Genesis 6

Genesis 6:1

Ikawa wakati

Msemo huu unatumika hapa kuonyesha alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.

wana wa kike wakazaliwa kwao

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wanawake wakazaa mabinti"

wana wa Mungu

Haipo wazi kama hii inamaanisha viumbe wa mbinguni au wanadamu. Kwa vyovyote vile, walikuwa viumbe ambao Mungu aliumba. Baadhi wanaamini maneno haya yanamaanisha malaika waliomuasi Mungu, yaani, roho chafu au mapepo. Wengine wanadhani hii inamaanisha watawala wa kisiasa wenye nguvu, na wengine wanadhani hii inamaanisha uzao wa Sethi.

roho yangu

Hapa Yahwe anaongelea kuhusu yeye mwenyewe na roho wake, ambaye ni Roho wa Mungu.

nyama

Hii ina maana wana mwili ambayo itakufa siku moja

Wataishi miaka 120

Maana yaweza kuwa 1) urefu wa kawaida wa watu ingepungua hadi miaka 120. "Hawataishi zaidi ya miaka 120" au 2) katika miaka 120 kila mtu atakufa. "Wataishi miaka 120 tu"

Genesis 6:4

Majitu makubwa

warefu sana, watu wakubwa

Hii ilitokea wakati

"Hawa majitu makubwa walizaliwa kwa sababu"

wana wa Mungu

Haipo wazi kama hii inamaanisha viumbe wa mbinguni au wanadamu. Kwa vyovyote vile, walikuwa viumbe ambao Mungu aliumba. Baadhi wanaamini maneno haya yanamaanisha malaika waliomuasi Mungu, yaani, roho chafu au mapepo. Wengine wanadhani hii inamaanisha watawala wa kisiasa wenye nguvu, na wengine wanadhani hii inamaanisha uzao wa Sethi.

Hawa walikuwa watu hodari zamani

"Majitu makubwa walikuwa wanaume hodari walioishi zamani" au "Hawa watoto wakakua kuja kuwa wapiganaji hodari walioishi zamani"

watu hodari

wanaume ambao ni wajasiri na washindi katika vita

watu wenye sifa

"watu maarufu"

Genesis 6:5

mwinamo

"mwelekeo" au "tabia"

mawazo ya mioyo yao

Mwandishi anazungumzia juu ya moyo kana kwamba ni sehemu ya mwili unaofikiri. "mawazo yao ya ndani ya siri"

ikamuhuzunisha moyo wake

Mwandishi anazungumzia juu ya moyo kana kwamba ni sehemu ya mwili unaoweza kuhisi huzuni. "alikuwa na huzuni sana mno juu ya hili"

Genesis 6:7

Nitamfutilia mbali mwanadamu ... katika uso wa nchi

Mwandishi anamzungumzia Mungu kuua watu kana kwamba Mungu alikuwa akisafisha uchafu katika nchi tambarare. "Nitawaangamiza wanadamu ..ili kwamba kusiwepo na watu katika nchi"

Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba

Baadhi ya lugha hutafsiri hii kama sentensi mbili. "Niliumba mwanadamu. Nitamfutilia mbali"

Nitamfutilia

"kuangamiza kabisa". Hapa "kuangamiza" inatumika katika hali ya hasi, kwa maana Mungu anazungumzia juu ya kuangamiza watu kwa sababu ya dhambi yake.

Nuhu akapata neema ya upendeleo machoni pa Yahwe

"Yahwe alimtazama Nuhu kwa upendeleo" au "Yahwe alifurahishwa na Nuhu"

machoni pa Yahwe

Hapa "machoni" inamaana ya mtazamo au mawazo. "katika mtazamo wa Yahwe" au " katika mawazo ya Yahwe"

Genesis 6:9

Taarifa ya Jumla:

Hii inaanza simulizi ya Nuhu, ambayo inayoendelea mpaka kwenye sura ya 9.

Haya yalikuwa matukio yanayomhusu Nuhu

"Hii ni taarifa ya Nuhu"

alitembea na Mungu

Kutembea na mtu ni sitiari ya kuwa na uhusiano wa karibu na yeye. "Nuhu alikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu" au "Nuhu aliishi kwa umoja na Mungu"

Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume

"Nuhu akawa na wana watatu wa kiume" au "Mke wa Nuhu akawa na wana watatu wa kiume"

Shemu, Hamu, na Yafethi.

"Wana wa kiume hawajaorodheshwa katika mpangilio wa kuzaliwa"

Genesis 6:11

Nchi

Maana yaweza kuwa 1) watu walioishi duniani au 2) "Dunia yenyewe"

iliharibika

Watu waliokuwa wakifanya uovu inazungumziwa kana kwamba walikuwa chakula kilichooza. "ilioza" au "ilikua na ouvu sana"

mbele za Mungu

Maana yaweza kuwa 1) "machoni pa Mungu" au 2) "katika uwepo wa Yahwe" kama 4:16.

na ilijaa ghasia

Mwandishi anazungumzia ghasia kana kwamba ni kitu kinachoweza kuwekwa ndani ya chombo na nchi kama chombo. "na kulikuwa na wanadamu wenye vurugu sana nchini" au "kwa sababu ilikuwa imejaa watu waliofanya mambo maovu baina yao"

tazama

Neno "tazama" hapa linatutahadharisha kuwa msikivu kwa taarifa ya kushtukiza inayofuata.

wote wenye mwili

Maana yaweza kuwa 1) wanadamu wote au 2) viumbe vyote vyenye mwili, ikijumlisha wanadamu na wanyama.

wameharibu njia zao

Namna mtu anavyoishi inazungumzwa kana kwamba ilikuwa njia au barabara. "waliacha kuishi kwa njia ambayo Mungu alitaka" au "waliishi katika njia ya uovu"

Genesis 6:13

wenye mwili

Maana yaweza kuwa 1) wanadamu wote au 2) viumbe vyote vyenye mwili, ikijumlisha wanadamu na wanyama.

inchi imejaa ghasia kutokana na wao

"watu nchini kote wana vurugu"

nitawaangamiza wao pamoja na nchi

"Nitawaangamiza wao pamoja na nchi" au "Nitawaangamiza wao nitakapoiangamiza nchi"

safina

Hii inamaanisha sanduku kubwa sana ambalo lingeweza kuelea juu ya maji hata katika dhoruba mbaya. "mtumbwi mkubwa" au "meli" au "tishali"

mti wa mvinje

Watu hawajui haswa huu ulikuwa mti wa aina gani. "mbao iliyotumika kuunda mitumbwi" au "mbao nzuri"

vifunike kwa lami

"sambaza lami juu yake" au "paka lami juu yake". Sababu ya kufanya hivi yaweza kuwekwa wazi: "kufanya isipitishe maji"

lami

Hiki ni kimiminiko chenye mafuta, kizito, na kinatacho ambacho watu huweka nje ya mtumbwi kuzuia maji kupenya katika nafasi za mbao hadi kwenye mtumbwi.

dhiraa

Dhiraa ilikuwa ni namba ya kipimo, kiasi kidogo tu kwa mita moja.

dhiraa mia tatu

"mita 138". Dhiraa mia tatu ni sawa na mita 138"

dhiraa hamsini

"mita ishirini na tatu"

dhiraa thelathini

"mita kumi na nne"

Genesis 6:16

paa la safina

Inawezekana hii lilikuwa paa lililochongeka au lililolala. Kusudi lake lilikuwa kulinda kila kitu ndani ya safina dhidi ya mvua.

dhiraa

Dhiraa ilikuwa ni namba ya kipimo, kiasi kidogo tu kwa mita moja.

ya chini, ya pili na ya tatu

"dari ya chini, ya katikati, na ya juu" au "dari tatu ndani"

dari

"sakafu" au "daraja"

Sikiliza

Mungu alinena hivi ili kusudi kusisitiza ya kuwa angefanya kile alichotarajia kukifanya. "Sikiliza" au "Sikiliza kile nachosema"

nimekaribia kuleta gharika ya maji

"Nimekaribia kutuma mafuriko ya maji" au "ninakaribia kusababisha mafuriko"

mwili wote

Hapa "mwili" inawakilisha viumbe vyote vya mwili, kujumlisha binadamu na wanyama.

wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai

Hapa "pumzi" inawakilisha uhai. "inayoishi"

Genesis 6:18

nitalifanya thabiti agano langu na wewe

"fanya agano kati yako na mimi"

na wewe

pamoja na Nuhu

Utaingia ndani ya safina

"Utaingia ndani ya safina" Baadhi ya tafsiri husema "Utaingia ndani mwa safina".

Kwa kila kiumbe hai chenye mwili, viwili vya kila aina utavileta ndani ya safina

"Unapaswa kuleta aina mbili ya kila aina ya kiumbe ndani ya safina"

kiumbe

mnyama ambaye Mungu aliumba

chenye mwili

Maana yaweza kuwa 1) wanadamu wote au 2) viumbe vyote vyenye mwili, ikijumlisha wanadamu na wanyama.

Genesis 6:20

kwa jinsi yake

"wa kila aina tofauti"

kitambaacho ardhini

Hii inamaana ya wanyama wadogo ambao hutambaa juu ya ardhi

viwili vya kila aina

Hii inamaana ya ain mbili ya kila aina ya ndege na mnyama.

viwe salama

"ili uweze kuwaweka wawe hai"

kwako ... kwa ajili yako .. chako

Hii inamaana ya Nuhu na ni katika umoja

chakula kinacholiwa

"chakula ambacho watu na wanyama hula"

Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya

Sentensi hizi mbili zinamaanisha jambo moja. Sentensi ya pili inafafanua ya kwanza na kuweka msisitizo ya kwamba Nuhu alimtii Mungu. Sentensi hizi zilizo sambamba zinaweza kuunganishwa kuwa kitu kimoja. "Kwa hiyo Nuhu alifanya kila kitu alichoambiwa na Mungu kufanya"