Surs 36

1 Kisha wale viongozi wa nyumba za mababu wa ukoo wa Gileadi mwana wa Machiri (ambaye alikuwa mwana wa Manase), ambao walikuwa wa ukoo wa uzao wa Yusufu, walikuja wakasema mbele za Musa na mbele za vionigozi wa familia za mababa wa watu wa Israeli. 2 Wakasema, "BWANA alikuamuru, wewe bwana wetu, kutupa mgao wa ardhi kwa kura kwa wana wa Israeli. Uliamuriwa na BWANA kutoa mgao wa Zerofehadi kaka yetu kwa binti zake. 3 Lakini hawa binti wameolewa na wanaume toka kabila zingine za wana wa Israeli, basi mgao wao wa ardhi utaondolewa kutoka kwenye mgao wa mababu zao. Utaongezwa kwenye mgao wa makabila ambayo wao wanaungana nao. Kwa sababu hiyo, Utaondolewa kwenye mgao uliopangwa kwenye urithi wetu. 4 Kwa sababu hiyo, wakati wa mwaka wa yubilee ya wana wa Israeli utakapofika, mgao wao utaunganishwa na kabila ile waliyoungana nao. Kwa sababu hii mgao wao utaondolewa kwenye mgao wa mababu zetu." 5 Basi Musa akawapa amri wana wa Israeli, kwa neno la BWANA. Akasema, "Kile wanachosema watu wa kabila la Yusufu kiko sahihi. 6 Hiki ndicho BWANA anaagiza kuhusu mabinti wa Zelofehadi. Anasema, 'Acha waolewa na wale ambao wao wanaofikiri ni vizuri zaidi, lakini lazima waolewe ndani ya kabila ya baba yao.' 7 Hakuna mgao wa watu utakaobadilika kutoka kabila moja kwenda jingine. Kila mtu wa Israeli ataendelea na mgao wa kabila ya baba y ake. 8 Kila mwanamke wa watu wa Israeli aliye na mgao kwenye kabila lake lazima aolewe na mtu wa ukoo unaotoka kwenye kabila la baba yake. Hii itafanyika hivyo ili kila mtu wa wana wa Israeli aweze kuwa na urithi kutoka kwa mababu zake. 9 Hakuna mgao utakaobadilika kutoka kabila lingine kwenda kabila lingine. Kila mtu wa kabila za watu wa Israeli atalinda urithi wake." 10 Kwa hivyo wale binti wa Zelofehadi walifanya kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa. Mahila, Tiriza, Hogila, Milika, na Noha, binti za 11 Zelofehadi, waliolewa na wana wa uzao wa Manase. 12 Waliolewa katika koo za uzao wa Manase mwana wa Yusufu. Kwa sababu hii, urithi wao ulibaki kwenye kabila la ukoo ambalo baba yao alikuwa anatoka. 13 Hizi ndizo amri na maagizo ambayo BWANAaliyatoa kupitia Musa kwa wana wa Israeli katika nyanda za Moabu karibu na Yorodani huko Yeriko.