Genesis 19

Genesis 19:1

Malaika wawili

Mwanzo 18 unasema ya kwamba wanamume wawili waliondoka kwenda Sodoma. Hapa tunajifunza ya kwamba ni kweli walikuwa malaika.

langoni mwa Sodoma

"malango wa mji wa Sodoma." Mji ulikuwa na kuta ukiuzunguka, na watu iliwabidi kupitia malango ili kuingia. Hii ilikuwa sehemu muhimu sana katika mji. Watu muhimu mara kwa mara walitumia muda wao pale.

akainama uso wake chini ardhini

Aliweka goti lake juu ya ardhi na kisha kugusa ardhi kwa kipaji cha uso wake na pua.

Bwana zangu

Huu ulikuwa usemi wa heshima Lutu alitumia kwa malaika.

nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu

"Tafadhali njooni na mkae ndani ya nyumba ya mtumishi wenu"

nyumba ya mtumishi wenu

Lutu anajitambulisha kama mtumishi ili kuonyesha heshima kwao.

muoshe miguu yenu

Watu walipenda kuosha miguu yao baada ya kusafiri.

muamke asubuhi

"muamke mapema"

usiku tutalala

Malaika wawili waliposema hivi, walikuwa wakimaanisha wao wenyewe, na sio Lutu. Wao wawili walipanga kukaa usiku pale mjini.

mjini

Hili ni eneo la wazi, lililo nje katika mji.

wakaondoka pamoja nae

"waligeuka na kuondoka pamoja naye"

Genesis 19:4

kabla hawaja lala

"kabla watu ndani mwa nyumba ya Lutu walipolala usingizi"

wanaume wa mji, wa Sodoma

"wanamume wa mji, yaani, wanamume wa Sodoma" au "wanamume wa mji wa Sodoma"

nyumba

"nyumba ya Lutu"

vijana kwa wazee

"kutoka kwa vijana hadi wazee". Hii ina maana "wanamume wa umri wote" na ina maana ya wanamume wa Sodoma ambao walikuwa wakizunguka nyumba ya Lutu.

walioingia kwako

"waliongia ndani ya nyumba"

kulala nao

"kushiriki tendo la ngono pamoja nao". Lugha yako yaweza kuwa na namna ya upole zaidi ya kusema hivi. "kuwajua karibu zaidi"

Genesis 19:6

nyuma yake

"nyuma yake" au "baada ya kuingia ndani"

Nawasihi, ndugu zangu

"nawaomba, ndugu zangu"

ndugu zangu

Lutu alizungumza kwa njia ya kirafiki kwa wanamume wa mji akitarajia wangemsikiliza. "rafiki zangu"

msitende uovu

"msifanye jambo la uovu hivi" au "msifanye jambo la uovu kama hili"

Tazama

"Sikiliza kwa makini" au"Angalia hapa"

hawajawahi kulala na

"hawajashiriki tendo la ngono na" Lugha yako inaweza kuwa na njia ya upole ya kusema hili. "hawajawajua"

lolote muonalo kuwa jema machoni penu

"lolote mnalotamani" au "lolote mnalofikiria ni sahihi"

chini ya kivuli cha dari yangu

Wanamume wawili walikuwa wageni katika nyumba ya Lutu, kwa hiyo alihitaji kuwalinda. Neno "dari" ni maana nyingine ya kusema nyumba na sitiari kwa Lutu kuwalinda. "ndani ya nyumba yangu, na Mungu anatarajia mimi niwalinde"

Genesis 19:9

Simama nyuma!

"Simama pembeni!" au "Toka katika njia yetu!"

huyu alikuja kukaa hapa kama mgeni

"Huyu hapa alikua hapa kama mtu wa nje" au "Huyu mgeni alikuja kuishi hapa"

huyu

"Lutu". Wanamume wanazungumza wao kwa wao. Kama hii haitakuwa wazi katika lugha yako, unaweza kuwafanya wanamume wazungumze na Lutu hapa.

na sasa amekuwa mwamuzi wetu

"na sasa anadhani ana mamlaka ya kutuambia kipi ni sahihi na kipi sio sahihi" au "lakini hatutamruhusu atuzuie kufanya kile tunachotaka kufanya"

na sasa ame...

"na ingawa hana sababu nzuri, amekuwa"

Sasa tuta...

"Kwa sababu unatuambia ya kwamba tunafanya uovu, tuta.."

tutakushugulilia vibaya wewe kuliko wao

Wanamume walikasirika kwa Lutu kusema, "Msitende uovu hivi" (19:6) kwa hiyo wanamtishia kutenda uovu zaidi ya vile Lutu alivyohofia mara ya kwanza. "tutakushughulikia uovu zaidi na wewe zaidi ya wao"

Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, na wakakaribia kuvunja mlango

Maana zaweza kuwa 1) "walizidi kuja karibu na mwanamume, kwa Lutu, hadi wakawa karibu sana kuweza kuvunja mlango" au 2) walimsukuma Lutu kwa mwili dhidi ya ukuta au mlango wa nyumba na walikuwa wakitaka kuvunja mlango.

huyo mtu ... Lutu

Hizi ni njia mbili zinazomfafanua Lutu.

Genesis 19:10

Lakini wale wanaume

"Lakini wageni wawili wa Lutu" au "Lakini malaika wawili"

wanaume wakamkamata Lutu na kumweka ndani na wakafunga

Lugha yako inaweza kuongezea ya kwamba wanamume walifungua mlango kwanza. "wanamume walifungua mlango vya kutosha mpaka kunyosha mikono yao na kuvuta ... na kisha wakafunga"

wageni wa Lutu wakawapiga kwa upofu wale wanaume

Msemo "wakawapiga kwa upofu" ni sitiari; wageni hawakuwapiga kwa mwili wanamume. "Wageni wa Lutu waliwapofusha wanamume" au "waliondoa uwezo wao wa kuona"

vijana na wazee kwa pamoja

"wanamume wa umri wote". Hii lugha unasisitiza ya kwamba wageni walipofusha wanamume wote. Hii inaweza kumaanisha uwakilishi wa kijamii kuliko umri. "vijana na wazee kwa pamoja"

Genesis 19:12

Basi wale watu wakamwambia

"Kisha wale wanamume wawili wakasema" au "Kisha malaika wawili wakasema"

Je una mtu mwingine yeyote hapa?

"Je una mtu mwingine wa familia yako ndani ya mji?" au "Je una mtu mwingine wa familia katika eneo hili?"

yeyote mwingine katika huu mji

"mtu mwingine katika familia yako anayeishi katika mji huu"

tunakaribia kuiangamiza

Neno "tunakaribia" hapa linajitegemea. Ni malaika wawili pekee wangeenda kuangamiza mji; Lutu hakuwa anaenda kuangamiza mji. Iwapo lugha yako ina namna ya kutenganisha "tunakaribia" basi itumike hapa.

mashitaka dhidi yake mbele ya Yahwe yamezidi

Hii inaweza kusemwa kwa namna nyingine ili kwamba nomino ya "mashtaka" inaelezwa kama kitenzi. "kwa hiyo watuwengi walikuwa wakimwambia Yahwe ya kwamba watu wa mji wanafanya mambo ya uovu"

Genesis 19:14

Lutu akatoka

"Kwa hiyo Lutu aliondoka nyumbani"

wakwe zake, wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake

wakwe zake, wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake Msemo wa "wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake" unafafanua maana ya "mkwe" hapa. "wanamume waliokuwa wakielekea kuwaoa binti zake" au "wachumba wa binti zake"

Alfajiri

"Kabla jua halijachomoza"

ondoka

"Ondoka sasa"

usipotelee katika adhabu ya mji huu

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili Yahwe asikuangamize pia atakapowaadhibu watu wa mji huu"

usipotelee katika adhabu

Mungu kuangamiza watu wa mji unazungumzwa kana kwamba mtu anafagia vumbi.

ya mji

Hapa "mji" una maana ya watu.

Genesis 19:16

Lakini akakawia-kawia

"Lakini Lutu alisita" au "Lakini Lutu hakuanza kuondoka"

Kwa hiyo watu wale wakamshika

"kwa hiyo wanamume wawili walimkamata" au "Kwa hiyo malaika walimkamata"

alimhurumia

"akawa na huruma kwa Lutu". Yahwe anaelezwa kama kuwa na "huruma" kwa sababu alikuwa akitunza uhai wa Lutu na familia yake badala ya kuwaangamiza alipoangamiza watu wa Sodoma kwa maovu waliofanya.

Walipowatoa nje

"Wanamume wawili walipowatoa familia ya Lutu nje"

jiponye nafsi yako!

Hii ilikuwa namna ya kuwaambia wakimbie ili wasife. "Kimbia na uokoe maisha yenu!"

usitazame nyuma

Msemo "katika mji" unaeleweka. "Usitazame nyuma katika mji" au "Usitazame nyuma katika Sodoma"

kwenye hili bonde

Hii ina maana bonde la Mto Yordani. Hii ina maana ya jumla ya eneo la Mto Yordani.

usije ukatoweshwa mbali

Inaeleweka ya kwamba watatoweshwa pamoja na watu wa mji. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "la sivyo Mungu atawaangamiza pamoja na watu wa mji"

ukatoweshwa mbali

Mungu kuwaangamiza watu wa mji inazungumziwa kana kwamba mtu anafagia vumbi.

Genesis 19:18

Mtumishi wenu amepata kibali machoni pako

Kupendezwa na mtu inazungumziwa kana kwamba "fadhila" ni kitu kinachoweza kupatikana. Pia, "machoni" ni lugha nyingine inayowakilisha mawazo au fikra za mtu. "Umependezwa na mimi"

Mtumishi wenu ame...

Lutu alikuwa akionyesha heshima kwa kumaanisha mwenyewe kama "mtumishi wako". "Mimi, mtumishi wako, nime..."

umenionesha wema ulio mkuu kwa kuokoa maisha yangu

Kitenzi cha "wema" kinaweza kuelezwa kama "wema". "Umekuwa mwema sana kwangu kwa kuokoa maisha yangu"

sitaweza kutorokea milimani, kwa sababu mabaya yataniwahi na nitakufa

Kutoweza kufika umbali wa kutosha mwa Sodoma pale ambapo Mungu anaangamiza mji unazungumziwa kana kwamba "uhalifu" ni mtu ambaye atamfukuza na kumfikia Lutu. "Familia yangu na mimi hakika tutakufa Mungu atakapoangamiza watu wa Sodoma, kwa sababu milima ipo mbali sana na sisi kufika kule salama"

maisha yangu ... sitaweza kutorokea ... yataniwahi na nitakufa

Inaonyesha ya kwamba familia ya Lutu itakufa pamoja naye. "maisha yetu ... hatuwezi kutoroka ... yataniwahi, na tutakufa"

niacheni nikimbilie pale ( Je Siyo mdogo ule?), na maisha yangu yataokolewa

Lutu alitumia swali hili la balagha kuwafanya malaika kutambua ya kwamba ule mji ni mdogo kweli. "acha nitoroke kule. Unaona jinsi gani ni mdogo. Ukituruhusu kufika pale tutaishi"

niacheni nikimbilie pale

Ombi kamili la Lutu linaweza kuwekwa wazi. "badala ya kuangamiza mji ule, niruhusu nitoroke pale"

maisha yangu yataokolewa

Inaonyesha ya kwamba maisha ya familia ya Lutu yataokolewa pamoja naye. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili kwamba tuweze kuishi" au "ili kwamba tuweze okoka"

Genesis 19:21

nimekubali ombi hili pia

"nitafanya kile ulichokiomba"

sitafanya chochote

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "sitaangamiza miji mingine"

Soari

Watafsiri wanaweza kuongeza maandishi yanayosema "Jina la Soari linafanana na neno la Kiebrania lenye maana ya "ndogo". Lutu aliuita mji huu "mdogo" katika Mwanzo 19:20.

Genesis 19:23

Jua lilikuwa limekwisha chomoza juu ya nchi

"Jua limechomoza juu ya nchi". msemo wa "juu ya nchi" unaweza kuachwa wazi.

Lutu alipofika Soari

Inaonyesha ya kwamba familia ya Lutu ilikuwa pamoja naye. "Lutu na familia yake walipofika Soari"

Yahwe akanyesha juu ya Sodoma na Gomora kiberiti na moto toka kwa Yahwe mbinguni

Msemo wa "kutoka kwa Yahwe" una maana ya nguvu ya Mungu kusababisha kiberiti na moto kuanguka juu ya mji. Yahwe alisababisha kiberiti na moto kuanguka kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora"

kiberiti na moto

Maneno haya yanatumika pamoja kuelezea umbo moja. "kiberiti kiwakacho" au "mvua kali"

miji ile

Kimsingi hii ina maana ya Sodoma na Gomora, lakini pia miji mingine mitatu.

vilivyomo katika miji

"watu waliokuwa wakiishi katika miji ile"

Genesis 19:26

akawa nguzo ya chumvi

"akawa kama sanamu ya chumvi" au "mwili wake ukawa kama jiwe refu la chumvi". Kwa sababu hakutii malaika aliyemwambia asitazame nyuma ya mji, Mungu alimfanya awe kama sanamu iliyotengenezwa na jiwe la chumvi.

tazama

Msemo wa "tazama" hapa unavuta nadhari juu ya taarifa ya kushangaza inayofuata.

kama moshi wa tanuru

Hii inaonyesha ya kwamba ulikuwa ni moshi mkubwa sana. "kama moshi utokao katika moto mkubwa sana"

Genesis 19:29

Taarifa ya Jumla:

Mstari wa 29 ni ufupi wa sura hii.

Mungu akamkumbuka Abrahamu

Hii inasema kwa nini Mungu alimuokoa Lutu. "kukumbuka" ni namna ya kusema "alimkumbuka". Hii haimaanishi Mungu alisahau juu ya Abrahamu. Ina maana alimfikiria Abrahamu na kuwa na huruma juu yake. "Mungu alimfikiria Abrahamu na kuwa na huruma juu yake"

katika maangamizi

"kutoka kwa maangamizi" au "kutoka kwa hatari"

Genesis 19:30

Lutu akapanda juu kutoka Soari na kwenda kuishi katika milima

Msemo "akapanda juu" unatumiwa kwa sababu Lutu alienda sehemu ya juu mlimani.

Genesis 19:31

Yule wa kwanza

"Binti wa kwanza wa Lutu" au "Binti mkubwa"

yule mdogo

"Binti mdogo" au "mdogo wake"

kulingana na desturi ya dunia yote

Hapa "dunia" ina maana ya watu. "kama watu sehemu zote hufanya"

kunywa mvinyo

Hii inaweza kuelezwa kwa uwazi ya kwamba lengo lao lilikuwa kumfanya alewe. "kunywa mvinyo hadi alewe" au "alewe kwa mvinyo".

ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu

Hii inazungumzia kuhusu kumpatia Lutu uzao kana kwamba familia yake ilikuwa na mtiririko mrefu. "ili kwamba tuweze kuzaa watoto ambao watakuwa uzao wa baba yetu"

hakujua ni wakati gani alikuja kulala, wala wakati alipo amka

"hakujua chochote kuhusu hili" au "hakujua ya kwamba alilala pamoja naye"

Genesis 19:34

Na tumnyweshe mvinyo ... wala wakati alipoamka

Hii inaweza kuelezwa kwa uwazi ya kwamba lengo lao lilikuwa kumfanya alewe. "kunywa mvinyo hadi alewe" au "alewe kwa mvinyo".

tumnyweshe mvinyo

Hii inaweza kuelezwa kwa uwazi ya kwamba lengo lao lilikuwa kumfanya alewe. "kunywa mvinyo hadi alewe" au "alewe kwa mvinyo".

Ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu

Hii inazungumzia kuhusu kumpatia Lutu uzao kana kwamba familia yake ilikuwa na mtiririko mrefu. "ili kwamba tuweze kuzaa watoto ambao watakuwa uzao wa baba yetu"

hakujua ni wakati gani alilala, wala wakati alipoamka

"hakujua chochote kuhusu hili" au "hakujua ya kwamba alilala pamoja naye"

Genesis 19:36

wakapata mimba kwa baba yao

"wakawa mimba kupitia baba yao" au "wakapatawatoto kwa baba yao"

Akawa

"Yeye ndiye"

wamoabu hata leo

"Wamoabu ambao wanaishi sasa"

hata leo

Neno "leo" lina maana ya kipindi ambapo mwandishi wa Mwanzo alipokuwa hai. Mwandishi alizaliwa na kuandika haya miaka mingi baada ya familia ya Lutu kuishi na kufa.

Benami

Hili ni jina la mwanamume.

watu wa Waamoni

"uzao wa Amoni" au "Watu wa Amoni"