1
Baada ya hayo, Ayubu alianza kusema na kuilani siku aliyozaliwa.
2
Akasema,
3
"Na ipotelee mbali siku niliyozaliwa mimi, usiku uliosema, 'Mimba ya mtoto wa kiume imetungwa.'
4
Siku hiyo na iwe giza; Mungu toka juu asiifikilie, wala mwanga usiiangazie.
5
Ishikwe na giza na giza la mauti liwe lake. Wingu na likae juu yake; kila kitu kiifanyacho siku kuwa giza kweli na kiitishe.
6
Usiku huo, na ukamatwe na giza tororo. Usihesabiwe miongoni mwa siku za mwaka; na usiwekwe katika hesabu ya miezi.
7
Tazama, usiku huo na uwe tasa; na sauti ya shangwe isiwe ndani yake.
8
Na wailani siku hiyo, hao wafahamuo namna ya kumuamsha lewiathani.
9
Nyota za mapambazuko yake zitiwe giza. Siku hiyo iutafute mwanga, lakini isiupate; wala makope ya mapambazuko isiyaone,
10
kwasababu haikuifunga milango ya tumbo la mama yangu, na kwasababu haikunifichia taabu machoni pangu.
11
Kwanini si-kufa wakati lipotokeza katika tumbo la uzazi? Kwanini sikuitoa roho yangu hapo mama aliponizaa?
12
kwanini magoti yake yalinipokea? Kwanini maziwa yake yanipokee hata ninyonye?
13
Kwa sasa ningelikuwa nimelala chini kimya kimya. Ningelala usingizi na kupata pumziko
14
pamoja na wafalme na washauri wa dunia, ambao walijijengea makaburi ambayo sasa ni magofu.
15
Au Ningelikuwa nimelala pamoja na wakuu wenye dhahabu, waliozijaza nyumba zao fedha.
16
Au pengine ningekuwa sijazaliwa, kama watoto wachanga wasio uona mwanga kabisa.
17
Huko waovu huacha kusumbua; huko waliochoka hupumzika.
18
Huko wafungwa kwa pamoja hupata amani; hawaisikii sauti ya msimamizi wa watumwa.
19
Wote wadogo na watu maarufu wako huko; mtumishi yuko huru kwa bwana wake huko.
20
Kwa nini yeye aliye mashakani kupewa mwanga? Kwa nini hao wenye uchungu moyoni kupewa uhai,
21
ambao hutamani mauti lakini hawapati; ambao huyachimbulia mauti zaidi ya kutafuta hazina iliyofichika?
22
Kwa nini kupewa mwanga ambao hushangilia mno na kufurahi walionapo kaburi?
23
Kwanini kupewa mwanga mtu ambaye njia zake zimefichika, mtu ambaye Mungu amemzungushia ukingo?
24
Kwa kuwa kushusha kwangu pumzi kwatokea badala ya kula; kuugua kwangu kumemiminika kama maji.
25
Maana jambo lile niliogopalo limenipata; nalo linitialo hofu limenijilia.
26
Mimi sioni raha, sipati utulivu, na sipati pumziko; badala yake huja taabu."