2 Mambo Ya Nyakati
Sura 34
1
Yosia alikuwa na umri wa miaka nane alipoanza kutawala; alitawala miaka thelathini na moja katika Yerusalemu.
2
Alifanya yaliyohaki katika macho ya Yahwe, na alitembea katika njia za Daudi babu yake, na hakugeuka mbali iwe kulia au kushoto.
3
Kwa maana ndani ya miaka minane ya ya utawala wake, alipokuwa bado kijana, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi, babu yake. Katika miaka ishirini, alianza kuisafisha Yuda na Yerusalemu kutoka sehemu za juu, vituo vya Maashera, na sanamu za kuchonga na sanamu za chuma ya kuyeyushwa.
4
Watu wakazivunja madhabahu za Baali katika uwepo wake; akazibomoa nguzo za Maashera na na zile sanamu za kuchonga, na sanamu za chuma ya kuyeyushwa katika vipande hadi zikawa mavumbi. Akayasambaza mavumbi juu ya makaburi ya wale ambao walizitolea sadaka.
5
Akaichoma mifupa ya makuhani wao juu ya madhabahu zao. Katika namna hii, akaisafisha Yuda na Yerusalemu.
6
Alifanya hivyo hivyo katika miji ya Manase, Efraimu, na Simeoni, sehemu zote hadi Neftali, na katika maeneo yaliyoizunguka.
7
Alizivunja madhabahu, akayapiga Maashera, na sanamu za kuchonga kuwa unga, na kuzisambaratisha madhabahu zote za uvumba katika nchi yote ya Israeli; kisha akarudi Yerusalemu.
8
Sasa katika kipindi cha miaka ishirini ya utawala wake, baada ya Yosia kuisafisha nchi na hekalu, alimtuma Shafani mwana wa Azali, Manaseya, akida wa mji, na Yoa mwana wa Yoahazi katibu, kuikarabati nyumba ya Yahwe Mungu wake.
9
Wakaenda kwa Hilkia, kuhani mkuu, na wakakabidhi kwake fedha ambazo zilikuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Mungu, ambazo Walawi, walinzi wa milingo, walikuwa wamekusanya kutoka Manase na Efraimu, kutoka kwa masalia wote wa Israeli, kutoka Yuda yote na Benyamini, na kutoka kwa wakaaji wa Yerusalemu.
10
Wakaikabidhi zile fedha kwa watu waliosimamia kazi ya hekalu ya Yahwe. Watu wale wakawalipa watendakazi walioikarabati na kulijenga tena hekalu.
11
Wakawalipa maseremala na wajenzi kwa ajili ya kununua mawe ya kuchonga na mbao kwa ajili ya kuungia, na kutengeneza boriti za nyumba ambazo baadhi ya wafalme wa Yuda waliziacha zikachakaa.
12
Watu waliifanya kazi kwa uaminifu. Wasimamizi wao Yahathi na Obadia, Walawi, wa wana wa Merari; na Zekaria na Meshulamu, kutoka kwa wana wa Wakohathi. Walawi wengine, wote kati ya wale waliokuwa wanamziki wazuri sana, kwa ukaribu waliwaelekeza watendakazi.
13
Walawi hawa walikuwa viongozi wa wale waliobeba vifaa vya ujenzi na watu wengine wote waliofanya kazi kwa namna yoyote ile. Pia palikuwa na Walawi ambao walikuwa makatibu, watawala na walinda lango.
14
Walipozileta fedha ambazo zilikuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe, Hilkia yule kuhani alikipata kitabu cha sheria ya Yahwe ambacho kilikuwa kimetolewa kupitia Musa.
15
Hilkia akamwambia Shafani yule mwandishi, "Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe". Hilikia akakileta kitabu kwa Shefani.
16
Shefani akakipeleka kitabu kwa mfalme, na pia akatoa taarifa kwake, akisema, "Watumishi wako wanafanya kila kitu walichokabidhiwa.
17
Walizitoa fedha zote ambazo zilipatikana katika nyumba ya Yahwe, na walizikabidhi katika mikono ya wasimamizi na watendakazi."
18
Shefani mwandishi akamwambia mfalme." Hilkia kuhani amenipa kitabu." Kisha Shefani akamsomea mfalme katika hicho kitabu.
19
Ikawa kwamba mfalme alipokuwa ameyasikia maneno ya sheria, aliyararua mavazi yake.
20
Mfalme akamwamuru Hilkia, Ahikamu mwana wa Shafani, Abdoni mwana wa Mika, Shafani mwaandishi, na Asaya, mtumishi wake, akisema,
21
"Nendeni mkaulize mapenzi ya Yahwe kwa ajili yangu, na kwa wale waliobaki katika Israeli na Yuda, kwa sababu ya maneno ya kitabu ambacho kimeokotwa. Kwa maana ni kuu, ghadhabu zake Yahwe zilizomiminwa juu yetu. Kwa kuwa ni kuu, kwa sababu babu zetu hawakuyasikiliza maneno ya kitabu hiki ili kuyatii yote yaliyokuwa yameandikwa ndani yake". (Badala ya "ambayo yamemiminwa juu yetu", baadhi ya matoleo yanasema " ambayo yamemulikwa dhidi yetu").
22
Kwa hiyo Hilkia, na wale ambao mfalme alikuwa amewaamuru, wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tohathi mwana wa Hasra, mtunza mavazi (aliishi katika Yerusalemu katika wilaya ya pili), na walizungumza naye katika namna hii.
23
Akasema kwao, "Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema: Mwambie mtu aliyewatuma kwangu,
24
Hivi ndivyo Yahwe anasema: Ona, niko karibu kuleta maafa juu ya sehemu hii na wakaaaji wake, laana zote zilizoandikwa katika kitabu walichokisoma mbele ya mfalme wa Yuda.
25
Kwa sababu wamenisahau na wametoa sadaka za uvumba kwa miungu mingine, ili kwamba waniweke katika hasira kwa matendo yote waliyofanya -- kwa hiyo hasira yangu itamiminwa juu ya hii sehemu, na haitazimwa. (Badala ya "ambayo yamemiminwa juu yetu", baadhi ya matoleo yana "amabyo yamemlikwa dhidi yetu".)
26
Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliyewatuma kumuuliza Yahwe alichopaswa kufanya, hivi ndivyo mtakavyosema kwake, 'Yahwe, Mungu wa Israeli anasema hivi: Kuhusu maneno uliyosikia,
27
kwa sababu moyo wako ulimbondeka, na ulijinyenyekeza mbele za Mungu ulipoyasikia maneno yake dhidi ya sehemu hii na wakaaji wake, na kwa sababu umejinyenyekeza mwenyewe mbele zangu, na umeyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nami pia nimekusikiliza —hili ni azimio la Yahwe—
28
ona, nitakukusanya kwa mababu zako. Utakusanywa katika kaburi lako kwa amani, na macho yako hayataona maafa yoyote nitakayoleta juu ya sehemu hii na wakaaji wake". Wale watu wakarudisha ujumbe huu kwa mfalme.
29
Mfalme akatuma wajumbe na kuwakusanya wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.
30
Kisha mfalme akaenda kwenye nyumba ya Yahwe, na watu wote wa Yuda wakaaji wa Yerusalemu, na makuhani, Walawi, na watu wote, kuanzia wakubwa hadi wadogo. Kisha akasoma mbele zao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichokuwa kimepatikana katika nyumba ya Yahwe.
31
Mfalme akasimama katika sehemu yake na kufanya agano mbele za Yahwe, kutembea mbele za Yahwe, na kuzishika amri zake, taratibu zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na roho yake yote, kuyatii maneno ya agano yaliyokuwa yameandikwa katika kitabu hiki.
32
Aliwasababisha wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini kusimama kwa agano. Wakaaji wa Yerusalemu wakatembea kwa agano la Mungu, Mungu wa babu zao.
33
Yosia akapeleka mbali mambo yote ya machukizo kutoka kwenye nchi iliyomilikiwi na watu wa Israeli. Akamfanya kila mtu katika Israeli amwabudu Yahwe, Mungu wao. Kwa maisha ya siku zake zote, hawakugeuka mbali kwa kutomfuata Yahwe, Mungu wa mababu zao.