Sura 1

1 Kile tulichokiona tangu mwanzo, kile tulichokisikia, kile tulichokiona kwa macho yetu, kile tulichokitazama, na mikono yetu imekishika kuhusu Neno la uzima. 2 Na ule uzima ulifanywa kujulikana wazi na tumeuona, na kuushuhudia, na kuwatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwako kwa Baba na ulifanywa kujulikana kwetu. 3 Kile tulichokiona na kukisikia twakitangaza kwenu pia, ili kwamba muweze kujumuika pamoja nasi, na ushirika wetu pamoja na Baba na Mwanae Yesu Kristo. 4 Na tunawaandikia mambo haya ninyi ili kwamba furaha yetu iwe timilifu. 5 Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake na kuwatangazia ya kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hakuna giza hata kidogo. 6 Kama tukisema kwamba tunaushirika naye na twatembea gizani, twadanganya na hatutendi kweli. 7 Lakini tukitembea katika nuru kama alivyo yeye nuruni, Twashirikiana sisi kwa sisi, na damu ya Yesu Kristo, mwanae yatutaka kutoka dhambini. 8 Kama tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, na kweli haimo ndani yetu. 9 Lakini tukizitubu dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote. 10 Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, twamfanya yeye kuwa muongo, na neno lake halimo ndani yetu.