Genesis 4

Genesis 4:1

Kaini na Habili walifanya kazi gani?

Kaini alilima udongo, na Habili alikuwa mchungaji.

Genesis 4:3

Kaini alileta sadaka gani kwa Yahwe?

Kaini alileta baadhi ya matunda ya ardhi.

Habili alileta sadaka gani kwa Yahwe?

Habili alileta baadhi ya wazawa wa kwanza wa mifugo yake na sehemu ya wanyama walionona.

Mungu aliitikiaje sadaka ya Kaini na Habili?

Yahwe alipokea sadaka ya Habili, lakini hakupokea sadaka ya Kaini.

Kaini alionyesha hisia gani?

Kaini alikasirika sana, na uso wake ukahuzunika.

Genesis 4:6

Yahwe alimwambia Kaini alitakiwa kufanya nini ili akubalike?

Yahwe alimwambia Kaini kufanya lililo jema na atakubalika.

Genesis 4:8

Baadae, nini kilitokea kwa Kaini na Habili shambani?

Kaini aliinuka juu na kumuua Habili.

Yahwe alipomuuliza Kaini ndugu yake alikuwa wapi, Kaini alisema nini?

Kaini alisema, "mimi sijui. Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu"?

Genesis 4:10

Laana ya Mungu juu ya Kaini ilikuwa ipi?

Laana ya Kaini ilikuwa kwamba nchi haitazaa nguvu yake kwake na angekuwa kimbizi na mzururaji.

Genesis 4:13

Yahwe alifanya nini kuhakikisha hakuna mtu wa kumuua Kaini?

Yahwe aliweka alama juu ya Kaini.

Genesis 4:16

Kaini alikwenda kuishi wapi?

Kaini aliishi katika nchi ya Nodi, mashariki mwa Edeni.

Genesis 4:18

Mzawa wa Kaini Lameki alikuwa na wake wangapi?

Lameki alikuwa na wake wawili.

Genesis 4:23

Lameki aliwaambia wake zake amefanya kitu gani?

Lameki aliwaambia wake zake ya kwamba amemuua mtu.

Genesis 4:25

Mwana mwingine aliyezaliwa kwa Adamu na Hawa alikuwa anaitwa nani?

Mwana mwingine wa Adamu na Hawa alikuwa anaitwa Sethi.

Watu walianza kufanya nini katika siku za mwana wa Sethi Enoshi?

Watu walianza kuliita jina la Yahwe.