sura 4

1 Tena alianza kufundisha kandokando ya bahari. Na umati mkubwa ulikusanyika ukamzunguka, akaingia ndani ya mtumbwi baharini, na kuketi ndani ya mtumbwi. Umati wote walikuwa pembeni mwa bahari ufukweni. 2 Na akawafundisha mambo mengi kwa mifano, na akasema kwao mafundisho yake. 3 Sikilizeni, mpanzi alienda kupanda. 4 Alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zilianguka njiani, na ndege wakaja wakazila. 5 Mbegu zingine zilianguka kwenye mwamba, ambako hapakuwa na udongo mwingi. Mara zikanyauka, kwa sababu hazikuwa na udongo wakutosha. 6 Lakini jua lilipochomoza, zilinyauka, kwa sababu hazikuwa na mzizi, zilikauka. 7 Mbegu ziingine zilianguka katikati ya miiba. Miiba ilikua na ikazisokota, na hazikuzaa matunda yeyote. 8 Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na zikazaa matunda wakati zikikua na kuongezeka, zingine zilizaa mara thelathini zaidi, na zingine sitini, na zingine mia". 9 Na akasema, "Yeyote mwenye masikio ya kusikia, na asikie!" 10 Yesu alipokuwa na, wale waliokuwa karibu naye na wale kumi na wawili walimuuliza kuhusu mifano. 11 Akasema nao, "Kwenu ninyi Mungu amewapa siri za ufalme. Lakini kwa ambao hawapo miongoni mwenu kila kitu ni kwa mifano, 12 ili wakitazama, ndiyo hutazama, lakini wasione, na wanaposikia ndiyo husikia, lakini wasielewe, nisemayo wasije wakageuka na kuacha dhambi Mungu akawasamehe." 13 Yesu akasema na wanafunzi wake, "Je hamuelewi mfano huu? Mtawezaje kuelewa mifano mingine?. 14 Mpanzi alipanda neno. 15 Baadhi ni watu walioanguka pembeni mwa njia, mahali neno lilipopandwa. Na walipolisikia, mara Shetani akaja na kulichukua neno ambalo lilipandwa ndani yao. 16 Na baadhi ni watu waliopandwa juu ya mwamba, ambao, wanapolisikia neno, kwa msisimko wanalipokea kwa furaha. 17 Hawana mizizi yoyote ndani yao, lakini huamini kwa muda mfupi. Halafu tabu na mahangaiko vinapokuja kwa sababu ya neno, mara huacha imani. 18 Na wengine ni wale waliopandwa katika miiba. Wanalisikia neno, 19 lakini masumbufu ya dunia, tamaa za mali, na tamaa za mambo mengine, huwaingia na kulisonga neno, na linashindwa kuzaa matunda. 20 Kisha kuna wale ambao wamepandwa kwenye udongo mzuri. Wanalisikia neno na kulipokea na huzaa matunda: baadhi ya watu thelathini, na baadhi ya watu sitini, na baadhi ya watu mia moja." 21 Yesu akawaambia, " Je huwa unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu, au chini ya kitanda? Huileta ndani na kuiweka juu ya kiango. 22 Kwa kuwa hakuna chochote kilichojificha ambacho hakitajulikana, na hakuna siri ambayo haitawekwa wazi. 23 Akiwapo mwenye masikio ya kusikia, na asikie!" 24 Akawaambia, " Iweni makini kwa kile mnachokisikia, kwa kuwa kipimo mpimacho, ndicho mtakachopimiwa, na kitaongezwa kwenu. 25 Kwa sababu yeye aliyenacho, atapokea zaidi, na yule asiyenacho, kwake vitachukuliwa hata vile alivyonavyo." 26 Akasema, "Ufalme wa Mungu umefananishwa na mtu aliyepanda mbegu katika udongo. 27 Alipolala usiku na kuamka asubuhi, na kukuta zimechipuka na kukua, ingawa hajui zilivyo chipuka. 28 Aridhi hutoa mbegu yenyewe; kwanza majani, halafu maua, halafu mbegu zilizo komaa. 29 Na wakati mbegu itakapo komaa mara hupeleka watu wenye mundu kuvuna, kwa sababu nafaka iko tayari kuvunwa." 30 Akasema, "nitumie mfano gani kuufananisha ufalme wa Mungu na nikitu gani, au tutumie mfano gani kuuelezea?. 31 Ni kama mbegu ya haradali, ambayo ilipopandwa ni ndogo sana kuliko mbegu zote duniani. 32 Hata, wakati imepandwa, inakuwa kubwa zaidi ya mimea yote ya bustani, na inafanya matawi makubwa, hata ndege wa angani huweza kufanya viota vyao kwenye kivuli chake." 33 Kwa mifano mingi yesu alifundisha na alisema maneno kwao, kwa kiasi walivyoweza kuelewa, 34 Na hakusema nao bila mifano. Lakini wakati alipokuwa peke yake, yao akawaelewesha kila kitu wanafunzi wake. 35 Katika siku hiyo, wakati wa jioni ulipotimia, akasema nao wanafunzi wake, "Twendeni upande wa pili wa bahari". 36 Hivyo wakauacha umati wa watu, wakamchukua Yesu, wakati huo tayari alikuwa ndani ya mtumbwi. Mitumbwi mingine ilikuwa pamoja naye. 37 Na upepo mkali wa dhoruba na mawimbi ya maji yalikuwa yakiingia ndani ya mtumbwi na mtumbwi ulianza kujaa maji. 38 Lakini Yesu mwenyewe alikuwa kwenye shetri, yani kwenye sakafu ya chini kwenye mashua amelala. Wakamwamsha, wakisema, "Mwalimu, unapaswa kuwa makini sisi tunakufa?" 39 Akaamka, akaukemea upepo na bahari, "'Ikawa shwari, na salama". Upepo ukakoma, na kukawa na utulivu mkubwa. 40 Akasema nao, "Kwa nini mnaogopa? Je hamna imani bado?" hampaswi kuogopa 41 Walijawa na hofu kubwa ndani yao na wakasemezana wao kwa wao, " Huyu ni nani hata upepo na bahari vya mtii?".