sura 6

1 Kutenda kasi pamoja pamoja tusii nde mpanganya mwajijopa neema jaka Sapanga bila matokeu gache. 2 kuba jupwaga wakati gogukubalike nakabi makine kwinu ni lisoba luwokovu . 3 Kasetubeka ilibo lu kuzuoia palonji jaka mundu jokape kwa kuba lasetujipai huduma jito ajileta klatika sipa mbija . 4 Badala jachi tujihakike twabete kwa matendu gitu goti , kwamba twatumishi baka Sapanga . twetwatumishi bachi kuwinji gutahimilipo , matesu , zike ugumu gwa maisha . 5 Kulapua , ipungu gasia kupete kutenda kasi kwa bidie kukukosa lugonu ichilo , na katika inzara . 6 katika usapi, maaripa , kuvumilia , wema , katika roho untaktifu , katika upendu halise. 7 Twatumishe bachi katika linenu la kweli katika machili gaka Sapanga . Tubi na silaha ya hake kwa ajile jukuboku kwasanalomi na guku shoto. 8 Tuhenga kasi katika heshima nu kuzalauliwa , kupete kashifa na sipa . Atutuhumu kuba twadanganyifo na wakati twe twakwele . 9 Tuhenga kasi kana kwamba ngasetumanyika na twakona twakamanyikana sapi. Tuhenga kasi kama bandu ba kuha nu undinga twakona twaka ishe . thenga kasikama babalimanga lakine si kama babahukamwile hadi kuwa. Tuhenga kasi kama twetubi na masikitiku , lakine masoba goti tutenda kuhekalea . 10 Tuhenga kasi kama masikine lakine twatajilisha binje . Tuhenga kasi kama kasetupata sindo lakine kama ba amilike kila sindo 11 Tulonji ukweli gwoti kwinu , Wokorinto , na mioju jitu jihogwichi ku upana . 12 Mioju jino kasejizuiliwa na twenga , bale uzuiliwi na hisia hinu mwabete . 13 Enu katika kubadilisha kwa hache nonjea kama kwa bana uhogula mioju jino kuupana . 14 Mwikongana na banga kuamine . kwa kuba gubi uhusianu bole kati ja hake nu uhase? nu gubi ushirika bole kati ja nuro na lwihe ? 15 Makubalianu bole kristu juhoto kuba naku nu Beliari? au jojuhamini jubi na sehemu bole na jwanga kuamine ? 16 Na gabi makubalianu bole kati jilihekalu laka Sapanga ni sanamo? kwakuba twetwilihekalu laka Sapanga jwapwaga " nitama kati jabu nukujenda kati jabu nikuba Sapanga jwabu na bombi bi biha bandu bango . 17 Kwahiyo umboka katikati jabu nabukijitenga nabombi " jupwaga Bambo ." mwakigusa sindu kisapu na karibia umbanganya . 18 Nikuba natati kwinu numbanganya mwibia mwabanango mwakanalomi na mwaka mbomba " , jupwaga Bambu mwene.