Genesis 19

Genesis 19:1

Lutu alipowaona wale malaika wawili wakija Sodoma, alitaka kuwapa nini?

Lutu aliwaomba ya kwamba wakae katika nyumba yake kwa usiku, na kisha kuondoka asubuhi.

Mwitikio wa malaika kwa Lutu ulikuaje?

Malaika walisema ya kwamba wangekaa usiku katika uwanja wa mjini.

Kwa msisitizo wa Lutu, hatimaye malaika waliamua kukaa wapi usiku huo?

Hatimaye, malaika walienda pamoja na Lutu katika nyumba yake kwa usiku huo.

Genesis 19:4

Wanamume wa mji waliozunguka nyumba ya Lutu walimtaka Lutu kufanya nini?

Wanamume walimtaka Lutu kuwatoa nje wanamume wale wawili waliomtembelea, ili waweze kulala nao.

Genesis 19:6

Lutu aliwapa nini wanamume wa mji kama mbadala?

Lutu aliwapa wanamume wa mji binti zake wawili badala ya wageni wawili.

Genesis 19:9

Wanamume waliitikiaje kwa ahadi ya Lutu?

Wanamume walimwambia Lutu kusimama nyuma na karibu wavunje mlango.

Genesis 19:10

Malaika walifanya nini punde?

Malaika walimvuta Lutu nyuma ndani ya nyumba na kuwapiga wanamume nje kwa upofu.

Genesis 19:12

Malaika walisema walitumwa kufanya nini na Yahwe?

Malaika walisema walitumwa kuangamiza huo mji.

Genesis 19:14

Wakwe za Lutu walipokeaje pale Lutu alipowaambia kuharakisha na kuondoka Sodoma kwa sababi ilikuwa inakaribia kuangamizwa?

Wakwe za Lutu walifikiri Lutu alikuwa akitania.

Asubuhi palipokucha, malaika walimwambia Lutu kufanya nini?

Malaika walimwambia Lutu kumchukua mke wake na binti zake na kuondoka nje ya mji.

Genesis 19:16

Kwa nini malaika waliwaleta Lutu na familia yake kwa kuwashika mikono yao nje ya mji licha ya Lutu kukawia-kawia?

Malaika waliwaweka nje ya mji kwa sababu Yahwe alikuwa amewahurumia.

Malaika walitoa maelekezo gani kwa Lutu walipokuwa nje ya mji?

Malaika walimwambia Lutu na familia yake kutoroka ili waokoe nafsi zao na kutotazama nyuma.

Genesis 19:21

Malaika aliwaruhusu Lutu na familia yake kutorokea wapi?

Lutu na familia yake waliruhusiwa kutorokea katika mji mdogo unaoitwa Soari.

Genesis 19:23

Yahwe alifanya nini Lutu alipofika Soari?

Yahwe alinyeshea chini salfa na moto kutoka mbinguni juu ya Sodoma na Gomora.

Genesis 19:26

Mke wa Lutu alifanya nini na nini kilitokea kwake?

Mke wa Lutu alitazama nyuma, naye akawa nguzo ya chumvi.

Abrahamu aliona nini mapema ya asubuhi alipotazama katika nchi yote ya bondeni?

Abrahamu aliona moshi ukipanda kutoka katika nchi kama moshi wa tanuru.

Genesis 19:30

Lutu alihamia wapi na kwa nini?

Kisha Lutu akahamia katika milima kwa sababu alikuwa na hofu ya kuishi Soari.

Genesis 19:31

Mabinti wa Lutu walikuwa na mpango gani iliyomhusisha baba yao.

Mabinti za Lutu walipanga kumlewesha baba yao, kisha kulala naye ili kwamba waweze kupata watoto.

Genesis 19:36

Makundi gani mawili yalitokana na binti wa Lutu?

Kundi la watu wa Wamoabi na Waamoni walitokana na mabinti wa Lutu.