Genesis 29

Genesis 29:4

Wanamume ambao Yakobo alizungumza nao walitoka wapi?

Wanamume walitoka Harani.

Ni nani pia aliyekuja na kundi la kondoo kisimani?

Raheli, binti wa Labani, pia alikuja kisimani pamoja na kundi la kondoo.

Genesis 29:9

Yakobo alifanya nini na kondoo wa Labani?

Yakobo aliviringisha jiwe kutoka mdomoni mwa kisima na kuwanywesha kondoo.

Genesis 29:11

Yakobo alimwambia nini Raheli, na kisha Raheli alifanya nini?

Yakobo alimwambia Raheli ya kwamba alikuwa ndugu wa baba yake, na kisha Raheli alikimbia na kumwambia baba yake.

Genesis 29:13

Labani aliitikiaje aliposikia kuhusu ujio wa Yakobo?

Labani alikimbia kukutana na Yakobo, akamkumbatia, akambusu, na kumleta katika nyumba yake.

Genesis 29:15

Waelezee mabinti wawili wa Labani.

Lea alikuwa binti mkubwa naye alikuwa na macho dhaifu, wakati Raheli alikuwa mdogo naye alikuwa mzuri wa umbo na muonekano.

Labani na Yakobo walifanya utaratibu gani kuhusu kazi ya Yakobo?

Walikubaliana ya kwamba Yakobo atamtumikia Labani kwa miaka saba kwa ajili ya Raheli.

Genesis 29:19

Kwa nini miaka saba ya kazi ilionekana kama sikuchache tu kwa Yakobo?

Miaka saba ya kazi ilionekana kama siku chache tu kwa sababu ya upendo Yakobo aliokuwa nao kwa Raheli.

Genesis 29:23

Labani alimdanganyaje Yakobo?

Labani alimpatia Lea kwa Yakobo, badala ya Raheli, usiku kabla ya harusi.

Labani alimpatia nani kwa Lea, awe mtumishi wake?

Labani alimpatia mtumishi wake wa kike Zilpa kwa binti yake Lea, awe mtumishi wake.

Genesis 29:26

Kwa nini Labani alisema amemdanganya Yakobo?

Labani alisema ya kuwa haikuwa utamaduni wao kumtoa binti mdogo katika ndoa kabla ya mzaliwa wa kwanza.

Labani na Yakobo walifanya utaratibu gani kuhusu kazi ya Yakobo?

Walikubaliana ya kwamba Yakobo atamtumikia Labani kwa miaka saba zaidi kwa ajili ya Raheli.

Genesis 29:28

Labani alimpatia nani Raheli, awe mtumishi wake?

Labani alimpatia Bilha kwa binti yake Raheli, awe mtumishi wake.

Genesis 29:31

Yahwe alifanya nini alipogundua ya kwamba Yakobo hakumpenda Lea?

Yahwe alimsababisha Lea kupata mimba, lakini Raheli akawa tasa.

Lea alikuwa akitumaini nini iwapo atamzalia wana Yakobo?

Lea alitumaini ya kwamba Yakobo angempenda iwapo atamzalia wana kwa ajili yake?

Jina la mwana wa kwanza wa Lea ni nani?

Jina la mtoto wa kwanza wa Lea alikuwa Rubeni.

Genesis 29:35

Lea alisema nini baada ya kumzaa Yuda?

Baada ya kumzaa Yuda Lea alisema, "Wakati huu nitamsifu Yahwe"