Genesis 15

Genesis 15:1

Yahwe alipojitokeza kwa Abramu, alimpatia Abramu tumaini gani?

Yahwe alimwambia Abramu kutokuwa na hofu, na kwamba alikuwa ngao ya Abramu na dhawabu yake kubwa sana.

Abramu alikuwa na wasiwasi juu ya nini?

Abramu alikuwa na wasiwasi kwa sababu alikuwa bado hana mtoto, na mtumishi wa nyumba yake alikuwa ndiye mrithi wake.

Genesis 15:4

Yahwe alisema ni nani angekuwa mrithi wa Abramu?

Yahwe alisema ya kwamba mmoja atokaye kutoka kwa mwili wa Abramu atakuwa mrithi wake.

Yahwe alisema Abramu atakuwa na vizazi vingapi?

Yahwe alisema ya kwamba Abramu angekuwa na vizazi vingi kama wingi wa nyota.

Genesis 15:6

Abramu aliitikiaje ahadi ya Yahwe, na kisha Yahwe alifanya nini?

Abramu alimuamini Yahwe, na Yahwe alimhesabia Abramu kuwa mwenye haki.

Abramu alimuuliza Yahwe swali gani kuhusu nchi?

Abramu alimuuliza Yahwe, "nitajuaje kuwa nitairithi?"

Genesis 15:9

Abramu alifanya nini na wanyama alioambiwa kuwaleta?

Abramu aliwakata wanyama mara mbili na kuwaweka kila nyama mkabala na nyenzake.

Genesis 15:12

Nini kilitokea kwa Abramu jua lilipokuwa linazama?

Jua lilipokuwa likizama chini, Abramu alilala usingizi mzito na giza kuu ya kutisha ikamfunika.

Yahwe alisema vizazi vya Abramu vitatumikishwa na kuteswa kwa muda gani?

Yahwe alimwambia Abramu vizazi vyake vitatumikishwa na kuteswa kwa miaka mia nne.

Genesis 15:14

Yahwe alisema nini kitatokea kwa taifa ambalo litatumikisha vizazi vya Abramu?

Yahwe alisema ya kwamba atahukumu taifa hilo.

Yahwe alisema maisha ya Abramu yatamalizikaje?

Yahwe alisema ya kwamba Abramu atakufa kwa amani katika uzee mwema.

Nini kitafikia kikomo kabla vizazi vya Abramu havijarudi katika nchi iliyoahidiwa kwao?

Dhambi ya Waamori itafikia kikomo kabla ya vizazi vya Abramu kurudi.

Genesis 15:17

Kitu gani kilitokea miongoni mwa vipande vya wanyama alioandaa Abramu usiku huo?

Chungu cha moshi wenye moto na miali ya mwanga ilipita kati ya vile vipande vya wanyama.

Yahwe alifanya agano gani na Abramu siku hiyo?

Yahwe alifanya agano na Abramu ya kwamba angempatia nchi hii uzao wa Abramu.