Sura 1

1 Wimbo ulio Bora, ambao ni wa Sulemani. Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake 2 O, laiti angenibusu na mabasu ya mdomo wake, kwa kuwa upendo wake ni bora kuliko mvinyo. 3 Mafuta yako ya upako yana manukato mazuri; jina lako ni kama marashi yaeleayo, hivyo wanawake wadogo wanakupenda. 4 Nichukuwe kwako, na tutakimbia. Mwanamke akizungumza mwenyewe Mfalme amenipeleka vyumbani mwake. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake; nina furahi kuhusu wewe; acha ni shereheke upendo wako; ni bora kuliko mvinyo. Ni halisi kwa wanawake wengine kupenda. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine. 5 Mimi ni mweusi lakini wa mzuri, enyi mabinti wa wanaume wa Yerusalemu - mweusi kama hema za Kedari, mzuri kama mapazia ya Sulemani. 6 Usinishangae kwasababu ni mweusi, kwasababu jua limeniunguza. Wana wa mama yangu walikuwa na hasira juu yangu; walinifanya mtunzaji wa mashamba ya mizabibu, lakini shamba langu la mizabibu sijalitunza. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake. 7 Niambie, wewe ambaye moyo wangu wakupenda, wapi unalishia mifugo yako? Wapi unapumzisha mifugo yako mchana? Kwa nini niwe kama mtu anaye akangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako? Mpenzi wake anamjibu 8 Kama haujui, uliye mzuri miongoni mwa wanawake, fuata nyayo za mifugo yangu, na ulishe watoto wako wa mbuzi karibu na hema za wachungaji. 9 Nina kulinganisha, mpenzi wangu, na farasi mzuri wakike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao. 10 Mashavu yako ni mazuri kwa mapambo, shingo yako na mikufu ya madini. 11 Nitakufanyia mapambo ya dhahabu yaliochanganywa na fedha. Mwanamke akiongea mwenyewe. 12 Wakati mfalme akiwa amelala kitandani mwake, marashi yangu yakasambaza arufu. 13 Mpenzi wangu kwangu ni kama mkebe wa marashi unaolala usiku kati ya maziwa yangu. 14 Mpenzi wangu kwangu ni kama kifurushi cha maua ya hena katika mashamba ya mizabibu ya Eni Gedi. Mpenzi wake anazungumza naye. 15 Sikiliza, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; ona, wewe ni mzuri; macho yako ni kama ya hua. Mwanamke anazungumza na mpenzi wake. 16 Sikiliza, wewe ni mtanashati, mpenzi wangu, jinsi gani ulivyo mtanashati. 17 Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi, na dari letu ni la matawi ya miberoshi.