Sura 19

1 Ikawa kwamba Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akapita nyanda za juu na kufika katika mji wa Efeso, na akakuta wanafunzi fulani huko. 2 Paulo akawaambia, "Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?" Wakamwambia, "Hapana, hatukuweza hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu." 3 Paul alisema, "Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani?" Wakasema, "Katika ubatizo wa Yohana. 4 Basi Paulo akajibu, "Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba. Akawaambia wale watu kwamba wanapaswa kumwamini yule ambaye angekuja baada yake, yaani, Yesu." 5 Watu waliposikia habari hii, wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6 Na ikawa Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao na wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri. 7 Jumla yao walikuwa wanaume wapatao kumi na wawili. 8 Paulo alienda katika sinagogi akanena kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu. Alikuwa akiongoza majadiliano na kuwashawishi watu kuhusu mambo yanayohusu ufalme wa Mungu. 9 Lakini Wayahudi wengine walikuwa wakaidi na wasiotii, walianza kusema mabaya kuhusu njia ya Kristo mbele ya umati. Basi Paulo aliachana nao na akawatenga waaminio mbali nao. Naye alianza kuongea na wao kila siku katika ukumbi wa Tirano. 10 Hii iliendelea kwa miaka miwili, kwa hiyo wote waliokuwa wanaishi katika Asia walisikia neno la Bwana, wote Wayahudi na Wayunani. 11 Mungu alikuwa akifanya matendo makuu kwa mikono ya Paulo, 12 kwamba hata wagonjwa waliponywa, na roho chafu waliwatoka, wakati walipochukua leso na nguo zilizotoka mwilini mwa Paulo. 13 Lakini palikuwapo Wayahudi wapunga pepo wakisafiri kupitia eneo hilo, waliliita jina la Yesu ili wawenza kuwa na nguvu juu ya pepo wabaya Waliposema, "Ninawaamuru mtoke kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri." 14 Waliofanya haya walikuwa wana saba wa kuhani Mkuu wa Kiyahudi, Skewa. 15 Roho wachafu wakawajibu, "Yesu namjua, na Paulo namjua; lakini ninyi ni nani? " 16 Yule roho mchafu ndani ya mtu akawarukia wapunga pepo na akawashinda nguvu na kuwapiga. Ndipo wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na kujeruhiwa. 17 Jambo hili likajulikana kwa wote, Wayahudi na Wayunani, ambao waliishi huko Efeso. Wakawa na hofu sana, na jina la Bwana likazidi kuheshimiwa. 18 Pia, wengi wa waumini walikuja na wakaungama na wakidhihirisha matendo mabaya waliyoyafanya. 19 Wengi waliokuwa wakifanya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya kila mtu. Wakati wao walipohesabu thamani ya vitu hivyo, ilikuwa vipande hamsini elfu vya fedha. 20 Hivyo Neno la Bwana likaenea kwa upana sana katika nguvu. 21 Sasa mambo haya yalipokwisha kukamilika, Paulo aliamua katika Roho kupitia Makedonia na Akaya akielekea Yerusalemu; Akasema, "Baada ya kuwako huko, yanipasa kuiona Rumi pia." 22 Paul akawatuma Makedonia wanafunzi wake wawili ambao walimtumikia, Timotheo na Erastu. Lakini yeye mwenyewe akabaki Asia kwa muda. 23 Wakati huo kulitokea ghasia kubwa huko Efeso kuhusu ile Njia. 24 Sonara mmoja jina lake Demetrio, ambaye aliyetengeneza visanamu vya fedha vya mungu Diana, alileta biashara kubwa kwa mafundi. 25 Hivyo akawakusanya mafundi wa kazi hiyo na kusema, "Waheshimiwa, mnajua kwamba katika biashara hii sisi tunaingiza pesa nyingi. 26 Mnaona na kusikia kwamba, si tu hapa Efeso, bali karibia Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuwageuza watu wengi. Anasema kwamba miungu iliyofanywa kwa mikono si miungu. 27 Na sio tu iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa haihitajiki tena, lakini pia na hekalu la mungu mke aliye mkuu Diana anaweza kuchukuliwa kuwa hana maana. Tena angeweza hata kupoteza ukuu wake, yeye ambaye Asia na dunia humwabudu." 28 Waliposikia haya, walijawa na hasira na wakapiga kelele, wakisema, "Diana wa Waefeso ni mkuu." 29 Mji wote ukajaa mkanganyiko, na watu wakakimbia pamoja ndani ya ukumbi wa michezo. wakawakamata wasafiri wenzake na Paulo, Gayo na Aristariko, waliotoka Makedonia. 30 Paulo alitaka kuingia katika umati wa watu, lakini wanafunzi walimzuia. 31 Pia, baadhi ya maafisa wa mkoa wa Asia ambao walikuwa marafiki zake wakampelekea ujumbe kwa nguvu kumwomba asiingie katika ukumbi wa michezo. 32 Baadhi ya watu walikuwa wakipiga kelele jambo moja na wengine lingine, kwa sababu umati wa watu ulikuwa umechanganyikiwa. Wengi wao hawakuweza hata kujua kwa nini walikuja pamoja. 33 Baadhi ya umati walimshauri Iskanda, ambao Wayahudi walikuwa wanasukuma mbele. Basi Iskanda akatoa ishara kwa mkono wake kutaka kutoa utetezi kwa kusanyiko. 34 Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili, wakisema "Diana ni mkuu wa Wafeso." 35 Baada ya karani wa mji kuunyamazisha umati, alisema, 'Enyi wanaume wa Efeso, ni nani asiyejua kwamba mji huu wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu la Diana mkuu na ile picha iliyoanguka kutoka mbinguni? 36 Kuona Basi kwamba mambo haya haiwezekani kuyakana, mnapaswa kuwa kimya na kufanya chochote haraka. 37 Kwa maana mmewaita watu hawa hapa mahakamani ambao si wezi wa hekalu wala si wenye kumkufuru mungu wetu mke. 38 Kwa hiyo, kama Demetrio na mafundi waliopamoja naye wana mashtaka dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na maliwali wapo. Na waletwe mbele ya shauri. 39 Lakini kama wewe ukitafuta chochote kuhusu mambo mengine, yatashughurikiwa katika kikao halali. 40 Kwa kweli tuko katika hatari ya kutuhumiwa kuhusu ghasia siku hii. Hakuna sababu ya machafuko haya, na hatutakuwa na uwezo wa kuyaeleza. 41 Baada ya kusema haya, aliwatawanya makutano.