja baadaye kuitwa Babiloni.
Bahari ya Chumvi( inayo itwa pia Bahari iliyo Kufa) ilikuwa kati ya kusini mwa Israeli upande wa magharibi na Moabu upande wa mashariki.
"Bahari ya Galilaya" ni jina la ziwa mashariki mwa Israeli. Katika Agano la Kale liliitwa "Bahari ya Shinerethi."
Bahari ya shamu ni jina la la bahari iliyokuwa Misri na Uarabbuni. Sasa inaitwa bahari ya Shamu.
Katika Biblia, "Bahari Kuu" au " bahari ya magharibi" inaelezea ile ambayo sasa ujulikana "Bahari ya Medeterenia," ambayo ilikuwa ni eneo la maji lilokulikana na watu wa Biblia.
Balaamu alikuwa nabii wa kipagani aliyeajiriwa na Mfalme Balaki kuwalaani Israeli walipokuwa wamepiga kambi katika Mto Yordan kaskazini mwa Moabu, wakijiandaa kuingia nchi ya Kanaani.
Baraba alikuwa mfungwa huko Yerusalemu wakati Yesu anakamatwa.
Barnaba ni miongoni mwa wakristo wa mwanzo aliyeishi wakati wa mitume.
Baruku ni jina la watu kadhaa katika Agano la Kale.
Bashani lilikuwa ni enea mashariki mwa Bahari ya Galilaya. Ilihusisha eneo ambalo kwa sasa ni sehemu ya Syria na milima ya Golani.
Batholomayo alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu.
Bathsheba alikuwa mke wa Uria, askari katika jeshi la Daudi. Baada ya kifo cha Uria, akawa mke wa Daudi, na mama wa Sulemani.
Beelzebuli ni jina lingine kwa Shetani, au mwasi. Wakati mwingine linaandikwa "Beelzebubu."
Katika nyakati za Agano la Kale, Beersheba ulikuwa mji uliokuwa umbali wa maili 45 kusini magharibi mwa Yerusalemu katika eneo la jangwa ambalo kwa sasa linaitwa Negevu.
Benaya lilikuwa jina la watu kadhaa katika Agano la Kale.
Benjamini alikuwa mwana wa mwisho wa Yakobo aliyezaliwa na Raheli mkewe. Jina lake linamaanisha mwana wa "mkono wangu wa kulia."
Katika nyakati za Agano Jipya, Berea(Beroya) ulikuwa mji wa Kigriki wenye mafanikio kusini mashariki mwa Masedonia, umbali wa kilometa 80 kusini mwa Thesalonike.
Beth Shemeshi lilikuwa jina la mji wa Kikanaani kama kilometa 30 magharibi ya Yerusalemu.
Betheli ulikuwa mji uliokuwa kaskazini mwa Yerusalemu katika nchi ya Kanaani. Hapo mwanzo uliitwa "Luzu."
Bethlehemu ulikuwa mji mdogo katika nchi ya Israeli, karibu na mji wa Yerusalemu. Ulijulikana pia kama "Efratha," ambalo pengine ndilo jina lake la awali.
Bethueli alikuwa mwana wa Nahori ndiguye Ibrahimu.
Boazi alikuwa mwisraeli aliyekuwa amemwoa Ruthi, babu wa mfalme Daudi, na babu wa Yesu Kristo.
Bonde la Kidroni ni bonde refu nje kidogo ya mji wa Yerusalemu, katikati ya ukuta wa mashariki na mlima wa Mizeituni.
Bonde lina kina zaidi ya mita 1,000 na urefu karibu wa kilomita 32. Wakati mfalme Daudi alipokuwaakimtoroka mwanaye Absalomu, alipita bonde la Kidroni kufika mlima wa Mizeituni. Mfalme Yosia na mfalme Asa wa Yuda waliamuru kwamba sehemu zilizoinuka na madhabahu za miungu wa uongo zivunjwe na kuchomwa; majivu yalitupwa bonde la Kidroni. Wakati wa utawala wa mfalme Hezekia, bonde la Kidroni ndipo makuhani walipotupa kila kitu kisicho kisafi walichokitoa kwenye hekalu. Malkia muovu Athalia aliuliwa katika bonde kwa sababu ya maovu aliyoyafanya.
Dameski ni mji mkuu wa nchi ya Shamu. Bado upo sehemu ile ile kama ulipokuwa kipindi cha Biblia.
Dameski ni moja ya miji kongwe, inayoendelea kukaliwa kwa uendelevu duniani.
Katika kipindi cha Abrahamu, Shamu ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa Aramu (ulio mahali ambapo sasa ni Shamu).
Katika Agano la Kale lote, kuna marejeo mengi ya miingiliano kati ya wakazi wa Dameski na watu wa Israeli.
Baadhi ya unabii wa Kibiblia zinatabiri uharibifu wa Dameski. Unabii huu unaweza kuwa umekamilika pale ambapo Shamu iliangamiza mji ule katika wakati wa Agano la Kale, au kunaweza kuwa na muda wa baadaye, utakaokuwa na uharibifu kamili wa mji huu.
Katika Agano Jipya, Mfarisayo Sauli (aliyejulikana baadaye kama Paulo) alikuwa njiani kukamata Wakristo katika mji wa Dameski ambapo Yesu alimkabili na kumfanya awe muumini.
Dani alikuwa mwana wa tano wa Yakobo na alikuwa mmoja wa makabila kumi na mawili ya Israeli. Eneo lililokaliwa na kabila la Dani sehemu ya kaskazini ya Kaanani pia lilipatiwa jina hili.
Katika kipindi cha Abrahamu, kulikuwa na mji ulioitwa Dani uliokuwa magharibi mwa Yerusalemu.
Miaka ya baadaye, katika kipindi ambapo taifa la Israeli lilipoingia katika nchi ya ahadi, mji tofauti ulioitwa Dani ulikuwa kama maili 60 kaskazini mwa Yerusalemu.
Msemo "Wadani" una maana ya vizazi vya Dani, ambao pia ni wanajumuiya wa ukoo wake.
Danieli alikuwa nabii wa Kiisraeli ambaye alikuwa kijana mdogo aliyechukuliwa mateka na mfalme wa Babeli Nebukadreza mnamo wa 600 KK.
Huu ulikuwa wakati ambapo Waisraeli wengine wengi kutoka Yuda walishikwa mateka huko Babeli kwa miaka 70.
Danieli alipewa jina la Kibabeli la Belteshaza.
Danieli alikuwa kijana aliyeheshimika na mwenye haki aliyemtii Mungu.
Mungu alimwezesha Danieli kutafsiri ndoto kadhaa au maono kwa wafalme wa Babeli.
Kwa sababu ya uwezo huu na kwa sababu ya hulka yake ya heshima, Danieli alipewa nafasi ya juu ya uongozi katika ufalme wa Kibabeli.
Miaka mingi baadaye, maadui wa Danieli walimdanganya mfalme wa Babeli Dario kutunga sheria inayokataza kumwabudu mtu yeyote isipokuwa mfalme. Danieli aliendelea kuomba kwa Mungu, kwa hiyo alikamatwa na kutupwa katika tundu la simba. Lakini Mungu alimkomboa na hakudhuriwa kabisa.
Dario lilikuwa jina la wafalme kadhaa wa Uajemi. Inawezekana "Dario" ilikuwa ni cheo na siyo jina.
"Dario, Mmedi" alikuwa mfalme aliyedanganywa kumfanya nabii Danieli kutupwa katika tundu la simba kama adhabu ya kumwabudu Mungu.
"Dario Muajemi" alisaidia kurahisisha ujenzi tena wa hekalu Yerusalemu katika kipindi cha Ezra na Nehemia.
Daudi alikuwa mfalme wa pili wa Israeli na alimpenda na kumtumikia Mungu. Alikuwa mwandishi mkuu wa kitabu cha Zaburi.
Daudi alipokuwa mvulana mdogo akichunga kondoo wa familia yake, Mungu alimchagua kuwa mfalme afuataye wa Israeli.
Daudi alikuwa mpiganaji hodari na aliongoza jeshi la Israeli katika vita dhidi ya maadui zake. Kumshinda kwake Goliati na Wafilisti kunajulikana sana.
Mfalme Sauli alijaribu kumuua Daudi, lakini Mungu alimlinda, na kumfanya awe mfalme baada ya kifo cha Sauli.
Daudi alitenda dhambi mbaya sana, lakini alitubu na Mungu alimsamehe.
Yesu, Masihi, anaitwa "Mwana wa Daudi" kwa sababu ni uzao wa Mfalme Daudi.
Delila alikuwa mwanamke wa Kifilisti aliyependwa na Samsoni, lakini hakuwa mke wake.
Delila alipenda pesa zaidi ya alivyompenda Samsoni.
Wafilisti walimhonga Delila kumdanganya Samsoni amwambie jinsi awezavyo kufanywa mnyonge. Nguvu yake ilipotoweka, Wafilisti walimkamata.
Katika kipindi cha zamani, Edeni ilikuwa eneo ambalo lilikuwa na bustani ambapo Mungu aliweka mwanamume na mwanamke wa kwanza kuishi.
Bustani ambayo Adamu na Hawa waliishi ilikuwa sehemu tu ambayo waliishi.
Sehemu husika ya eneo la Edeni halina uhakika, lakini Mito ya Hidekeli na Frati zilitiririka katikati yake.
Neno "Edeni" hutokana na neno la Kiebrania lenye maana ya "kufurahishwa sana na".
Edomu ilikuwa jina lingine la Esau. Eneo ambalo aliishi pia kukajulikana kama "Edomu" na baadaye, "Idumaya". "Waedomu" walikuwa vizazi vyake.
Eneo la Edomu lilibadilisha maeneo baada ya muda. Ulikuwa zaidi kusini ya Israeli na baadaye kupanuka katika kusini mwa Yuda.
Katika wakati wa Agano Jipya, Edomu ilifunika nusu ya kusini ya mkoa wa Yuda. Wagiriki waliita "Idumaya"
Jina "Edomu" ina maana ya "nyekundu" ambayo inaweza kumaanisha ukweli kwamba Esau alifunikwa na nywele nyekundu alipozaliwa. Au inaweza kumaanisha mchuzi mwekundu ambao Esau aliuza kwa haki yake ya mzawa wa kwanza.
Katika Agano la Kale, nchi ya Edomu mara kwa mara hutajwa kama adui wa Israeli.
Kitabu kizima cha Obadia kinahusu uharibifu wa Edomu. Manabii wengine wa Agano la Kale pia walizungumza tabiri hasi dhidi ya Edomu.
Efeso ulikuwa mji wa zamani wa Kigiriki katika fukwe ya magharibi ya pale ambapo siku ya sasa ni Uturuki.
Katika kipindi cha Wakristo wa kwanza, Efeso ilikuwa mji mkuu wa Asia, ambao ulikuwa mkoa mdogo wa Kirumi katika kipindi hicho.
Kwa sababu ya eneo lake, mji huu ulikuwa kitovu muhimu sana katika biashara na safari.
Hekalu la kipagani linalojulikana kwa kuabudu mungu wa Artemi (Diana) ilikuwa Efeso.
Paulo aliishi na kufanya kazi Efeso kwa zaidi ya miaka miwili na baadaye kumteua Timotheo kuwaongoza waumini mapya kule.
Kitanu cha Waefeso katika Agano Jipya ni barua ambayo Paulo aliandika kwa waumini wa Efeso.
Efraimu alikuwa mwana wa pili wa Yusufu. Vizazi vyake, Waefraimu, waliunda moja ya kabila kumi na mbili za Israeli.
Kabila la Efraimu lilikuwa moja la makabila kumi ambayo yalikuwa katika sehemu ya kaskazini ya Israeli.
Mara nyingine jina la Efraimu linatumika katika Biblia kumaanisha ufalme wote wa kaskazini wa Israeli.
Efraimu ilikuwa eneo lenye milima na miinuko mingi sana, kutokana na kumbukumbu zenye "nchi yenye milima Efraimu" au "milima ya Efraimu".
Efrata ilikuwa jina la mji na eneo katika sehemu ya kaskazini ya Israeli. Mji wa Efrata baadaye uliitwa "Bethehemu" au "Efrata-Bethlehemu".
Efrata ilikuwa jina la mmoja wa wana wa Kalebu. Mji wa Efrata yawezekana uliitwa baada yake.
Mtu ambaye alikuwa ametoka mji wa Efrata alikuwa akijulikana kama "Mwefrathi".
Boazi, babu mkuu wa Daudi, alikuwa Mwefrathi.
Ekroni ni mji mkuu wa Wafilisti, uliopo maili tisa barani kutoka bahari ya Mediteraniani.
Hekalu la mungu wa uongo Baal-zebubu ilikuwa Ekroni.
Pale Wafilisti walipokamata sanduku la agano, walilichukua hadi Ashdodi, kisha kuhamisha hadi Gathi na Ekroni kwa sababu Mungu aliendelea kusababisha watu kuugua na kufa katika kila mji sanduku lilipokuwa likipelekwa. Hatimaye Wafilisti walirudisha sanduku Israeli.
Pale mfalme Ahazia alipoanguka kutoka kwenye paa ya nyumba yake na kujiumiza, alifanya dhambi kwa kujaribu kutafuta kutoka kwa mungu wa uongo Baal-zebubu wa Ekroni kama angekufa au la kutokana na majeraha yake. Kwa sababu ya dhambi hii, Yahwe alisema ya kuwa angekufa.
Elamu alikuwa mwana wa Shemu na mjukuu wa Nuhu.
Vizazi vya Elamu vilikuwa vinaitwa "Waelami" na waliishi katika eneo lililoitwa "Elamu".
Eneo la Elamu lilikuwa kusini mashariki mwa Mto Hidekeli, ambayo sasa ni Irani magharibi.
Eleazari lilikuwa jina la wanamume kadhaa katika Biblia.
Eleazari alikuwa mwana wa tatu wa kaka yake Musa Haruni. Baada ya Haruni kufa, Eleazari akawa kuhani mkuu Israeli.
Eleazari lilikuwa pia jina la mmoja wa "wanamume hodari" wa Daudi.
Eleazari mwingine alikuwa mmoja wa uzao wa Yesu.
Eliakimu lilikuwa jina la wanamume wawili katika Agano la Kale.
Mwanamume mmoja aliyeitwa Eliakimu alikuwa msimamizi wa kasri chini ya Mfalme Hezekia.
Mwanamume mwingine aliyeitwa Eliakimu alikuwa mwana wa Mfalme Yosia. Alifanywa mfalme wa Yuda na farao wa Misri, Necho.
Necho alibadili jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu.
Elisabeti alikuwa mama wa Yohana Mbatizaji. Jina la mume wake lilikuwa Zakaria.
Zakaria na Elisabeti hawakuwahi kuweza kupata watoto, lakini katika uzee wao, Mungu alimuahidi Zakaria ya kwamba Elisabeti angezaa mtoto wa kiume.
Mungu alitunza ahadi yake, na punde Zakaria na Elisabeti wakaweza kupata mimba, naye akazaa mtoto wa kiume. Walimuita mtoto yule Yohana.
Elisabeti pia alikuwa jamaa kwa Mariamu, mama wa Yesu.
Elisha alikuwa nabii katika Israeli wakati wa tawala za wafalme wa Israeli: Ahanu, Ahazia, Yehoramu, Yehu, Yehoahazi, na Yehoashi.
Mungu alimwambia nabii Eliya kumpaka mafuta Elisha kama nabii.
Eliya alipochukuliwa kwenda mbinguni katika kibandawazi cha moto, Elisha akawa nabii wa Mungu kwa wafalme wa Israeli.
Elisha alifanya miujiza mingi, ikiwemo kuponya mwanamume kutoka Shamu aliyekuwa na ukoma na kufufua kutoka kwa wafu mtoto wa mwanamke kutoka Shunemu.
Eliya alikuwa mmoja wa manabii muhimu sana wa Yahwe. Eliya alitabiri katika wakati wa tawala za wafalme kadhaa wa Israeli au Yuda, akiwemo Mfalme Ahabu.
Mungu alifanya miujiza mingi kupitia Eliya, ikiwemo kumfufua mvulana mfu kurudi katika uhai.
Eliya alimkaripia Mfalme Ahabu kwa kuabudu mungu wa uongo Baali.
Aliwapa changamoto manabii wa Baali katika mtihani ambao ulithibitisha ya kwamba Yahwe ni Mungu mmoja wa kweli.
Katika mwisho wa maisha ya Eliya, Mungu alimchukua kimuujiza juu mbinguni angali bado yu hai.
Miaka mia moja baadaye, Eliya, pamoja na Musa, walijitokeza na Yesu juu ya mlima na waliongea pamoja juu ya kurudi, kuteseka na kufa kwa Yesu Yerusalemu.
Engedi ni jina la mji katika nyika ya Yuda kusini mashariki mwa Yerusalemu.
Engedi ilikuwa mahali mwa ukingo wa magharibi wa Bahari ya Chumvi.
Sehemu ya jina lake, "chemichemi" ina maana ya chemichemi ya maji ambayo inatiririka chini kutoka kwenye mji hadi baharini.
Engedi ilijulikana kwa kuwa na mashamba ya mizabibu mizuri na ardhi yenye rutuba nyingine, yawezekana kutokana na mwendelezo wa umwagiliaji kutoka kwa chemichemi ya maji.
Kulikuwa na ngome katika Engedi ambayo Daudi alitoroka kule alipokuwa akifukuzwa na Mfalme Sauli.
Esau alikuwa mmoja wa mapacha wana wa Isaka na Rebeka. Alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa. Pacha ndugu yake alikuwa Yakobo.
Esau aliuza haki yake ya mzawa wa kwanza kwa kaka yake Yakobo kwa kubadilishana na bakuri la chakula.
Kwa kuwa Esau alizaliwa kwanza, baba yake Isaka alitakuwa kumpatia baraka maalumu. Lakini Yakobo alimdanganya Isaka kumpatia hiyo baraka badala yake. Mara ya kwanza Esau alikuwa na hasira sana hadi alitaka kumuua Yakobo, lakini baadaye alimsamehe.
Esau alikuwa na watoto wengi na wajukuu, na vizazi hivi viliunda kuni kubwa la watu walioishi katika nchi ya Kaanani.
Esta alikuwa mwanamke wa Kiyahudi ambaye alikuwa malkia wa ufalme wa Ashuri katika kipindi cha mateka ya Babeli kwa Wayahudi.
Kitabu cha Esta kinaelezea simulizi ya jinsi Esta alivyokuwa mke wa mfalme wa Waashuri Ahasuero na jinsi Mungu alivyomtumia kukomboa watu wake.
Esta alikuwa yatima ambaye alikuzwa na binamu yake mkubwa, Mordekai.
Kutii kwake kwa baba yake wa kambo kulimsaidia kuwa mtiifu kwa Mungu.
Esta alimtii Mungu na kuweka maisha yake hatarini ili kuwakomboa watu wake, Wayahudi.
Simulizi ya Esta inaelezea utawala wa Mungu wa enzi juu ya matukio na historia, haswa jinsi anavyolinda watu wake na kutumika kupitia wale wanaomtii.
Ethiopia ni nchi katika Afrika iliyo kusini mwa Misri mpakana mwa Mto wa Naili magharibi na katika Bahari ya Shamu mashariki. Mtu kutoka Ethiopia na "mtu wa Ethiopia".
Ethiopia ya zamani ilikuwa kusini mwa Misri na ilijumuisha nchi ambayo kwa sasa ni sehemu ya baadhi ya nchi za Afrika, kama Sudani, Ethiopia ya sasa, Somalia, Kenya, Uganda, Afrika ya Kati na Chadi.
Katika Biblia, Ethiopia mara nyingine huitwa "Kushi" au "Nubia".
Nchi za Ethiopia ('Kushi') na Misri mara nyingine hutajwa pamoja katika Biblia, labda kwa sababu zilikuwa karibu na nyenzake na watu wake yawezekana walikuwa na mababu wa kufanana.
Mungu alimtuma Filipo mwinjilisti katika jangwa ambapo alisambaza habari njema kuhusu Yesu na towashi wa Ethiopia.
Ezekieli alikuwa nabii wa Mungu wakati wa kipindi cha uhamisho ambapo Wayahudi wengi walipelekwa Babeli.
Ezekieli alikuwa kuhani aliyeishi katika ufalme wa Yuda ambapo yeye na Wayahudi wengine wengi walikamatwa na jeshi la Babeli.
Kwa zaidi ya miaka ishirini, yeye na mke wake waliishi Babeli karibu na mto, na Wayahudi walikuja pale kumsikiliza akizungumza ujumbe kutoka kwa Mungu.
Miongoni mwa wafalme wengine, Ezekieli alitabiri juu ya uharibifu na ujenzi wa Yerusalemu na hekalu.
Pia alitabiri kuhusu ufalme wa baadaye wa Masihi.
Ezra alikuwa kuhani wa Israeli na mtaalamu wa sheria ya Kiyahudi ambaye aliweka kumbukumbu ya historia ya kurudi kwa Waisraeli Yerusalemu kutoka Babeli ambapo Israeli alikuwa mateka kwa miaka 70.
Ezra aliweka kumbukumbu ya sehemu hii ya historia ya Israeli katika kitabu cha kibiblia cha Ezra. Inawezekana aliandika kitabu cha Nehemia, kwa maana vitabu hivi viwili asili yake ilikuwa kitabu kimoja.
Ezra aliporudi Yerusalemu aliimarisha Sheria, kwa maana Waisraeli waliacha kutii Ssheria za Sabato na walioana na wanawake ambao walitenda dini za kipagani.
Ezra pia alisaidia kujenga hekalu ambalo liliharibiwa na Wababeli walipoteka Yerusalemu.
Kuna wanamume wengine wawili wanaoitwa Ezra waliotajwa katika Agano la Kale.
Hapo nyakati za kale wafalme waliotawala nchi ya Misri waliitwa Mafarao.
Filipi ulikuwa mji muhimu na koloni la Rumi lililokuwa Makedonia kaskazini mwa Ugiriki ya kale.
Mtume Filipo alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu alikuwa anatoka mji wa Bethsaida.
Katika kanisa la kwanza huko Yerusalemu Filipo alikuwa mmoja wa viongozi saba waliochaguliwa ili kuwajali masikini, Wakristo wenye uhitaji hasa wajane.
Finehasi ni jina la watu wawili katika agano la kale.
Nyakati za kale Finisia lilikuwa taifa lenye utajiri lililokuwa Kanaani karibu na pwani ya barari ya Mediteraniani, kaskazini mwa Israeli.
Gabrieli ni jina la mmoja wa malaika wa Mungu. Anatajwa kwa majina kadhaa, kote katika Agano la kale na Jipya.
Mungu alimtuma Gabrieli kumwambia nabii Danieli maana ya maono aliyoyaona. Muda mwingine, Danieli alipokuwa akiomba, malaika Gabrieli alipaa kwake na kutabiri kuhusu kile kitakachotokea hapo baadaye. Danieli alimfafanua kama "mwanamume". Katika Agano Jipya inaandikwa ya kwamba Gabrieli alitokana na Zakaria kutabiri ya kwamba mke wake mzee Elizabeti angepata mwana wa kiume, Yohana. Miezi sita baada ya hapo, Gabrieli alitumwa kwa Mariamu kumwambia ya kwamba Mungu angemuwezesha kwa miujiza kupata mimba ya mtoto amabye angekuwa "Mwana wa Mungu". Gabrieli alimwambia Mariamu kumuita mwanawe "Yesu" .
Gadi ni jina la mmoja wa wana wa Yakobo, yaani, Israeli.
Familia ya Gadi ilikuja kuwa moja ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Mwanamume mwingine katika Biblia aitwaye Gadi alikuwa nabii, ambaye alimkabili Mfalme Daudi kwa dhambi ya kufanya sensa ya watu wa Israeli. Miji ya Baalgadi na Migdalgadi kila moja wapo ni maneno mawili katika maandishi asili na mara nyigine huandikwa " Baali gadi" na "Migdali Gadi".
Katika kipindi cha Agano Jipya, Galataia ulikuwa mkoa mkubwa wa Kirumi ulioko sehemu ya kati ya mahali ambapo sasa ni nchi ya Uturuki.
Sehemu ya Galatia ilikuwa mpaka na Bahari Nyeusi upande wa Kaskazini. Ilikuwa mpakani na mikoa ya Asia, Bithinia, Kapadocia, Selisia na Pamfilia.
Mtume Paulo aliandika barua kwa Wakristo walioishi katika mkoa wa Galatia. Barua hii ni kitabu cha Agano Jipya cha "Wagalatia".
Sababu moja ambayo Paulo aliandika barua yake kwa Wagalatia ilikuwa kusisitiza tena injili ya wokovu kwa neema, na sio kazi.
Wakristo Wayunani wa Galatia walifundishwa na Wakristo wa Kiyahudi kule ya kwamba ilikuwa lazima kwa waumini kukaa na baadhi ya sheria za Kiyahudi.
Galilaya ni eneo la kaskazini ya Israeli, kaskazini ya Samaria. "Mgalilaya" alikuwa mtu ambaye aliishi Galilaya.
Galilaya, Samaria, na Yudea ilikuwa miji mitatu ya msingi ya Israeli wakati wa Agano Jipya.
Galilaya imepakana upande wa mashariki na ziwa kubwa liitwalo "Ziwa la Galilaya".
Yesu alikua na kuishi katika mji wa Nazareti Galilaya.
Miujiza mingi na mafundisho ya Yesu yalifanyika katika eneo la Galilaya.
Gathi ilikuwa moja ya miji mikubwa mitano ya Wafilisti. Ilikuwa kaskazini mwa Ekroni na mashariki ya Ashdodi na Ashkeloni.
Hodari wa Kifilisti Goliati alitoka katika mji wa Gathi.
Katika wakati wa Samueli, Wafilisti waliiba sanduku la agano kutoka Israeli na kulipeleka katika hekalu lao la kipagani kule Ashdodi. Baadaye likahamishwa kwenda Gathi na baadaye Ekroni. Lakini Mungu aliwaadhibu watu wa miji hiyo na maradhi, kwa hiyo walilirudisha Israeli tena.
Daudi alipokuwa akitoroka kutoka kwa Mfalme Sauli, alielekea Gathi na kuishi kule kwa muda pamoja na wake zake wawili na wanamume mia sita waliokuwa wafuasi wake waaminifu.
Wakati wa Biblia, Gaza ulikuwa mji tajiri wa Kifilisti uliokuwa pwani mwa Bahari ya Mediteranea, kama kilomita 38 kusini ya Ashdodi. Ilikuwa moja ya miji mitano mikuu ya Filisti.
Kwa sababu ya mahali ilipo, Gaza ilikuwa bandari muhimu ambapo masuala ya kibiashara yalifanyika kati ya makundi ya watu wengi tofauti na mataifa.
Leo, mji wa Gaza bado ni bandari muhimu katika kanda ya Gaza, ambayo ni eneo la nchi iliyoko katika pwani ya Bahari ya Mediteranea iliyopakana na Israeli upande wa kaskazini na mashariki, na kusini mwa Misri.
Gaza ilikuwa mji ambao Wafilisti walimchukua Samsoni baada ya kumkamata.
Filipo mwinjilisti alikuwa akitembea katika barabara ya jangwa kuelekea Gaza alipokutana na towashi wa Ethiopia.
Gerari ni mji na sehemu katika nchi ya Kaanani, iliyopo kusini magharibi mwa Hebroni na kaskazini magharibi mwa Beersheba.
Mfalme Abimeleki alikuwa mtawala wa Gerari pale Abrahamu na Sara walipokuwa pale.
Wafilisti walitawala eneo la Gerari wakati wa kipindi Waisraeli waliishi Kaanani.
Katika kipindi cha Mfalme Daudi, Geshuri ilikuwa ufalme mdogo uliokuwa upande wa mashariki wa Ziwa la Galilaya, kati ya nchi za Israeli na Aramu.
Mfalme Daudi alimuoa Maaka, binti wa mfalme wa Geshuri na akamzalia mwana wa kiume, Absalomu.
Baada ya kumuua ndugu yake Amnoni, Absalomu alikimbilia kaskazini mashariki mwa Yerusalemu hadi Geshuri, umbali wa kama maili 88. Alikaa kule miaka mitatu.
Gethsemane ilikuwa bustani ya mizeituni mashariki mwa Yerusalemu mbali ya bonde la Kidroni karibu na Mlima wa Mizeutuni.
Bustani ya Gethsemane ilikuwa sehemu ambapo Yesu na wafuasi wake walienda kuwa wenyewe na kupumzika, mbali na mikusanyiko.
Ilikuwa Gethsemane ambapo Yesu aliomba kwa huzuni kubwa, kabla ya kukamatwa pale na viongozi wa Kiyahudi.
Gibea ni jina la mji ambao ulikuwa kaskazini mwa Yerusalemu na kusini ya Betheli.
Gibea ilikuwa eneo la kabila la Benyamini.
Ilikuwa eneo la vita kubwa kati ya Wabenyamini na Israeli.
Gibeoni ilikuwa mji ambao ulikuwa kama kilomita 13 kaskazini magharibi mwa Yerusalemu. Watu walioishi Gibeoni walikuwa Wagibeoni.
Wagibeoni waliposikia jinsi Waisraeli wameangamiza miji ya Yeriko na Ai, waliogopa.
Kwa hiyo Wagibeoni walikuja kwa viongozi wa Israeli Gilgali na kuvunga kuwa watu kutoka nchi ya mbali.
Viongozi wa Israeli walidanganywa na kufanya makubaliano na Wagibeoni ya kwamba watawalinda na kutowaangamiza.
Gideoni alikuwa mwanamume wa Kiisraeli ambaye aliinuliwa na Mungu kuwakomboa Waisraeli kutoka kwa adui zao.
Katika kipindi ambacho Gideoni aliishi, kundi la watu lijulikanalo kama Midiani waliendelea kuwashambulia Waisraeli na kuangamiza mazao yao.
Ingawa Gideoni aliogopa, Mungu alimtumia kuwaongoza Waisraeli kupigana dhidi ya Midiani na kuwashinda.
Gideoni pia alimtii Mungu kwa kuangusha madhabahu chini ya miungu wa uongo wa Baali na Ashera.
Hakuwaongoza tu watu katika kuwashinda adui zao lakini pia aliwatia moyo kutii na kumwabudu Yahwe, Mungu mmoja wa ukweli.
Gileadi ni jina na eneo la milima mashariki mwa mto Yordani, ambapo kabila la Waisraeli la Gadi, Rubeni na Manase waliishi.
Eneo hili pia lilijulikana kama "nchi ya mlima wa Gileadi" au "Mlima Gileadi".
"Gileadi" ilikuwa jina la wanamume kadhaa katika Agano la Kale. Mmoja wa wanamume hawa alikuwa mjukuu wa Manase. Gileadi mwingine alikuwa baba wa Yefta.
Msemo Gilgali ulikuwa mji kaskazini mwa Yeriko na ilikuwa sehemu ya kwanza ambayo Waisraeli waliweka kambi baada ya kuvuka mto Yordani kuingia Kaanani.
Kula Gilgali, Yoshua aliweka mawe kumi na mawili kutoka mto uliokauka wa Mto Yordani ambao walimaliza kuuvuka.
Gilgali ulikuwa mji ambao Eliya na Elisha walishi walipovuka Yordani pale Eliya alipochukuliwa kwenda mbinguni.
Kulikuwa na sehemu zingine pia zijulikanazo kama "Gilgali" katika Agano la Kale.
Neno "gilgali" lina maana ya "mduara wa mawe" labda kumaanisha sehemu ambapo dhabahu ya mduara ilijengwa.
Katika Agano la Kale, jina hili mara nyingi hujitokeza kama "gilgali". Hii inaweza kuonyesha ya kwamba haikuwa mahali bayana lakini ilikuwa ufafanuzi wa ain fulani ya sehemu.
Katika kipindi cha Agano Jipya, Giriki ilikuwa mkoa katika Ufalme wa Kirumi.
Kama nchi ya siku ya sasa ya Giriki, ilikuwa katika peninsula ambayo ilikuwa mpakani na Bahari ya Mediteranea, Bahari ya Aegea, na Bahari ya Ionia.
Mtume Paulo alizuru miji kadhaa ya Giriki, na kuimarisha makanisa katika miji ya Korintho, Thesalonike, na Filipi na labda mingine.
Watu ambao hutoka Giriki wanaitwa "Wagiriki" na lugha yao ni "Kigiriki". Watu kutoka mikoa mingine ya Kirumi pia walizungumza Kigiriki, ikiwemo Wayahudi wengine.
Mara nyingine msemo "Giriki" hutumika kumaanisha Mataifa.
Msemo "Golgotha" ni jina la mahali ambapo Yesu alisulubiwa. Inatokana na neno la Kiaramea ambalo lina maana ya "Fuvu la kichwa" au "Mahali pa fuvu la kichwa".
Golgotha ilikuwa mahali nje ya kuta za mji wa Yerusalemu, eneo la karibu. Labda ilikuwa mahali ya mteremko wa Mlima wa Mizeituni.
Katika tafsiri za Kiingereza za zamani za Biblia, Golgotha inatafsiriwa kama "Kalivari" ambayo inatokana na neno la Kilatini kwa ajili ya "fuvu la kichwa".
Tafsiri nyingi za Biblia hutumia neno ambalo huonekana au kusikika kama "Golgotha" kwa maana maana yake tayari imefafanuliwa katika maandisha ya Biblia.
Goliati alikuwa mwanajeshi mrefu sana, na mkubwa sana katika jeshi la Wafilisti ambaye aliuwawa na Daudi.
Goliati alikuwa kati ya mita mbili au tatu kwa urefu. Mara nyingi huchukuliwa kama jitu kwa sababu ya umbo lake kubwa.
Ingawa Goliati alikuwa na silaha bora zaidi na mkubwa kuliko Daudi, Mungu alimpa Daudi nguvu na uwezo wa kumshinda Goliati.
Waisraeli walitangazwa washindi juu ya Wafilisti kama matokea ya ushindi wa Daudi juu ya Goliati.
Gomora ilikuwa mji katika bonde lenye rutuba, karibu na Sodoma ambapo mpwa wa Abrahamu Lutu alichagua kuishi.
Mahali haswa pa Gomora na Sodoma hapajulikani, lakina kuna viashiria ya kwamba inaweza kuwa mahali moja kwa moja kusini mwa Bahari ya Chumvi, karibu na Bonde la Sidimu.
Kulikuwa na wafalme wengi vitani katika eneo ambapo Sodoma na Gomora na ilikuwepo.
Familia ya Lutu ilipokamtwa katika ugomvi kati ya Sodoma na miji mingine, Abrahamu na wanamume wake waliwakomboa.
Sio muda baada ya hapo, Sodoma na Gomora ziliteketezwa na Mungu kwa sababu ya uovu wa watu walioishi pale.
Gosheni ni jina la eneo la nchi yenye rutuba ambalo lilikuwa mahali katika Mto Naili katika sehemu ya kusini ya Misri.
Yusufi alipokuwa mtawala wa Misri, baba yake na ndugu na familia zao walikuja kuishi Gosheni kutoroka njaa Kaanani.
Wao na uzao wao waliishi vzuri Gosheni kwa zaidi ya miaka 400, lakini walilazimishwa katika utumwa na farao wa Kimisri.
Hatimaye Mungu alimtuma Musa kuwasaidia watu wa Israeli kuondoka nchi ya Gosheni na kutoroka utumwa.
Habakuki alikuwa ni nabii wa Agano la Kale aliyeishi kipindi cha Mfalme Yehoyakimu alipokuwa akiitawala Yuda. Pia, nabii Yeremia alikuwa bado yuko hai katika kipindi hicho. Nabii huyu aliandika kitabu cha Habakuki mnamo mwaka 600 KK, katika kipindi ambacho Wababeli walikuwa wameuhusuru mji wa Yerusalem na kuchukua watu wengi wa Yuda na kuwapeleka matekani. Yahweh alimpa Habakuki unabii kuhusu Wakaldayo (Wababeli) ambao wangekuja na kuwateka watu wa Yuda. Moja kati ya misemo maarufu na iliyojulikana sana ya nabii Habakuki ni "Mwenye haki ataishi kwa imani."
Habili alikuwa mtoto wa Adamu na Hawa. Alikuwa ndogo wake na Kaini.
Habili alikuwa mfugaji.
Habili alitoa sadaka ya baadhi ya mifugo yake kwa Mungu.
Mungu alipendezwa na sadaka ya Habili.
Mtoto wa kwanza wa Adamu na Hawa, Kaini alimuua Habili.
Hagai alikuwa ni nabii wa Yuda katika kipindi ambacho Wayahudi walikuwa wamerudi kutoka matekani huko Babeli.
Hagai alitabiri katika kipindi ambacho watu wa Israeli walikuwa chini ya utawala wa liwali Zerubabeli.
katika kipindi hiki pia, nabii Zekaria alikuwa akitabiri yaani Hagai na Zekaria walifanya kazi katika kipindi kimoja.
Hagai na Zekaria waliwasihi sana Wayahudi ili walijenge Hekalu ambalo lilikuwa limebomolewa na Wababeli chini ya mfalme Nebukadreza.
Hajiri alikuwa ni mwanamke wa Kimisri alikuwa mtumwa wa Sara. Sara alimtoa Hajiri kwa Ibrahimu ili aweze kuzaa naye, baada ya kuona kuwa yeye (Sara) hana uwezo wa kuzaa . Hajiri alipata mimba na akamzalia Ibrahim mwana, Ishmaeli. Mungu aliiangalia taabu ya Hajiri katika jangwa na akaahidi kuubariki uzao wa Hajiri.
Hamathi ulikuwa ni mji muhimu sana kasikazini mwa Kanaani. Wahamathi walikuwa ni uzao wa mtoto wa Nuhu, Kanaani. Jina 'Lebo Hamathi' huenda linarejelea mlima ulikuwa karibu na mji wa Hamathi. Baadhi ya tafsiri hufasiri 'Lebo Hamathi' kama "Mlango wa Hamathi" Mfalme Daudi alimshinda mfalme Tou wa Hamathi, ushindi ambao uliwafanya kuwa katika makubaliano na mahusiano mazuri. Hamathi ulikuwa ni mji wa bohari au ghala la mfalme Sulemani, mahali ambapo alitunza hazina yake. Ni katika nchi hii ya Hamathi ambapo mfalme Zedekia aliuawa na mfalme Nebukadreza, pia ni mahali ambapo mfalme Yehoyazi alikamatwa na Farao wa Misri. Neno 'Wahamathi' laweza kutafsiriwa kama ' watu wa Hamathi'
Hamori alikuwa mkanaani aliyeishi katika mji wa Shekemu katika kipindi ambacho Yakobo na familia yake walikuwa wakiishi karibu na Sukothi. Alikuwa ni Mhivi. Yakobo alinunu eneo la maziko kutoka kwa wana wa Hamori. Wakali wakiwa huko mwana mmoja wa Hamori, Shekemu alimbaka binti wa Yakobo aliyeitwa Dina. Kaka zake na Dina walilipiza kisasi kwa familia ya Hamori na kuwaua watu wote katika mji wa shekemu.
Hamu ni mtoto wa pili kati ya wana watatu wa Nuhu. katika gharika kuu la kidunia ambalo liliigharikisha dunia yote, Hamu na ndugu zake pamoja na wake zao walikuwa pamoja na baba yao, Nuhu katika safina. Baada ya gharika, kulikuwa na tukio la Hamu kutomweshimu baba yake, Nuhu. Na matokeo yake, Nuhu alimlaani mtoto wa Hamu alilyeitwa Kanaani pamoja na uzao wake wote, ambao baadaye walijulikana kama Wakanaani.
Hana alikuwa ni mama wa nabii Samwel. Alikuwa ni mmoja kati ya wake waili wa Elikana.
Hana alikuwa tasa, alikuwa hawezi kuzaa mtoto. Hiki kilikuwa ni kilio kikubwa sana kwa Hana.
Hana alimwomba Mungu kwa bidii sana hekaluni ili apate mtoto. Hana alimwahidi Mungu kumtoa mtoto huyu ili amtumikie Mungu.
Mungu alimpa haja yake na mtoto Samweli alipokuwa na umri wa kutosha, alimleta ili atumike hekaluni hekaluni.
Mungu alimpa Hana watoto wengine baada ya hayo.
Jina Hanania limetumika katika Agano la Kale kurejelea watu mbalimbali. Hanania mmoja alikuwa ni mwisraeli aliyechukuliwa matekani huko Babeli ambaye Jina lake lilibadilishwa na kuwa 'Shadraka.' kutoka na tabia na uwezo wake, alipewa nafasi nzuri maana alikuwa mtumwa wa kifalme. Hanania (Shadraka) na vijana wengine wawili wa Kiisraeli walitupwa katika tanuru la mot kwasababu walikataa kumwabudu wa mfalme wa Babeli. Mungu alionesha uwezo wake kwa kuwalinda ili wasije wakadhurika. Hanania mwingine alikuwa ni mzao wa ukoo wa Mfalme Sulemani. Kulikuwa na Hanania mwingine tofauti aliyekuwa nabii wa uongo katika kipindi cha nabii Yeremia. Mtu mmoja aliyeitwa Hanania alikuwa ni kuhani aliyesaidia kuongoza sherehe katika kipindi cha Nehemia.
Harani alikuwa kaka mdogo wa Ibrahimu na baba yake na Lutu. harani pia lilikuwa ni jina la mji ambao Ibrahimu na familia yake waliishi kwa muda mfupi walipokuwa njiani kutoka Uru kwenda nchi ya Kanaani. Mtu mwingine tofauti aliyeitwa Harani alikuwa ni mtoto wa Kalebu. Mtu wa tatu katika Biblia aliyeitwa Harani alikuwa ni wa uzao wa Lawi.
Haruni alikuwa kaka yake na Musa. Mungu alimchagua Haruni kuwa kuhani mkuu wa kwanza wa watu wa Israeli. Haruni alimsaidia Musa kuzungumza na Farao kuhusu kuwaachia huru wana wa Israeli. Wakati wana wa Israeli wanasafiri jangwani, Haruni alitenda dhambi kwa kutengeneza sanamu ili watu waiabudu. Pia Mungu alimchagua Haruni na uzao wake kuwa makuhani.
Hili lilikuwa jina la mwanamke wa kwanza. Jina lake linamaanisha "uhai" au "kuishi".
Mungu alimuumba Hawa kutoka kwa ubavu ambao aliuchukua kutoka kwa Adamu.
Hawa aliumbwa kuwa "msaidizi" wa Adamu. Alikuja kando ya Adamu kumsaidia katika kazi ambayo Mungu aliwapa kufanya.
Hawa alijaribiwa na Shetani (kwa mfano wa nyoka) na alikuwa wa kwanza kufanya dhambi kwa kula tunda ambalo Mungu aliwaambia kutokula.
Hebroni ulikuwa ni mji uliokuwa katika milima mirefu na ya miamba kama maili 20 hivi kusini mwa Yerusalemu. Mji huu ulijengwa mnamo mwaka 2000 KK katika kipindi cha Abramu. Mji huu ulitajwa mara nyingi katika mtiririko wa matukio mbalimbali katika Agano la Kale. Mji wa Hebroni ulikuwa na wajibu na nafasi ya muhimu sana katika maisha ya Mfalme Daudi. Wana kadhaa wa Mfalme Daudi kama vile Absalomu walizaliwa huko. Mji huu uliharibiwa na Warumi mnamo mwaka 70 BK.
Henoko ni jina la wanamume wawili katika Agano la Kale.
Mwanamume mmoja aliyeitwa Henoko alitokana kwa Sethi. Alikuwa babu mkuu wa Nuhu.
Henoko huyu alikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu na alipokuwa na miaka 365, Mungu alimchukua kwenda mbinguni bila ya kufa.
Mwanamume tofauti aliyeitwa Henoko alikuwa mwana wa Kaini.
Katika kipindi kirefu cha maisha ya Yesu, Herode Antipa alikuwa ni mtawala wa Dola ya Kirumi iliyojumuisha jimbo la Galilaya. Antipa mara nyingine alitajwa kama 'Mfalme" kama alivyokuwa baba yake, Herode Mkuu, ingawa hakuwa mfalme kweli. Herode Antipa alitawala robo au moja ya nne ya Dola ya Kirumi na hivyo aliitwa Herode 'Tetraki' yaani mkuu wa mkoa. Antipa ni 'Herode' aliye Yohamuru Yohana mbatizaji auawe kwa kukatwa kichwa. Alikuwa ni Herode Antipa pia aliyemwuuliza Yesu maswali kabla ya kusulubiwa kwake. Maherode wengine katika Agano Jipya walikuwa ni mtoto wa Antipa (Agripa) na mjukuu ( Agripa wa pili) aliyetawala kipindi cha mitume.
Herode mkuu alikuwa akitawala Uyahudi
Herodia alikuwa ni mke wa Herode Antipa huko Uyahudi kipindi cha Yohana Mbatizaji. Herodia alikuwa mke halali wa kaka yake na Antipa, aliyeitwa Philipo, lakini baadaye aliolewa na Herodi Antipa kinyume na sheria. Yohana mbatizaji aliwakemea Herode na Herodia kwa sababu ya ndoa yao haramu. Na kwasababu hiyo, Yohana alifungwa gerezani na baadaye aliuawa kwa kukatwa kichwa.
Hezekia alikuwa ni mfalme wa 13 wa ufalme wa Yuda. Alikuwa ni mfalme aliyemtumaini Mungu na kumtii. Tofauti na baba yake, Ahazi aliyekuwa mfalme mwovu, Mfalme Hezekia alikuwa ni mfalme mzuri aliyeharibu maeneo yote ya ibada ya miungu katika Yuda. Wakati Hezekia alipougua na alipokuwa karibu kufa, alimwomba Mungu sana ili alinde na kuhifadhi maisha yake. Mungu alimponya na alimruhusu kuishi miaka 15 zaidi. Mungu alifanya muujiza kwa Hezekia kwa kurudisha muda nyuma. Mungu alijibu maombi ya Hezekia kwa kuwaokoa watu wake kutoka mikononi mwa Mfalme Senakaribu wa Siria, aliyekuwa akiwashambulia.
Hilikia lilikuwa ni jina la kuhani mkuu katika kipindi cha utawala wa mfalme Yosia. Hilikia alipata kitabu cha sheria, katika kipindi ambacho hekalu lilifanyiwa matengenezo na akamuru kitabu hicho kipelekwe kwa mfalme Yosia. Baada ya kusomewa kitabu cha sheria, Yosia alihuzunika na aliwafanya watu wa Israeli kumwabudu Yahweh tena na kutii sheria zake. Mtu mwingine aliyeitwa Hilikia alikuwa ni mwana wa Eliyakimu na alifanya kazi ikulu kipindi cha utawala wa mfalme Hezekia.
Mlima Horebu ni jina jingine la mlima Sinai, mahali ambapo Mungu alimpa Musa vipande vya mawe vya amri kumi za Mungu. Mlima Horebu huitwa Mlima wa Mungu Musa aliiona kichaka kilichokuwa kinawaka moto wakati akichunga kondoo katika mlima Horebu. Katika mlima Horebu, Mungu alifunua agano lake kwa Waisraeli kwa kuwapa vipande vya mawe vilivyo na Amri juu yake. Ni mahali ambapo Mungu alimwambia Musa kuupiga mwamba ili maji yatoke kwa ajili ya waisraeli katika kipindi walichokuwa wanazunguka jangwani. Sehemu maalumu ulipo mlima huu haijulikani, huenda ni sehemu ya kusini ambayo kwa sasa inajulikana kama 'Penisula ya Sinai Inawezekana kuwa Horebu lilikuwa ni jina kamili la mlima na kwamba Mlima Sinai ina maana ya milima ya Sinai kwa kurejelea ukweli kwamba Mlima Horebu ulikuwa katika jangwa la Sinai.
Hosea alikuwa ni nabii wa Israeli aliyeishi na kutabiri mnamo mwaka 750 KK. Huduma yake Hosea ilidumu kwa miaka mingi katika vipindi vya wafalme kadhaa, kama vile Yeroboam, Zekaria, Yotham, Ahazi, Hoshea, Uzia na Hezekia. Hosea aliambiwa na Mungu kuoa kahaba aliyeitwa Gomeri . Ingawa alikuwa mwanamke aliyekuwa si mwaminifu, Hosea aliambiwa aendelee kumpenda. Hii ilikuwa picha inayoonyesha Upendo wa Mungu kwa ajli ya watu wake, Israeli waliokuwa si waaminifu. Hosea alitabiri kinyume na watu wa Israeli kwasababu ya dhambi zao, akiwaonya kugeuka na kuacha kuabudu miungu.
Hoshea lilikuwa ni jina la Mfalme wa Israeli na baadhi ya watu wengine katika Biblia. Hoshea mwana wa Ala, alikuwa ni Mfalme wa Israeli kwa miaka tisa katika kipindi ambacho Ahazi na Hezekia walikuwa wafalme wa Yuda. Yoshua mwana wa Nuni aliitwa Hoshea hapo awali. Musa alilibadilisha jina lake na kuwa Yoshua kabla ya kumtuma pamoja na wale wanaume kumi na mmoja kuipeleleza nchi ya Wakanaani. Baada ya kufa kwa Musa, Joshua aliwaongoza watu wa Israeli kuimiliki nchi ya Kanaani. Mtu mwingine aliyeitwa Hoshea alikuwa ni mwana wa Azazia na alikuwa ni mmoja wa viongozi wa Waefraimu.
Ikonio ulikuwa mji sehemu ya kusini kati ya nchi ambayo sasa ni Uturuki.
Katika safari ya kwanza ya kimisionari ya Paulo, yeye na Barnaba walienda Ikonio baada ya Wayahudi kuwalazimisha kuondoka katika mji wa Antiokia. Kisha wayahudi wasioamini na Wayunani ndani ya Ikonio walipanga pia kumponda mawe Paulo na watumishi wenzeka, lakini walitoroka katika mji wa karibu wa Listra. Baada ya watu kutoka Antiokia na Ikonia kuja Listra na kuwachochea watu kumponda mawe Paulo.
Isaka alikuwa mwana pekee wa Abrahamu na Sara. Mungu aliwaahidi kuwapa mwana wa kiume ingiwa walikuwa wazee sana.
Jina "Isaka" linamaanisha "kicheko." Mungu alipomuambia Abrahamu kuwa Sara atazaa mwana wa kiume, Abrahamu alicheka kwa sababu wote walikuwa wazee sana. Baada ya muda, Sara pia alicheka aliposikia taarifa hii. Lakini Mungu alitimiza ahadi yake na Isaka alizaliwa kwa Abrahamu na sara katika uzee wao. Mungu alimuambia Abrahamu kuwa agano alilofanya na Abrahamu itakuwa pia ya Isaka na vizazi vyake milele. Wakati Isaka alikuwa kijana, Mungu aliijaribu imani ya Abrahamu kwa kumuamuru kumtoa isaka kama sadaka. Mwana wa Isaka, Yakobo, alikuwa na wana kumi na mbili ambao uzao wao baadaye ukawa makabila kumi na mbili ya taifa la Israeli.
Isakari alikuwa mwana wa tano wa Yakobo. Mama yake alikuwa Lea.
Kabila la Isakari lilikuwa moja ya makabila kumi na mbili ya Israeli. Nchi ya Isakari ilikuwa jirani na Naftali, Zabuloni, Manase, na Gadi. Ilikuwa chini ya bahari la Galilaya.
Isaya alikuwa nabii wa Mungu aliyetabiri wakati wa utawala wa wafalme wanne wa Yuda: Uzia, Yothamu, Ahazi, na Hezekia.
Aliishi Yerusalemu wakati Waashuri walipokuwa wakivamia mji, wakati wa utawala wa Hezekia. Kitabu cha Agano la Kale cha Isaya ni moja ya vitabu vikuu vya Biblia. Isaya aliandika unabii mwingi ulitokea wakati wa uhai wake. Isaya anajulikana zaidi kwa unabii alioandika kumhusu Masihi uliotimia miaka 700 baadaye wakati Yesu alipoishi duniani. Yesu na wanafunzi wake walinukuu utabiri wa Isaya kuwafundisha watu kuhusu Masihi.
Ishmaeli alikuwa mwana wa Abrahamu na mtumwa wa Kimisri Hagai. Kuna wana kadhaa pia katika Agano la Kale wanaoitwa Ishmaeli.
Jina "Ishmaeli" linamaanisha, "Mungu husikia." Mungu aliahidi kumbariki mwana wa Abrahamu, Ishmaeli, lakini hakuwa mwana ambaye Mungu aliye ahidi kuweka agano lake naye. Mungu alimlinda Hagai na Ishmaeli walipotumwa jangwani. Wakati Ishmaeli alipokuwa akiishi katika jangwa la Parani, alimuoa mwanamke wa Misri. Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa afisa wa jeshi kutoka Yuda aliyeongoza kundi la wanaume kumua gavana aliyeteuliwa na mfalme wa Kibabeli, Nebukadreza. Pia kuna wanaume wengine wanne walioitwa Ishmaeli katika Agano la Kale.
Majina Kadeshi, Kadesh-Barnea, na Meriba Kadeshi yote yanazungumzia mji muhimu katika historia ya Israeli ambao ulikuwa sehemu ya kusini ya Israeli, karibu na eneo la Edomu.
Mji wa Kadeshi palikuwa oasisi, mahali palipokuwa na maji na udongo wenye virutubisho katikati ya jangwa liitwalo Sini. Musa alituma wapelelezi kumi na mbili katika nchi ya Kanaani kutoka Kadesh-Barnea. Israeli pia waliweka kambi Kadeshi wakati wakizunguka-zunguka jangwani. Kadesh-Barnea ndipo Miriamu alipofia. Ilikuwa Kadesh-Barnea ambapo Musa hakumtii Mungu na kuupiga mwamba kupata maji kwa ajili ya Waisraeli, badala ya kuzungumza nayo kama Mungu alivyomuagiza. Jina "Kadeshi" linatoka katika neno la Kihebrania lenye maana ya "takatifu" au "kuwekwa tofauti."
Kaini na mdogo wake Abeli walikuwa atoto wakwanza wa Adam na Hawa wametajwa katika Biblia.
Neno "Kaisari" lilikuwa jina au jina la heshima lililotumika kwa watawala wengi wa Dola ya Rumi. Katika Biblia, hili neno linahusisha kwa tawala tatu tofauti tofauti.
Katika majina kama Kaisari Agustino au Tiberia Kaisari, "Kaisari" inaweza kutamkwa karibia na vile lugha ya taifa inavolitamka.
Kaisaria ulikuwa mji wa muhimu katika pwani ya Bahari ya Meditrania, kama 39 kilomita kusini mwa Mlima Karmeli Kaisaria Filipi ulikuwa mji unaoonyesha kusinimagharibi sehemu ya Israeli, karibu na Mlima Herimoni.
Kalebu alikuwa mmoja wa wapelelezi wa Israeli ambao walitumwa na Munsa kuipeleleza nchi ya Kanaani.
Kana kilikuwa kijiji au mji katika Galilaya, maili tisa kaskazini mwa Nazareti.
Kanaani alikuwa mtoto wa Hamu, ambaye alikuwa moja ya watoto wa Nuhu. Wakanaani walikuwa vizazi vya Kanaani.
Kapranaumu kilikuwa kijiji cha uvuvi katika kusini magaharibi ya pwani ya Bahari ya Galilaya.
Mlima Karmeli ni mlima uliokuwa pwani mwa bahari ya Mediteraniani kaskazini mwa nchi tambarare ya Sharon. Urefu wake ni mita 546.
Kedari lilikuwa jina la mwana wa pili wa Ishmaeli. Lilikuwa pia jina la mji muhimu ambalo linawezekana kuwa liliitwa baada ya huyo mwanamme
Mji wa Kaderi inapatikana katika eneo la kaskazini la Arabia karibu na mpaka wa kusini ya Filisti. Katika nyakati za Biblia, palikuwa panajulikana kwa ukuu na uzuri wake. Wazawa wa Kaderi waliunda kundi kubwa la watu linaloitwa "Kaderi." Usemi "hema za Kedari nyeusi" inamaanisha hema za nywele nyeusi za mbuzi ambamo watu wa Kaderi waliishi. Watu hawa walifuga kondoo na mbuzi. Pia walitumia ngamia kwa kusarifishia vitu. Katika Biblia, usemi "utukufu wa Kedari" inamaanisha ukuu wa mji na watu wake.
Kedeshi ulikuwa mji wa Kanaani uliochukuliwa na Waisraeli walipoingia Kanaani.
Mji huu ulikuwa sehemu ya kaskazini mwa Israeli, katika kipande walichopewa kabila la Naftali. Kedeshi ulikuwa moja ya miji iliyochaguliwa kwa ajili ya makuhani wa Kilawi kuishi, kwa sababu hawakuwa na ardhi yao wenyewe. Ilitengwa pia kama "mji wa ukimbizi."
Kefa alikuwa kuhani wa Israeli katika kipindi cha Yohana Mbatizaji na Yesu.
Kilikia ni mkoa mdogo wa Rumi uliokuwa kusini mashariki mwa nchi ya Uturuki.
Kipro ni kisiwa katika bahari ya Mediteraniani karibu kilometa 64 kusini mwa nchi ya sasa ya Uturuki.
Katika agano jipya Kolosai ulikuwa mji katika Rumi nchi ambayo sasa ni kusini mangharibi mwa uturuki. Wakolosai ni watu walioishi Kolosai.
Kora lilikuwa jina la wanaume watatu katika Agano la Kale.
Mmoja wa wana wa Esau aliitwa Kora. Alikuwa kiongozi katika jamii yake. Kora pia alikuwa mzawa wa Lawi na kwa hiyo alitumika katika maskani kama kuhani. Alikuwa na wivu juu ya Musa na Haruni na kuongoza kundi la watu kuwapinga. Mwanamme wa tatu aliyeitwa Kora aliorodheshwa kama uzao wa Yuda.
Koreshi alikuwa mfalme wa Uajemi aliyetengeneza himaya ya Uajemi katika mwaka wa 550 Kabla ya Kristo kwa njia ya kutawala Kijeshi. Katika historia alijulikana kama Koreshi mkuu.
Korintho ulikuwa mji katika nchi ya Ugiriki maili 50 mangharibi mwa Athene. Wakorintho walikuwa watu walioishi Korintho.
Kornerio alikuwa mtu wa Mataifa, asiye Myahudi afisa wa jeshi la Rumi.
Krene ulikuwa mji wa Kigiriki kaskazini mwa pwani ya Afrika kwa upande wa bahari ya Mediteraniani, moja kwa moja kusini mwa kisiwa cha Krene.
Krete ni kisiwa kilichokuwepo kusini mwa fukwe ya Ugiriki. Mkrene ni mtu aliyeishi katika kisiwa hicho.
Kushi lilikuwa jina la mtoto mkubwa na Nuhu, Hamu. Pia alikuwa babu wa Nimrodi. Kaka zake wawili waliitwa Misri na Kanaani.
Katika Agano la Kale, Labani alikuwa mjomba na baba mkwe wa Yakobo.
Yakobo aliishi na nyumba ya Labani Padan-aramu na kuchunga kondoo na mbuzi wake kama sharti la ndoa kwa binti wa Labani. Pendeleo la Yakobo kwa mabinti wa Labani lilikuwa Raheli kuwa mke wake. Labani alimdanganya Yakobo na kumfanya kumuoa binti yake mkubwa Lea kabla ya kumpa Raheli kama mke wa pili.
Lameki lilikuwa jina la wanaume wawili waliotajwa katika kitabu cha Mwanzo.
Lameki wa kwanza aliyetajwa alikuwa uzao wa Kaini. Alijivunia kwa wake zake wawili kuwa alimuua mtu kwa kumuumiza. Lameki wa pili alikuwa uzao wa Sethi. Alikuwa pia baba wa Nuhu.
Lazaro na dada zake, Mariamu na Martha, walikuwa marafika wa karibu wa Yesu. Mara nyingi alikaa nao katika nyumba yao Bethania.
Lazaro anajulikana zaidi kwa kufufuliwa na Yesu kutoka wafu baada ya kuzikwa kaburini kwa siku kadhaa. Viongozi wa Kiyahudi walikasirika na kuwa na wivu kuwa Yesu alifanya muijiza huu na wakatafuta njia ya kumua Yesu na Lazaro. Yesu pia alitoa fumbo kuhusu maskini ombaomba na mtu tajiri ambapo ombaomba aliitwa "Lazaro."
Lea alikuwa mmoja wa wake wa Yakobo. Alikuwa mama wa wana kumi wa Yakobo ambao uzao wao ni miongoni wa makabila kumi na mbili ya Israeli.
Baba wa Lea alikuwa Labani, aliyekuwa kaka wa mama yake Yakobo, Rebeka. Yakobo hakumpenda Lea kama alivyompenda mke wake mwingine Raheli, lakini Mungu alimbariki kwa wingi Lea kwa kumpa watoto wengi. Mmoja wa wana wa Lea, Yuda, alikuwa babu wa mfalme Daudi na Yesu.
Labanoni ni sehemu nzuri yenye milima iliyopo mwambao wa Bahari Kuu, kaskazini mwa Israeli. Katika nyakati za Biblia, eneo hili lilikuwa limejaa misonobari, kama seda na mvinje.
Mfalme Sulemani alituma wafanyakazi Lebanoni kuvuna miti ya seda kwa ajili ya kujengea hekalu la Mungu. Lebanoni ya zamani waliishi watu wa Fonikia ambao walikuwa wajenzi wenye ujuzi wa meli zilizotumika kwa viwanda vya biashara vizuri. Miji ya Tiro na Sidoni ilikuwa Lebanoni. Ilikuwa katika miji hii ambamo rangi ya zambarau ilitumika kwanza.
Neno "Lewiathani" linamaanisha mnyama mkubwa sana aliyekuwepo zamani katika maandishi ya kwanza ya Agano la Kale, katika vitabu vya Ayubu, Zaburi na Isaya.
Lewiathani anaelezwa kuwa kama joka, mwenye nguvu na mkali na mwenye uwezo wa kufanya maji yaliyomzunguka "kuchemka." Maelezo yake yanakaribiana na yale ya wanyama wakubwa sana waliokuwepo zamani. Nabii Isaya anaelezea Lewiathani kama "joka wa kutereza". Ayubu anaandika kama mtu mwenye ujuzi mzuri wa Lewiathani, kwa hiyo inawezekana kuwa huyu mnyama alikuwepo wakati wa uhai wake.
Listra ni jina mji katika Asia ndogo ambao Paulo alitembelea katika moja ya safari zake za kimisionari. Ilikuwa katika eneo la Likaonia ambapo sasa ni nchi ya Uturuki ya leo.
Paulo na wenzake walitoroka kwenda Derbe na Listra walipotishwa na Wayahudi Ikonio. Akiwa Listra, Paulo alikutana na Timotheo aliyekuwa mwinjilisti mwenzake na mpandaji wa makanisa. Baada ya Paulo kumponya kilema Listra, watu walijaribu kuwaabudu Paulo na Barnaba kama miungu, lakini mitume waliwakemea na kuwazuia kufanya hivyo.
Luka alikuwa mwandishi wa vitabu viwili vya Agano Jipya: injili ya Luka na kitabu cha Matendo ya Mitume.
Katika barua yake kwa Wakolosai,Paulo alimtaja Luka kama daktari. Paulo anamtaja Luka kwenye barua zake mbili. Inadhaniwa kuwa Luka alikuwa Mgiriki na Myunani kabla hajamjua Kristo. Katika injili yake, Luka anajumuisha matukio yanayoonesha upendo wa Yesu kwa watu wote, Wayahudi na Wayunani. Luka alifuatana na Paulo katika safari mbili za kimisionari na kumsaidia na kazi zake, Katika maandiko kadhaa ya awali ya kanisa, inasemekana kuwa Luka alizaliwa katika mji wa Antiokia ndani ya Shamu.
Lutu lilikuwa jina la mpwa wa Abrahamu. Alikuwa mwana wa ndugu yake Abrahamu, Harani. Lutu alisafiri na Abrahamu kwenda nchi ya Kanaani na kuishi katika mji wa Sodoma Lutu alikuwa babu wa Wamoabi na Waamoni. Wafalme maadui walipovamia Sodoma na kumteka Lutu, Abrahamu alikuja na mamia kadha ya wanaume kumuokoa Lutu na kurudisha mali zake. Watu walioishi katika mji wa Sodoma walikuwa watu waovu sana kwa hiyo Mungu aliuangamiza mji huo. Lakini kwanza alimwambia Lutu na familia ya kuuondoka mji ili watoroke.
Maaka alikuwa mmoja wa wana wa kaka yake Ibrahimu Nahori. Watu wengine katika Agano la kale walikuwa na jina hili.
Katika Agano jipya, eneo lililo upande wa kaskazini wa Ugiriki.
Malaki alikuwa mmoja wa manabii wa Mungu kwa ufalme wa Yuda. Aliishi katika ya miaka 500 kabla Kristo kuwa ulimwenguni.
Hawa walikuw wanaume watano kwa jina Manase katika Agano la Kale:
Mariamu alikuwa mwanamke kutoka Bethania aliye mfuata Yesu.
Mariamu Magdalena alikuwa miongoni mwa wanawake waliyo muamini Yesu na kumfuata katika huduma yake. Alijulikana kama kama Yesu aliye mponya kutoka kwa mapepo saba waliyo mtawala.
Mariamu alikuwa mwanamke mdogo aliye ishi katika mji wa Nazarethi aliye poswa kuolewa na Yusufu. Mungu alimchagua Mariamu kuwa mama wa Yesu Mesia, Mwana wa Mungu.
Martha alikuwa mwanamke kutoka Bethania alimfuta Yesu.
Mathayo alikuwa mmoja wa wanaume kumi na mbili Yesu aliyo wachagua kuwa mitume wake. Alijulikana kama pia kama Lawi, mwana wa Alfayo.
Media ulikuwa mji wa zamani uliyo kuwa mashariki mwa Asiria na Babilonia, na kaskazini mwa Elamu na Persia. Watu waliyo ishi katika utawala wa Media walitwa "Wamede."
Kipindi cha Abramu akiishi, Melkizedeki alikuwa mfalme wa mji wa Salemu (baadae, "Yerusalelmu")
Memfisi ilikuwa mji mkuu wa Misri wa zamani, pembeni mwa Mto Nile.
Mesheki ni jina la wanaume wawili katika Agano la Kale.
Mesopotamia ni sehemu ya nchi katika ya Tigrisi na Mto Frati. Sasa ipo katika nchi inayo julikana kama Iraqi.
Wagirgashi walikuwa kundi la watu wanaoishi karibu na Bahari ya Galilaya katika nchi ya Kaanani.
Walikuwa uzao wa mwana wa Hamu Kaanani na kwa hiyo walikuwa moja wa kundi la watu wengi ambao pia walijulikana kama "Wakaanani".
Mungu aliahidi Waisraeli ya kwamba angewasaidia kuwashinda Wagirgashi na makundi mengine ya Wakaanani.
Kama watu wote wa Kaanani, Wagirgashi waliabudu miungu ya uongo na kufanya mambo maouvu kama sehemu ya ibaaa hiyo.
Msemo "Mgiriki" una maana ya lugha inayozungumzwa katika nchi ya Giriki. Giriki pia ilizungumziwa kote katika Ufalme wa Kirumi. Msemo "Kigiriki" una maana ya "kuzungumza Kigiriki".
Kwa kuwa watu wasiokuwa Wayahudi katika Ufalme wa Kirumi walizungumza Kigiriki, Watu wa mataifa mara kwa mara humaanisha "Wagiriki" katika Agano Jipya, haswa inapolinganishwa na Wayahudi.
Msemo "Wayahudi wa Kigiriki" walikuwa wakimaanisha Wayahudi ambao walizungumza Kigiriki kulinganisha na "Wayahudi wa Kiebrania" ambao walizungumza Kiebrania pekee, au labda Kiaramea.
Njia zingine za kutafsiri "Kigiriki" zinaweza kujumuisha "kuzungumza Kigiriki" au "Kigiriki cha kitamaduni" au "Kigiriki".
Pale inapomaanisha wasio Wayahudi, "Giriki" inaweza kutafsiriwa kama "watu wa mataifa"
Wahiti walikuwa ni uzao wa Hamu kupitia kwa mtoto wake Kanaani. Walifanyika kuwa dola kubwa katika eneo ambalo kwa sasa linaitwa Uturuki na Kaskazini mwa Palestina. Ibrahimu alinunua sehemu ya ardhi kutoka kwa Efroni, Mhiti ili aweze kumzika Sara katika pango huko. Hatimaye, Ibrahimu na wazao wake kadhaa walizikwa katika pango hilo pia. Wazazi wa Esau walihuzunika sana baada ya Esau kuoa wanawake Wahiti. Mmoja kati ya watu wa Daudi aliyekuwa na nguvu aliitwa Uria Mhiti. Miongoni mwa wanawake aliowaoa Sulemani walikuwa ni Wahiti. Wanawake hawa wa kigeni waliugeuza moyo wa Sulemani kutoka kwa Mungu kwasababu ya miungu waliyoiabudu. Wahiti walikuwa mara zote ni hofu kwa waisraeli, kimwili na kiroho pia.
Wahivi walikuwa ni moja kati ya makundi saba ya watu walioishi katika nchi ya Kanaani. Kama ilivyokuwa kwa makundi yote, Wahivi walikuwa ni uzao wa Kanaani, aliyekuwa ni mjukuu wa Nuhu. Shekemu mhivi alimbaka Dina, binti wa Yakobo na kaka zake na Dina walilipiza kisasi kwa kuwauwa Wahivi wengi. Katika kipindi ambacho Yoshua aliwaongoza waisraeli kuiteka nchi ya Kanaani, Waisraeli walidanganywa na kufunga mkataba na Wahivi badala ya kuwaangamiza.
Midiani alikuwa mwana wa Ibrahimu na mkewe Ketura. Pia ni jina la kundi la watu na eneo upande wa kaskazini mwa Jangwa la Kiarabu sehemu ya kusini mwa nchi ya Kanani. Kundi la watu liliitwa "Wamidiani."
Mika alikuwa nabii wa Yuda katika ya miaka 700 kabla ya Yesu, wakati nabii Isaya alipo kuwa ana hudumu Yuda. Mwanaume mwingine aliye itwa Mika aliishi kipindi cha waamuzi.
Mikaeli ni mkuu wa malaika wa tiiifu na watakatifu. Yeye ni malaika pekee anaye tajwa kama "malaika mkuu" wa Mungu.
Alipo kuwa mdogo, Miriamu aliongozwa na mama yake kumlinda mdogo wake Musa aliye kuwa katika kikapu miongoni mwa Mto Nile.
Misri ni nchi katika sehemu ya kaskazini ya Afrika, kusini mashariki mwa nchi ya Kaanani. Mmisri ni mtu ambaye anatoka katika nchi ya Misri.
Katika miaka ya zamani, Misri ilikuwa nchi yenye nguvu na utajiri.
Misri ya zamani iligawanyika katika sehemu mbili, Misri ya Chini (sehemu ya kaskazini ambapo mto hutiririka chini kuelekea baharini) na Misri ya Juu (sehemu ya kusini). Katika Agano la Kale, sehemu hizi zinajulikana kama "Misri" na "Pathrosi" katika lugha ya maandishi asili.
Wakati mwingine ambapo kuna chakula kichache Kaanani, wakuu wa koo walisafiri kwenda Misri kununua chakula kwa ajili ya familia zao.
Kwa miaka mia moja hivi, Waisraeli walikuwa watumwa Misri.
Yusufu na Mariamu walishuka chini Misri na mtoto mdogo Yesu kutoroka kwa Herode Mkuu.
Mizpa ni jina la baadhi ya miji inayo tajwa katika Agano la Kale. Ina maana, "mnara wa doria"
Mji wa Babeli ulikuwa makao makuu wa jimbo la Babeli ya kale, ambao pia ulikuwa sehemu ya Himaya ya Babeli.
Mji wa Bethani ulikuwa katika bonde la mteremko wa Mlima wa Mizeituni, kama maili mbili mashariki ya Yerusalemu,
Mji wa Daudi ni jina la Yerusalemu na Bethlehemu.
Lawi alikuwa mmoja wa wana kumi na mbili wa Yakobo, au Israeli. Neno "Mlawi" inamaanisha mtu aliyemmoja wa kabila la Israeli ambalo babu yao alikuwa Lawi.
Walawi walihusika na kulitunza hekalu na kuendesha taratibu za kidini, zikiwemo kutoa sadaka na maombi. Makuhani wote wa Kiyahudi walikuwa Walawi, wazawa wa Lawi na sehemu ya kabila la Lawi. (Ingawa Walawi wote hakuwa makuhani.) Makuhani wa Kilawi walitengwa na kuwekwa wakfu kwa kazi maalum ya kumtumikia Mungu hekaluni. Wanaume wengine wawili wenye jina "Lawi" walikuwa mababu wa Yesu na majina yao yako kwenye ukoo katika injili ya Luka. Mwanafuzi wa Yesu, Mathayo, pia aliitwa Lawi.
Mlima Hermoni ni jina la mlima mrefu wa Israeli chini ya Lebanoni.
Mlima wa Mizeituni ni mlima au kilima kikubwa karibu na mashariki mwa mji wa Yerusalemu. Una mita787 kwenda juu.
Moabu alikuwa mwana wa kwanza wa binti wa Lutu. Pia likawa jina la nchi ambapo yeye na familia yake waliishi. Neno "Moabu" la husu mtu wa uzao wa Moabu au anaishi katika nchi ya Moabu.
Modekai alikuwa mwanaume wa Kiyahudi katika nchi ya Jemi. Alikuwa mlinzi wa binamu wake Esta, ambaye baadae alikuwa mke wa mfalme wa Kijemi, Ahasuerusi
Moleki lilkuwa jina la miungu wa uongo ambao Wakanani waliabudu.
Waperizi walikuwa watu wa kundi fulani katika nchi ya Kanaani. Ni machache yamezungumzwa juu ya kundi hili.
Mishaeli ni jina la wanaume wa tatu katika Agano la Kale.
Frati ni jina la moja ya mito minne ambayo ilitiririka katika bustani ya Edeni. Ni mto ambao umetajwa sana katika Biblia.
Mto wa sasa unaitwa Frati na upo eneo la Mashariki ya Kati na ni mrefu zaidi na mto muhimu zaidi Asia.
Pamoja na Mto Hidekeli, Frati inapakana na eneo la nchi inayojulikana kama Mesopotamia.
Mji wa zamani wa Uri ambapo Abrahamu alitoka ulikuwa mdomo wa Mto Frati.
Mto huu ulikuwa moja ya mipaka ya nchi ambayo Mungu aliahidi kumpa Abrahamu (Mwanzo 15:18).
Wakati mwingine Mto Frati hujulikana kama "ule Mto"
Nili ni mto mrefu na mpana katika kaskazini mashariki mwa Africa. Unajulikana kama mto rasmi wa Misri.
Mto Yordani ni mto unaotiririka toka kaskazini hadi kusini, na inaunda mpaka wa mashariki wa nchi iliyokuwa inaitwa Kanaani.
Leo, mto Yordani unatenganisha Israeli magharibi kutoka Yordani mashariki. Mto Yordani unatiririka katikati ya Bahari ya Galilaya na kuishia katika Bahari iliyo Kufa. Wakati Yoshua anawaongoza Waisraeli kuelekea Kanaani, ilibidi wavuke mto Yordani. Kwa sababu palikuwa parefu sana, Mungu alisimamisha maji kutembea kwa miujiza ili watu wavuke. Mara nyingi Biblia katika Biblia Mto Yordani unajulikana ka "Yordani."
Msemo "mtu wa Mungu" ni heshima ya kutaja nabii wa Yahweh. Pia utumika kuhusu malaika wa Yahweh.
Musa alikuwa nabii na kiongozi wa watu wa Israeli kwa miaka 40.
Kwa ujmla, "muumbaji" ni mtu anaye tengeneza au kufanya vitu.
Waamori walikuwa watu wenye nguvu sana ambao ni uzao wa mjukuu wa Nuhu Kanani.
Wayebusi walikuwa kundi la watu walioishi nchi ya Kanaani. Walikuwa uzao wa mwana wa Hamu, Kanaani.
Wayebusi waliishi katika mji wa Yebusi, ambalo jina lake lilibadilishwa baadaye kuwa Yerusalemu mfalme Daudi alipoutawala. Melkizedeki, mfalme wa Salemu, inawezekana alikuwa Myebusi kwa asili.
Katika Agano la Kale, Naamani alikuwa mkuu wa jeshi wa mfalme Aramu.
Naftali alikuwa mwana wa sita wa Yakobo. Uzao wake uliunda kabila la Naftali, ambalo lilikuwa moja ya kabila la Israeli.
Nahori lilikuwa jina la ndugu wawili wa Ibrahimu: babu yake na kaka.
Nahumu alikuwa nabii aliye ubiri kipindi ambacho mfalme mouvu Manase alitawala Yuda.
Nathani alikuwa nabii mwaminifu wa Mungu aliye ishi kipindi cha Daudi akiwa mfalme wa Israeli.
Nazarethi ni mji katika mji wa Galilaya kusini mwa Israeli. Ilikuwa kama kilomita 100 kaskazini mwa Yerusalemu, iliyo chukuwa kam siku tatu hadi tano kufika kwa miguu.
Nebukadneza alikuwa mfalme wa Utawala wa Babiloni ambaye jeshi lake kuu liliwashinda makundi ya watu na mataifa.
Negevi ni jangwa kusini mwa Israeli, kusini magharibi wa Bahari ya Chumvi.
Nehemia alikuwa Muisraeli aliye ishi Babiloni wakati watu wa Israeli na Yuda walip chukuliwa mateka na Wababiloni.
Ninawi ilikuwa mji mkuu wa Asyria. Mninawi alikuwa mtu aliye ishi Ninawi.
Nuhu alikuwa mwanaume aliye ishi miaka 4,000 iliyo pita, kipindi ambacho Mungu alipotuma garika duniani kuharibu watu waovu. Mungu alimwambia Nuhu ajenge meli kubwa ambayo yeye na familia yake waliweza kuishi wakati mafuriko yalipo funika dunia.
Maelezo 'nyumba ya Daudi' yanarejelea familia au uzao wa Mfalme Daudi. Neno 'nyumba ya Daudi' laweza kutafsiriwa kama '' uzao wa Daudi'' au ''familia ya Daudi." Yesu ni sehemu ya nyumba ya Daudi kwasababu alikuwa ni uzao wa Daudi. Wakati mwingine neno 'nyumba ya Daudi' hurejelea watu wa familia ya Daudi wale ambao wakali hai. Mara nyingine laweza kuwajumuisha wazao wa Daudi hata wale waliokwisha kufa.
Obadia alikuwa nabii wa Agano la Kale aliye tabiri dhidi ya watu wa Edomu, waliyo kuwa wazao wa Esau. Pia palikuwa na wanaume wengine waliyo itwa Obadia katika Agano la Kale.
Omri alikuwa mkuu wajeshi aliye kuwa mfalme wa sita wa Israeli.
Padan-aramu lilikuwa jina la mji ambao familia ya Abrahamu waliishi kabla ya kuhamia kwenye nchi ya Kanaani. Inamaanisha "uwazi wa Aramu."
Aramu, Padan-aramu na Aramu-Nahariamu zilikuwa sehemu za mji mmoja ambao kwa sasa ni zipo katika nchi ya Syria.
Parani ni jangwa lililopo mashariki mwa Misri na kusini mwa nchi ya Kanaani. Pia kulikuwa na mlima Parani ambalo yaweza kuwa jina lingine la mlima Sinai.
Paulo alikuwa kiongozo wa kanisa la kwanza aliyetumwa na Mungu kupeleka habari njema kwa makundi mengi ya watu.
Peori na Mlima Peori ni mlima uliokuwepo kaskazini mwa bahari ya chunvi katika mji wa Moabu.
Petro alikuwa mmoja wa mitume wa Yesu. Alikuwa kiongozi wa muhimu katika kanisa la kwanza.
Pilato alikuwa kiongozi wa serikali ya Rumi katika Yudea aliyumuhukumu Yesu kifo.
Ponto ulikuwa mkoa wa Rumi katika kipindi cha himaya ya Rumi na kanisa la kwanza. ilikuwa karibu na kusini mwa pwani ya Bahari nyeusi na kaskazini ambapo sasa ni nchi ya Uturuki.
Potifa alikuwa kiongozi wamuhimu sana kwa Farao wa Misri katika kipindi ambacho Yusufu aliuzwa utumwani kwa Waishmaili.
Prisila na Akula mume wake walikuwa Wakristo wa Kiyahudi waliofanya kazi na mtume Paulo katika kazi yake ya kimishenari.
Rabai ulikuwa mji wa muhimu sana kwa watu wa Waamoni.
Rahabu alikuwa mwanamke aliyeishi Yeriko Waisraeli walipovamia mji. Alikuwa kahaba.
Raheli alikuwa mmoja wa wake wa Yakobo. Yeye na dada yake Lea walikuwa watoto wa mjomba wake Yakobo.
Rama ulikuwa mji wa zamani wa Israeli uliokuwa kilometa 8 toka Yerusalemu. Ulikuwa mji ambao Benyamini aliishi.
Ramothi ulikuwa mji wa muhimu sana katika milima ya Gileadi karibu na mto Yordani. Pia iliitwa Romothi Gileadi.
Rebeka alikuwa mjukuu wa kaka yake na Abrahamu yaani Nuhu.
Rehoboamu alikuwa mmoja wa wana wa mfalme Sulemani na alikuja kuwa mfalme baada ya Sulemani kufa.
Rimoni ni jina la mtu na jina la mahali lililotajwa sehemu katika Biblia. Pia lilikuwa jina la mungu wa uongo.
Rubeni alikuwa mtoto wa kwanza wa Yakobo. Mama yake alikuwa Lea.
Katika agano jipya mji wa Rumi ulikuwa mji muhimu wa himaya ya Warumi. Sasa ni mji kuu wa Itali.
Ruthu alikuwa mwanamke Mmoabu aliyeolewa na Muisraeli aliyeamia Moabu na familia yake wakati ambao waamuzi wanaongoza Israeli.
Sadoki lilikuwa ni jina la kuhani mkuu aliyekuwa mtu mhimu katika Israeli wakati wa utawala wa Mfalme Daudi.
Sakothi ni jina la miji miwili ya Agano la Kale. Neno, "sakothi" lina maana ya "hifadhi."
Samaria ilikuwa jina la mji na maeneo yake jirani kaskazini mwa Israeli. Eneo hili lilikuwa katikati ya Milima ya Sharoni magharibi na Mto Yordani mashariki.
Samsoni alikuwa mmoja wa waamuzi, au mkombozi, wa Israeli. Alitoka kabila la Dani.
Samweli alikuwa nabii na muamuzi wa mwisho wa Israeli. Alimpaka mafuta Sauli na Daudi kama wafalme juu ya Israeli.
Sara alikuwa mke wa Ibrahimu.
Sauli alikuwa mwanaume wa Kiisraeli ambaye Mungu alimchagua kuwa mfalme wa kwanza wa Israeli.
Sedekia, mwana wa Yosia, alikuwa mfalme wa mwisho wa Yuda (597- 587 KK). Lakini pia kuna watu kadhaa katika Agano la Kale wenye jina Sedekia.
Senakeribu alikuwa mfalme mkubwa wa Assiria aliye sababisha Ninawi kuwa tajiri, na mji wa muhimu.
Katika kitabu cha Mwanzo, Sethi alikuwa mwana wa tatu wa Adamu na Hawa.
Sharoni lilikuwa jina la ardhi ya rotuba pembeni ya Bahari ya Mediterenia, kusini mwa Mlima Karmeli. Unajulikana pia kama "Mlima wa Sharoni."
Wakati wa zamani, Sheba ulikuwa mji wa zamani wa kisasa au eneo la nchi lililo kuwa karibu na kusini mwa Arabia.
Shekemi ni mji uliyopo maili 40 kaskazini mwa Yerusalemu. Shekemi ni jina pia la mwanaume katika Agano la Kale.
Shemu alikuwa mmoja wa wana wa Nuhu aliye enda nae kwenye safina kipindi cha gharika ya ulimwengu inayo elezwa katika kitabu cha Mwanzo.
Shilo ulikuwa mji wa ukuta wa Kikanani uliyo shindwa na Waisraeli chini ya uongozi wa Yoshua.
Shimei ni jina la wanaume kadhaa wa Agano la Kale.
Shinari ina maana ya "nchi ya mito miwili" na lilikuwa jina la mlima au eneo kusini mwa Mesopotamia.
Sidoni alikuwa mwana wa kwanza wa Kanani. Pia kuna mji wa Kikanani unao itwa Sidoni, labda uliitwa baada ya mwana wa Kanani.
Sila alikuwa kiongozi miongoni mwa waamini wa Yerusalemu.
Katika Biblia, kuna wanaume kadhaa wenye jina Simeoni.
Simoni alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu.
Mlima Sinai ni jina la mlima uliyo upande wa kusini wa unao julikana kama Sinai Peninsula kwa sasa. Pia ulijulikana kama "Mlima wa Horebu."
Soari ulikuwa mji mdogo Alipokimbilia Lutu wakati Mungu alipoiaribu Sodoma na Gomora.
Sodoma ulikuwa mji kusini mwa kanani ambapo mpwa wa Ibrahimu Lutu aliishi na mke na watoto wake.
Stefano anajulikana kama Mkristo wa kwanza kuuawa, sababu ya imani yake kwa Yesu. Maisha yake na kifo yameandikwa kwenye kitabu cha Matendo.
Sulemani alikuwa mmoja wa wana wa Mfalme Daudi. Mama yake alikuwa ni Bathsheba.
Syria ni nchi iliyopo kaskazini mashariki ya Israeli. Wakati wa kipindi cha Agano Jipya, ilikuwa mkoa chini ya utawala wa Serikali ya Kirumi.
Tairi ulikuwa mji wa zamani wa Kanani eneo la pwani mwa Bahari ya Mediterenia, katika eneo ambalo sasa ni sehemu nchi ya Lebanoni. Watu wake waliitwa "Watairi."
Tamari ni jina la wanawake kadhaa katika Agano la Kale. Ni jina la miji ya maeno kadhaa katika Agano la Kale.
Tarishishi lilikuwa jina la wanaume wawili wa Agano la Kale. Lilikuwa jina la mji.
Tarso ulikuwa mji uliyo fanikiwa katika mko wa Kirumi wa Silisia, ambao sasa ni Uturuki ya kati.
Tera alikuwa mzao wa mwana wa Nuhu, Shemu. Alikuwa mwana wa Abramu, Nahori na Harani.
Katika kipindi cha Agano Jipya, Thesalonika ulikuwa mji mkuu wa Makedonia katika utawala wa zamani wa Rumi. Watu waliyo ishi kwenye mji waliitwa "Wathesalonike."
Thomaso alikuwa mmoja wa wanaume kumi na mbili Yesu aliye wachagua kuwa wanafunzi na baadae, mitume. Alijulikana kama "Didimasi" yenye maana ya "pacha."
Tikiko alikuwa mmoja wa watumishi wa Paulo wa injili.
Timotheo alikuwa jina mdogo kutoka Lystra aliye kuwa mwaamini katika Kristo kutokana na huduma ya Paulo mjini kwake. Baadae alijiunga na Paulo kwenye safari kadhaa za misheni na kusaidia chunga waamini wapya.
Tirza ulikuwa mji muhimu wa Kanani uliyo chukuliwa na Waisraeli. Lilikuwa jina la binti wa Gileadi, mzao wa Manase.
Tito alikuwa Mpagani alikuja kuwa mwamini kupitia huduma ya Paulo mtume. Alifunzwa na Paulo kuwa kiongozi mwanzo wa makanisa.
Mji wa Troa ulikuwa bandari kaskazini magharibi mwa pwani ya eneo la Rumi huko Asia.
Kuna wanaume kadhaa kwenye Agano la Kale waliyo kuwa na majina "Tubali."
Uajeni ni nchi ambayo ilikuja kuwa ngome kubwa iliyoundwa na mfalme Cyrus mwaka 550 kabla ya Kristo. Nchi ya uajemi ilikuwa kusini mashariki mwa Babeli na Ashuru ambayo kwa sasa ni Irani.
Uarabuni ni sehemu kubwa sana duniani yenye kilomita za mraba 3,000,000. Inapatikana kusini mashariki mwa Israeli na imepakana na bahari ya shamu, bahari ya Arabia na ghuba ya uajemi.
Usemi "ufalme wa Israeli" unamaanisha sehemu ya kaskazini mwa taifa la Israeli wakati makabila kumi na mbili ya Israeli yalipogawanyika katika falme mbili baada ya Sulemani kufa.
Ufalme wa Israeli wa kaskazini ulikuwa na makabila kumi na ufalme wa Yuda ulikuwa na makabila mawili. Mji mkuu wa ufalme wa Israeli ulikuwa Samaria. Ilikuwa kama kilomita 50 kutoka Yerusalemu, mji mkuu wa Yuda. Wafalme wote wa ufalme wa Israeli walikuwa waovu. Waliwashawishi watu kutumikia sanamu na miungu ya uongo. Mungu aliwatuma Waashuri kuvamia taifa la Israeli. Waisraeli wengi walikamatwa na kupelekwa kuishi Ashuru. Waashuri waliwaleta wageni kuishi miongoni mwa watu waliobaki wa Israeli. wageni hawa waliowana na Waisraeli, na uzao wao ukawa watu wa Samaria.
Ufilisti ni jina la mji mkubwa katika nchi ya Kanaani iliyopo pwani mwa Bahari ya Mediteraniani.
Ukaldayo ulikuwa mkoa wa kusini mwa Mesopotamia au Babeli. Watu walioishi katika mkoa huo waliitwa Wakaldayo.
Uri ulikuwa mji muhimu pembeni mwa Mto Frati katika mji wa zamani wa Kalidea, ambao ulikuwa sehemu ya Mesopotamia. Hili eneo lilikuwa ambapo sasa ni Iraqi.
Uria alikuwa mwanaume mwenye haki na mmoja wanajeshi hodari wa Mfalme Daudi. Utajwa kama "Uria Mhiti"
Uzia alikuwa mfalme wa Yuda akiwa ni umri wa miaka 16 na akatawala miaka 52, ambao ulikuwa utawala mrefu. Uzia alijulikana kama "Azaria."
Katika agano la kale kwenye kitabu cha Esta, Vashti alikuwa mke wa Ahasuero mfalme wa Uajemi.
Wafilisti walikuwa kundi la watu waliokaa katika mji wa Ufilisti kando ya bahari ya Mediteraniani. Jina lao linamaana ya "watu wa baharini"
Wakerethi walikuwa kundi la watu ambao walikuwa kama sehemu ya Wafilisti. Pia imeandikwa kama "Wakerethi."
Katika nyakati za Biblia, mji wa Yafa ulikuwa mji muhimu wa kibiashara uliopo Bahari ya Kati, kusini mwa uwanda wa Sharoni.
Eneo la zamani la Yafa ndio mji wa leo wa Yafa, ambayo sasa ni sehemu ya Tel Aviv. Katika Agano la Kale, Yafa ndio mji ambao Yona alipanda boti kwenda Tarshishi. Katika Agano Jipya, mwanamke wa Kikristo aitwaye Tabitha alifia Yafa na Petro alimfufua.
Yafethi alikuwa mmoja wa wana watatu wa Nuhu.
Wakati wa mafuriko wa ulimwengu wote uliofunika dunia yote, Yafethi na ndugu zake wawili walikuwa na Nuhu katika safina, pamoja na wake zao. Wana wa Nuhu kawaida huorodheshwa hivi, "Shemu, Hamu, na Yafethi." Hii inaashiria kuwa Yafethi alikuwa mdogo kati ya hao ndugu.
Yakobo, mwana wa Alfayo, alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu.
Jina lake linatolewa katika orodha ya wanafunzi wa Yesu katika injili za Mathayo, Marko, na Luka. Ametajwa pia katika kitabu cha Matendo ya Mitume kama mmoja wa kumi na moja ambao walikuwa pamoja wakiomba Yerusalemu baada ya Yesu kurudi juu mbinguni.
Yakobo, mwana wa Zebedayo, alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili. Alikuwa na ndugu yake mdogo aliyeitwa Yohana ambaye pia alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu.
Yakobo na ndugu yake Yohana walifanya kazi kwa kuvua samaki na baba yao Zebedayo. Yakobo na Yohana waliitwa jina la utani "wana wa ngurumo," labda kwa sabau walikuwa wepesi kukasirika. Petro, Yakobo, na Yohana walikuwa wanafunzi wa karibu zaidi na Yesu na walikuwa naye kwa matukio ya ajabu kama vile Yesu alipokuwa juu ya mlima na Eliya na Musa na Yesu alipomfanya msichana aliyekufa kurudia uhai wake. Huyu ni Yakobo tofauti na yule aliyeandika kitabu katika Biblia. Lugha zingine zinalazimika kuandika majina yao tofauti ili kuweka wazi kuwa walikuwa watu wawili tofauti.
Yakobo alikuwa mwana wa Mariamu na Yusufu. Alikuwa mmoja wapo wa wadogo zake Yesu.
Ndugu zake wengine Yesu walikuwa ni, Yusufu, Yuda na Simoni Wakati wa uhai wa Yesu, Yakobo na ndugu zake hawakuamini kuwa Yesu ndiye Masihi. Baadaye, baada ya Yesu kufufuka katika wafu, Yakobo alimuamini na kuwa kiongozi katika kanisa la Yerusalemu. Kitabu cha Agano Jipya cha Yakobo ni barau ambayo Yakobo aliwaandikia Wakristo waliokimbilia nchi zingine kutoroka mateso.
Yakobo alikuwa pacha mdogo aliyekuwa mwana wa Isaka na Rebeka.
Jina la Yakobo linamaanisha "anakamata kisigino" ambao ni usemi unaomaanisha, "hudanganya." Wakati yakobo alipozaliwa, alikuwa akishilia kisigino cha pacha wake Esau. Miaka mingi baadaye, Mungu alibalisha jina la Yakobo kuwa "Israeli," inayomaanisha, "anashindana na Mungu." Yakobo alikuwa mjanja na muongo. Alipata njia ya kupata baraka za mwana wa kwanza na kurithi haki kutoka kwa kaka yake, Esau. Esau alikasirika na kupanga kumuua, kwa hiyo Yakobo akaondoka nchini mwake. Lakini baada ya miaka Yakobo alirudi na wake zake na watoto katika nchi ya Kanaani ambamo Esau alikuwa akiishi, na familia zao ziliishi kwa amani zikiwa jirani. Yakobo alikuwa na wana kumi na mbili. Uzao wao ukawa makabila kumi na mbili ya Israeli. Mwanaume tofauti aitwaye Yakobo ameorodheshwa kama baba wa Yusufu katika ukoo wa Mathayo.
Yeftha alikuwa mpiganaji kutoka Gileadi aliyetumika kama mhukumu juu ya Israeli.
Katika Wahebrania 11:32, Yeftha anasifiwa kama kiongozi muhimu aliyewatoa watu wake kutoka kwa maadui zake. Aliwaokoa Waisraeli kutoka kwa wamoabi na kuwaongoza watu wake kuwashinda Waefraimu. Hata hivyo, Yeftha alifanya kiapo cha kipumbavu na haraka kwa Mungu kilichosababisha yeye kumtoa sadaka binti yake.
Yehoramu lilikuwa jina la wafalme wawili tofauti katika Agano la Kale. Wafalme wote hao wawili walijulikana kama "Yoramu."
Mfalme mmoja Yehoramu alitawala ufalme wa Yuda kwa miaka minane. Alikuwa mwana wa Mfalme Yehoshafati. Huyu ndiye mfalme anayejulikna zaidi kama Yoramu. Mfalme Yehoramu mwingine alitawala ufalme wa Israeli kwa miaka kumi na mbili. Alikuwa mwana wa Mfalme Ahabu. Mfalme Yehoramu wa Yuda alitawala wakati wa manabii Yeremia, Danieli, Obadia, na Ezekieli wakitabiri katika ufalme wa Yuda. Yehoramu pia alitawala kwa muda kiasi wakati baba yake Yehoshafati alipokuwa akitawala Yuda. Tafsiri zingine zinaweza kuchagua kutumia jina "Yehoramu" pale ambapo huyu mfalme wa Israeli anatajwa na "Yoramu" kwa mfalme wa Yuda. Njia nyingine ya kumtambua vizuri kila mmoja ni kuongeza jina la baba yake.
Yehoshafati ni jina la angalua watu wawili katika Agano la Kale.
Mtu anayejulikana vizuri zaidi kwa hili jina ni Mfalme Yehoshafati ambaye alikuwa mfalme wa nne kutawala ufalme wa Yuda. Alirejesha amani kati ya Yuda na Israeli, na kuangamiza madhabahu ya miungu wa uongo. Yehoshafati mwingine alikuwa "mtunza kumbukumbu" wa Daudi na Sulemani. Kazi yake ilikuwa pamoja na kuandika nyaraka kwa ajili ya mfalme kusaini na kurekodi historia ya matukio muhumi yaliyotokea katika ufalme.
Yehoyada alikuwa kuhani aliyemsaidia kumficha na kumlinda mwana wa mfalme Ahazia, Yoashi hadi alipofikisha umri wa kuweza kutangazwa kuwa mfalme.
Yehoyada alimpangia mamia ya walinzi kumlinda Yoashi alipokuwa mdogo wakati akitangazwa kuwa mfalmena watu hekaluni. Yehoyada aliwaongoza watu kuondoa madhabahu yote ya mungu wa uongo Baali. Maisha yake yote yaliyosalia, kuhani Yehoyada alimshauri mfalme Yoashi kwa kumsaidia kumtii Mungu na kuwatawala watu kwa hekima. Mwanamme mwingine aliyeitwa Yehoyada alikuwa baba wa Benaya.
Yehoyakimu alikuwa mfalme aliyetawala ufalme wa Yuda.
Yehoyakimu alikuwa mfalme alipokuwa na miaka 18. Alitawala miezi mitatu tu na baada ya hapo alikamatwa na jeshi la Babeli na kupelekwa Babeli. Wakati wa utawala wake mfupi, Yehoyakimu alifanya uovu kama babu yake mfalme Manase na baba yake Mfalme Yehoyakimu alivyofanya.
Yehoyakimu alikuwa mfalme muovu aliyetawala ufalme wa Yuda, kuanzia mwaka 608 K.K. Alikuwa mwana wa mfalme Yosia. jina lake mwanzoni lilikuwa Eliakimu.
Farao wa Misri Neko alibadili jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu na kumfanya kuwa mfalme wa Yuda. Neko alimlazimisha Yehoyakimu kulipa kodi ya juu kwa Misri. Yuda ilipovamiwa baadaye na mfalme Nebukadreza, Yehoyakimu alikuwa miongoni mwao wale walikamatwa na kupelekwa Babeli. Yehoyakimu alikuwa mfalme mwovu aliyeingoza Yuda mbali na Yahwe. Nabii Yeremia alitabiri dhidi yake.
Yehu lilikuwa jina la wanaume wawili katika Agano la Kale.
Yehu mwana wa Hanani alikuwa nabii wakati wa utawala wa Mfalme Ahabu na Mfalme Yehoshafati wa Yuda. Yehu mwana (uzao) wa Yehoshafati alikuwa jemedari katika jeshi la Israeli ambaye alitiwa mafuta kuwa mfalme kwa amri ya nabii Elisha. Yehu aliua vitu viwili viovu: Mfalme Yoramu wa Israeli na Mfalme Ahazia wa Yuda. Mfalme Yehu pia aliwaua ndugu wote wa mfalme wa zamani Ahabu, na akafanya yule malkia muovu Yezebeli auwawe. Yehu aliaangamiza sehemu zote za kumuabudia Baali ndani ya Samaria na kuwaua manabii wote wa Baali. Mfalme Yehu alimtumikia Mungu mmoja wa kweli, Yahwe, na alikuwa mfalme juu ya Israeli kwa miaka ishiri na nane.
Yeremia alikuwa nabii wa Mungu katika ufalme wa yuda. Kitabu cha Agano la Kale cha Yeremia kina unabii wake.
Kama manabii wengi, Yeremia mara nyingi ilimbidi kuwaonya watu wa Israeli kuwa Mungu atawaadabisha kwa dhambi zao. Yeremia alitabiri kuwa Wababeli wataiteka Yerusalemu, jambo lililowafanya baadhi ya watu wa Yuda kukasirika. Kwa hiyo walimuweka katika kisima kilichokauka na kumuacha humo kufa. Lakini mfalme wa Yuda aliwaamuru watumishi wake kumuokoa Yeremia kutoka katika kisima. Yeremia aliandika kuwa alitamani macho yake yawe "chemchemi ya machozi," kuonesha masikitiko yake makali kuhusu uasi na mateso ya watu wake.
Yeriko ulikuwa mji wenye nguvu katika nchi ya Kanaani. Ulikuwa magharabi mwa mto wa Yordani na kaskazini mwa Bahari ya Chumvi.
Kama Wakanaani wote, watu wa Yeriko waliabudu miungu ya uongo. Yeriko ulikuwa mji wa kwanza katika nchi ya Kanaani ambao Mungu aliwaambia Waisraeli kuuteka. Wakati Yoshua alipowaongoza Waisraeli dhidi ya Yeriko, Mungu alifanya muujiza mkubwa kuwasaidia kuushinda huo mji.
Yeroboamu mwana wa Nebati alikuwa mfalme wa kwanza wa ufalme wa kaskazini wa Israeli kati ya 900-910 K.K. Yeroboamu mwingine, mwana wa mfalme Yoashi, alitawala juu ya Israeli karibu miaka 120 baadaye.
Yahwe alimpa Yeroboamu mwana wa Nebati utabiri kwamba atakuwa mfalme baada ya Sulemani na kwamba atayatawala makabila kumi ya Israeli. Sulemani alipokufa, makabila kumi ya kaskazini mwa Israeli yalimkaidi mwana wa Sulemani, Rehoboamu na badala yake walimfanya Yeroboamu kuwa mfalme wao, wakimuacha Rehoboamu kama mfalme wa makabila mawili tu ya kusini, Yuda na Benyamini. Yeroboamu alikuwa mfalme muovu aliyewaongoza watu kutomuabudu Yahwe na badala yake aliweka sanamu kwa ajili yao kuabudu. Waflame wengine wote wa Israeli walifuata mfano wa Yeroboamu na walikuwa wafalme waovu kama yeye alivyokuwa. Karibu miaka 120 baadaye, mfalme mwingine Yeroboamu alianza kutawala ufalme wa kaskazini mwa Israeli. Yeroboamu huyu alikuwa mwana wa Yoashi na alikuwa muovu kama wafalme wengine wote waliopita wa Israeli walivyokuwa. Licha ya haya yote, Mungu alikuwa na huruma juu ya Israeli na kumsaidia huyu mfalme Yeroboamu kuongeza ardhi na kuimarisha mipaka ya eneo lao.
Yerusalemu mwanzoni ulikuwa mji wa zamani wa Kikanaani ambao baadaye ulikuwa mji muhimu zaidi katika Israeli. Inapatikana karibu kilomita 34 magharibi mwa Bahari ya Chumvi na kaskazini mwa Bethlehemu. Bado ni mji mkuu wa Israeli ya leo.
Jina "Yerusalemu" imetajwa kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Yoshua. Majina mengine ya mji huu katika Agano la Kale ni pamoja na "Salemu", "mji wa Yebusi," na "Sayuni." "Yerusalemu" na "Salemu" zote zina msingi wa "amani" katika maana. Yerusalemu mwanzoni ilikuwa ngome ya Yebusi iitwayo "Sayuni" amabyo mfalme Daudi aliikamata na kuifanya kuwa mji wake mkuu. Mwana wa Daudi Sulemani alijenga hekalu la kwanza Yerusalemu, katika mlima Moria, ambao ulikuwa mlima ambao Abrahamu alimtoa Isaka kama sadaka kwa Mungu. Hekalu lilirudiwa kujengwa hapo baada ya kutetezwa na Wababeli. Kwa sababu hekalu lilikuwa Yerusalemu, sherehe kuu za Kiyahudi ziliadhimishwa huko. Watu kawaida husema kwenda "juu" Yerusalemu kwa sababu palikuwa mlimani.
Yese Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi, na mjukuu wa Ruthu na Boazi.
Majina "Yethro" na "Reueli" yote yanamaanisha baba wa mke wa Musa, Sipora. Kulikuwa kuna watu wawili wengine wenye jina "Reueli" katika Agano la Kale.
Wakati Musa alipokuwa mchungaji katika nchi ya Medani, alimuoa binti wa mwanamme wa Medani aitwaye Reueli. Baadaye Reueli anajulikana kama "Yethro, kuhani wa Medani." Inawezekana kuwa "Reueli" lilikua jina la ukoo. Mungu alipozungumza na Musa kutoka kichaka cha moto, Musa alikuwa akichunga kondoo wa Yethro. Muda mwingine baadaye, baada ya Mungu kuwaokoa Waisraeli kutoka Misri, Yethro alikuja kwa Waisraeli jangwani na kumpa Musa ushauri mzuri kuhusu kuhukumu mambo ya watu. Alimuamini Mungu aliposikia miujiza yote Mungu aliyoifanya kwa watu Waisraeli ndani ya Misri. Mmoja wa wana wa Esau alitwa Reueli. Mwanamme mwingine Reueli anatajwa katika uzao wa Waisraeli aliyerudi kutishi Yuda baada ya kutekwa kwa Babeli kuisha.
Yezebeli alikuwa mke muovu wa mfalme Ahabu wa Israeli.
Yezebeli alimshawishi Ahabu na Israeli nzima kuabudu sanamu. Pia aliua manabii wengi wa Mungu. Yezebeli alisababisha mtu asiye na hatia aitwaye Nabothi kuuwawa ili Ahabu aibe shamba la mizabibu la Nabothi. Yezebeli hatimaye aliuwawa kutokana na maovu yote aliyotenda. Eliya alitabiri jinsi atakavyokufa na ikatokea hivyo hivyo kama alivyotabiri.
Yezreeli lilikuwa jina la mji muhimu Israeli katika eneo la kabila la Isakari, lililokuwa kusini magharibi mwa Bahari ya Chumvi.
Mji wa Yezreeli ni moja ya alama za magharibi za uwanda wa Megido, ambayo pia unaitwa "Bonde la Yezreeli." Wafalme kadhaa wa Israeli walikuwa na majumba yao ya utawala katika mji wa Yezreeli. Bustani la mizabibu la Nabothi ilikuwa karibu na nyumba ya mfalme Ahabu ndani ya Yezreeli. Nabii Eliya alitabiri dhidi ya Ahabu huko. Mke muovu wa Ahabu, Yezebeli, aliuwawa Yezreeli. Matukio mengine ya muhimu yalitokea katika mji huu, yakiwemo mapigano kadhaa.
Yoabu alikuwa kiongozi muhimu wa jeshi kwa mfalme Daudi katika utawala wake wote.
Kabla Daudi hajawa mfalme, Yoabu tayari alikuwa mmoja wa wafuasi wake waminifu. Baadaye, wakati wa utawala wa Daudi kama mfalme wa Israeli, Yoabu alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la mfalme Daudi. Yoabu alikuwa pia mpwa wa mfalme Daudi kwa kuwa mama yake alikuwa mmoja wa madada zake Daudi. Wakati mwana wa Daudi, Absalomu, alipomsaliti kwa kujaribu kuuchukua ufalme, Yoabu alimuua Absalomu ili kumlinda mfalme. Yoabu alikuwa mpambanaji mwenye hima na aliua watu wengi waliokuwa maadui wa Israeli.
Yoashi lilikuwa jina la watu kadhaa katika Agano la Kale.
Yoashi mmoja alikuwa baba wa mkombozi mmoja wa Israeli, Gideoni. Mwanamme mwingine aliyeitwa Yoashi alikuwa uzao wa mwana wa mwisho wa Yakobo, Benyamini. Yoashi anayejulikanai vizuri zaidi alikuwa mfalme wa Yuda akiwa na umri wa miaka saba. Alikuwa mwana wa Ahazia, mfalme wa Yuda aliyeuwawa. Yoashi alipokuwa mtoto mdogo, shangazi yake alimuokoa kuuliwa kwa kumficha hadi alipokuwa na umri wa kutosha kufanywa mfalme. Mfalme Yoashi alikuwa mfalme mzuri ambaye mwanzoni alimtii Mungu. Ila hakutoa sehemu zilizo inuka na Waisreali wakaanza tena kuabudu sanamu. Mfalme Yoashi alitawala Yuda wakati wa baadhi ya miaka mfalme Yehoashi alipotawala Israeli. Walikuwa wafalme wawili tofauti.
Yoeli ni jina la nabii ambaye inawezekana aliishi wakati wa utawala wa mfalme Yoashi wa Yuda. Kuna watu wengine pia katika Agano la Kale wenye jina Yoeli.
Kitabu cha Yoeli ni moja ya vitabu vifupi vya kinabii katika sehemu ya mwisho ya Agano la Kale. Maelezo pekee tuliyonayo kumhusu nabii Yoeli ni kwamba jina la baba yake ni Pethueli. Katika mahubiri yake ya Pentekoste, mtume Paulo alinukuu kutoka kitabu cha Yoeli.
Yohana alikwa mwana wa Zekaria na Elisabeti. Kwa kuwa "Yohana" lilikuwa jina lililozoeleka, mara nyingi huitwa "Yohana Mbatizaji" ili kumtofautisha na watu wengine waitwao Yohana, kama mtume Yohana.
Yohana alikuwa nabii ambaye Mungu alimtuma kuwaanda watu kumuamini na kumfuata Masihi. Yohana aliwaambia watu kutubu dhambi zao, kumgeukia Mungu, na kuacha kutenda dhambi, ili wawe tayari kumpokea Masihi. Yohana alibatiza watu wengi katika maji kama ishara ya kwamba wanatubu dhambi zao na kuziacha. Yohana aliitwa "Yohana Mbatizaji" kwa sababu alibatiza watu wengi. Hakikisha kuwa watu wataelewa kuwa "Mbatizaji" haiimaanishi kanisa kwa hili jina. Inaweza kulazimu kusema, "Yohana aliyebatiza".
Yohana alikuwa mmoja wa mitume kumi na mbili na rafiki wa karibu wa Yesu.
Yohana na ndugu yake Yakobo walikuwa wana wa mvuvi wa samaki aitwaye Zebedayo. Katika injili aliyoandika kuhusu maisha ya Yesu, Yohana alijieleza kama "mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda." Hii inaonehsa kuwa Yohana alikuwa rafiki wa karibu wa Yesu. Mtume Yohana aliandika vitabu vitano katika Agano Jipya: injili ya Yohana, Ufuno wa Yesu Kristo, na barua tatu zilionadikwa kwa waumini wengine. Noti kuwa mtume Yohana alikuwa mtu tofauti na Yohana mbatizaji.
Yohana Marko, pia akijulikana kama "Marko," alikuwa mmoja wa wanaume waliosafiri na Paulo katika safari zake za kimisionari. Inawezekana kuwa yeye ndiye mwandishi wa Injili ya Marko.
Yohana Marko alifuatana na binamu ya Barnaba na Paulo katika safiri yao ya kwanza ya kimisonari. Wakati Paulo alipowekwa gerezani Yerusalemu, waumini walikuwakimuombea katika nyumba ya mama yake Yohana Marko. Marko hakuwa mmoja wa mitume wa awali, lakini alifundishwa na Paulo na Petro na alifanya nao kazi katika huduma.
Yona alikuwa nabii wa Kihebrania katika Agano la Kale.
Kitabu cha Yona kinaelezea hadithi ya wakati Mungu alipomtuma Yona kuhubiri kwa watu wa Ninawi. Yona alikataa kwenda Ninawi na badala yake akapanda katika meli iliyokuwa inaelekea mji mwingine. Mungu alisababisha dhoruba kali kuilemea meli. Watu waliukuwa wakidafiri katika meli walipogundua kuwa Yona hakuwaanamtii Mungu, walimtupa katika bahari na dhoruba ikakoma. Yona alimezwa na samaki mkubwa na akawa tumboni mwake kwa siku tatu, mchana na usiku. Baada ya hayo, Yona alienda Ninawi na kuwahubiri watu wa huko, na wakaziacha dhambi zao.
Yonathani ni jina la angalau wanaume kumi katika Agano la Kale. Jina linamaanisha "Yahwe ametoa."
Rafiki wa karibu wa Daudi , Yonathani, ndiye anayejulikna zaidi katika Biblia kwa hili jina. Yonathani alikuwa mwana kwanza wa mfalme Sauli. Yonathani wengine waliotajwa katika Agano la Kale ni pamoja na: uzao wa Musa, mpwa wa mfalme Daudi, makuhani kadhaa, akiwemo mwana wa Abiathari; na mwandishi wa Agano la Kale ambaye nyumba yake ilitumika kumfunga nabii Yeremia.
Yoramu mwana wa Ahabu alikuwa mfalme Israeli. Wakati mwingine anajulikana kama "Yehoramu."
Mfalme Yoramu wa Israeli alitawala wakati mmoja kama Yehoramu wa Yuda. Yoramu alikuwa mfalme muovu aliyeabudu miungu ya uongo na kusababisha watu wa Israeli kutenda dhambi. Mfalme Yoramu wa Israeli pia alitawala wakati wa nabii Eliya na Obadia. Mwanamme mwingine aitwaye Yoramu alikua mwana wa mfalme wa Hamathi wakati Daudi ni mfalme.
Kuna Waisraeli kadhaa kwenye Biblia waitwao Yoshua. Anayejulikana zaidi ni Yoshua mwana wa Nuni aliyekuwa msaidizi wa Musa na baadaye kuwa kiongozi muhimu wa watu wa Mungu.
Yoshua alikuwa mmoja wa wapelelezi kumi na mbili amabo Musa aliwatuma tafiti nchi ya ahadi. Pamoja na Kalebu, Yoshua aliwasihi watu wa Israeli watu kutii amri ya Mungu kuingia nchi ya ahadi na kuwashinda Wakanaani. Miaka mingi baadaye, baada ya Musa kufa, Mungu alimchagua Yoshua kuwaongoza watu Waisraeli kwenda nchi ya ahadi. Katika mapambano ya kwanza na maarufu zaidi dhidi ya Wakanaani, Yoshua aliwaongoza Waisraeli kuuangamiza mji wa Yeriko. Kitabu cha Agano la Kale cha Yoshua kinaelezea jinsi Yoshua alivyowaongoza Waisraeli katika kuichukua mamlaka nchi ya ahadi na jinsi alivyopanga sehemu tofauti za nchi kwa kila kabila la Israeli kuishi. Yoshua mwana wa Yosadaki anatajwa katika vitabu vya Hagai na Zekaria; alikuwa kuhani mkuu aliyesaidia kujenga tena kuta za Yerusalemu. Kuna wanaume kadhaa wengine waitwao Yoshua waliotajwa katika koo na sehemu zingine katika Biblia.
Yosia alikuwa mfalme mcha Mungu aliyetawala juu ya ufalme wa Yuda kwa miaka thelathini na moja. Aliwaongoza watu wa Yuda kutubu na kumuabudu Yahwe.
Baada ya baba yake mfalme Amoni kuuwawa, Yosia akawa mfalme juu ya Yuda akiwa na miaka minane. Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, mfalme Yosia alimuamuru kuhani mkuu Hilkia kulijenga tena hekalu la Mungu. Wakati hili likifanyika, vitabu vya Sheria vilipatikana. Vitabu vya Sheria viliposomwa kwa Yosia, alisikitishwa na jinsi watu wake walivyokuwa hawamtii Mungu. Aliamuru kwamba sehemu zote za kuabudia sanamu ziteketezwe na makuhani wa miungu wa uongo wauwawe. Pia aliwaamuru watu kuanza kuadhimisha sherehe ya Pasaka tena.
Katika Agano la Kale kuna wanaume watatu wenye jina Yothamu.
Mwanaume mmoja aitwaye Yothamu alikuwa mwana wa mwisho wa Gideoni. Yothamu alisaidia kumshinda kaka yake mkubwa Abimeleki, ambaye aliwauwa ndugu zake wengine wote. Mwanamme mwingine aitwaye Yothamu alikuwa mfalme juu ya Yuda kwa miaka kumi na sita baada ya kifo cha baba yake Uzia (Azaria). Kama baba yake, Yothamu alimtii Mungu na likuwa mfalme mzuri. Lakini hakuondoa sehemu za kuabudia sanamu na hii ilisababisha watu wa Yuda baadaye kumgeuka Mungu tena.
Yuda alikuwa mmoja wa wana wakubwa wa Yakobo. Mama yake alikuwa Lea. Uzao wake uliitwa "kabila la Yuda."
Alikuwa ni Yuda aliyewaambia ndugu zake kumuuza mdogo wao Yusufu kama mtumwa badala ya kumuuacha afe katika shimo. Mfalme Daudi na wafalme wote baada yake walikuwa uzao wa Yuda. Yesu pia alikuwa uzao wa Yuda. Utawala wa Sulemani ulipoisha na taifa la Israeli kugawanyika, ufalme wa Yuda ulikuwa wa sehemu ya kusini mwa nchi. Katika kitabu cha Agano Jipya cha Ufunuo, Yesu anaitwa "Simba wa Yuda." Maneno "Yahudi" na mji wa "Yuda" yametoka katika jina "Yuda."
Neno "Yuda" linamaanisha sehemu katika nchi ya Israeli ya zamani. Wakati mwingine linatumika katika maana finyu na wakati mwingine katika maana pana.
Wakati mwingine"Yuda" inatumika katika maana finyu kumaanisha jimbo lililo sehemu ya kusini ya Israeli ya zamani magharibi tu mwa Bahari iliyo Kufa. Wakati mwingine "Yuda" inamaana pana na inamaanisha majimbo yote ya Israeli ya zamani, ikiwemo Galilaya, Samaria, Perea, Edomu na Yuda. Maana pana ya Yuda (mfano. Luka 1:5) inaweza kutafsiriwa kama "nchi ya Yuda" na katika maana finyu (mfano Luka 1:39) inaweza kutafsiriwa kama "jimbo la Yuda" kwa sababu hii ndio sehemu ya nchi ya Israeli ya zamani ambapo kabila la Yuda ya lilikuwepo.
Yuda Iskariote alikuwa mmoja wa mitume wa Yesu. Alikuwa ndiye aliyemsaliti Yesu kwa viongozi wa Kiyahudi.
Jina "Iskariote" inaweza kumaanisha "kutoka Keriothi", labada kuashiria kuwa Yuda alikulia katika huo mji. Yuda Iskariote alitunza fedha ya mitume na mara kwa mara aliiba kutumia kwa ajili yake. Yuda alimsaliti Yesu kwa kuwaambia viongozi wa dini mahali alipo Yesu ili wamkamate. Baada ya viongozi wa dini kumhukumu Yesu kifo, Yuda alijuta kuwa alimsaliti Yesu kwa hiyo akarudisha fedha ya usaliti kwa viongozi wa Kiyahudi na kisha kujiua. Mtume mwingine pia aliitwa Yuda na alikuwa mmoja wandugu wa Yesu. Kuna wanaume wengi waitwao Yuda katika Biblia, kama vile ndugu yake Yesu na mtume mwingine.
Yuda mwana wa Yakobo alikuwa mmoja wa mitume kumi na mbili wa Yesu. Huyu hakuwa Yuda Iskariote.
Mara nyingi katika Biblia, wanaume wenye majina ya kufanana hutofautishwa kwa kutaja walikuwa wana wa nani. Hapa Yuda anatajwa kama "mwana wa Yakobo." Mwanamme mwingine aitwaye Yuda alikuwa ndugu yake Yesu. Kitabu cha Agano Jipya cha"Yuda" kinawezekana kuwa kimeandikwa na ndugu yake Yesu Yuda, kwa kuwa anajitambulisha kama "ndugu yake Yakobo." Yakobo alikuwa ndugu mwingine wa Yesu. Inawezekana kuwa kitabu cha Yuda kiliandikwa na mwanafunzi wa yesu, Yuda mwana wa Yakobo.
Kabila la Yuda lilikuwa kubwa zaidi kati ya makabila kumi na mbili ya Israeli. Ufalme wa Yuda uliundwa na makanila ya Yuda na Benyamini.
Baada ya mfalme Sulemani kufa, taifa la Israeli liligawanyika katika falme mbili: Israeli na Yuda. Ufalme wa Yuda ulikuwa ufalme wa kusini, uliokuwa magharabi mwa Bahari ya Chumvi. Mji mkuu wa ufalme wa Yuda ulikuwa Yerusalemu. Wafalme wanane wa Yuda walimtii Yahwe na kuwaongoza watu kumwabudu yeye. Wafalme wengine wa Yuda walikuwa waovu na kuwaongoza watu kuabudu sanamu. Zaidi ya miaka 120 baada ya Ashuru kuishinda Israeli (ufalme wa kaskazini), Yuda ilitekwa na taifa la Babeli. Wababeli waliangamiza mji na hekalu, na kuwachukua watu wengi wa Yuda kwenda Babeli kama watekwa.
Yusufu alikuwa baba wa duniani wa Yesu na kumkuza kama mwanaye. Alikuwa mtu mwenye haki aliyefanya kazi kama seremala.
Yusufu alikuwa amemchumbia binti wa Kiyahudi aitwaye Mariamu, ambaye Mungu alimchagua kuwa mama wa Yesu Masihi. Malaika alimuambia Yusufu kwamba Roho Mtakatifu alimsababisha Mariamu kuwa na mimba, na kwamba mtoto wa Mariamu alikuwa ni mwana wa Mungu. Baada ya Yesu kuzaliwa, malaika alimuonya Yusufu kumpeleka mtoto na Mariamu Misri ili kumtoroka Herode. Yusufu na familia yake waliishi katika mji wa Nazareti ya Galilaya alipojipatia kipato kwa kufanya kazi ya useremala.
Yusufu alikuwa mwana wa kumi na moja wa Yakobo na mwana wa kwanza wa mama yake Raheli.
Yusufu alikuwa mwana kipenzi wa baba yake. Ndugu zake walimuonea wivu na wakamuuza katika utumwa. Wakati akiwa Misri, alisingiziwa na kuwekwa gerezani. Licha ya mateso yake, Yusufu alibaki mwaminifu kwa Mungu. Mungu alimuweka katika nafasi ya pili ya madaraka katika Misri na kumtumia kuwaokoa watu katika kipindi ambapo kulikuwa na chakula kidogo. Watu wa Misri, pamoja na watu wake, waliepusha na njaa.
Zabuloni alikuwa mwana wa mwisho wa Yakobo na Lea na ni jina la mojawapo wa makabila kumi na mbili ya Israeli
Zakaria alikuwa nabii aliyetabiri wakati wa utawala wa Mfalme Dario I wa Uajemi. Kitabu cha Zakari katika Agano la Kale kina unabii wake, ambacho kinawasihi mateka waliorudi kulijenga tena hekalu.
Katika Agano Jipya, Zakaria alikuwa kuhani wa kiyahudi aliyekuja kumzaa Yohana Mbatizaji.
Zakayo alikuwa mtoza ushuru katika mji wa Yeriko aliyepanda katika mti ili aweze kumwona Yesu aliyekuwa amezungukwa na kundi kubwa la watu.
Zebedayo alikuwa mvuvi kutoka Galilaya anayejulikana kwa sababu ya wanawe, Yakobo na Yohana, waliokuwa wanafunzi wa Yesu. Hawa wamekuwa wakitajwa katika Agano Jipya kama "wana wa Zebedayo."
Zefania, mwana wa Kushu, alikuwa nabii aliyeishi Yerusalemu na kutabiri wakati wa utawala wa Mfalme Yosia. Aliishi wakati mmoja na Yeremia.
Zerubabeli lilikuwa jina la Waisraeli wawili katika Agano la Kale.