2 Mambo Ya Nyakati Sura 8

1 Ikawa karibu ya mwisho wa miaka ishirini, kipindi ambacho Sulemani alikuwa ameijenga nyumba ya Yahwe na ya kwake mwenye, 2 kwamba Sulemani akaiajenga miji ambayo Hiramu alikuwa amempa, na ndani yake akawaweka watu wa Israeli. 3 Sulemani akauavamia Hamathzoba, akaushinda. 4 Akaijenga Tadmori katika nyika, na miji yote ya hazina, ambayo aliijenga katika Hamathi. 5 Pia akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji iliyozungushiwa kwa ukuta, malango, na makomeo. 6 Akaujenga Baalathi na miji yote ya hazina aliyoimiliki, na miji yote kwa ajili ya magari yake na miji kwa ajili ya wapanda farasi wake, na chochote alichotamani kujenga kwa ajili ya starehe zake katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika nchi zote zilizokuwa chini ya utawala wake. 7 Kuhusu watu wengine wote ambao walikuwa wamesalia wa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, Wayebusi, ambao hawakuwa wa Israeli, 8 watoto wao ambao waliachwa baada yao katika nchi, ambao watu wa Israeli hawakuwaangamiza—Sulemani akawafanyisha kazi kwa nguvu, ndivyo walivyo hata leo. 9 Vile vile, Sulemani hakuwafanyisha kazi kwa nguvu watu wa Israeli. Badala yake, wakawa wanajeshi wake, maakida wake, wakuu wake, na maakida wa magari ya majeshi yake na wapanda farasi wake. 10 Pia hawa walikuwa wakuu wa wakuu wakisimamia wasimamizi waliokuwa wa mfalme Sulemani, walikuwa 250, waliowasimamia watu walioifanya kazi. 11 Sulemani akamleta binti Farao nje ya mji wa Daudi kwenye nyumba aaliyokuwa amemjengea, kwa maana alisema, "Mke wangu lazima asiishi katika nyumba ya Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu kila linapokuja sanduku la Yahwe ni pakatifu". 12 Kisha Sulemani akatoa sadaka za kuteketezwa kwa Yahwe juu ya madhabahu yake ambayo alikuwa ametengeza mbele ya ukumbi. 13 Akatoa sadaka kama ilivyohitaka ratiba ya kila siku; akazitoa, kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa katika amri ya Musa, katika siku za Sabato, miezi mipya, na katika siku zilizopangwa mara tatu kila mwaka: Sikukuu ya mikate isiyochachwa, sikukuu ya majuma, na sikuku ya vibanda. 14 Katika kuyatunza maagizo ya baba yake Daudi, Sulemani akayapanga makundi ya makuhani kwenye kazi yao, na Walawi kwenye nafasi zao, ili kumsifu Mungu na kuhudumu mbele za makuhani, kama ilivyotakiwa katika ratiba ya kila siku. Pia akawateua walinda lango kwa zamu zao kwa kila lango, kwa maana Daudi, mtu wa Mungu, alikuwa ameagiza hivyo pia. 15 Watu hawa hawakupotea kutoka kwenye amri ya mfalme kwa makuhani na Walawi kuhusu jambo lolote, au kuhusu vyumba vya hazina. 16 Kazi yote aliyoagizwa na Sulemani ikakamilika, kutoka siku ya msingi wa nyumba ya Yahwe ulipowekwa hadi ilipokamilika. Nyumba ya Yahwe ikamalizika. 17 18 Kisha Sulemani akaenda Esion geberi, na Elothi, juu ya pwani katika nchi ya Edomu. Hiramu akatuma meli zake kupitia watumishi wake ambao walikuwa wana maji wenye uzoefu. Wakasafiri na watumishi wa Sulemani hadi Ofiri. Wakachukua kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambazo walimletea Sulemani.