Genesis 12

Genesis 12:1

Abramu alipokuwa akiishi Harani, Yahwe alimwambia Abramu afanye nini?

Yahwe alimwambia Abramu kuacha nyumba ya baba yake na kwenda katika nchi ambayo angemuonyesha Abramu.

Ahadi gani aliyoifanya Yahwe kwa Abramu?

Yahwe aliahidi ya kwamba angembariki Abramu, kumfanya kuwa taifa kubwa, na kubariki familia zote za duniani kupitia kwake.

Genesis 12:4

Nani alisafiri pamoja na Abramu?

Abramu alisafiri pamoja na Sarai, mke wake, na Lutu, mwana wa ndugu yake.

Abramu alisafiri katika nchi gani?

Abramu alisafiri katika nchi ya Kaanani.

Genesis 12:6

Yahwe alipomtokea Abramu, alitoa ahadi gani kwake?

Yahwe aliahidi ya kwamba uzao wa Abramu utaishi Kaanani.

Genesis 12:8

Abramu alimuabuduje Yahwe?

Abramu alijenga madhabahu kwa ajili ya Yahwe na kuliita jina la Yahwe.

Genesis 12:10

Abramu alisafiri kwenda wapi, alipoondoka Kaanani?

Abrahamu alisafiri kwenda Misri, alipoondoka Kaanani.

Alipoingia Misri, Abramu alihangaishwa na nini?

Abramu alihangaishwa na Wamisri kumuua na kuchukua mke wake Sarai kwa sababu alikuwa mzuri.

Abramu alimwambia Sarai awaambie nini Wamisri wote juu yake?

Abramu alimuomba Sarai kuwaambia Wamisri ya kwamba yeye alikuwa dada wa Abramu.

Genesis 12:14

Nini kilitokea kwa Sarai alipoingia Misri?

Farao alimchukua Sarai katika nyumba yake.

Genesis 12:17

Nini kilitokea kwa Farao katika kipindi hiki?

Yahwe akampiga Farao na nyumba yake na mapigo makuu.

Farao alimuuliza Abramu swali gani?

Farao alimuuliza Abramu kwa nini alimwambia ya kwamba Sarai alikuwa dada yake badala ya mke wake.

Farao alifanya nini na Abramu na Sarai?

Farao aliwaondoa Abramu na Sarai.