Genesis 8

Genesis 8:1

akamtazama

"akamkumbuka" au "alimfikiria"

safina

Hii inamaanisha sanduku kubwa sana ambalo lingeweza kuelea juu ya maji hata katika dhoruba mbaya. "mtumbwi mkubwa" au "meli" au "tishali"

Chemichemi za vilindi pamoja na madirisha ya mbingu vikafungwa

"Maji yaliacha kutoka chini ya ardhi na mvua zikaacha kunyesha." Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu alifunga chemichemi za vilindi na madirisha ya mbinguni"

chemichemi za vilindi

"maji kutoka chini ya ardhi"

madirisha ya mbingu vikafungwa

Hii ina maana ya mvua kuacha kunyesha. Hii ina maana ya mvua. Inaelezea anga kama dari ambalo hutunza maji juu yake kutodondoka ardhini. Madirisha, au milango, ya anga yalipofunguliwa, maji yalifunguka chini kupitia kwao. "anga ikafungua" au "milango ya anga ikafunguka"

Genesis 8:4

ikatulia

"ikatua" au "ikasimama juu ya ardhi ngumu"

katika mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya ... mwezi wa kumi

Kwa sababu Musa aliandika kitabu hiki, inawezekana ana maana ya mwezi wa saba na mwezi wa kumu kwa kalenda ya Kihebrania, lakini hii haipo wazi.

Katika siku ya kwanza ya mwezi

"Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kumi"

vikaonekana

Hii inaweza kuwekwa wazi: "ikaonekana juu ya uso wa maji"

Genesis 8:6

Ikatokea kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi. "Ikawa kwamba"

Ikatokea kwamba ... dirisha la safina ambayo aliitengeneza

Msemo "ambayo alitengeneza" unazungumzia kuhusu madirisha. Baadhi ya lugha zaweza kufanya msemo huu kuwa sentensi tofauti. "Nuhu alitengeneza dirisha katika safina. Ikaja kuwa baada ya siku arobaini ndipo dirisha likafunguliwa"

kunguru

ndege mweusi anayekula zaidi nyama ya mizoga ya wanyama

akaruka mbele na nyuma

Hii ina maana ya kwamba kunguru aliendelea kuacha safina na kurejea.

hadi maji yalipo kauka

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "hadi pale upepo ulipokausha maji" au "hadi maji yalipokauka"

Genesis 8:8

kutua unyayo wake

"kutua" au "kutulia juu ya". Ina maana ya kutua juu ya kitu ili kupumzika kupaa.

unyayo wake ... akarudi ... akamchukua

Neno "njiwa" kwa lugha ya mwandishi ni la kike. Unaweza kutafsiri msemo huu na kiwakilishi cha "hiki ... huyu ... hii" au "yake ... yeye ... yeye" kulingana na namna gani lugha inamfafanua njiwa.

Akanyoosha ... naye

Ukitumia kiwakilishi cha kiume kwa neno "njiwa" inaweza kuhitaji kuongeza jina la Nuhu ili kukwepa mchanganyo. "Nuhu alimtuma njiwa," "Nuhu alinyosha mkono wake mbele" n.k.

Genesis 8:10

Tazama

"Sikiliza kwa makini" au "Hii ni muhimu"

jani bichi la mzeituni lililochumwa

"jani ambalo njiwa alichuma kutoka katika mzeituni"

lililochumwa

"kunyofoa"

Akasubiri siku saba zingine

"Alisubiri tena siku saba"

Njiwa hakurudi kwake tena

Iwapo watu hawataelewa unaweza kutoa sababu wazi: "Hakurudi tena kwake kwa sababu alipata sehemu ya kutua".

Genesis 8:13

Ikawa kwamba

Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

katika mwaka wa mia sita na mwaka wa kwanza

"Nuhu alipokuwa na umri wa miaka 601"

mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi

Kwa sababu Musa aliandika kitabu hiki, inawezekana ana maana ya mwezi wa saba na mwezi wa kumu kwa kalenda ya Kiebrania, lakini hii haipo wazi.

maji yalikuwa yamekauka katika nchi

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "maji yaliyofunika nchi yalikauka" au "upepo ulikausha maji yaliyofunika nchi"

kifuniko cha safina

Hii ina maana ya kifuniko kilichozuia maji ya mvua kuingia ndani ya safina.

tazama

Neno "tazama" linatuambia kuwa makini kwa ajili ya taarifa muhimu inayafuatia.

Katika mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi

siku ya saba ya mwezi - "Katika siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili." Hii inaweza kuwa na maana ya mwezi wa pili katika kalenda ya Kihebrania, lakini haipo wazi.

nchi ilikuwa imekauka

"ardhi ilikuwa imekauka kabisa"

Genesis 8:15

Toka nje ... 17Wachukuwe

"Ondoka ...Chukua" Baadhi ya tafsiri husoma "Njoo nje ... Leta nje".

kila kiumbe hai chenye mwili

"kila aina ya kiumbe hai" Maana yaweza kuwa 1) wanadamu wote au 2) viumbe vyote vyenye mwili, ikijumlisha wanadamu na wanyama.

kwa kuzaliana na kuongezeka

Hii ni lahaja. Jazeni nchi na watu. Mungu alitaka wanadamu na wanyama kuzaliana, ili waweze kuwa wengi wa aina yao.

Genesis 8:18

Nuhu akatoka nje

Baadhi ya tafsiri husoma "Nuhu akaja nje"

kwa kabila zao

"katika makundi ya aina yao wenyewe"

Genesis 8:20

akajenga madhabahu kwa Yahwe

"akajenga madhabahu kwa makusudi ya Yahwe" au "akajenga madhabahu kwa ajili ya kumuabudu Yahwe." Inawezekana alijenga kwa mawe.

wanyama walio safi ... ndege walio safi

Hapa "safi" ina maana ya kwamba Mungu aliruhusu wanyama hawa kutumika kama sadaka. Baadha ya wanyama hawakutumika kwa ajili ya sadaka na waliitwa "wasio safi".

kutoa sadaka ya kuteketezwa

Nuhu aliwaua wanyama na kuwachoma kabisa kama sadaka kwa Mungu. "aliwachoma wanyama kama sadaka kwa Yahwe"

harufu nzuri ya kuridhisha

Hii ina maana ya harufu nzuri ya nyama ya kuchomwa.

akasema moyoni mwake

Hapa neno la "moyo" lina maana ya mawazo na hisia za Mungu.

laani ardhi

"kuleta madhara makubwa kwenye nchi"

kwa sababu ya mwanadamu

Hii inaweza kuwa wazi: "kwa sababu mwanadamu ni mwenye dhambi"

nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto

"kutoka miaka yao ya utotoni wanakuwa wakifanya mambo maovu" au "walipokuwa wadogo, walitaka kufanya mambo maovu"

nia za mioyo yao

Hapa neno "mioyo" lina maana ya mawazo, hisia, haja na ridhaa ya watu. "mwelekeo wao" au "tabia yao"

tokea utoto

Hii ina maana ya mtoto mwenye umri mkubwa. "kutoka ujana wao"

Wakati nchi isaliapo

"wakati nchi inapoendelea kudumu" au "Kadri nchi inavyoendelea kuwepo"

majira ya kupanda mbegu

"msimu wa kupanda"

baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi

Misemo hii miwili ina maana ya aina mbili za majira katika mwaka.

kiangazi

kipindi kikavu na cha joto cha mwaka

majira ya baridi

kipindi cha baridi kidogo na theluji katika mwaka

havitakoma

"havitaacha kuwepo" au "havitaacha kutendeka" . Hii inaweza kuelezwa katika hali ya chanya. "vitaendelea"