1
Ahabu akamwambia Yezebeli mambo yote ambayo Eliya amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga.
2
Ndipo Yezebeli alipotuma mjumbe kwa Eliya, akisema, "miungu wanifanye hivyo na mimi, na zaidi yake, kama kesho muda kama huu sitayafanya maisha yako kuwa kama mmoja wa hao manabii waliokufa."
3
Eliya aliposikia hayo, akaiinuka na akakimbia kwa ajili ya kuokoa maisha yake akaja mpaka Beerisheba, ambao ni mji wa Yuda, na akamwacha mtumishi wake huko.
4
Lakini yeye mwenyewe akaenda mwendo wa siku moja huko jangwani, akaja akakaa chini ya mti wa mretemu. Akajiombea mwenyewe kufa, akasema, "Sasa yatosha, BWANA, ichukue roho yangu, kwa kuwa mimi si mzuri kuliko mababu zangu waliokufa."
5
Kwa hiyo akalala chini ya mretemu. Ghafula malaika akamgusa na akamwambia, "Inuka ule."
6
Eliya akatazama, karibu na kichwa chake kulikuwa na mkate uliokuwa umeokwa kwa mkaa na gudulia la maji. Kwa hiyo akala na kunywa na kulala tena.
7
Malaika wa BWANA akaja tena mara ya pili akamgusa na kumwambia, "Inuka ule, kwa sababu safari bado ndefu kwako."
8
Kwa hiyo akainuka na kula na kunywa, naye akasafiri kwa nguvu ya chakula hicho kwa siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
9
Akaingia kwenye pango akakaa humo. Kisha neno la BWANA likamjia likimwambia, "Unafanya nini hapa, Eliya?"
10
Eliya akajibu, "Nimeona wivu mwingi kwa BWANA, Mungu wa majeshi, kwa kuwa watu wa Israeli wameliacha agano lako, wameziharibu madhabahu zako, na wamewaua manabii wako kwa upanga. Sasa ni mimi, pekee yangu, nimebaki na wanataka kuichukua roho yangu.
11
BWANA akamwambia, "Nenda nje ukasimame kwenye mlima mbele yangu." Kisha BWANA akapita, na upepo mkali ukaupiga mlima ukavunja miamba katika vipande vipande mbele ya BWANA, lakini BWANA hakuwemo kwenye huo mlima. Kisha baada ya upepo, tetemeko likaja, lakini BWANA hakuwemo kwenye hilo tetemeko.
12
Kisha baada ya tetemeko, moto ukaja, lakini BWANA hakuwemo kwenye moto. Ndipo baada ya moto, sauti ya upole ikaja.
13
Naye Eliya alipoisikia sauti, akafunika uso wake kwa vazi lake, akatoka nje, akasimama kwenye lango la hilo pango. Na sauti ikaja kwake ikisema, "unafanya nini hapa?,
14
Eliya akajibu, "nimeona wivu sana kwa ajili ya BWANA, Mungu wa majeshi, kwa kuwa watu wa Israeli wameliacha agano lako, wamezihariibu madhabahu zako, na wamewaua manabii kwa upanga. Sasa, ni mimi pekee yangu, nimebaki na wanajaribu kuichukua roho yangu."
15
Kisha BWANA akamwambia, "Nenda, rudi kwa njia yako kwenye jangwa la Dameski, na utakapofika utamtia mafuta Hazaeli awe Mfalme wa Shamu,
16
na utamtia mafuta Yehu mwana wa Nimshi kuwa mfalme wa Israeli, na utamtia mafuta Elisha mwana wa Shafeti wa Abeli Mehola kuwa nabii mahali pako.
17
Itakuwa hivi Yehu atamwua kila mmoja atakayejaribu kutoroka upanga wa Hazaeli, na kwamba Elisha atamwua kila atakayejaribu kukwepa upanga wa Yehu.
18
Lakini nitawaacha watu elfu saba katika Israeli kwa ajili yangu, ambao magoti yao hayajawahi kupigwa kwa Baali, na ambao midomo yao haijambusu."
19
Kwa hiyo Eliya akaondoka mahali pale na akamkuta Elisha mwana wa Shafati, akilima na jozi za makisai kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe alikuwa akilima na ile jozi ya kumi na mbili. Eliya akaenda mpaka kwa Elisha akamtupia vazi lake juu yake.
20
Elisha naye akawaacha wale makisai akamkimbilia Eliya; akamwambia, "Tafadhali naomba nikambusu baba yangu na mama yangu kisha nitakufuata." Naye Eliya akamwambia, "Rudi, lakini fikiria juu ya kile nilichokufanyia."
21
Kwa hiyo Elisha akarudi toka kwa Eliya na akachukua ile jozi ya makisai, akawaua wale wanyama, na akapika ile nyama kwa kuni za ile nira. Kisha akawapa watu wakala. Kisha akaamka, akamfuata Eliya akamtumikia.