Genesis 37

Genesis 37:1

nchi aliyokaa babaye, katika nchi ya Kanaani

"katika nchi ya Kaanani ambapo baba yake aliishi"

Haya ndiyo matukio yaliyomhusu Yakobo

Sentensi hii inatambulisha habari ya watoto wa Yakobo katika Mwanzo 37:1-50:26. Hapa "Yakobo" ina maana ya familia yake nzima. "Hii ni habari ya familia ya Yakobo"

umri wa miaka kumi na saba

"umri wa miak 17"

Bilha

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Raheli.

Zilpa

Hili ni jina la mtumishi wa kike wa Lea.

wake

"suria". Wanawake hawa walikuwa watumishi wa Lea na Raheli waliopewa kwa Yakobo kumzalia watoto.

akaleta taarifa yao mbaya kuhusu wao

"taarifa mbaya kuhusu kaka zake"

Genesis 37:3

Basi

Neno hili linatumika hapa kuweka alama ya badiliko kutoka kwa simulizi kwenda kwa taarifa ya nyuma kuhusu Israeli na Yusufu.

akampenda

Hii ina maana ya upendo wa kindugu au upendo wa kirafiki au kifamilia. Huu ni upendo wa kawaida wa binadamu kati ya marafiki na ndugu.

wa uzee wake

Hii ina maana ya kwamba Yusufu alizaliwa wakati Israeli alikuwa mzee. "aliyezaliwa wakati Israeli alipokuwa mtu mzee"

Akamshonea

"Israeli alimshonea Yusufu"

vazi zuri

"joho zuri"

hawakuongea naye vema.

"hawakuweza kuongea kwa namna ya upole kwake"

Genesis 37:5

Yusufu akaota ndoto, na akawambia ndugu zake. Wakamchukia zaidi

Huu ni ufupi wa matukio ambayo yatatokea katika 37:6-11.

Wakamchukia zaidi

"Na kaka zake Yusufu walimchukia zaidi ya walivyomchukia hapo awali"

Tafadhari sikilizeni ndoto hii niliyoiota

"Tafadhali sikilizeni ndoto hii niliyoipata"

Genesis 37:7

Taarifa ya Jumla:

Yusufu anaeleza kaka zake kuhusu ndoto yake.

Tazama

Neno la "tazama" hapa linatuamsha kuvuta nadhari kwa taarifa ya kushangaza inayofuata.

tulikuwa

Neo "tulikuwa" ina maana ya Yusufu na inajumuisha kaka zake wote.

tukifunga miganda ya nafaka

Nafaka inapovunwa inafungwa katika makundi na kupangwa katika rundo hadi muda wa kuzitenga nafaka kutoka kwa majani makavu.

na tazama

Hapa neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Yusufu alishangazwa na kile alichokiona.

mganda wangu ukainuka na kusimama wima ... miganda yenu ikasogea na kuuinamia mganda wangu

Hapa miganda ya nafaka inasimama wima na kupiga magoti kana kwamba ilikuwa watu. Miganda hii inawakilisha Yusufu na kaka zake.

Je ni kweli utatutawala? Je utatutawala juu yetu?

Misemo hii miwili ina maana moja. Kaka zake Yusufu wanatumia swali kumkejeli Yusufu. Inaweza kuandikwa kama kauli. "Hutaweza kuwa mfalme wetu, na hatutainama chini kwako!"

utatutawala juu yetu

Neno la "yetu" lina maana ya kaka zake Yusufu lakini sio Yusufu.

kwa ajili ya ndoto zake na maneno yake

"kwa sababu ya ndoto yake na kile alichokisema"

Genesis 37:9

Akaota ndoto nyingine

"Yusufu akapata ndoto nyingine"

nyota kumi na moja

"nyota 11"

baba yake akamkemea. Akamwambia

"Israeli alimkaripia, akisema"

Je umeota ndoto ya namna gani hii? Je mama yako ... kukuinamia mpaka chini?

Israeli anatumia swali kumrekebisha Yusufu. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Ndoto hii uliyoota sio ya kweli. Mama yako, kaka zako, na mimi hatutainama chini mbele yako!"

wivu

Hii ina maana kuwa na hasira kwa sababu mtu mwingine amefanikiwa au ana umaarufu zaidi.

akaliwema jambo hilo moyoni

Hii ina maana ya kwamba aliendelea kufikiria kuhusu maana ya ndoto ya Yusufu. "aliendelea kufikiria kuhusu maana ya ndoto ile"

Genesis 37:12

Je ndugu zako hawalichungi kundi huko Shekemu?

Israeli anatumia swali kuanza mazungumzo. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Ndugu zako wanachunga kundi huko Shekemu".

Njoo

Hapa inasemekana ya kwamba Israeli anamuomba Yusufu kujiandaa kuondoka kuonana na ndugu zake. "Jiandae"

nipo tayari

Yupo tayari kuondoka. "Nipo tayari kuondoka"

Akamwambia

"Israeli akamwambia Yusufu"

uniletee neno

Israeli anamtaka Yusufu kurudi na kumuambia kuhusu kaka zake na hali ya mifugo. "njoo uniambie utakakikuta" au "niletee taarifa"

kutoka katika bonde

"kutoka bondeni"

Genesis 37:15

Mtu mmoja akamwona Yusufu. Tazama, Yusufu alikuwa akizunguka kondeni

"Mtu mmoja akamkuta Yusufu akizunguka kondeni"

Tazama

Hii inaweka alama mwanzo wa tukio jingine katika simulizi kuu. Inaweza kuhusisha watu tofauti kuliko matukio ya nyuma.

Unatafuta nini?

"Ni nini unatafuta"

Tafadhari, niambie, wapi

"Tafadhali niambie wapi"

wananalichunga kundi

"wakichunga kundi"

Dothani

Hili ni jina la mahali ambalo lipo kama kilomita 22 kutoka Shekemu.

Genesis 37:18

Wakamwona kutokea mbali

"Ndugu zake Yusufu wakamwona alipokuwa bado yupo mbali"

wakapanga njama ya kumwua

"wakafanya njama ya kumuua"

mwotaji anakaribia

"anakuja yule mwenye ndoto zile"

Njoni sasa

Msemo huu unaonyesha ya kwamba kaka zake walitekeleza mipango yao. "Kwa hiyo sasa"

Mnyama mkali

"mnyama wa hatari" au "mnyama mkali"

amemmeza

amemla kwa hamu

Nasi tutaona ndoto zake zitakuwaje

Ndugu zake walipanga kumuua, kwa hiyo ni kejeli kuzungumzia kuhusu ndoto zake kuwa kweli, maana angekuwa amekwisha kufa. "Kwa njia hiyo tutahakikisha ndoto zake haziji kuwa kweli"

Genesis 37:21

alilisikia

"alisikia walichokuwa wakisema"

kutoka katika mikono yao

Msemo "mikono yao" una maana ya mipango ya kaka zake ya kumuua. "kutoka kwao" au "kutoka kwa mipango yao"

Tusiuondoe uhai wake

Msemo wa "kuondoa uhai wake" ni tasifida kwa kumuua mtu. "Tusimuue Yusufu"

Msimwage damu

Ukanushaji unaweza kuwekwa juu ya kitenzi. Pia "kumwaga damu" ni tasifida ya kuua mtu. "Usimwage damu yoyote" au "Usimuue"

msiweke mikono yenu juu yake

Hii ina maana ya kumdhuru au kumjeruhi. "msimdhuru"

ili kwamba aweze kumwokoa

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Rubeni alisema hivi ili aweze kumuokoa Yusufu"

mikono mwao

Msemo wa "mikononi mwao" una maana ya mpango wa kaka zake kumuua. "kutoka kwao" au "kutoka kwa mipango yao"

kumrudisha

"na kumrudisha"

Genesis 37:23

Ikawa

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama juu ya tukio muhimu la simulizi.

walimvua vazi lake zuri

"walichana joho lake zuri kutoka kwake"

vazi lake zuri

"joho zuri"

Genesis 37:25

Wakakaa chini kula mkate

"Mkate" ni lugha nyingine kwa "chakula". "Walikaa chini kula chakula" au "Ndugu zake Yusufu walikaa chini kula"

Walipoinua macho yao na kuangalia, na, tazama, msafara

Hapa kuangalia juu inazungumziwa kana kwamba mtu aliinua macho yake juu kihalisia. Pia, neno "tazama" linatumika hapa kuvuta nadhari ya msomaji kwa kile walichokiona wanamume hawa. "Walitazama juu na ghafla wakaona msafara"

ulikuwa

"umebeba"

viungo

vikolezo

malhamu

kitu chenye mafuta chenye harufu tamu kinachotumiwa kwa ajili ya kuponya na kulinda ngozi. "dawa"

wakisafiri kuvichukua kuelekea Misri

"kuwaleta mpaka Misri". Hii inaweza kuwekwa wazi zaidi. "kuwaleta chini hadi Misiri kuviuza"

Ni faida gani kama tutamwua ndugu yetu na kufunika damu yake?

Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Hatupati faida yoyote kumuua ndugu yetu na kufunika damu yake"

kufunika damu yake

Huu ni msemo wenye maana ya kuficha kifo cha Yusufu. "kuficha mauaji yake"

Genesis 37:27

kwa Waishmaeli

"kwa wanamume hawa ambao ni vizazi vya Ishmaeli"

tusiweke mikono yetu juu yake

Hii ina maana ya kutomdhuru au kumjeruhi. "msimuumize"

ni ndugu yetu, nyama yetu

Neno la "nyama" ni lugha nyingine lenye maana ya ndugu. "ni ndugu wetu wa damu"

ndugu zake wakamsikiliza

"Kaka zake na Yuda walimsikiliza" au "Kaka zake Yuda walikubaliana naye"

Kimidiani ... Waishmaeli

Majina yote mawili yana maana ya kundi moja la wafanyabiashara ambao ndugu zake Yusufu walikutana nao.

kwa vipande ishirini vya fedha

"kwa bei ya vipande 20 vya fedha"

wakamchukua Yusufu mpaka Misri

"wakampeleka Yusufu Misri"

Genesis 37:29

Rubeni akarudi kwenye shimo, na, tazama, Yusufu hakuwemo shimoni

"Rubeni alirudi kwenye shimo, na akashangazwa kuona ya kwamba Yusufu hakuwepo mle" Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Rubeni alishangazwa kukuta ya kwamba Yusufu aliondoka.

Akararua mavazi yake

Hili ni tendo la mawazo na uchungu mkubwa. Hii inaweza kuandikwa kwa uwazi zaidi. "Alikuwa na majonzi mpaka akararua nguo zake"

Kijana yuko wapi? Na mimi, je niende wapi?"

Rubeni anatumia maswali kuweka msisitizo kwa tatizo ambalo Yusufu hapatikani. Hivi vinaweza kuandikwa kama kauli. "Kijana ametoweka! Siwezi kurudi nyumbani sasa!"

Genesis 37:31

vazi la Yusufu

Hii ina maana ya joho zuri ambalo baba yake alimtengenezea.

damu

"damu ya mbuzi"

wakalipeleka

"walileta joho lile"

amemrarua

"amemla"

Yusufu ameraruliwa katika vipande.

Yakobo anadhani ya kwamba mnyama pori amerarua mwili wa Yusufu vipande vipande. "hakika imemchana Yusufu katika vipande vipande"

Genesis 37:34

Yakobo akararua mavazi yake

Hili ni tendo la mawazo na uchungu mkubwa. Hii inaweza kuandikwa kwa uwazi zaidi. "Yakobo alikuwa na majonzi mpaka akararua nguo zake"

kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake

Hapa "viuno" ina maana ya sehemu ya katikati ya mwili au kiuno. "akavaa magunia"

wakainuka

Hapa ujio wa watoto kwa baba yao inazungumziwa kama "kuinuka juu". "wakaja kwake"

lakini alikataa kufarijiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "lakini hakutaka wamfariji"

Hakika nitashuka kuzimu nikimwombolezea

Hii ina maana ataomboleza kutoka sasa hadi pale atakapokufa. "Kweli nitakapokufa na kwenda kuzimu bado nitakuwa naomboleza"

Wamidiani wakamwuza

"Wamidiani walimuuza Yusufu"

kepteni wa walinzi

"kiongozi wa wanajeshi waliokuwa wakimlinda mfalme"