Genesis 9

Genesis 9:1

Zaeni, mkaongezeke, na muijaze nchi

Hii ni baraka ya Mungu. Alimwambia Nuhu pamoja na familia yake kuzaliana wanadamu wengine kama wao, ili kwamba wawe wengi wa aina yao. Neno "mkaongezeke" linafafanua jinsi gani wanapaswa "kuzaana"

Hofu na utisho wenu vitakuwa juu ya kila mnyama aliye hai ... na juu ya samaki wote wa baharini

Mwandishi anazungumzia hofu na utisho kana kwamba ni vitu vya mwili ambavyo vingeweza kuwa juu ya wanyama. "Kila mnyama hai ... na samaki wote wa baharini watakua na hofu kubwa sana juu yako"

Hofu na utisho wenu

maneno "hofu" na "utisho" zina maana moja na husisitiza jinsi wanyama walivyokuwa wanaogopa binadamu. "Hofu ya utisho kwako" au "Hofu ya kutisha kwako"

kila mnyama aliye hai juu ya nchi

Hili ni moja kati ya makundi manne ya wanyama ambayo mwandishi ameorodhesha, na sio ufupisho wa wanyama waliosalia atakaowataja hapo baadae

ndege

Huu ni msemo wa jumla kwa vitu vinavyopaa. "wanyama warukao" au "vitu vinavyoruka"

juu ya kila kitu kiendacho chini juu ya ardhi

Hii inajumuisha aina yote ya wanyama.

Vimetolewa katika mikono yenu

Mkono ni lugha mbadala kwa mamlaka ambayo mkono ulikuwa nayo. Hii inaweza kuwa katika hali ya kutenda. "Vimetolewa katika mamlaka yako" au "Nimeviweka chini ya mamlaka yako"

Genesis 9:3

Taarifa ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu pamoja na watoto wake.

uhai ... damu

"Damu ni alama ya uhai". "Mungu alikuwa akiwaamuru watu wasile nyama ambayo bado ina damu ndani yake. Walipaswa kutoa kwanza damu"

Genesis 9:5

Taarifa ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu pamoja na watoto wake.

Lakini kwa ajili ya damu yenu

Hii inatofautisha damu ya mwanadamu na damu ya wanyama

kwa ajili ya damu yenu

Inaonyesha ya kwamba damu imemwagwa, au imemwagika, au mwagikia. "iwapo yeyote atasababisha damu yako kumwagika" au "iwapo yeyote atamwaga damu yako" au "iwapo yeyote atakuua"

uhai

Hii ina maana ya uhai wa mwili.

nitataka malipo

Malipo haya yana maana kifo kwa yule muuaji, sio fedha. "Nitataka yeyote atakayekuua kulipa"

Kutoka katika mkono

Hapa neno "mkono" lina maana ya yule mtu anayehusika na jambo kutendeka.

Kutoka katika mkono wa kila mnyama nitaitaka

"Nitataka mnyama yeyote atakayetoa uhai wako kulipa"

Kutoka katika mkono wa kila mtu, yaani, kutoka katika mkono wa yule ambaye amemuua ndugu yake, nitataka fidia kwa ajili ya uhai wa mtu huyo.

"Nitataka mtut yeyote atakayetoa uhai wa mtu mwingine kulipa"

Kutoka katika mkono

Msemo huu una maana ya mtu katika hali ya ukaribu sana. "Kutoka kwa mtu huyo kabisa"

ndugu

Hapa "ndugu" inatumika kama kumbukumbu ya jumla kwa jamaa, kama wanajumuiya wa kabila moja, ukoo au kikundi cha watu.

Yeyote amwagaye damu ya mtu, kwa njia ya mtu damu yake itamwagwa

Kumwaga kwa damu ni sitiari kwa ajili ya kuua mtu. Hii ina maanisha kama mtu atamuua mtu, mtu mwingine anapaswa kumuua muuaji. japokuwa, "damu" ina umuhimu sana katika kipengele hichi na inapaswa kutumiwa katika tafsiri ikiwezekana.

kwa sababu ilikuwa ni katika mfano wa Mungu kwamba Mungu alimuumba mtu

"kwa sababu Mungu aliumba watu wafanane na yeye" au "kwa sababu niliumba watu katika mfano wangu"

zaeni na kuongezeka

Hii ni baraka ya Mungu. Alimwambia Nuhu na familia yake kuzaa wanadamu wengine kama wao wenyewe, ili kusudi waweze kuwa wengi zaidi. Neno "kuongezeka" linafafanua jinsi ya wao "kuzaa"

Genesis 9:8

Kisha Mungu akazungumza na Nuhu na wanae pamoja naye

Mungu alikuwa akizungumza nao tayari. Msemo huu unaweka alama ya mabadiliko juu ya kile Mungu alichokuwa akienda kukizungumzia. "Mungu aliendelea kuzungumza na Nuhu pamoja na watoto wake" au "Kisha Mungu akaendelea kusema"

Kwa ajili yangu

Msemo huu unatumika kwa Kiingereza kuweka alama ya mabadiliko juu ya kile Mungu alichokuwa akizungumzia juu ya Nuhu na wanawe walichopaswa kufanya na kuzungumzia juu ya nini Mungu angefanya.

kulithibitisha agano langu pamoja nawe

"fanya agano kati yako na mimi"

Genesis 9:11

Maelezo ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu na wanawe.

ninalithibitisha agano langu pamoja nanyi

"kwa kusema hivi, ninafanya agano langu pamoja na wewe"

mwili

Maana zaweza kuwa 1) binadamu wote au 2) wenye viumbe wote, kujumlisha binadamu na wanyama.

Tena hapatatokea gharika ya kuangamiza nchi

"Hakutakuwa tena na gharika ambalo litaangamiza nchi". Kutakuwa na gharika, lakini hazitaangamiza dunia nzima.

ishara

Hii ina maana ya ukumbusho wa jambo lililoahidiwa.

agano ... kwa vizazi vyote vya baadaye

Agano hili linamhusu Nuhu na familia yake na pia vizazi vyote vitakavyofuata.

Genesis 9:14

Maelezo ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu na wanawe.

itakuwa nitakapoleta

"Itakapokuwa". Ni jambo ambalo hutokea mara nyingi.

upinde wa mvua ukaonekana

Haipo wazi ni nani atauona upinde wa mvua, lakini kwa sababu agano upo kati ya Yahwe na watu, iwapo utataka kusema nani atauona upinde wa mvua, ni vyema kuwataja wote Yahwe na watu. Hii inaweza kutafsiriwa katika hali ya kutenda. "watu pamoja na mimi tunauona upinde wa mvua"

upinde wa mvua

mstari wa rangi wenye mwanga unaojitokeza katika mvua ambapo jua hungaa kutoka nyuma ya mtazamaji.

nitakumbuka agano langu

Hii haimaanishi ya kwamba Mungu angesahau kwanza. "Nitafikiria juu ya agano langu"

yangu na ninyi

Neno "ninyi" ni wingi. Mungu anazungumza na Nuhu na wana wa Nuhu.

kila kiumbe hai cha wote mwenye mwili

"kila aina na kiumbe hai"

mwenye mwili

Maana zaweza kuwa 1) binadamu wote au 2) wenye viumbe wote wenye mwili, kujumlisha binadamu na wanyama.

Genesis 9:16

Maelezo ya Jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza na Nuhu na wanawe.

ili kukumbuka

"ili kwamba nikumbuke" au "ili kwamba nitafikiria juu ya"

kati ya Mungu na kila kiumbe

Mungu anazungumza hapa. "kati yangu na kila kiumbe hai"

kila kiumbe hai cha wote wenye mwili

"kila aina ya kiumbe hai"

Kisha Mungu akamwambia Nuhu

Mungu alikuwa tayari anazungumza na Nuhu. Msemo huu unaweka alama ya sehemu ya mwisho ya kile Mngu alichokuwa akisema. "Mungu alimalizia kwa kusema kwa Nuhu" au "Kwa hiyo Mungu akasema kwa Nuhu"

Genesis 9:18

Maelezo ya Jumla

Mistari ya 18-19 inatambulisha wana watatu wa Nuhu, ambao watakuwa sehemu muhimu katika simulizi ifuatayo.

baba

Hamu alikuwa baba wa Kaanani wa halisi.

Genesis 9:20

mkulima

"mtu wa ardhi"

akalewa

"alikunywa divai nyingi sana"

uchi

Maandishi haisemi jinsi gani mwili wa Nuhu ulikuwa uchi alipokuwa amelala kalewa. Mapokeo ya wanawe yalionyesha ya kwamba ilikuwa suala la aibu.

Genesis 9:22

baba yake

Hii ina maana ya Nuhu.

Genesis 9:24

Maelezo ya Jumla:

Katika mistari ya 25-27 Nuhu anatamka laana juu ya mwana wa Hamu na baraka juu ya ndugu za hamu. Kile alichokisema Nuhu juu yao pia iliwahusu uzao wao.

Maelezo ya Jumla:

Misemo tofauti katika mistari hii inakusudiwa kuonyesha ya kwamba hii ilikuwa shairi.

alipozinduka kutoka katika ulevi wake

"akawa mtulivu"

mtoto wake mdogo

Hii ina maana ya Hamu. "mwanawe mdogo, Hamu"

Alaaniwe Kanaani

"Ninakulaani Kaanani" au "Na mambo mabaya yafanyike kwako Kaanani"

Kanaani

Huyu alikuwa mmoja wa wana wa Hamu. "mwana wa Hamu Kaanani"

mtumishi kwa watumishi wa ndugu zake

"mtumishi wa chini wa kaka zake" au "mtumishi mwenye umuhimu wa chini kabisa kati ya ndugu zake"

ndugu zake

Hii inaweza kumaanisha ndugu zake Kaanani au ndugu zake kwa ujumla.

Genesis 9:26

Maelezo ya Jumla:

Hii ni shairi.

Yahwe , Mungu wa Shemu, abarikiwe

"Yahwe na asifiwe, Mungu wa Shemu" au "Yahwe, Mungu wa Shemu, anastahili sifa" au "Ninamsifu Yahwe, Mungu wa Shemu"

Kanaani na awe mtumishi wake

"Na Kaanani awe mtumishi wa Shemu". Hii inajumlisha uzao wa Kaanani na Shemu.

Mungu na apanue mipaka ya Yafethi

Maana zaweza kuwa 1) "Mungu na afanya mipaka ya Yafethi mikubwa" au 2) "Mungu na asababishe Yafethi kuwa na uzao mwingi"

na afanye makazi yake katika hema za Shemu

"na mfanye aishi kwa amani na Shemu". Hii inajumlisha uzao wa Yafethi na Shemu.

Kanaani na awe mtumishi wake

"Na Kaanani awe mtumishi wa Yafethi". Hii inajumlisha uzao wa Kaanani na Yafethi.